winnerian
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 335
- 530
Imesainiwa mikataba minne na kwa ufupi tu fedha zote zinatokana na waafrica ikiwemo Watanzania maana ni za Bank ya Maendelo ya Africa lakini cha kusikitisha na kushangaza wote waliopewa zabuni hizi ni wakandarasi kutoka china, katika wakandarasi wote wanne wote ni wachina.
Naomba kama mzalendo wa Africa (Tanzania) jiulize maswali haya kisha utafakari na wazalendo wengine kwa ujumla ni wapi hasa tunataka kufika kimaendeleo kama iwapo pesa zetu wenyewe tumeziachia wachina na tumebaki kuwatumikia wao na kisha wanaenda kufanya maendeleo katika taifa lao huko uchina.
1. Je, Serikali yetu (Tanzania) inayo nia ya dhati kabisa ya kuendeleza sekta nyeti kama hizi (ukandarasi na usimamizi ikiwa ni consultants pamoja na wahandis) ambazo ndizo zinazochukua asilimia kubwa na bajeti yetu kila mwaka (kodi zetu)?
2. Kwanini wanasiasa wanashindwa kuonoa umuhimu wa kuwawezesha wakandarasi katika dhamira ya kweli kabisa (practically) ya kuwajengea uwezo kwa kutunga sera (policies) rafiki na wezeshi kwa wazawa kuweza kupata zabuni kubwa zenye bajeti kubwa na kepelekea kubakiza pesa zetu hapa hapa ndani?
3. Kwanini serikali na viongozi wa kisiasa wamekua ndio chanzo cha kuwasifia makandarasi kutoka nje ya nchi kama china huku wakiwasimanga wale wa ndani ambao wana nia ya kukua (sio wote wenye nia ya kukua, wengine ni matapali)?
Jiulize maswali mengi ukiwa unatafakari kwa kukumbuka yafuatayo:
1. Kumbuka kuwa miradi hii minne ina jumla ya Billion takrabani mia sita - Kama zingebaki hapa nchini zingeweza kulipa kodi, vijana wangepata ajira, mzunguko wa pesa ungekuwa mzuri na kikubwa sana tungekuwa wanufaika wa pesa za mkopo wa Bank ya Maendeleo ya Afrika kwasababu zingebaki mikononi mwetu lakini sasa hatutabaki hata na senti moja, zote zitanda china.
2. Kama wangepewa wazawa kwa kuwanunulia mitambo kisha kuwakata katika malipo yao ya kila mwezi (interim certificates) basi wa kufanya hivyo tungeweza kuwa na wakandarasi hodari na wenye uwezo wa kufanya kazi hata kimataifa kama wanavyofanya wachina wenyewe, sababu wangepata ujuzi, uzoefu, mitambo mipya na bora pamoja na fursa ya kukuza uchumi wao na wa nchi kwa ujumla.
3. Kwa kutumia mfano wa hii miradi minne ni dhahiri kwamba serika ina vingozi na wanasiasa wasiokua na maono ya kizazi kijacho kwa sababu moja kubwa, kama serikali ingetunga sera, sheria, kanuni, mikataba n.k zote hizi ziweze kumnufaisha mzawa wa Taifa lako inamaanisha hata wajukuu hawana cha kufaidika katika nchi ya wenyewe hapo baadae na watakuwa watumwa wa china.
4. Serikali yetu (Tanzania) inasomesha watalaamu wengi lakini wakimaliza masomo yao hawana cha kufanya maana zabuni zote kubwa kubwa wanafanya wachina na watu wengine kutoka mataifa ya mbali. Serikali haioni kama inapoteza nafasi ya kuajiri wananchi wake kupitia setka banafsi bali viongoze wetu wamebaki kuwaonea wivu matajiri na kuwanyanyasa wawezavyo huku wakiwamwagia sifa kemkem watu wa nje kuwa wanaweza kuliko wa ndani.
5. Siasa cha uchama na ukanda zimezidi kushamiri, wabunge wamezidi kuwa mbumbumbux1000000, hawana muda wa kutizama sera, sheria pamojoa na kanuni za kuwawezesha wazao badala yake wanaenda bungeni kusemana na kupigana vijembe, uccm, uchadema, ucuf na uact wazalendo ndio ajenda kuu ya Taifa letu.
Natoa rai kubwa kwamba sera na sheria zitungwe kuwawezesha wakandarasi wa ndani na sio kuwanyanyapaa kwamba hawawezi. Zitungwe sheria kalli ikibidi wekeni kipengele cha kunyonga kabisa kwa wale watakaoleta mzahaa katika kukuza uchumi na utaalaamu wa Taifa kwa maslahi wazao wetu wa hapo mbeleni.
Tenda kubwa zipewe wazao kisha serikali iwanunulie mitambo na iwakate kidogo kidogo katika malipo ya miradi itakayotoa.
Wasanifu na wasimamizi watoke hapa hapa ndani. Kwa sasa tunao wahandisi wa kutosha kufanya kazi kubwa na nzuri, hatupo tena miaka ya uhuru 1961 huko n.k n.k.
Ni mimi mzalendo mwenzenu. Tusibaki tu kwenye CCM na CHADEMA kunayo mambo mengine ya kuyaangazia macho yetu.