Mikataba mibovu sio kwenye madini tu, Mbuga za Wanyama na umilikishaji ardhi kule nako kunatisha.

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
CCM ni kama muchwa, nilikua najaribu kufuatilia baadhi ya tararibu za mikataba ya vitalu vya uwindaji kwenye mbuga zetu za wanyama na Umilikwaji ardhi kwa baadhi ya wawekezaji hakika kunatisha. Kuna makampuni yamepewa vitaulu vya uwindaji mpaka muda wao uishe sidhani kama kuna vizazi vyetu vitabahatika kuwaona baadhi ya Wanyama.Kuna wawekejaji wamemilikishwa mashamba makubwa ambayo yamejiotea nyasi hata kazi.

Kumbe tunapigwa kwingi sio madinini tu, Utawala chini ya CCM ni hatari sana, yaani si wa kuwaamini kabisa maana wanatutwisha mzigo mkubwa sana kwenye maendeleo ya taifa letu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nashangaa watu wamekomalia suala la madini wanasahau rasilimali ardhi, ajira sekta binafsi, utalii/wanyamapori, bidhaa subsrandard kutoka nje ya nchi...n.k.
Matatizo yetu yapo mengi sana na inabidi tuyakabili kiakili bila kukurupuka..!
Cha ajabu the same level of thinking that created our problems is still the one entrusted by multitudes to provide the way forward..!!
 
haha huko kwenye maliasili lazima mpendwa wenu ataguswa..leo...par.d tours...
 
Hujui unachoongelea! bora ukae kimya kuliko kupotosha watu! kwanza uwindaji wa kitalii haufanyiki katika hifadhi za taifa (national parks), kule ni utalii wa picha, sinematography and the like! no consumption at all!
Pili Uwindaji Wa Kitalii Unafanyika Kwenye Mapori Ya Akiba ( Game Reserves) hapa kwa asilimia zaidi ya 90, pia kwenye mapori tengefu (game controlled areas), maeneo ya hifadhi za jamii (wildlife management areas), na maeneo ya wazi ambako kuna wanyamapori! Vilevile B4 Hunting Blocks Allocation Kunafanyika Wildlife Sencus, Na Pia Wavunaji Wanapewa Kiasi Cha Kuvuna Na Wanasimamiwa Kwa Mujibu Wa Sheria! Local Hunting Imesitishwa Kwa Sasa! Ningeeleza Mengi Sana, Ila Nadhani Hayo Yanatosha Ili Kuweka Mambo Sawa Na Kutoa Upotoshaji Kama Anavyotaka Kutuaminisha Mleta Uzi Ambaye Hata Hajui Tofauti Ya Hifadhi Za Taifa, Mapori Ya Akiba, Mapori Tengefu!
 
  • Thanks
Reactions: NHS

Similar Discussions

Back
Top Bottom