fundimchundo
JF-Expert Member
- Jul 23, 2010
- 616
- 904
Tabia hizi za kuropoka ropoka zinaendekezwa na watu waliojipendeza kwa Kiongozi mkuu ambaye naye alipenda sana kusifia.Tukiwa tunataka kuomba kwao tunaanza kuwapamba kwa kuwaita marafiki wa maendeleo. Tukishashiba na kutaka kuwatukana tunawaita mabeberu, ni akili zile zile za kujihami za kiafrika.
Kibaya zaidi JPM mpaka anakufa alitakiwa akatibiwe Ujerumani kwa hao hao mabeberu lakini kwa sababu alikwisha nyea kambi akakubali kuteseka kimya kimya mpaka kifo kilipomfika.
Ni mentality fulani zinazopitwa na wakati kadri siku zinavyokwenda.
Ilipotolewa Hoja Bungeni ya kufanya Ukaguzi mahususi juu ya Mikopo ya Awamu wa 5, wapo watu walitoa povu wakidai JPM hakukopa. Yupo Mtangazaji wa Star TV alikuwa analaani Hoja hiyo kwenye Kipindi anachoongoza cha Tuongee Asubuhi.
Naamini kuwa hivi sasa anajutia kauli zake, maana sasa imedhihirika kuwa Awamu ya Tano, kwa miaka 5 tu, ilikopa kuliko Awamu ya 4 kwa miaka 10.
Tena mikopo ya Kibiashara, yenye Riba kubwa sana.
Utawala wa Awamu ya 5 uligubikwa na ghilba nyingi sana