(Mikasa ya kusisimua) PADRI MLA NYAMA ZA WATU -1

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,268
33,040
Kwa kuanza kujisimulia, Padri Moses anakataa katakata kutaja ni Padri wa madhehebu gani ya dini, kwani Anglikana na Romani wanatumia kofia hiyo ya upadri.

“Nimeshasema kuwa, naziba ili jamii inayonizunguka isielewe kitu chochote kutoka kwangu na siri hii ya aibu,” ndivyo alivyoanza kusimulia Padri Moses ‘Faza Moze’.

Anaendelea:
“Ilikuwa mwaka 1999, mwezi Desemba wakati wakristo wanajiandaa kwa sherehe ya Krismasi, kanisani walikuja wazee wawili ambao ni wageni machoni pangu miongoni mwa waumini wa kanisa langu hilo.

Walikaa fomu moja na waumini wengine, lakini katika kukaa walitenganishwa na mzee mmoja. Nikiwa naendelea na ibada, kila wakati niliwaona wale wazee wageni wakiangaliana kwa kupitia mgongoni kwa yule mzee aliyewatenganisha.
Kwa sababu moyo wangu ulikosa amani na wao, nikawa nawakazia macho hatua kwa hatua ili nione kila walichokuwa wakikifanya.

Kuna wakati nilishtuka sana kuona mmoja wao akibadilika sura na kuwa kama ya bundi, lakini nilipojiweka sawa kushangaa, akarudi katika sura ya kawaida, na mwenzake akacheka kama vile alijua mwenzake amegeuka sura na mimi nimeogopa.
Ndipo nilipoanza kukumbuka ujaji wao kama ulifanana na mazingira ya kuwa waumini wangu. Nikakumbuka kuwa, wakati wanaingia, walipitia njia zote za uumini, na pia walionekana ni wanyenyekevu kupita hata waumini wangu wa kila siku.

Wakati nikiwaza hayo, ghafla mmoja wa wale wazee alisimama mbele yangu bila kumwona akitoka kwenye fomu kuja mbele, nikashituka, lakini kumbe waumini wengine waliniona nilivyoshituka, wakakaza macho kwangu wakishangaa.
Nilikatisha maneno ya ibada na kuinua mikono juu kisha nikafanya ishara ya msalaba, kwa jina la baba, la mwana na la roho…

Akapotea mbele ya macho yangu na kuonekana amekaa na mwezake kama mwanzoni, wakacheka sana lakini si kwa kutoa sauti.

Kufuatia tukio hilo ambalo lilikuwa geni, niliendelea kuwaangalia wazee hao bila kusema kitu chochote.
Mmoja wa wazee hao aliponiona nimewakazia macho, alininyoshea kidole cha shahadu nikapoteza uwezo wa kuona.
Nikiwa katika hali hiyo, nilihisi kama kuna mtu amenigusa juu ya bega langu la kushoto ndipo nilinyosha mkono wangu ili nimguse.

Baada ya kufanya hivyo, nilifumbuka macho lakini jambo la kushangaza sikumuona mtu huyo na nilipoangalia mbele walikokaa waumini, niliwaona wale wazee wawili wakicheka huku wakiniangalia.

Je, nini kitatokea? Usikose kusoma sehemu ya pili ya mkasa huu wa kweli, Padri Mla Nyama za Watu. Maoni, ushauri meseji 0784 275714 au osanjelus@yahoo.com.
 
PADRI MLA NYAMA ZA WATU - 2


Nikakumbuka kuwa, wakati wanaingia, walipitia njia zote za uumini, na pia walionekana ni wanyenyekevu kupita hata waumini wangu wa kila siku.
Wakati nikiwaza hayo, ghafla mmoja wa wale wazee alisimama mbele yangu bila kumwona akitoka kwenye fomu kuja mbele, nikashituka, lakini kumbe waumini wengine waliniona nilivyoshituka, wakakaza macho kiwangu wakishangaa.
Nilikatisha maneno ya ibada na kuinua mikono juu kisha nikafanya ishara ya msalaba, kwa jina la baba, la mwana na la roho…

Akapotea mbele ya macho yangu na kuonekana amekaa na mwezake kama mwanzoni, wakacheka sana lakini si kwa kutoa sauti.

"Nilishtuka sana, nikafikicha macho kuyaweka sawasawa kwani yalionekana kama yana ukungu wa moshi.
Yalipokaa sawasawa, nikaendelea na ibada lakini mwili wangu ukiwa umechoka sana, hauna nguvu tena mwilini kama kuna vitu vunatembeatembea.

Baadhi ya waumini walipata picha hiyo, kwamba sikuwa sawasawa, lakini walikuwa hawajui kama nilikuwa naona watu wa ajabu.

Nilipofika eneo la kuongea maneno ambayo ikawalazimu waumini wasimame, wale wazee wawili wakawa wa kwanza kusimama kabla sijamaliza maneno na wakawa warefu kuliko waumini wangine.

Kurefuka kwao kama kuliambatana na moshi mkubwa wa moto wa kuni.
Nilipowaangalia waumini wengine walionekana hakuna wanalolijua kuhusu maono yangu kwani walisimama, wakafunga mikono kwa unyenyekevu mkubwa wakinisikiliza.

Kama wangekuwa wamegundua kitu, basi hata wale waumini waliokaa jirani wangejua, kwani wao walikuwa wakinitazama tu wakati jirani yao kuna mambo ya ajabu!
Nilikata maneno ya ibada na kuwaamuru waumini wakae, wakatii lakini mshangao:

"Humu ndani kuna watu wawili naona kama si wa imani yetu," nilisema.
Waumini wote wakawa wanageukageuka na kutazamana wakiwatafuta hao watu wawili.

Walichokifanya wale wazee sasa, muumini aliyekaa katikati yao alipogeuka kumwangalia mmoja wao, wakaonekana wote wamekaa pamoja na yule muumini akawa amekaa pembeni yao, kwa hiyo alipogeuka akawa anamwangalia muumini ambaye anamfahamu.

"Naamini hakuna atakayeweza kuwaona, maana wanatumika sana na ibilisi," nilisema.
Ninawapa muda wa wao kujisema ni akina nani?" Nilisema huku nikiwaangalia kwa kuwakazia macho huku waumini nao wakinikazia macho mimi na kuyafuatilia ninakoangalia.

Je, nini kitatokea? Usikose kusoma sehemu ya pili ya mkasa huu wa kweli, Padri Mla Nyama za Watu. Maoni, ushauri meseji 0784 275714 au osanjelus@yahoo.com.
 
PADRI MLA NYAMA ZA WATU - 3


Mara walipotea machoni pangu. Niliwaambia waumini kuwa, wametoweka na nikaonesha mahali walipokuwa wamekaa.
Yule mzee aliyewekwa kati akasema, anachojua yeye ni kwamba, waumini waliokwenda kukaa kulia na kushoto kwake ni wanawake na alitaka kuwauliza kisa cha kukaa upande ule wa wanaume.

Basi, niliendelea na ibada huku kila muumini akionekana hana amani moyoni. Hata pale alipoingia mtu na kuliza mlio wa viatu sakafuni, waumini wote waligeuka kuangalia mpaka ikabidi mimi nisitishe kuendelea na ibada ili waumini wamalize kuangalia.

Ibada ilipokwisha, niliingia kwenye chumba nikavua mavazi ya utumishi, nikabaki na mavazi yangu ya kawaida. Nikiwa natoka nje ya chumba, ghafla nikaona giza nene mbele.

Nikawahi kushika flemu ya mlango huku nikiwa nahakikisha sianguki au kukanyaga sehemu ambayo siyo ardhi. Mpaka hapo nilikuwa siunganishi tatizo la kuona giza na uwepo wa wale waumini wawili wa ajabu ajabu.
"Mtumishi wa Mungu kwema?" Nilisikia sauti ikiniuliza.

"Siyo kwema kabisa."
"Unaona nini mbele?"
"Naona giza."

"Fumba macho."
Nilifumba.
"Haya fumbua sasa."
Nilifumbua.

Nikaendelea kuona kama kawaida, lakini hakukuwepo na mtu yeyote aliyesimama mbele, nyuma, kulia wala kushoto kwangu.
Lakini pamoja na hali hiyo, niliisaka ile sauti akilini mwangu na kuigundua kuwa, ilikuwa ya yule mzee aliyekaa jirani na wale watu wa ajabu.

"Khaa!" Nilijikuta nikishangaa sasa.
Nilitembea kwa mwendo wa haraka hadi kwa waumini waliokuwa wamesimama nje ya kanisa wakiongea, wengine wakisalimiana na kuulizana maisha, kwani waumini wengi huitumia Jumapili kuonana na kuongea mambo yao mbalimbali ya maisha.

Nilizungusha macho kumwangalia yule mzee, nikamwona katikati ya watu akicheka na kupiga soga na wazee wenzake, nikamfuata, lakini huku waumini ninaowapita wakinisalimia, wengine wakionekana kutaka kujua kile kisa cha ndani ya kanisa.
Wakati nakaribia kumfikia, nilijiuliza mwenyewe, je, kweli kwa sauti ile kama angekuwa ni yeye angeshafika katikati ya watu?

"Kama ni hivyo, mbona sasa wakati nafumbua macho sikumwona mbele yangu?"
"Faza pole na majukumu bwana," yule mzee niliyekuwa namfuata alinisalimia na kuwawahi wenzake wote aliosimama nao. Sauti yake niliikumbuka vizuri sana, ndiyo ile iliyonielekeza mpaka nikafumbua macho.

"Nimeshapoa mzee wangu."
Wazee wengine nao pia wakanisalimia huku wakinipa mikono.
"Eti mzee ulikuwa unasemaje?" Nilimuuliza yule mzee.
"Wapi?" Na yeye aliniuliza.

"Hukusimama na mimi pale mlangoni?"
"Mlangoni! Wapi?"
"Kule kwenye chumba?"
"Hata, hapana."

Wazee wengine nao wakaonesha kunishangaa mimi, nikajisikia soni kwa nafasi yangu ya u-Padri.
"Oke, sawa basi."
Nilitembea kwenda kwenye ofisi yangu, lakini nyuma nikamsikia mzee mmoja akisema.
"Kwani mzee Makwaya imekuwaje?"

"Sijui chochote," mzee Makwaya alijibu, hali ya mshangao na minong'ono ya chini kwa chini iliendelea hadi ilipofika mahali nikawa siwasikii.
Kule ofisini nilikuwa peke yangu, nikainamia mezani na kuwaza ile hali mwanzo hadi pale ilipofikia nikaona giza nene mbele yangu.

"Hivi, wale ni akina nani?"
"Ni kwanini walinijia kanisani?"
"Wametumwa au?"
Nikiwa naendelea kuwaza hivyo, mara nikasikia sauti ndani ya ofisi.

"Unaendeleaje mtumishi wa Mungu?"
Ilikuwa ni sauti ya yule yule mzee Makwaya.
Nilishtuka sana, nikaangalia kila kona ya ofisi.

Je, nini kitatokea? Usikose kusoma sehemu ya pili ya mkasa huu wa kweli, Padri Mla Nyama za Watu. Maoni, ushauri meseji 0784 275714 au osanjelus@yahoo.com.
 
Nilijifanya kushtuka na kwamba siyajui hayo huku ukweli ni kwamba, kila kitu alichokiaongea mimi ndiye nilikuwa kinara ingawa si kweli kwamba tuliwalimisha.

"Sasa waliwatambua?"
"Hapana, mchawi unaweza kumtambua?"
"Kweli huwezi."

"Eee, mchawi hata akiwa baba yako au mama yako, anaweza kukuingilia na usimjue, labda kama una malaika wakali," alisema.
Tuliagana, akaendelea na safari yake na mimi na safari yangu. Mbele nikasimamishwa na mzee mmoja, huyu mzee tunaelewana sana kupita wote wanaoabudu katika kanisa lile. ENDELEA…

"Bwana nilikuwa nataka kuja kwako," alisema.
"Sasa?"
"Sasa basi, labda niongee hapa hapa."
"Ongea mzee wangu."

Alianza kwa kuniambia kuwa, kuna watu wanajiandaa kwenda kwa Askofu kutoa malalamiko kuhusu siku ambayo mimi nilipanda madhabahuni na pajama badala ya mavazi ya kitumishi.

Nilishtuka sana kusikia hivyo, nikamuuliza majina ya hao wazee, miongoni mwao ni wale wote waliosimama siku hiyo na kujifanya wanajua zaidi, akiwemo yule tuliyemcheza mpira yeye na mkewe usiku.

"Aaa, sasa kwani kuvaa pajama jamani si bahati mbaya tu, wao walichukuliaje?"
"Wao walichukulia ulikuwa unatuwangia. Na hivi sasa kanisa limegawanyika, wengine wanasema wewe ni mwanga, wengine wanakataa, Padri hawezi kuwa mwanga."

"Wewe unanichukulia mimi ni nani?" Nilimuuliza yule mzee.
"Ni mtumishi wa Mungu aliye hai."
"Sawa, usimwambie mtu maneno hayo, waache wafikirie hivyo hivyo."

Tuliagana, akaondoka zake lakini mbele kidogo, nikasimamishwa na mwanamke mmoja, mzee sana, yaani bibi kizee, sijawahi kumwona hata siku moja. Lakini kwa rika langu angeweza kuwa mama yangu mzazi.
"Shikamoo mama."
"Marhaba, hujambo mwanangu?"

"Sijambo mama, haya unasemaje?"
"Ah! Nina usemi basi, njaa tu."
"Hujala mama?"

"Nimekula, tena nimeshiba sana," alinijibu.
"Sasa njaa ya nini?"
"Nyama."
"Nyama! Nyama gani mama, ya ng'ombe?"

Badala ya kunijibu, alinisogelea hadi mlangoni kabisa kwenye gari, akanyoosha shingo ili kunifikia sikioni.
"Nyama nzito."
"Mh! Mama, mbona sijakuelewa, nyama nzito ni ipi?"

"Ile yenye minofu minene."
"Mbona siijui, ya nguruwe?"
"Hapana, ya mtu! Najua unaweza kufanya nikapata."

Damu zilinisisimka mwili mzima, nikahisi kupoteza fahamu huku nikiwa nawaza yule mama alinifikiriaje au alisikia nini kuhusu mimi mpaka kusema maneno yale.
"Sasa mama, mimi nyama ya mtu nitaipata wapi?"

"Popote pale."
"Kama wapi?" Nilimuuliza.
"Utanipa hunipi?" Aliuliza kwa sauti ya juu sasa.

Nilitaka kufunga kioo cha gari niondoke, lakini kwa vile sikuwa nimemjua kiundani sana, niliamua kuacha.
"Nataka uniletee nyumbani kwangu usiku wa leo."
"Wapi?"
"N'takuonesha," alisema huku akianza kutembea kwenda upande mwingine.

Sikujua atanionesha kwa mimi kumnyima nyama ya mtu au wapi atapatikana ili nimpe hiyo nyama. Niliamua kumpuuza na kuendelea na safari yangu.
Nilifika njia panda moja ambapo nilitakiwa kwenda kulia, lakini nikaona kuna mlima upande huo ambapo kawaida huwa hakuna mlima kama nilivyoona pale.

Nilisimama kwa muda wa kama nusu dakika nikiuangalia ule mlima. Ulianza kurefuka, ukaendelea kidogo kidogo huku ukiota majani ya kijani pembeni. Urefu wake ulizidi hata mlima Kilimanjaro, lakini kufumba na kufumbua ukafutika na kusindikizwa na sauti nzito.

"Huo urefu wa mlima ndiyo utakuwa wako katika ulimwengu wa kichawi."
Ile sauti ikakata, barabara ikaonekana kama kawaida, nikaelekea upande huo.

***
Usiku wa siku hiyo, nikiwa nyumbani, nilianza kumfikiria yule mama aliyesema anataka nyama ya mtu na alivyoondoka. Pia nilifikiria ni kwanini baada ya kuondoka tu, mbele ya safari yangu ndiyo mlima mkubwa ukachipuka kimaajabu?

Nikiwa bado nawaza, nikachukuliwa na usingizi mzito sana, kuja kushtuka nikasikia filimbi ya kuitwa kwenye makutano yetu wachawi.

Nilisimama, nikageuka kuangalia kitandani, nikanyoosha mkono pembeni na kuchukua shuka jeupe, nikalivaa kama taulo, kufumba na kufumbua nilikuwa kwenye makutano yetu. Waliokwishafika walikuwa wakipiga ngoma na kucheza huku wote waliokuwa wakicheza wakitumia mguu mmoja kutembelea eneo lile lote.
Baada ya wachawi wengi kufika, nilisimama katikati yao na kunyoosha mikono yangu juu, wakatulia, nikapiga makofi, wote wakaunga kwa makofi.

"Pa pa pa pa pa!"
Kabla sijasema, mwanamke mmoja wa kanisani ambaye pia ni mchawi alipita mbele akasimama jirani yangu, huku akiinamisha kichwa akasema:
"Unanikumbuka mkuu?"

Nilimwangalia kwa umakini sana, nikawaza kwanini anasema vile wakati wachawi wote wa kanisani tunajuana na ni siri yetu.
"Nakufahamu vizuri sana," nilimjibu nikimkazia macho.

"Uliniona wapi?"
"Khaa! Wewe si tuko pamoja hapa na pia kule kanisani?" Nilimhoji.
"Ndiyo najua, lakini je hukumbuki leo tumeonana mahali?"

"Sikumbuki, labda unikumbushe wewe."
Alinikazia macho huku taratibu akianza kuzeeka na nguo alizovaa zikianza kubadilika. Ilifika mahali akawa ni yule bibi kizee aliyeniomba nimpatie nyama ya mtu na kesema atanionesha.

Je, nini kitatokea? Usikose baadae.....
 
PADRI MLA NYAMA ZA WATU - 7...

Baada ya wachawi wengi kufika, nilisimama katikati yao na kunyoosha mikono yangu juu, wakatulia, nikapiga makofi, wote wakaunga kwa makofi.
"Pa pa pa pa pa!"
Kabla sijasema, mwanamke mmoja wa kanisani ambaye pia ni mchawi alipita mbele akasimama jirani yangu, huku akiinamisha kichwa akasema:
"Unanikumbuka mkuu?"
Nilimwangalia kwa umakini sana, nikawaza kwanini anasema vile wakati wachawi wote wa kanisani tunajuana na ni siri yetu.
"Nakufahamu vizuri sana," nilimjibu nikimkazia macho.
"Uliniona wapi?"
SASA ENDELEA…
"Khaa! Wewe si tuko pamoja hapa na pia kule kanisani?" Nilimhoji.
"Ndiyo najua, lakini je, hukumbuki leo tumeonana mahali?"
"Sikumbuki, labda unikumbushe wewe."
Alinikazia macho huku taratibu akianza kuzeeka na nguo alizovaa zikianza kubadilika. Ilifika mahali akawa ni yule bibi kizee aliyeniomba nimpatie nyama ya mtu na kusema atanionesha.
"Ha!" Mimi nilishtuka kumwona akiwa vile.
"Ee," alisema.

"Si umenikumbuka sasa?"
"Ndiyo mama."
"Haya endelea," alisema akarudia katika hali yake ya kawaida.
Kifupi sikuwa nimejua maana ya tukio lile. Lakini pia sikutaka kuhoji wala kuuliza kwa mchawi mwingine.
Mimi niliendelea kuongea maneno ambayo hadi leo huwa najiuliza yalitoka wapi!

"Leo ni siku ya kupanga mikakati mikubwamikubwa ya kuangamiza watu, hasa wale wanaojifanya wanakwenda sawa sawa, sawa?"
"Sawa," walinijibu.
Niliwaambia nimetumwa kutoka kwa kiongozi mkuu wa wachawi duniani kote akisema kuwa, kumekuwa na ongezeko kubwa la wanawake wanaozaa salama.
"Si kweli jamani?"
"Kweli."
Nikawaambia miongoni mwa mikakati inayotakiwa kufanywa ni pamoja na huo, kuhakikisha wanawake kuzaa salama kunapungua na ikiwezekana kufa kabisa, kivipi?

"Tunatakiwa kuhakikisha tunawashughulikia wajawazito wote ili wanapokwenda kujifungua wapasuliwe, sawa?"
"Sawa."
"Kingine! Kingine, ni kuchukua damu za watoto wachanga waliopo matumboni."
Watu walipiga makofi sana, ikafika mahali wakawa wanachezacheza.
"Sasa kwa kuanza kazi hii, usiku huu huu tunaanza kuingia mitaani mpaka asubuhi. Halafu tutarudi majumbani kupumzika kama saa moja tu, kisha tutatoka tena na kurudi mitaani kushughulikia wanawake wanaokwenda kliniki asubuhi, sawa?"
Walisema sawa huku wakitawanyika katika vikunndi vidogovidogo vyenye wachawi watano watano.

Wachawi siku zote wanapenda sana hilo, miongoni mwa masharti yao ni kutumia namba zisizogawanyika kwa mbili katika kila walifanyalo, mfano, kutembea katika makundi ya watu watatu, watano, saba, tisa, kumi na moja.
Au hata wanapotaka kutengeneza kitu kwa siku, hupenda kutumia namba hizo hizo, siku tatu, tano, saba, tisa nakadhalika. Hizi namba hupendwa hata na waganga wa kienyeji, mara nyingi akikupa dawa au masharti fulani atakwambia utafanya hivi kwa siku tatu, tano, saba, tisa na kuendelea.

Ndivyo walivyoondoka wachawi wenzangu, na mimi nikaongozana na wengine wawili, jumla tukawa watatu.
Kila safari ilikuwa na kinara wake, kwenye kundi langu mimi niliendelea kuwa kinara katika safari hiyo.
Mimi na wale wenzangu tulikwenda kuingia kwenye nyumba moja ambayo tulikuwa tukiamini kuwa, kuna mwanamke ambaye ni mjamzito.

Ni ajabu, kwani kwa muda huo tulimkuta yeye na mumewe wamekaa sebuleni wanaongea, mtoto wao mmoja alikuwa amelala kwenye kochi kubwa hapo hapo sebuleni.
Niliwasimamisha wenzangu ambao walikuwa nyuma yangu, wakasimama huku wakipeleka vichawa pembeni kuona mbele. Nilisimama na kuwageukia wote nikalaza kidole changu kwa kuwawekea alama mdomoni kama ishara ya kusema shiiii.

Nilipomaliza kufanya kwa ishara hiyo, niliwageukia wale watu, nilimsogelea yule mwanamke maana lengo sasa lilikuwa ni kuhakikisha namtoa mtoto ndani ya tumbo.
Nilipomfikia na kuwa naye sambamba, nilinyoosha mkono na kulishika tumbo bila mwenyewe kufahamu kama anashikwa tumboni.
Nililiminyaminya lile tumbo, nikautembeza mkono kila kona huku naendelea kuliminya, ghafla alishtuka na kulishika tumbo lake kwa maumivu ya kushtukiza.

"Nini tena?" Mumewe alimuuliza na yeye akionekana ameshtuka sana.
"Tumbo mume wangu, tumbo," alianza kulia.
"Linafanyaje?"
"Linakata sana mume wangu."
Mumewe alisimama, wakati huo huo mimi nilirudi nyuma na kusimama na wenzangu mstari mmoja. Tukawa tunaita kwa mikono, ghafla kitoto kichanga kikiwa hewani kilielea kuja kwetu tukiwa tumekinga mikono ili kukipokea kisigonge ukuta.

Lakini wakati wote huo, yule mwanamke alionekana bado ni mjamzito kama awali huku akiendelea kulalamikia maumivu ya tumbo lake.
Nilikibeba kitoto kile na kukielekezea juu kisha nikamkabidhi mchawi mwingine aliyekuwa kushoto kwangu.
"Twende hospitali basi," alisema mume, lakini mke hakujibu kwani alikuwa tayari kwa lolote lile ambalo lingetokea. Na sisi tulikubaliana kwenda mpaka huko hospitali kuangalia kitakachotokea.

Je, nini kitatokea? Usikose baadae...............
 
[h=1]PADRI MLA NYAMA ZA WATU - 8...[/h]Mumewe alisimama, wakati huo huo mimi nilirudi nyuma na kusimama na wenzangu mstari mmoja. Tukawa tunaita kwa mikono, ghafla kitoto kichanga kikiwa hewani kilielea kuja kwetu tukiwa tumekinga mikono ili kukipokea kisigonge ukuta. Lakini wakati wote huo, yule mwanamke alionekana bado ni mjamzito kama awali huku akiendelea kulalamikia maumivu ya tumbo lake. Nilikibeba kitoto kile na kukielekezea juu kisha nikamkabidhi mchawi mwingine aliyekuwa kushoto kwangu. "Twende hospitali basi," alisema mume, lakini mke hakujibu kwani alikuwa tayari kwa lolote lile ambalo lingetokea. Na sisi tulikubaliana kwenda mpaka huko hospitali kuangalia kitakachotokea. SASA ENDELEA…
"Safari ilianza kwa mke na mume kuelekea hospitali huku sisi tukiwa tumeshafika kwa njia zetu za kichawi.
Manesi walimpokea vizuri sana mgonjwa huyo huku wakimwambia mumewe kuwa, amefanya vizuri kumwahisha hospitali kwa sababu hali yake ni mbaya zaidi.
"Lakini atapona?"
"Atapona tu, usiwe na wasiwasi."

Nesi mmoja aliposema hivyo, mimi nilimfuata yule mgonjwa na kumwekea tena mkono kichwani nikamgandamiza naye akaanza kulia kwa sauti huku akishika tumbo lake.
"Mama nakufa, mume wangu nakufa," alilalamika.
Manesi walikimbia huku na kule wakimtafutia dawa za kumpa.
Ilifika wakati nikawaita wachawi wenzangu waliokuwa wamesimama nyuma yangu, wakasogea, nikawaambia wakinge mikono kwa yule mwanamke, wakafanya hivyo, kitoto kikatoka kikiwa katika hali ya umauti.
Tuliondoka mpaka kwenye uwanja wa nyumba yake, pale tukaweka mduara na kukiweka kile kichanga chini.

Tulikimwagia mchanga mpaka kikawa hakionekani kisha ule mchanga tukauchota kidogo na kuutia kwenye kitambaa cheusi, mmoja wa wachawi akakichukua kuutunza kwa ajili ya matumizi mengine.
Usiku huo huo, tulikwenda kwa mwanamke mwingine ambaye naye ni miongoni mwa wambeya wa kanisani kwa kupita mitaani na kusambaza habari kuwa, mimi ni mchawi wa kutupwa.
Tulimkuta amelala hoi, huyu mwanamke hakuwa na mume, tulimchukua juu juu akiwa bado amelala hadi nje kwake, tukamtafutia fagio ili afagie uwanja usiku huo huo.

Alikuwa akifagia huku tunampiga kwa fimbo na kuumia, tulifanya hivyo mpaka akaanguka chini na kupoteza fahamu, tukamchukua mpaka kitandani kwake, sisi tukaondoka zetu.
Kwa vile kule hospitali kulikuwa na wanawake wengine waliokuwa wajawazito wakisubiri kujifungua, niliamuru turudi ili kufanya uharibifu wetu ambao ungewaweka pabaya wajawazito wote walikwenda kujifungua kwenye hospitali ile.

Tulifikia mapokezi ambapo mjamzito mmoja alikuwa bado hajapewa kitanda, tulimzunguka na kuanza kumng'ong'a huku tukimgusagusa usoni na kichwani bila mwenyewe kujua kama kuna wachawi, ila akawa anapepea mikono karibu na uso wake akiamini anaguswa na mbu au wadudu wa usiku.
Baada ya dakika kama tatu, niliamuru wachawi kusimama kisha nikamfuata na kumshika tumbo kwa kulipapasa, pale pale akaanza kujinyoganyonga, ndugu zake wakamzunguka na kumuuliza kama anajisikia vibaya tena.
"Eee," alijibu kwa uvivu na kuchoka sana.

Ndugu mmoja akaenda mbio kwa manesi huku wengine wakiwalaani kwamba, toka wamempeleka mgonjwa wao pale hakuna kitu kilichofanyika zaidi ya kuendelea kupeana habari za filamu za Kinaijeria.
Mara, nesi mmoja akaja akiwa ameongozana na yule ndugu aliyewafuata, wakamchukua yule mgonjwa kwenye kitanda, lakini wakati wanakwenda mimi nikamtoa yule mama mjamzito na kubakisha kitenge chake, lakini manesi na ndugu waliendelea kujua wanamburuza yule mwanamke mjamzito.
Mimi nilipokelewa na wachawi wenzangu huku tukiendelea kuliminyaminya tumbo lake. Tulifanya vile ili tumbo likae vibaya na kushindwa kuzaa sawasawa hivyo apigwe kisu cha upasuaji.

Walipofika kwenye mlango wa wadi ya kuzalia, nilimrudisha kitandani, wakaingia naye maana hali yake ilikuwa mbaya sana.
Lakini wachawi wote tukazama ndani ya ile wadi ambako kulikuwa na wajawazito wengine watatu, jumla wakawa wanne na yule tuliyekwenda naye sisi.
Wachawi wote tukasimama pembeni na kuanza kucheza ngoma za kichawi lakini kwa kuimba nyimbo bila kuwepo kwa ngoma.
Muda si mrefu, wakaingia wachawi wa kundi jingine, wakaungana na sisi, tukawa wengi sana mpaka manesi wakaanza kulalamika kuwa, ndani mle kuna joto AC hazifanyi kazi sawasawa.

"Hizi AC yaani zimekufa nguvu kabisa siku hizi," alisema nesi mmoja akiziangalia kwa macho.
Ikawa kila mchawi anatoka kwa zamu yake na kwenda kumdandia tumboni mjamzito mmoja, kisha anarudi, anatoka mwingine.
Kichawi, kwa kufanya hivyo pekee kunafanya tumbo la mjamzito kukaa vibaya hivyo si rahisi kuzaa salama mpango ambao sisi tulikuwa tunautaka.
Mjamzito mmoja akapiga kelele akisema anahisi kama amewekewa jiko la mkaa lenye moto kwenye tumbo lake. Akalia sana.
"Sasa unalia nini?" Nesi alimuuliza.

"Kwani sisi ndiyo tuliokupa hiyo mimba, starehe yako mwenyewe unatupigia kelele sisi," alisema nesi mwingine.
Sisi wachawi tuliendelea na zoezi letu huku tukipongezana kwamba kazi inakwenda vizuri, mpaka saa kumi alfajiri wajawazito wote walikuwa wamepasuliwa na kutolewa watoto, kitoto kimoja kikafa kwani tulikiziba pumzi.

***
Ilikuwa Jumapili iliyofuata, tukiwa ndani ya ibada kanisani, mimi nimesimama madhabahuni, akasimama mzeee mmoja bila kuruhusiwa wala kunyoosha kidole.
Nilitupia jicho baya sana, kwani nilihisi ana kitu kuhusu mimi tu. Sikumwambia kitu, ila yeye akasema:
"Padri ninataka kusema kitu mbele ya waumini wenzangu, mbele ya kanisa na mbele ya Mungu muumba wa mbingu na nchi."
Je, nini kitatokea? Usikose baadae.....
 
[h=1]PADRI MLA NYAMA ZA WATU - 9..[/h]Moyoni nilitamani sana yule mzee atokee ili akabiliane na zile tuhuma zile ambazo mimi zilinifika shingoni na niliingiwa na kinyongo na kazi ile ya kichawi ambapo awali niliambiwa hakuna ambaye angeweza kutuona wakati tukiwa kwenye matukio yetu.

"Eee Bwana niepushe na aibu hii, sirudii tena mimi, nimeshajirekebisha," nilisali kimoyomoyo peke yangu pale mbele ya madhabahu. Nikajikuta nakohoa pia bila sababu.
Ghafla mzee mwingine akanyoosha kidole, wakawa wawili sasa. Lakini pia wakati yule akiendelea kuongea na vile vidole viwili vikiwa juu, mke wa yule mzee aliyekuwa akiongea naye akanyoosha kidole.
SASA ENDELEA…

"Mbaya zaidi, watu waliotuingilia kutufanyia hivyo huwezi kuamini ukiambiwa, hii ni aibu kwa kanisa na pia ni kufa kiroho. Mungu hawezi kuuvumilia ubaya huu."
Wakati anazidi kubomoa, mimi haja ndogo ilinibana, nikawa navumilia tu.
Nilitamani ardhi ipasuke, mimi niingie ndani mwake na nisionekane tena maishani mwangu. Mwili ulinitetemeka, akili ikanipotea, nikawa sijui niamue nini.

"Hali ikiwa hivi kuna siku humu huku kanisani watu watashikania mapanga kutoana damu, hakiyanani vile."
Yule mzee alipomaliza kusema hayo, akaa ghafla kama vile alishikwa na kukalishwa kwa nguvu.
Nikataka kusema muda umekwisha, lakini mzee mmoja kati ya wale walionyoosha vidole alisimama hata bila kuruhisiwa, alipoona mwenzake amekaa tu.

"Nashukuru sana na mimi kwa kupata muda huu. Zamani uchawi hapa kanisani ulikuwa ni msemo tu, si kitu ambacho kinatingisha, lakini mimi nina habari kwamba, sasa uchawi umo ndani kabisa ya hili kanisa, tena washiriki ukitajiwa majina unaweza kubisha hadi unaanguka chini.

"Mimi kama nitapata baraka za waumini wenzangu niko tayari nitaje majina, lakini nilindwe."
Nilimwangalia vizuri yule mzee nikamwona kama ametumwa, kwani wakati anaongea, hakuwa ananiangalia mimi, wala mtu mwingine, alaiinama tu huku akibwabwaja.

"Sema."
"Wataje."
"Waweke wazi bwana."

"Tutajie."
"Tuambie."
Hayo yalikuwa maneno ya waumini wa kanisa lile ambayo yalinichanganya kabisa. Baadhi ya waumini wakawa wanainama kunong'onezana huku wakiniangalia kwa kuniibiaibia.
"Niwataje?" Yule mzee aliuliza tena kwa sauti ya juu.

"Watajeeee."
Wakati huo, yule mzee mwingie na yule mke wa yule wa kwanza, vidole vyao vilikuwa bado juu wakiomba nafasi ya wao kuongea.

"Eti niwataje?"
Inaonekana aliniuliza mimi kwani aliniangalia. Na hapo ndipo nilipojua kuwa, hata mimi niko ndani ya tuhuma za kutajwa kwani kama nisingekuwemo, yule muumini angeniuliza hivi, ‘eti mtumishi wa Mungu niwataje?' sasa hakusema mtumishi kwa sababu alishajua sina cha utumishi wala uchungaji.

"Nalinda heshima ya kanisa, siwataji, ila nawataka waache mara moja tabia hiyo," alimaliza yule mzee na kukaa.
Ghafla tena akasimama mzee mwingine hiku akiendelea kunyoosha kile kidole chake.
Jamani muda naona umetuishia, siwezi kuruhusu mambo hayo, ila nitaunda kamati ya kushughulikia, matokeo yatatangazwa humu humu kanisani.

"Lini?" Waumini walihoji kwa pamoja.
"Eee, Jumapili ijayo."
"Tuhakikishie."
"Ha! Niwahakikishie kwani mimi ndiye mchawi?" Nilijibu kwa jabza sasa.

"Mh!"
"Mh!"
"Mh!"
Waumini waligunia chini kwa chini. Sasa sikujua waliguna kwa sababu ya majibu yangu au kwa sababu walishajua mimi ni mchawi. Hiyo iliniuma sana, lakini sikuwa na jinsi zaidi ya kusema hivyo.

Kilichonishangaza zaidi hata wale wazee wenye hekima zao katika kanisa hakuna aliyetoa sauti kuongea kitu kwa kunitetea wala kutengeneza amani.
Nilimaliza ibada, watu wakatoka nje mmoja baada ya mwingine. Lakini kule nje wakasimama katika makundi makundi isivyo kawaida.

Halafu wakawa wanaonekana wakiongea kwa tahadhari sana, kwani kila mara walionekana kuangalia mlango wa kuingilia kanisani na wa ofisini kwangu.
Na mimi nilitoka nje na kuiacha ofisi tupu, nikasimama ili kuangalia nini kinaendelea kwa waumini wangu, lakini nao wakaanza kutimka mmoja mmoja.

Hoja kwamba walinigundua mimi ilipata nguvu baada ya baadhi ya waumini kunipita tu wakati wanaondoka wakati su jambo la kawaida kwao.
"Mama," nilimwita muumini mmoja, akasimama. Mimi ndiyo nikamfuata aliposimamia.
"Mama kwani kuna nini leo?" Nilimuuliza.

"Hujui?"
"Sijui kitu."
"He he! Uchawi kanisani," alisema.
"Sasa mbona watu wananitenga?" Nilimuuliza, lakini badala ya kunijibu akaondoka zake haraka.

Ghafla nikasikia mlango wa ofisini kwangu ukigongwa kwa nguvu kama kuna mtu ndani, nikaenda haraka.
Kufika nikamkuta yule mzee tuliyekwenda kuwanga naye usiku nyumbani kwa wale waumini.
"Umefanya nini sasa? Ona yaliyokupata." Aliniiliza kwa hasira sana.
Je, nini kitatokea? Usikose baadae
 
[h=1]PADRI MLA NYAMA ZA WATU - 10....[/h]Na mimi nilitoka nje na kuiacha ofisi tupu, nikasimama ili kuangalia nini kinaendelea kwa waumini wangu, lakini nao wakaanza kutimka mmoja mmoja.

Hoja kwamba walinigundua mimi ilipata nguvu baada ya baadhi ya waumini kunipita tu wakati wanaondoka wakati su jambo la kawaida kwao.

"Mama," nilimwita muumini mmoja, akasimama. Mimi ndiyo nikamfuata aliposimamia.

"Mama kwani kuna nini leo?" Nilimuuliza.
"Hujui?"
"Sijui kitu."

"He he! Uchawi kanisani," alisema.
"Sasa mbona watu wananitenga?" Nilimuuliza, lakini badala ya kunijibu akaondoka zake haraka.

Ghafla nikasikia mlango wa ofisini kwangu ukigongwa kwa nguvu kama kuna mtu ndani, nikaenda haraka.

Kufika nikamkuta yule mzee tuliyekwenda kuwanga naye usiku nyumbani kwa wale waumini.
"Umefanya nini sasa? Ona yaliyokupata." Aliniuliza kwa hasira sana.
SASA ENDELEA MWENYEWE…

"Kwani kosa langu ni nini?" Nilimuuliza na mimi nikiamini sikuwa na hatia, bali yeye ndiye aliniingiza mkenge.
"Wewe umekwenda kanisani bila kumwomba mkuu kwa sala."
"Mkuu gani?"

"Kwani mkuu wako kwa sasa ni nani?"
"SI Mungu!"
"Ha ha ha ha! Siyo Mungu, Mungu yupi kwanza, yule wako wa zamani?"

"Hata sasa."
"Amekwambia nani, hujui kama umeshasajiliwa kwa mkuu wa giza? Kuanzia siku ile pale wewe ni wa mkuu wa giza kama sisi."

"Oke, turudi kwenye msingi wa maongezi, kosa langu ni lipi?"
"Kosa nimeshakwambia, leo kanisani kila mtu amekushangaa wewe kwa jinsi ulivyokuwa umevaa nguo za kulalia madhabahuni, lakini wewe mwenyewe ulidhani umevaa joho."

Moyo ulinilipuka lip. Nikashangaa sana huku nikijiuliza maswali mengi na kuvuta picha ya jinsi nilivyoonekana.

Lakini mpaka hapo, nilipojiangalia mwenyewe nilikuwa nimevaa joho la utumishi, sasa hizo nguo za kulalia ni zipi!
"Mbona nimevaa inavyotakiwa?" Nilimuuliza.
"Ndivyo unavyojidanganya?"

"Kh! Si hivi, kwani we hunioni?"
Yule mzee alicheka, akaangalia chini kisha akatembeza mkono wake chini kama anafuta, ukawa na vumbi kisha akanipaka lile vumbi usoni kwangu.

Pale pale nilipojiangalia, kweli nilionekana nimevaa pajama ya kulalia, ya chini na ya juu.

Nilishtuka zaidi, mwili ukaingiwa na ganzi na kuanza kuhisi mshangao niliousababisha kwa waumini wangu, nikaanza kupitia maongezi ya wale waumini waliosimama kuongea wakisema hivi:
"Mbaya zaidi, watu waliotuingilia kutufanyia hivyo huwezi kuamini ukiambiwa, hii ni aibu kwa kanisa na pia ni kufa kiroho. Mungu hawezi kuuvumilia ubaya huu."

"Hali ikiwa hivi kuna siku humu humu kanisani watu watashika mapanga kutoana damu, hakiyanani vile."
(Mzee mwingine anasimama).

"Nashukuru sana na mimi kwa kupata muda huu. Zamani uchawi hapa kanisani ulikuwa ni msemo tu, si kitu ambacho kinatingisha, lakini mimi nina habari kwamba, sasa uchawi umo ndani kabisa ya hili kanisa, tena washiriki ukitajiwa majina unaweza kubisha hadi unaanguka chini.

"Mimi kama nitapata baraka za waumini wenzangu niko tayari nitaje majina, lakini nilindwe."
"Sema."
"Wataje."

"Waweke wazi bwana."
"Tutajie."
"Tuambie."

"Niwataje?"
"Watajeeee."
"Eti niwataje?"

"Nalinda heshima ya kanisa, siwataji, ila nawataka waache mara moja tabia hiyo."
"Niachieni mimi, nitalifanyia kazi na matokeo yatatangazwa humu kanisani."

"Lini?"
"Eee, Jumapili ijayo."
"Tuhakikishie."

"Ha! Niwahakikishie kwani mimi ndiye mchawi?" (Waumini wanaguna).
"Mh!"
"Mh!"
"Mh!"

(Anamwita muumini mmoja nje).
"Mama kwani kuna nini leo?"
"Hujui?"
"Sijui kitu."

"He he! Uchawi kanisani."
"Sasa mbona watu wananitenga?"
(Yule mama anaondoka haraka).

"Oooph! Kweli nitakuwa nimeumbuka sana, sasa?" Nilimuuliza yule mzee baada ya kuwaza hayo yote yalivyokuwa kwenye ibada.
"Hakuna cha sasa, hapa kampeni moja tu, kuhakikisha wale wote waliosimama kuuliza maswali wanakufa."

"Mh! Kwa njia gani. Halafu na wewe una makosa, kwanini usije kunishtua pale madhabahuni kuwa nimevaa pajama?" Nilimwambia na kumuuliza yule mzee.

"Nilijitahidi lakini kukufikia pale mbele ikawa kazi. Unajua makanisa karibu yote yana nguvu ya Mungu mbele, huwezi kufika kirahisi. Mimi nilisimama kushoto kwako nikawa nakuangalia."

Tukiwa tunaongea hayo, mara mama mmoja akasimama mbele yetu, ni muumini wa kanisani lakini sikujua kama ni mchawi.
"Leo padri umechemsha sana," alisema akiwa amesimama mbele yetu huku akihema kwa nguvu.

Tulimwaangalia kwa umakini sana huku tukionesha uso wa mshangao.

"Kwani unajua chochote?" Nilimuuliza.
"Kuhusu nini?" Naye aliuliza.
"Kwani umesemaje wewe?"

"Nimesema leo umechemsha sana madhabahuni kwako."
"Ndiyo maana nimekuuliza kwani unajua chochote?"
"Najua, si nimekuona. Unakujaje kwenye madhabahu ya Bwana ukiwa umevaa pajama?"

Mwili wote ulikufa ganzi tena, nikahisi roho inataka kumrudia aliyeiumba, mwili kwenda mavumbini.
"Kwani unadhani mimi sijui kitu kuhusu wewe kujiunga na Mungu wa giza, najua."

Niliendelea kumkodolea macho ya mshangao.
Yule mzee alimwangalia sana, akamuuliza.
"Wewe upo kwenye kambi ya mzee Masomo?"

"Ndiyo," alijibu yule mwanamke lakini akionekana kama hana habari sana na yule mzee kuliko mimi. Akaniuliza.
"Ni kwanini umeamua kumtumikia Mungu wa upepo?"
"Sijamtumikia mimi," nilimjibu kwa hasira.

Wote, yaani yule mwanamke na yule mzee wakacheka.
"Umechelewa sana, kama unataka kufa endeelea kusema hivyo," yule mzee aliniambia kwa sauti ya kukazia, nikaogopa mwenyewe.

Yule mwanamke akasimama sawasawa kisha akainama kidogo aliponyanyua shingo, akasema:
"Padri mimi nimekuja na ujumbe wako, naamini utaupokea na utaufanyia kazi haraka sana, naomba uupokee."

"Ujumbe gani na umetoka kwa nani?" Nilimuuliza nikimwangalia kuuona huo ujumbe wenyewe, kama ni barua au maneno tu.

Je, nini kitatokea? baadae
 
[h=1]PADRE MLA NYAMA ZA WATU - 11..[/h]Mwili wote ulikufa ganzi tena, nikahisi roho inataka kumrudia aliyeiumba, mwili kwenda mavumbini.
"Kwani unadhani mimi sijui kitu kuhusu wewe kujiunga na Mungu wa giza, najua."
Niliendelea kumkodolea macho ya mshangao.
Yule mzee alimwangalia sana, akamuuliza.

"Wewe upo kwenye kambi ya mzee Masomo?"
"Ndiyo," alijibu yule mwanamke lakini akionekana kama hana habari sana na yule mzee kuliko mimi. Akaniuliza.
"Ni kwanini umeamua kumtumikia Mungu wa upepo?"
"Sijamtumikia mimi," nilimjibu kwa hasira.
Wote, yaani yule mwanamke na yule mzee wakacheka.
"Umechelewa sana, kama unataka kufa endeelea kusema hivyo," yule mzee aliniambia kwa sauti ya kukazia, nikaogopa mwenyewe.

Yule mwanamke akasimama sawasawa kisha akainama kidogo aliponyanyua shingo, akasema:
"Padri mimi nimekuja na ujumbe wako, naamini utaupokea na utaufanyia kazi haraka sana, naomba uupokee."
"Ujumbe gani na umetoka kwa nani?" Nilimuuliza nikimwangalia kuuona huo ujumbe wenyewe, kama ni barua au maneno tu.
ENDELEA MWENYEWE…

"Ni maneno tu Padri," alisema huku yule mzee akimkazia macho.
"Una maanisha nini?"
"Kwani hujui?"
"Ningejua nisingekuuliza."
"Ulikujaje kanisani vile?"
"Hilo ndilo tunalolizungumza hapa."
"Hapa hatuzungumzi, ni kuachana na huyu, sisi tukutane usiku kwa ajili ya kupanga mikakati mizito mizito ya kuua wale wote walijidai ni vinara kwa kusimama na kusema sema ovyo," alisema yule mzee.
Tulikubaliana kuwa hivyo, wote tukatoweka, kwa ahadi ya kukutana usiku ili kupanga hiyo mikakati mizito ya kuua.

***
Ilikuwa ni usiku wa saa sita, nikiwa nimemaliza kusali kwa Mungu wangu, sasa nausaka usingizi mwingine wa awamu ya pili.
Nilipokuwa naanza kusinziasinzia tu, nikasikia kishindo tii!
Nikashtuka na kuangalia mle chumbani, nikaona miguu ya watu karibia kumi, lakini niliona kuanzia miguuni hadi kwenye magoti, lakini kwa upande wa nyuma.

Hii miguu ilikuwa minene, na ilitembea kwa mwendo wa pole kutoka pale iliposimama kuelekea ukutani.
Halafu ghafla nikawa naona ile miguu inaongezeka katika kuonekana kwake, yaani inaonekana zaidi ya magotini na kuelekea juu hadi kwenye mapaja.
Nikasikia sauti nzito:

"Sisi ni wenzako, tumekuja, amka."
Niliamka polepole kitandani mpaka nikakaa, nikaangalia kulia na kushoto, wote wakajionesha moja kwa moja. Wengine niliwafahamu, wengine sikuwafahamu.
"Simama," yule mzee wangu alisema akiniangalia na tena akawa ananyoosha mkono kuelekea kwangu kama vile alikuwa akitaka na mimi nimpe mkono wangu ili anishike.
Nilinyoosha mkono, nikamshika, naye akanishika, nikasimama lakini mwili ukiwa mzito sana.

Nilipoweza kusimama vizuri mwenyewe, mwanamke mmoja akanirushia nguo nyeusi, ikanivaa mwilini, watu wakapiga makofi chumbani kwangu, nikashangaa sana kwani sikuona ni jambo la kawaida watu wengi kuwemo ndani ya chumba changu na kupiga makofi na kelele za vifijo kwa wingi.
Yule mzee akasema wote tushikane, yaani kila mmoja aliposimama amshike mwenzake mkono, wote tukafanya hivyo, tukashikana mikono.

Kufumba na kufumbua tukawa kwenye mti mmoja mkubwa sana, chini palikuwa na moto mkubwa uliokuwa unawaka kwa kasi huku waliouzunguka moto ule wakiwa wanacheza ngoma ya kienyeji.
Kufika kwetu kukasababisha wasitishe ngoma na kuungana na sisi, wote tukasimama mstari mmoja.
Tukiwa mstarini, mzee mmoja akasimama mbele na kusema kuwa, mkutano ule ulikuwa ni maalum kwa ajili ya kunisimika mimi kuwa kiongozi wa kundi mojawapo la wachawi akidai naweza.
Nilinyoosha mkono ili kupinga, lakini wachawi wote walikataa wakisema aliyoyaongea bosi wao ni ya kweli kabisa.
Basi, nilipitishwa mbele huku nikiwa sijui itakuwaje na wachawi wengine walinisindikiza huku wakipiga makofi kwa furaha ya mimi kusimikwa.

"Haya, piga magoti hapa," yule mzee aliniamuru.
Nilipiga magoti kwa unyenyekevu wa hali ya juu huku nikishikanisha mikono kama ninavyokuwaga mbele za Mungu wangu.
Yule mzee alinishika kichwa, pale pale mwili wote ukabadilika, nikajiona shujaa, jasiri, sina woga na wala siogopi kitu cha kufikiria au kuonekana.
Kisha akaanza kusema maneno ya kilugha na sijui alikuwa akitumia lugha gani.

Alitumia muda wa kama dakika tano kusema kilugha alipokuja kubadilisha, akasema Kiswahili na pale pale nikahisi nipo usingizini, nikaota ndoto.
Nilikuwa nikipita kwenye kundi la watu nikiwa uchi wa mnyama, lakini watu walikuwa hawanioni kama napita na nikaelekea kwenye ukingo wa barabara huku nikiwa nawashika vichwa watu niliokuwa nawapita.

Hakuna aliyejua hata kwa dalili kama kuna mchawi anapita katikati yao, hivyo nikajiona ni jasiri na mjanja kuliko wajanja wengine wote wa dunia hii ya mambo na vituko.
Niliposhtuka kutoka katika ndoto hii, nilijiona nipo bado chini na wachawi wenzangu wakiniangalia kwa macho ya ushindi.
Nilisimama haraka, nikasema:
"Si muda wa kupoteza huu, wako wanaojifanya wanajua, lazima wakatoke uhai."
"Ndiyo," wachawi wakaitikia.

"Na sasa kila wote mjipange vikundi vitano, vya watu wanne wanne na kwenda kukabiliana na uovu huu, mume makini sana," nilisema.
"Sawa, tutakuwa makini," walisema kwa pamoja.
Nilipomaliza kusema, niliwachagua wachawi watatu na mimi wa nne, wengine wakachaguana hivyo hivyo, safari ya kwenda kuvamia nyumba za wale watu waliojifanya wana maswali mengi kanisani ilianza pale pale huku mimi nikiwa jasiri kabisa, siogopi mtu wala sihofii maisha yangu ya baadaye.
"Mtakuwa mnanifuata mimi ninavyofanya, sawa jamani?" Niliwaambia watu wangu huku tukisonga mbele.
"Sawa mkuu."

Je, nini kitatokea? Usikose baadae....
 
[h=1]PADRI MLA NYAMA ZA WATU -12...[/h]Hakuna aliyenyoosha mkono, hii ilinifanya niamini kuwa, hakuna mchawi aliyekuwa na uwezo wa kupambana na wajumbe wale.
"Mimi mwenyewe nitasimamia mapambano," nilisema kwa hasira sasa.
Tukiwa bado pale pembeni ya barabara, mara lilitokea basi jingine, wachawi wakafurahia na kutaka kwenda kusimama barabarani, lakini niliwakatalia na kuwaambia nitawafafanulia sababu.

Lilipopita, ndipo nikawaambia kuwa, hakuna basi linalopita muda ule hata siku moja, kama ni kuchelewa, basi ingekuwa basi moja na si zaidi ya hapo.
Wakati nasema, lile basi kwa mbele lilionekana kukata kona kuingia porini, likapotelea huko huku nyasi sikionekana kulala kuashiria kuwa, zilikuwa zikikanyagwa.
Mara likatokea basi jingine, safari hii hili lilikuwa likipiga honi mfululizo huku kukisikika kelele kubwa kutoka kwa abiria walioko ndani ya basi.

Niliwaamuru wachawi nusu wavuke barabara haraka, wengine wabaki na mimi. Kwa maana kwamba, basi litapita katikati yetu.
Ikawa hivyo, lilikuja na kupita katikati, lakini kabla halijatumaliza, lililipuka!
SASA ENDELEA…

"Puuu!"
Wengi walishtuka sana kwa mshtuko, lakini akili zilipokaa sawa wote wakashangilia…
"Haya turudini kule," niliwaamuru huku nikijua tutakuta kitu gani.
Sisi ni wachawi, kutembea kwetu si kwa kibinadamu, ni suala la kufumba na kufumbua tu tayari tulirudi kwenye kilinge chetu.
Tulimkuta mchawi mmoja, kwani mmoja alitufuata sisi kule kutupa taarifa.

Tulimkuta peke yake bila wajumbe wale waliofuata nyama, tulipomuuliza wako wapi, akageuka kuangalia pembeni.
Watu wawili walikuwa wamelala kwa kujikunja kama vile walikuwa wanasikia baridi sana.
"Vipi tena?" Nilimuuliza yule mchawi mwenzetu.
"Sijui, mimi nimeona ghafla wanaanguka hapa, niliposhtuka wakapaa na kutua pale. Lakini sijui chochote kile."
"Waliondoka muda gani?"
"Muda uleule mlipoondoka nyinyi kwenda kuongeza damu, halafu alipoondoka mwenzangu muda kidogo ndo wakatua."
Tulikwenda kuwaangalia, kila mmoja mwili uliungua moto, hakuna hata mmoja aliyekuwa na nafuu.

Walikuwa wakilia huku wakitetemeka kama vile walikuwa wakisikia baridi kali wakati wa majira ya mvua.
Nilinyoosha mkono na kuwashika wote kwa mpigo:
"Mmetumwa kumbe?" Niliwauliza kwa sauti ya ujasiri.
"Ndiyo."
"Kufanyaje?"
"Kuchukua deni la damu."
"Sasa kwanini mliingia mambo mengine?"
"Tuliambiwa tuwapime ili kujua uwezo wenu."
"Mlitumwa na nani?"
"Mkubwa wetu."

"Kwani sisi tuna uadui na nyinyi?"
"Hata sisi wenyewe tulikuwa tunashangaa sana wakati tunapewa maagizo haya."
"Simameni," niliwaamuru, wakasimama wote.
Kusema ule ukweli walikuwa wameungua sana, licha ya kusimama lakini kwa hali ya kawaida, hakuna hata mmoja aliyetakiwa kusimama, na kama ingekuwa ni binadamu nje ya uchawi, wangekuwa wameshapoteza uhai wao.
"Tembeeni."

Walitembea, kila mmoja hatua kama mbili, wakaanguka.
Tulijua nini kinakwenda kuwapata, hivyo tuliwaruhusu kichawi kurudi walikotumwa huku sisi tukiandaa namna ya kukabiliana na makombora ya wenzetu kwani tulijua kitendo tulichowafanyia ni kama tulichokoza nyuki.
Katika vita kama ile, huwa inategemea na uwezo na uzoefu wa kila mchawi, welevu wale ni muda wa kukaa katika kazi ya uchawi.
Mimi nilijiamini sana si kwa muda mrefu wa kukaa katika kazi ya uchawi, bali kwa ushupavu na uhodari wa kufanya uchawi, ndiyo maana wengi walikuwa wakiniogopa kwa ajili hiyo. Ni muda mchache sana nimejiingiza katika uchawi lakini tayari nilikuwa kiongozi mkubwa tu na kuweza kupambana na maangamizi.

Tukiwa kwenye eneo letu husika, mimi nilisimama katikati, nikaamuru painuliwe ili nisimame juu kabisa niweze kuongea na kila mchawi.
Wachawi wawili walisogea, wakachota mchanga wa pale niliposimama wakaurusha juu, wakati ukirudi chini wakawa wanaupuliza na ndivyo pale niliposimama palivyokuwa panainuka juu na kusababisha kichuguu kirefu kidogo huku nikiwa nimesimama juu yake.

Nilipokuwa naanza kuwahutubia nilichotaka, upepo mkali sana ulivuma toka pande zote, yaani mashariki, magharibi, kusini na kaskazini.
Mshtuko zaidi ulitupata pale tulipobaini kwamba, upepo huo uliambatana na joto kali sana, mfanowe hakuna, tena linalounguza.
"Uwiii,"
"Jamani."
"Mamaweee."
"Ooo."

"He!
"Haaa!"
"Jamani tunakufa."
"Ohooo!"
Hiyo ilikuwa misemo ya baadhi ya wachawi walipokumbwa na ule upepo wenye joto kali sana.
Nilijua tuko katikati ya mapambano makali sana, hakuna kingine zaidi ya kuhakikisha ushindi bado unakuwa wa kwetu licha ya kuvamiwa.

Sauti za magari kama yale mabasi zilisikika, ikawa kama zinapita toka upande mmoja, kwenda pande nyingine huku sauti za abiria zikiwa zinasikika vyema kama vile kila mmoja alikuwa akiongea na abiria na mwenzake.

Nilinyoosha mkono juu ili kuuzuia ule upepo lakini hali ndiyo kwanza ikazidi kuwa mbaya.
Je, nini kitatokea? Usikose baadae......
 
[h=1]PADRI MLA NYAMA ZA WATU -13...[/h]Nilipokuwa naanza kuwahutubia nilichotaka, upepo mkali sana ulivuma toka pande zote, yaani mashariki, magharibi, kusini na kaskazini.
Mshtuko zaidi ulitupata pale tulipobaini kwamba, upepo huo uliambatana na joto kali sana, mfanowe hakuna, tena linalounguza.
"Uwiii,"
"Jamani."
"Mamaweee."
"Ooo."
"He!
"Haaa!"
"Jamani tunakufa."
"Ohooo!"
Hiyo ilikuwa misemo ya baadhi ya wachawi walipokumbwa na ule upepo wenye joto kali sana.
Nilijua tuko katikati ya mapambano makali sana, hakuna kingine zaidi ya kuhakikisha ushindi bado unakuwa wa kwetu licha ya kuvamiwa.
Sauti za magari kama yale mabasi zilisikika, ikawa kama zinapita toka upande mmoja, kwenda pande nyingine huku sauti za abiria zikiwa zinasikika vyema kama vile kila mmoja alikuwa akiongea na abiria na mwenzake.
Nilinyoosha mkono juu ili kuuzuia ule upepo lakini hali ndiyo kwanza ikazidi kuwa mbaya.
SASA ENDELEA…

"Ilifika mahali niliamini kuwa, mwelekeo wa upepo ule ni mbaya kiasi kwamba, lazima mmoja au zaidi yetu wafe ili kutuliza ghasia ile.


Ndipo nilipoamua kukemea kwa sauti kama vile wachungaji wanavyotoa mapepo, lakini pia haikusaidia.
Mchawi mmoja, mwanamke akaanguka chini kama aliyepigwa ngwara na mtu, damu zikamtoka kinywani huku akilia sana na kusema anakufa kwa sababu mbele yake anaona moto mkubwa.

Picha niliyoipata kichwani ni kwamba, mchezo ule hakuwa wa wale wachawi, bali mkono wa Mungu uliingilia kati kwa kutenda maajabu yake huku akionesha ukuu na uwezo.

Ni kweli, yule mwanamke aliyeanguka alinyoosha miguu, akakata roho, lakini tukiwa tunaendelea kufikiria hali ya mwenzetu na umauti wake, ghafla mwingine alianguka chini, huyu ni mwanaume.

Kishindo cha uangukaji ni kile kile kama cha yule wa awali. Sikuona sababu ya kuwaacha wengine eneo lile. Ilibidi niwaamuru kila mchawi akimbilie kwake na kuhusu wale tuwaache, mambo mengine yatajulikana kesho yake kama kutakucha salama.

Kweli, wachawi wote wakachangukana kila mmoja na njia yake. Mimi pia nilishika njia yangu mpaka kwenye makazi yangu ya kitumishi, nikaingia chumbani japo kwa njia ya kichawi, nikaoga ili kulala.
Usingizi haukuchelewa kunipata, lakini nikiwa usingizini niliota ndoto hii:

Eti nilikuwa ndani ya kanisa siku ya ibada ya Jumapili, kiongozi mkuu wa kanisa ambaye anaishi makao makuu alifika ghafla, bila taarifa ya awali kwamba angekuja.
Waumini wakasimama, wakamsalimia huku ibada ikiendelea kwani mimi sikutaka kuacha. Alinyoosha mkono kwangu na kusema:

"Naomba simamisha ibada mara moja."
Nilisimamisha, nikabaki nimeduwaa nikimkodolea macho ya mshangao.
Akaja hadi madhabahuni, akasimama sambamba na mimi akawageukia waumini.

"Nimekuwa nikisikia mengi sana kuhusu huyu padri. Na kila nilichosika nilikifanyia uchunguzi na kugundua ni kweli. Kwa hiyo sasa, kuanzia leo namsimamisha na kwamba, si mtumishi tena wa kanisa hili."
Nilishtuka kutoka usingizini na kukaa huku nikihema sana.
Usikose sehemu ya mwisho baadae.......
 
[h=1]PADRI MLA NYAMA ZA WATU -14....[/h]
Nilishtuka kutoka usingizini na kukaa huku nikihema sana.
SASA ENDELEA…
Siku ya ibada Jumapili ilifika nikiwa sina raha, sina amani wala sijisikii kuendesha ibada.

Lakini kwa vile nilikuwa sina mtu wa kusimama badala yangu, nilioga, nikavaa mavazi ya utumishi na kwenda ibadani.

Nakumbuka ilikuwa kwenye kipindi cha nyimbo wakati wa kutoa sadaka, nikiwa nimekaa kwenye kiti na huku kidogo nikiwa na amani kwani baada ya sadaka ibada huwa haichelewi kwisha, kwa hiyo ndoto yangu ingekuwa ni upuuzi mtupu na si tukio la kweli, nikasikia mlio wa gari likisimama nje.

Waumini wote waligeuka kuangalia mlango mkubwa kama vile kuna mtu walijua anakuja.
Na mimi macho yangu yakiwa mlangoni, ghafla aliingia mkuu wa kanisa letu akiwa ameongozana na watu wengine wawili.

Nilisimama, yeye akaja mbele, wale watu wawili wakakaa kwenye dawati kama waumini wengine.
Nilinyoosha mkono kumpa yule mkuu kama salama, akakataa.
"Sitaki mkono wako, naomba simamisha ibada mara moja."
Nilisimamisha, nikabaki nimeduwaa nikimkodolea macho ya mshangao.

Akaja hadi madhabahuni, akasimama sambamba na mimi akawageukia waumini.
"Nimekuwa nikisikia mengi sana kuhusu huyu padri. Na kila nilichosika nilikifanyia uchunguzi na kugundua ni kweli. Kwa hiyo sasa, kuanzia leo namsimamisha na kwamba, si mtumishi tena wa kanisa hili."

Nilijisikia miguu ikikosa nguvu, nikaanguka. Nilipokuja kuzinduka, nilikuwa hospitalini, pembeni yangu alikuwepo dada yangu kwa mama na baba mmoja, alinipa pole kwa yote.
"Dada," nilianza kusema.

Usikose sehemu ya mwisho baadae......
 
[h=1]PADRI MLA NYAMA ZA WATU -15...[/h]
Nilijisikia miguu ikikosa nguvu, nikaanguka. Nilipokuja kuzinduka, nilikuwa hospitalini, pembeni yangu alikuwepo dada yangu kwa mama na baba mmoja, alinipa pole kwa yote.
"Dada," nilianza kusema.
SASA ENDELEA…

"Nakusikia kaka."
"Yaliyotokea yote ni uwezo wa Mungu, ametaka kuniambia kuwa, yeye hachezewi wala hajaribiwi, ni kweli Mungu hataki mtu vuguvugu, kwa hiyo namkiri kwa mara ya tena kwamba yeye ndiye Muumba wa mbingu na nchini."
"Ni kweli kaka, lakini we unadhani kwanini umesimamishwa utumishi wa Mungu?"

"Dada, kumbe hufahamu? Da! Nilimtumikia shetani."
"Kwa njia gani kaka?"
"Njia ya kishetani."

"Ipi hiyo kaka?"
"Nilikuwa shetani mimi mwenyewe."
"Kaka mimi sijakuelewa."

"Nilikuwa mchawi dada."
"Ha! Kaka."
"Nimeamua kutubu dada ndiyo maana nimekwambia, naacha kuanzia sasa."

Dada alilia sana, na mimi nikajisikia vibaya, nilinyoosha miguu na mikono…"
Akataa roho!


''Mwisho.''
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom