Mikasa ya kusisimua jini mahaba linanitesa-6 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mikasa ya kusisimua jini mahaba linanitesa-6

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MziziMkavu, Oct 11, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Nilimwambia sikuwa na tatizo la kwenda kwao isipokuwa aniwezeshe kimaisha ili nami niwe na maisha mazuri, akaniambia jambo hilo liliwezekana nisiwe na wasiwasi.

  Maimuna aliniambia licha ya kuwa na uwezo wa kunifanya niwe tajiri mkubwa ninayeheshimika, hatofanya hivyo isipokuwa atahakikisha napata riziki yangu ya kila siku bila matatizo.

  Baada ya kuongea naye kwa muda aliniaga na kuahidi kuja kunichukua ili nikakufahamu nyumbani kwao kabla ya kufunga naye ndoa kisha akatoweka kwa kupitia kwenye pembe ya nyumba.

  Maimuna alipoondoka, nilijilaza kitandani na kutafakari hatima ya maisha yangu itakuwaje baada ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na jini huyo. Nilipomamka sikumsimulia mama habari za jini huyo ndipo nilijiandaa na kwenda shuleni, nikiwa shuleni sikuwa na raha badala yake nilitumia muda mwingi nikimtafakari jini Maimuna.

  Kama ilivyokawaida ya vijana kuwa na wapenzi, nami nilitokea kumpenda sana msichana mmoja tuliyekuwa tunasoma naye ambapo nilimtongoza na kumweleza nia yangu ya kumuoa mara tutakapohitimu masomo.

  Msichana huyo ambaye alikuwa akiishi na bibi yake alinipenda sana, lakini hatukuwahi kufanya mapenzi licha ya mara kwa mara kuwa karibu. Kutokana na ukaribu wetu, sikuona sababu za kumficha habari za jini aliyekuwa akinisumbua ndipo siku moja baada ya kutoka shuleni nilimweleza habari za Maimuna.

  Mpenzi wangu huyo alistaajabu sana ndipo alikwenda kumfahamisha bibi yake, baada ya kupita siku kadhaa bibi yake aliniita na kuniambia angenifanyia dawa ambayo ingemkimbiza jini huyo.

  Nilipoelezwa hivyo nilifurahi kwani nilihitaji sana kubaki huru, nikiwa kwa bibi huyo ambaye alikuwa akielewa tiba za asili alitengeneza hirizi kubwa nyeusi akanivalisha katika mkono wangu wa kushoto. Baada ya kunivalisha alinieleza nisiivue hata siku moja wala nisimuoneshe mtu yeyeto na kusisitiza kwenda kinyume na maagizo yake ningempa nafasi jini huyo kuendelea kunisumbua.

  Niliporudi nyumbani sikumfahamisha mama kama nilifungwa hirizi katika mkono wangu, usiku ulipoingia nilianza kuumwa kichwa pamoja na mwili wote.

  Ukiacha maumivu ya sehemu hizo, niliishiwa nguvu ndipo mama alinitafuta dawa za malaria nikameza. Licha ya kutumia dawa hizo hali yangu ilizidi kuwa mbaya.

  Kutokana na hali hiyo, nilikaa nyumbani siku tatu bila kuhudhuria shuleni na sikuthubutu kuvua shati kwa kuhofia mama angeiona hirizi niliyofungwa na bibi wa mpenzi wangu.

  Siku ya nne nikiwa nimezoofu mama aliingia chumbani kwangu na kuniona nikiwa nimefungwa hirizi, alipigwa butwaa na kuniuliza niliitoa wapi ndipo nilimweleza ukweli.

  Mama alikasirika sana na kusema ndiyo iliyokuwa ikisababisha maradhi yaliyonisumbua, aliikata na kwenda kuichoma moto.

  Muda mfupi baada ya kufunguliwa hirizi hiyo, nilipata nafuu ndipo mama alimfuata yule bibi na kumuuliza sababu za kunifunga hirizi bila idhini yake.

  Kwa kuwa mama alichukizwa sana na kitendo hicho, ulizuka ugomvi mkubwa katika yake na yule bibi ambapo alimuonya kutorudia tena mchezo huo.

  Tangu siku hiyo yule bibi na mama hawakuelewana, ambapo mama alinionya nisiendelee kuwa na uhusiano na mjukuu wake.

  Kwa kuwa nilikuwa nampenda sana nilikubali mdomoni lakini moyoni nilipanga kutomuacha msichana huyo, sikuwa tayari kumpoteza kirahisi.

  Usiku wa siku hiyo nikiwa nimelala, nilisikia sauti nzuri ya msichana akiimba wimbo wa kihindi Nikiwa najiuliza msichana huyo alikuwa nani ndipo nilishangaa kumuona Maimuna akiwa amesimama pembeni ya kitanda changu.

  Jini huyo aliyekuwa amependeza sana na kunukia manukato mazuri alinisababi kwa kusema; "Asalam alaykhm?" Nikaitikia; "Alaykhum salamu!"

  Itaendelea wiki ijayo,usikose.
  Baada ya salamu alinipa pole kwa kuumwa kisha alinieleza kila kitu kuhusu yule bibi aliyenifunga hirizi na kuniambia kwa kuwa lengo lake lilikuwa ni kumfukuza yeye angemtambua.

  Maimuna alinionya niache kujihusisha na yule msichana wangu, kwa kuwa nilikuwa nampenda sana binti huyo nilimwambia ingekuwa vigumu kumuacha.

  Jini huyo aliniuliza ugumu ulikuwa wapi,nikamwambia wenzangu wote walikuwa na wapenzi wao sasa ningeishije bila kuwa na mpenzi ndipo alinieleza alikuwepo yeye.

  Nilimwambia yeye hakuwa binadamu wa kawaida hivyo ingekuwa vigumu kuwa naye wakati wote tofauti na mpenzi wangu ambaye tuliishi jirani.

  Maimuna alisisitiza niachane na msichana huyo lakini niligoma ndipo alinieleza nitaona, nilipomuuliza alimaanisha nini alisema nisubiri kushuhudia ambacho angemfanya.
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Jini Mahaba linanitesa -7
  Mikasa ya kusisimus

  Jini huyo aliniuliza ugumu ulikuwa wapi,nikamwambia wenzangu wote walikuwa na wapenzi wao sasa ningeishije bila kuwa na mpenzi ndipo alinieleza yeye alikuwepo.

  Nilimwambia yeye hakuwa binadamu wa kawaida hivyo ingekuwa vigumu kuwa naye wakati wote tofauti na mpenzi wangu ambaye tuliishi jirani.

  Maimuna alisisitiza niachane na msichana huyo lakini niligoma ndipo alinieleza nitaona, nilipomuuliza alimaanisha nini alisema nisubiri kushuhudia ambacho angemfanya.

  Kama ilivyokuwa kawaida ya Maimuna kila aliponitembelea kupenda kufanya mapenzi, baada ya kunieleza mambo ya yule bibi alivua nguo zake na kujilaza kitandani na kuanza 'kunichokoza.

  Jini huyo ambaye ni mtundu katika masuala ya mahaba, alianza kunishika hapa na pale mpaka nikajikuta mapigo ya moyo wangu yanakwenda mbio na damu kunichemka.

  Kufuatia hali hiyo, 'nilimvamia' na kuanza kuyachezea vizuri matiti yake madogo mithili ya embe 'ng'ong'o' na sehemu zingine za mwili wake na kumfanya jini huyo kutoa miguno ya raha.

  Baada ya kila mmoja wetu kupagawa, tulizama katika dimbwi la mahaba mazito ambapo kazi ilikuwa ni bandika bandua mpaka majogoo.
  Kutokana na uwezo wangu wa kufanya mapenzi bila kuchoka, Maimuna alinishukuru sana na kuahidi kuendelea kunipenda siku zote ndipo aliniaga akaondoka kwa kupitia ukutani.

  Alhamisi iliyofuata usiku nikiwa nimelala chumbani kwangu, nilisikia msichana akiimba wimbo wa kihindi ndipo niligundua alikuwa Maimuna.

  Nilifahamu hivyo kwa sababu kila alipokuwa akija kunitembelea alipenda kuimba wimbo wa maadhi ya kihindi, sekunde chache baadaye jini huyo alikuwa amekaa pembeni ya kitanda changu huku akinukia manukato mazuri.

  Alinisabahi na baada ya salamu alinibusu nami nikajibu mapigo, kwa kuwa nilihitaji sana kuezeshwa kimaisha na jini huyo, nilimuomba anipe utajiri na ruhusa ya kuoa.

  Maimuna alitabasamu na kunifahamisha kuwa ingawa alikuwa na uwezo wa kunipa utajiri hatothubutu kufanya hivyo, kwa sababu nitakapokuwa tajiri ningemsahau Mungu.

  Alinifahamisha kwamba yeye na ndugu zake wanatoka katika ukoo wa Sharif hivyo kitendo cha kumpa utajiri kilikuwa ni kwenda kinyume na maagizo ya Mwenyezi Mungu.

  Kuhusu kuoa, jini huyo aliniambia kwa kuwa nilikuwa nimebalehe aliniruhusu kufanya hivyo lakini mwanamke nitakayemuoa awe anayempenda yeye na si msichana wangu.

  Nilipomuuliza mwanamke anayempenda yeye yukoje, akasema; Mwenye subira, mcha Mungu na mwenye huruma.
  Baada ya kunieleza hivyo nilimwambia hata mimi na wazazi wangu tunaweza kumtafuta msichana wa aina hiyo lakini Maimuna alikataa na kusema angemtafuta yeye.

  Kwa kuwa bado nilikuwa nasoma nilimuuliza mwanamke huyo angemleta lini, jini huyo alinifahamisha kwamba mara nitakapokuwa mkubwa.

  Nilimwambia kwa kuwa nilikuwa nimebalee nilihitaji kuwa na mpenzi wa kutoka naye wakati wa sikukuu kama ilivyokuwa kwa wenzangu, lakini jini huyo alikataa na kunieleza hakupenda zinaa.

  Baada ya kunieleza hivyo, Maimuna alinifahamisha kwamba Alhamisi angefika kunichukuwa ili twende kukatembee na tukiwa huko tungeongea mambo mengi.

  Kulipokucha sikumwambia mama habari za jini huyo ambapo nilijiandaa nikaenda shuleni, nikiwa darasani nilitumia muda mwingi kumuwaza Maimuna.

  Niliendelea na masomo mpaka siku ya Alhamisi usiku ndipo jini huyo alifika, baada ya salamu aliniambia alifika kunichukuwa twende tukatembee kama alivyoniahidi.

  Sikuweza kumpinga zaidi ya kumweleza nilikuwa tayari kuondoka naye, baada ya kumwambia hivyo jini huyo aliambia nifumbe macho.

  Nilipofumba nilipoteza fahamu, nilipozinduka nilijikuta tukiwa tumeketi sehemu yenye mapango ambayo ilikuwa na rangi nzuri za kuvutia na upepo ukivuma. Tukiwa hapo, jini huyo alinieleza alikuwa akinipenda sana na lazima tungefunga ndoa.

  Alinifahamisha kuwa nyumbani kwao kulikuwa chini ya bahari na pale ilikuwa sehemu yake ya kupumzika, aliongeza kuwa duniani walikuwa wakifika kwa shughuli maalum.

  Nilipomuomba anieleze ni shughuli gani iliwaleta dunaini, jini huyo alikataa kunieleza.
  Fuatilia wiki ijayo ujue undani wa maisha ya Nassor na jini Maimuna.

  badala yake alinifahamisha kwamba katika familia yao walizawali yeye na kaka yake ambaye alinieleza ningemfahamu baadaye.
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Jini Mahaba linanitesa -8
  Mikasa ya kusisimus

  Nassor alipomuomba amweleze shughuli hiyo, jini huyo alikataa. Nini kilifuata wakiwa huko? Ungana nami ujue undani wa mkasa huu wa kuhuzunisha…

  Licha ya kumbembeleza sana anieleze shughuli iliyowaleta, Maimuna alikataa na badala yake alinifahamisha kuwa katika familia yao walizawali wawili yeye na kaka yake ambaye alisema ningemfahamu baadaye.

  Nilipomuuliza walivutiwa na kitu gani kutoka kwa binadamu, jini huyo alijibu kwamba walikuwa wakitupenda tu na wanajisikia raha kuwa na uhusiano na binadamu.

  Tukiwa eneo hilo ambalo nashindwa namna ya kuelezea uzuri wake, Maimuna alinifahamisha kwamba siku nyingine angenipeleka kunitambulisha kwa wazazi wake kisha kufunga naye ndoa.
  Baada ya kunieleza hivyo aliniomba nifumbe macho ambapo nilifikiri alitaka kunishitukiza (Surprise) jambo fulani ndipo nilifumba macho.

  Nilipofumba, ghafla nilipoteza fahamu na nilipozinduka nilijikuta nikiwa nimelala kitandani kwangu na jini huyo.Jambo hilo lilinishangaza lakini sikumuuliza chochote.

  Kwa kuwa kulikuwa kumepambazuka, jini huyo aliahidi angefika kunitembelea tena siku ya Alhamisi ndipo aliniaga na kutoweka kwa kupitia dirishani.

  Ingawa jini huyo alinikataza nisimweleze mtu yeyote habari zake, kulipokucha niliamua kumfahamisha mama kila kitu na kuwa tayari kwa lolote ambalo lingetokea.

  Mama ambaye alikuwa mzoefu wa masuala ya majini kwa sababu naye alikuwa na jini wake aliyekuwa akimsumbua, aliniambia nisihofu ndipo alimfahamisha babu yangu mmoja ambaye hivi sasa ni marehemu.

  Babu huyo alinieleza nisihangaike kwenda kwa waganga kwa sababu jini anayenisumbua ni wa ukoo wetu hivyo nisigefanikiwa kumkimbiza isipokuwa alinishauri niwe naswali swala tano, kutoa sadaka na kutenda mambo mema.
  Kufuatia masharti niliyopewa na babu nami kuwa kijana niliyetoka kubalehe, nilimwambia nisingeweza kuyatekeleza kwani nilihitaji kuwa na rafiki wa kike.

  Baada ya kutoa kauli hiyo, mama alimfahamisha babu kuhusu jini huyo kunizuia kuwa na mpenzi ambapo alishangaa na kusisitiza kwamba nikitaka kumtuliza jini huyo ni mimi kuswali swala tano,kutoa sadaka na kutenda mema.
  Licha ya ushauri huo, sikuwa tayari kufanya hivyo badala yake nilipanga kuendelea na msichana wangu ambaye tulipendana sana.
  Kwa kuwa nilikuwa nampenda sana msichana wangu, niliendelea kuwa na uhusiano naye ambapo tulipotoka shuleni tuliongozana kwenda kwa bibi yake na sehemu nyingine.

  Siku moja Alhamisi usiku, jini Maimuna alifika akiwa amechukia sana kwani bila ya kunisalimu aliniuliza kwanini niliendelea kuwa na msichana wangu ambaye alinikataza.

  Nilimwambia ilikuwa vigumu sana kumuacha ndipo jinni huyo alinieleza ningeona yeye na msichana huyo nani alikuwa zaidi ya mwenzake kisha akatoweka kwa kupitia dirishani.
  Siku iliyofuata nilikwenda shuleni kama kawaida lakini jambo la kushangaza sikumuona mpenzi wangu, kitendo hicho kilinipa hofu kwani haikuwa kawaida yake.

  Tulipotoka shuleni nilikwenda nyumbani kwa bibi yake ambapo nilimkuta akiwa hoi kitandani, nilipomuuliza alisumbuliwa na nini alinifahamisha kwamba aliumwa mwili wote.
  Kufuatia maradhi yaliyokuwa yakimsumbua ambayo nilijua yalisababishwa na jini Maimuna, msichana huyo alikaa nyumbani muda mrefu bila kuhudhuria shuleni.

  Kwa kuwa bibi yake alikuwa mtaalam wa dawa za asili, siku moja nilipofika kumjulia hali mwenzangu alinieleza kwamba jini wangu ndiye alimdhuru mjukuu wake na kama asingepona nilikuwa nimetangaza vita.

  Kufuatia hofu niliyokuwa nayo nilikwenda kumfahamisha mama juu ya suala hilo,mama alinieleza kwamba nikitaka msichana huyo apone usiku niwe nachoma udi na kufukiza moshi wake huku nikisema maneno yafuatayo;
  "Nakuomba radhi jini wangu naomba umponye msichana wangu awe na afya njema".

  Siku iliyofuata nilikwenda kumuona msichana huyo na kumkuta bado ana hali mbaya,bibi yake alizidi kusisitiza kwamba asipopona tungemtambua na kuongeza kuwa alitangaza vita dhidi ya familia yetu na jini Maimuna.

  Usiku wa siku hiyo, yule bibi alifanya ndumba za kumuangamiza jini Maimuna bila kufahamu jini huyo alikuwa na uwezo mkubwa kuliko yeye.

  Usiku nikiwa nimelala, alifika jini huyo akanisabahi na baada ya salamu alinifahamisha kwamba alikerwa sana na kitendo alichofanyiwa na yule bibi.
  Alifanywa nini?
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Jini Mahaba linanitesa -9
  Mikasa ya kusisimus

  Kwa kuwa nilikuwa nampenda sana msichana wangu, nilipotoka shuleni nilikwenda kumuona ambapo nilimkuta akiwa amepata nafuu.

  Nilifurahi sana kumuona akiwa katika hali hiyo ambapo tuliongea kisha nilirejea nyumbani, nilipompa mama habari ya kupona kwa mwenzangu, naye alifurahi.

  Siku hiyo jioni nilikwenda kucheza na wenzangu na kurejea nyumbani usiku, mama ambaye hakufurahishwa na kitendo hicho alinikanya na kunisihi niwe narejea nyumbani mapema.

  Niliendelea na masomo hadi siku ya Alhamisi usiku nikiwa nimelala, nilimsikia jini Maimuna akija huku akiimba wimbo wa Kihindi.
  Nikiwa naangaza huku na huko kuona angepitia wapi kati ya ukutani na dirishani, nilishangaa kumuona akiwa amekaa kitandani kwangu.

  Jini huyo alinisabahi kwa kusema; "Asalam alaykhum?" Nikaitikia alaykhum salam!.
  Baada ya salamu aliniambia kwamba siku iliyofuata niende nikamuamgalie yule bibi wa mpenzi wangu ndipo nitaamini hakupaswa kuchezewa hata kidogo.

  Nilipomuuliza alimfanya nini alikataa kunieleza na kusisitiza kukicha niende nikamuone, nilimuahidi nikiamka salama ningeenda.

  Kama kawaida jini huyo aliponitembelea hakupenda kuondoka bila kupata joto langu,alianza kunifanya visa vya hapa na pale ndipo alinipandisha mzuka nami nikajibu mapigo.

  Kwa kuwa nilielewa maeneo ambayo nilipomshika alipagwa, niliyagusa na kumfanya awe hoi. Baada ya kuhakikisha 'ameiva' sikumchelewesha, nilimpa dozi ya uhakika iliyomfanya afurahi na roho yake.

  Kufuatia kumkimbiza mchakamchaka,Maimuna alinishukuru na kusema hatoniacha na kwamba angepambana na mwanamke yeyote ambaye angeingilia penzi letu.

  Jini huyo alinisifu kwamba 'kazi' niliiweza na ndicho kilichomfanya anipende na kuamua nifunge naye ndoa. Ingawa nilijifahamu uwezo wangu wa kufanya mapenzi upo juu, nilikataa sifa alizonipa.

  Maimuna aliniambia ingawa aliwahi kufanya mapenzi na majini wenzake, hakuna aliyeweza kukata kiu yake kama mimi kwani nilimpa vitu hadimu kupatikana ujinini.

  Nilimshukuru kwa sifa alizonimwagia ndipo tuliendelea kuongea hadi alfajiri ambapo jini huyo aliniaga na kusisitiza nisiache kwenda kumuona bibi yangu kisha alitoweka kwa kupitia ukutani.

  Kutokana na uchovu niliokuwanao kufuatia kibarua kizito nilichokuwa nacho usiku kucha, nilipojilaza nilipitiwa na usingizi hadi saa tatu asubuhi ndipo nilishituka baada ya mama kunigongea mlango.

  Nilipoamka aliniuliza kwanini sikwenda shuleni nilimdanganya nilikuwa najisikia vibaya, kwa kuwa alielewa matatizo yangu hakuendelea kunibughudhi.

  Baada ya kupata kifungua kinywa nilikwenda kwa bibi wa mpenzi wangu, nilipofika nilishangaa kumkuta akiwa nyumbani.
  Nilipomuuliza kwanini hakwenda shuleni, alinifahamisha kwamba bibi yake alipokwenda msalani usiku wa kuamkia siku hiyo, alianguka na kupooza upande mmoja.

  Kwa kuwa nilielewa kilichokuwa kikiendelea, nilimpa pole nikarudi nyumbani na kumfahamisha mama mkasa uliompata bibi huyo.

  Mama alimshangaa sana bibi huyo kuamua kupambana na jini ambaye alikuwa na uwezo mkubwa sana, hata hivyo alimuonea huruma na kuahidi kwenda kumjulia hali.

  Jambo la kuhuzunisha kabla mama ajaenda kumuona, ilipofika siku ya Jumapili jioni bibi huyo alifariki dunia na kuacha watu wakiulizana aliugua ugonjwa gani uliomuondoa ghafla.

  Ingawa watu wengi walistaajabishwa na kifo cha ghafla cha bibi huyo, mimi na mama tulielewa kilichotokea.
  Hata hivyo, ndugu na watoto wa bibi huyo ambao hawakuridhishwa na mazingira ya kifo cha mama yao, walikwenda kuwaona wataalam ambao waliwaeleza kwamba bibi huyo aliuawa na jini wangu hivyo kutangaza vita na familia yetu.
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Jini Mahaba linanitesa -10
  Mikasa ya kusisimus

  Alhamisi iliyofuata usiku, nilimsikia Maimuna akiimba wimbo wa kihindi ambapo aliingia chumbani kwangu na kuanza kucheka.
  Kutokana na hali, niliomba anieleze jambo lililomfurahisha lakini badala ya kunijibu aliniambia; "Nafikiri sasa umenifahamu mimi ni nani?"

  Nikiwa natafakari kauli hiyo, jini huyo alinifahamisha kwamba nami nikimletea ujeuri angeniua kama alivyomuua yule bibi.

  Baada ya kunieleza hivyo, tulifanya mapenzi kisha tulilala hadi alfajiri ambapo nilishituka kutoka usingizini kufuatia jini huyo kunichokoza kwa kunishika maungoni mwangu.

  Kwa kuwa nilielewa alichokihitaji, nami nilijibu mashambulizi na nilipomuona amepagawa nilimuweka sawa na kilichoondelea hapo nashindwa kukielezea.

  Ingawa tulitumia saa moja kupeana raha ya dunia, kila mmoja wetu alifurahi na roho yake ndipo mpenzi wangu huyo aliniaga na kutoweka kwa kupitia dirishani.
  Baada ya jini huyo kutoweka, nilianza kutafakari mustakabali wa maisha yangu kwani nilielewa nikimkosea Maimuna adhabu yangu ingekuwa kifo.

  Kufuatia kitendo cha bibi kuuawa, uhusiano na mpenzi wangu ulikwisha kabisa ambapo niliendelea na masomo hadi nilipohitimu.
  Siku moja ya Alhamisi usiku, Maimuna alifika kunitembelea, baada ya salamu alinifahamisha kwamba nijiandae na safari ya kwenda kunitambulisha kwa wazazi wake.

  Alinifahamisha atafika kunichukua siku ya Alhamisi, baada ya kunieleza hivyo tulifanya mapenzi kisha aliniaga, akaondoka.
  Siku moja kabla jini huyo hajaja kunichukuwa, nilimuaga mama na ndugu zangu kwamba kesho yake ningeenda kumtembelea mjomba wangu aliyekuwa akiishi kijiji cha Kapalamsenga kilichopo Kigoma vijijini.

  Mama hakuwa na kipingamizi ambapo alinitakia safari njema bila kujua safari yangu ilikuwa ya kwenda ujinini nyumbani kwa wazazi wa Maimuna.

  Kama ambavyo aliniahidi, siku ya Alhamisi usiku Maimuna alifika na baada ya salamu alinishika mkono wa kulia na kuniambia nifumbe macho.

  Nilipofumba nilipoteza fahamu na nilipozinduka nilijikuta nikiwa katika mji mzuri sana uliokuwa na majengo ya ghorofa, lami nzuri iliyoteleza,ambapo magari ya kifahari yalikuwa yakipita.
  Kwa ujumla kila kitu nilichokiona huko kilikuwa kizuri sana tofauti na vitu vilivyopo duniani, mji huo pia uliangazwa na taa nzuri za rangi muda wote.

  Mara baada ya kufika, Maimuna alinipeleka nyumbani kwa wazazi na ndugu zake ambao walifurahi sana kuniona.
  Baada ya utambulisho jini huyo alinipeleka chumbani kwake ambako kulikuwa na sofa, kitanda kikubwa cha futi sita kwa sita na vitu vingi vya thamani kama vilivyopo duniani.

  Tukiwa chumbani, Maimuna aliniuliza nilipendelea kula chakula gani nilimweleza ugari kwa samaki aliyekaangwa.Baada ya kumfahamisha hivyo alielekea jikoni ambapo hakuchukuwa muda mrefu aliniletea chakula hicho.
  Nilipomaliza kula tuliendelea na maongezi ndipo ndugu, jamaa na marafiki wa jini huyo kutoka sehemu mbalimbali walifika kunisalimu.

  Nilikaa huko ujinini kwa muda wa siku tatu ambapo ilipangwa siku ambayo tungefunga ndoa na Maimuna, lakini kabla sijarudi duniani baba ya jinni huyo mzee Sharif aliniita sebuleni kwake.

  Nikiwa nimeketi na mzee huyo, alinieleza alifurahi sana mimi kumpenda binti yake na kuahidi kutufanyia sherehe kubwa mara tutakapofungua ndoa.

  Hata hivyo, alinieleza kwamba alielewa sana matatizo ya binadamu hivyo kama nilimpenda binti yake nitulie kwani hakuhitaji ukorofi.

  Siku hiyo tuliongea mambo mengi na mzee huyo ndipo siku iliyofuata tukiwa chumbani kwa Maimuna alinieleza nifumbe macho.
  Baada ya kufanya hivyo, nilipoteza fahamu na nilipozinduka nilijikuta nikiwa karibu na maeneo ya nyumbani kwetu. Kwa kuwa nilielewa kilichotokea nilirudi nyumbani ambapo mama alinipokea kwa furaha.

  Aliponiuliza hali ya mjomba na ndugu zetu wengine, nilimdanganya kwamba niliwakuta salama na waliwasalimu. Mama alifurahi sana kupata taarifa hizo bila kuelewa nilikwenda ujinini.

  Tuliendelea na maisha mpaka nilipohitimu elimu ya msingi ndipo tulihama Kigoma na kwenda kuishi Tabora, tukiwa huko siku moja ya Alhamisi nikiwa nimelala jini Maimuna alifika na kuanza kuniita; "Nassor! Nassor!"

  Mambo ndio kwanza yanaanza. Yapo matukio mengi ya kusikitisha na kukupa mafunzo. Endelea kuwa nami mpaka mwisho wa mkasa huu, naamini utajifunza jambo fulani....
   
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Jini Mahaba linanitesa -11
  Mikasa ya kusisimus

  Kwa kuwa ulipita muda mrefu bila jini huyo kunitembelea nilijiuliza ni nani aliyekuwa akiniita lakini punde nilimuona Maimuna akiwa amesimama pembeni ya kitanda changu.

  Alinisalimu kwa kusema; "Asalam alaykhum?" Baada ya kuitikia salamu yake aliniuliza; "Za siku mpenzi wangu?" Nikamjibu zilikuwa nzuri.

  Jini huyo aliniomba msamaha kufuatia kitendo chake cha kutokuja kunitembelea kwa muda mrefu na kuongeza kuwa alishindwa kufanya hivyo kwa sababu ya ubize aliokuwa nao.

  Nilipomuuliza alijuaje kama tulihamia Tabora, Maimuna alinijibu kwamba hata kabla mama yangu hajafikiria suala la kuhama alikuwa anaelewa.

  Kama kawaida baada ya maongezi, jini huyo aliyependa sana kufanya mapenzi, alianza uchokozi wake ndipo nilijibu mashambulizi ambayo yalihitimishwa kwa 'kufinyana' mpaka alfajiri. Kabla hajaondoka alinishukuru kwa mapenzi shatashata niliyompa na kuniambia nijiandae kwa safari ya kwenda kwao ujijini.

  Aliongeza kuwa safari hiyo ilikuwa mahusus kwa ajili ya kufunga naye ndoa ambayo ilisubiriwa kwa hamu na wazazi, ndugu, marafiki na jamaa zao. Kabla Maimuna hajaondoka alinionya nisimweleze mtu yeyote suala hilo na kwamba iwe siri yangu, alisema kama ningekiuka maagizo yake angenipa adhabu kali.

  Kwa hofu ya kudhuriwa na jini huyo nilimweleza nisingefanya hivyo, jini huyo alifurahi sana ndipo alinikumbatia na kunibusu na kusema alikuwa akinipenda kwa dhati.

  Nilimshukuru kwa kunipenda ndipo aliniaga na kutoweka kupitia ukutani kama ilivyokuwa kawaida yake. Alipoondoka nilianza kutafakari juu ya safari ya kwenda kwao.

  Kufuatia kufanya mapenzi kwa muda mrefu na jini huyo, kulipokucha nilikuwa mchovu sana ambapo mama aliniuliza nilikuwa nasumbuliwa na kitu gani.Nilimfahamisha ulikuwa uchovu wa kawaida, mama ambaye alikuwa akielewa nilikuwa nikitembelewa na jini mahaba alitabasamu.

  Kufuatia tabasamu lake, nilielewa alifahamu usiku nilikuwa na kibarua kizito ndipo nilichukua maji na kwenda kuoga.

  Siku hiyo sikutoka kabisa nyumbani badala yake nilitumia muda mwingi nikiwa nimelala chumbani kwangu, mchana mama aliniaga akaenda kwa mjomba.

  Ilipofika saa tisa alasiri, nikiwa nimejilaza kitandani nilisikia sauti ya mwanamke akiimba wimbo wa kihindi, moja kwa moja nilielewa alikuwa ni mpenzi wangu Maimuna.

  Nilishangazwa sana na ujio wake kwani hakuwa na kawaida ya kunitembelea mchana, ukiacha muda huo pia siku aliyopenda kuja kwangu ilikuwa ni alhamisi.

  Nikiwa najiuliza ilikuaje aje siku ya Jumatatu na si alhamisi, ghafla nilimuona akiwa amesimama pembeni ya kitanda changu akitabasamu.

  Alinisalimu ambapo nilijibu salamu yake, baada ya salamu alinieleza aliamua kuja muda huo kwa kunishtukiza (Surprise) ili kunionesha ni jinsi gani alinipenda na alihitaji kuwa nami wakati wote.

  Nilimshukuru kwa upendo wake kwangu ndipo jinni huyo aliyekuwa kapendeza kwa mavazi na kunukia marashi mazuri alichojoa nguo zake na kulala kitandani.

  Ingawa nilikuwa nimechoka sana kufuatia zoezi la kikubwa tulilofanya usiku,nilipoyaona maungo yake nilijikuta napatwa hamu ya 'kulitafuna tunda'. Wakati nikiwa katika hali hiyo, Maimuna alijilaza kifuani kwangu na kuanza kuchezea ndevu zangu taratibu huku akihamia maeneo mengine.

  Jini huyo hakuishia hapo, alinipiga mabusu motomoto yaliyonifanya nipagawe ndipo nami sikumuangusha kwani nijibu mashambulizi yaliyomfanya alainike kama mlenda! Kutokana na joto alililopata jini huyo ambaye nashindwa namna ya kuulezea uzuri wake, alianza kulitaja jina langu na kunisifia kwa utundu niliomfanyia.

  Kwa kuwa wote tulikuwa katika hatua ya mwisho, tulijikuta tumezama katika kisiwa cha wapendao ambapo ilikuwa mshikemshike nguo kuchanika.

  Ingawa siku hiyo niliamka nikiwa mchovu, nilistaajabu nilivyoweza kuumudu mpambano wa mchana huo kwa kiwango kikubwa kwani nilipeperusha bendera ya ushindi mara saba. Maimuna ambaye furaha yake ilikuwa ni kufanya mapenzi, alifurahi sana na kuniambia ingawa alikutana na wanaume majini, lakini mimi ndiye nilimkuna mpaka kumoyo.

  Kufuatia sifa alizonimwagia, nilipanga kila tutakapokutana naye kumpa mambo makubwa ili anipe utajiri aliokataa kunipa.

  Niliamini hakuna njia nyingine ambayo ningeitumia kumlainisha jini huyo na kuamua kunitoa katika umaskini zaidi ya kumfurahisha tuwapo faragha. Jini huyo alifurahia penzi nililompa na kunifahamisha safari ya kwenda kwao ilikuwepo hivyo niendelee kujiandaa, kabla hajaondoka alisisitiza nisimwambie mtu yeyote mambo yetu.
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Jini Mahaba linanitesa
  Mikasa ya kusisimus

  Jumatano iliyofuata Maimuna alifika na kuniuliza kama nilikuwa naendelea kumsikiliza mama yangu, nilimfahamisha kuwa mama alikubali kumuoa ndipo jini huyo alifurahi sana.

  Kufuatia furaha aliyokuwa nayo, jini huyo alinifahamisha kuwa akifika kwao atawaeleza wazazi wake kwamba mama yangu aliniruhusu kumuoa.

  Baada ya kuongea kwa muda, jini huyo ambaye alikuwa akipenda sana kufanya mapenzi, alianza kunichokoza kwa kunishika taratibu maeneo yangu nyeti na sehemu zingine za mwili wangu mpaka damu ikaanza kunienda mbio.

  Kufuatia hali niliyokuwa nayo, sikuona sababu ya kumchelewesha nilijibu mashambulizi yaliyomfanya jini huyo apagawe ndipo tulizama katika dimbwi la mahaba.

  Tulipomaliza kufanya mapenzi, Maimuna alinifahamisha siku iliyofuata angefika kunichukuwa ili twende naye kwao kwa ajili ya kufunga ndoa.

  Kulipokucha nilimfahamisha mama kila kitu kuhusu Maimuna ndipo alinionya nisimweleze mtu yeyote juu ya safari yangu, saa nane usiku Maimuna alifika akiwa amependeza sana.

  Baada ya salamu aliniomba nifumbe macho, nilipofumba nilipoteza fahamu. Nilipozinduka nilijikuta nikiwa kwenye mji mzuri sana.

  Mji huo ulikuwa na maghorofa mazuri, bustani zenye maua yaliyotoa harufu nzuri, barabara za lami na vitu vingine vya kuvutia. Kwa ujumla uzuri wa mjini huo nashindwa namna ya kuelezea.

  Tukiwa katika mji huo, Maimuna alinifahamisha kwamba tusingeenda kwa wazazi wake ambao walikuwa wakiishi katika mji mwingine badala yake alitaka tustarehe kwanza ndipo twende kwao kwa ajili ya kufunga ndoa.

  Aliponieleza hivyo, nilimfahamisha nilikuwa nikimsikiliza yeye mwenyeji wangu. Kufuatia kumweleza hivyo, jini huyo alitabasamu na kunieleza atahakikisha ananifurahisha kwa kila kitu kwa kipindi chote nitakachokuwa kwao.

  Wakati tukiongea tulikuwa tumesimama nje ya jengo moja zuri sana tukiangalia magari ya kifahari yakipita kwenye barabara iliyokuwa mita chache kutoka eneo tulilokuwepo. Kwa kuwa mimi pekee sikuwa mwarabu, kila jini aliyeniona alikuja kunisabahi.

  Baadhi ya madereva, walisimamisha magari yao na kuja kunisabahi na kunikaribisha kwao. Kwa ujumla kila jini niliyekutana naye alionesha upendo kwangu.

  Kitendo hicho kilimfurahisha sana Maimuna ambaye aliwafahamisha majini wenzake kwamba mimi ndiye mume wake mtarajiwa na nilikwenda ujijini kwa lengo la kufunganaye ndoa.

  Baada ya kukaa eneo lile kwa muda, Maimuna alimpungia mkono dereva mmoja ambaye alikuwa akiendesha benzi lenye rangi nyeusi ndipo dereva huyo alikata kona na kuja kumsikiliza.

  Kaka huyo alitusalimu ndipo Maimuna alimuomba atupeleke kwenye hoteli moja iliyopo ufukweni mwa bahari, tulipopanda aliondoa gari ambapo tulitumia kama dakika arobaini na tano tukafika katika hoteli hiyo.

  Jambo la kushangaza nje ya hoteli hiyo sikuona mtu hata mmoja zaidi ya magari ya kifahari yaliyoegeshwa sehemu ya maegesho, mara baada ya kuteremka, Maimuna alifungua pochi yake akatoa makaratasi fulani akampa yule dereva.

  Dereva huyo alishukuru kisha akaondoka, Maimuna alinishika kiunoni tukaanza kuelekea kwenye lango kubwa la kuingia katika hoteli hiyo.

  Kilichonishangaza zaidi ni kwamba licha ya kuingia katika hoteli hiyo, sikumuona mtu yeyote na hata tulipofika mapokezi hapakuwa na mtu ndipo tulikaa katika kochi moja zuri.

  Tulikaa hapo kwa muda wa dakika kumi ndipo alitokea babu mmoja aliyekuwa na ndevu ndefu, kavaa kanzu na kibaghalashia, akatusalimu na baada ya salamu Maimuna alinifahamisha kuwa babu huyo alikuwa mhudumu pekee wa ile hoteli, nikashangaa.
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Jini Mahaba linanitesa -
  Mikasa ya kusisimus

  Yule mzee alituuliza tulitaka vyumba vya ghorofani au vilivyokuwa chini ya jengo hilo, Maimuna alimwambia kwa kuwa alikuwa na mimi ambaye sikuufahamu vizuri mji wao, atupatie chumba cha ghorofani.

  Baada ya kuelezwa hivyo, yule babu alisema tumsubiri kidogo ndipo alielekea katika ukuta uliokuwa upande wetu wa kushoto ambapo nilistaajabu kuuona ukifunga kama lifti za kupandia kwenye maghorofa marefu.

  Nikiwa naendelea kushangaa, Maimuna aliniambia nisishangae kwa sababu maisha ya majini na binadamu yalikuwa tofauti sana japo kuna baadhi ya mambo yalifanana.

  Alinieleza kuwa majini huwa hawapendi kupita milangoni badala yake hutumia sehemu za madirisha na ukutani, aliongeza kuwa ingawa katika hoteli ile kulikuwa na milango na lifti za kawaida ilikuwa mahusus kwa ajili ya wageni kutoka duniani.

  Kufuatia kunieleza hivyo, nilimuuliza kama ningeweza kukutanishwa na binadamu wenzangu ambao walikuwepo katika ili hoteli. Maimuna alicheka na kuniambia ilikuwa ni nadra sana wanadamu kufika ujinini.

  Aliongeza kuwa sio majini wote wana uwezo wa kuja duniani kuwachukuwa wanadamu kisha kwenda nao kwao, alisema waliokuwa na uwezo huo ni majini waliotokea katika koo maarufu zilizoko ujijini.

  Maimuna alipoona nazidi kumdadisi mambo ya kwao, aliniambia siku moja atanisimulia kila kitu kinachofanywa na majini. Kabla sijamuuliza swali lingine, nilishangaa kuona ukuta ukifunguka kama mlango ndipo yule babu alitoka.

  Kilichonishangaza zaidi, babu huyo hakuvaa kama alivyovaa awali, safari hii alivaa msuli wenye vyumbavyumba, kanzu fupi pamoja na kilemba kilichofanana na msuli.

  Yule babu alimkabidhi Maimuna funguo na kumwelekeza twende chumba namba kumi kilichopo juu kabisa ya ghorofa, ambapo jini huyo alinishika mkono na kunieleza tulielekea kupanda lifti ambayo sikuiona zaidi ya kuona ukuta tu.

  Tulipoukaribia ukuta huo ulifunguka kama mlango tukaingia, jambo la kushangaza lifti hiyo haikuwa tofauti na zilizopo duniani kwani kulikuwa na namba zilizoonyesha tulikuwa ghorofa ya ngapi na kulikuwa na balbu zilizotoa mwanga mzuri.
  Tofauti niliyoiona ni kwamba maandishi yaliyokuwemo yaliandikwa kwa lugha ya Kiarabu badala ya kiswahili, tukiwa ndani ya lifti hiyo Maimuna alibonyeza kitufe kilichoonesha namba thelathini na tano.

  Muda mfupi lifti ilisimama na mlango ulifunguka, tulipotoka nilistaajabu kuona tumepita kwenye ukuta.

  Maimuna ambaye alikuwa amefurahi sana, alinishika mkono na kuniongoza kwenye korido hadi tulipofika katika chumba namba kumi.

  Ingawa palikuwa na mlango, jini huyo aliongoza hadi kwenye ukuta uliokuwa upande wa kushoto.
   
 9. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Kama ilivyokuwa awali nilielewa tungeingia ndani kwa kupitia eneo hilo, kwa kuwa alinieleza milango ilikuwa mahusus kwa ajili ya kutumiwa na binadamu waliokwenda ujijini, nilimuuliza iweje anipitishe ukutani?
  Kufuatia swali hilo, jini Maimuna alitabasamu na kuniambia kutokana na mazoea ya kupita ukutani, alisahau kama alikuwa na mgeni kutoka duniani.

  Jini huyo alinikabidhi ule ufunguo na kuniambia nifungue mlango wa chumba namba kumi ambapo nilifanya hivyo, nilipomuomba tuingie alinifahamisha niingie kwanza mimi kisha yeye angefuata.

  Kama ambavyo jini huyo aliniagiza, niliingia katika chumba hicho na kuanza kushangaa vitu vya thamani vilivyokuwemo na jinsi kilivyokuwa kikimeremeta kwa rangi ya dhahabu.

  Nikiwa naendelea kushangaa, nilishituka baada ya kuona ukuta uliokuwa upande wangu wa kushoto ukiachia na Maimuna akiingia huku akitabasamu.

  Mara baada ya kuingia ule ukuta ulirudi katika hali yake ya kawaida ndipo alinifuata nilipokuwa nimesimama akanikumbatia na kunieleza ingawa aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na majini weenzake, mimi niliwapita kwa kila kitu.

  Baada ya kunieleza hivyo alinibusu kisha aliniongoza hadi kwenye sofa kubwa lililokuwa limetanda kutoka ukuta mmoja hadi mwingine, tukiwa hapo aliniuliza kama nilipapenda nikamwambia palikuwa pazuri sana.

  Jini huyo alinifahamisha kwamba kila kitu kilichonivutia kiliandaliwa na yule babu ambaye huko ujijini alifahamika sana na kuheshimiwa na kila mtu, aliongeza kuwa hata rais wao alikuwa akimheshimu babu huyo.

  Nilipomuuliza babu huyo alimudu vipi kutoa huduma katika hoteli ile peke yake, Maimuna alinieleza kuwa kutokana na uwezo waliopewa na mwenyezi mungu kwa majini ilikuwa kazi ndogo.

  Baada ya kuongea kwa muda, jini huyo aliniomba tutoke nje ili anionyeshe uzuri wa mji wao. Aliniambia nifungue mlango ningemkuta nje.

  Aliponieleza hivyo alijongea kwenye ukuta wa kushoto ambao uliachia akatoka nje, nami kwa kutumia ufunguo nilifungua mlango nikatoka nje na kumkuta Maimuna akinisuburi kwenye kochi lililokuwa kwenye korido
  Tukiwa hapo jini huyo aliniongoza tukapanda juu kabisa ya ghorofa hilo ambapo nilistaajabu kuona mji mzuri sana uliokuwa na maghorofa mazuri na marefu sana.

  Ukiacha majengo hayo, mji huo ambao nashindwa namna ya kuelezea uzuri wake, ulikuwa na miti mirefu na bustani za maua.

  Jini huyo alinionyesha baadhi ya majengo hayo kuwa zilikuwa ofisi, hospitali, shule, misikiti na majengo waliyoishi majini wa kawaida na matajiri wakubwa.

  Pia alinionyesha sehemu zilizokuwa wazi na kuniambia vilikuwa viwanja vya kuchezea mpira, mikutano, sherehe za harusi na mambo mengine.

  Nilistaajabu kuona mambo ya huko ujijini hayakutofautiana na duniani isipokuwa tofauti kubwa ni kwamba hakukuwa na mchana kwani muda wote mji wao ulikuwa ukimeremeta kwa taa nzuri za rangi.

  Kufuatia hali hiyo nilimuuliza Maimuna walikuwa wakilala muda gani, jini huyo alicheka na kuniambia walipojisikia kuchoka walikuwa wakipumzika kama binadamu au kwenda kustarehe kwenye kumbi za burudani.

  Nilipomuuliza wakiwa kwenye starehe wanakunywa bia au kilevi chochote, Maimuna aliniambia ni kosa kubwa sana kwa majini kutumia pombe.

  Alinieleza kwamba hawathubutu kufanya hivyo kwa sababu wanafuata sana maadili ya dini yao ya Kiislam.

  Nassor alikaa ujijini kwa muda gani? Maajabu gani mengine aliyoyaona?
   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Kwa kuwa mimi na Maimuna tulikaa juu ghorofani, ilikuwa sio rahisi majini waliofika kustarehe katika ile hoteli kutuona, lakini sisi tuliwaona vizuri sana!
  Tuliendelea kuongea na Maimuna mambo mbalimbali ya majini hadi saa moja usiku ndipo kijana mmoja aliyekuwa na mpenzi wake walipanda ghorafani kwa ajili ya kupunga upepo.

  Majini hao walipofika eneo tulilokaa walimtambua Maimuna na kumsabahi, baada ya salamu walinisalimu ndipo Maimuna aliwafahamisha kwamba mimi ndiye yule mpenzi wake wa duniani ambaye alikuwa akija kunitembelea mara kwa mara.

  Baada ya kuelezwa hivyo, wale majini ambao hawakuwahi kufika duniani walifurahi sana na kunikaribisha kwao, waliomba kabla sijaondoka niwatembelee kwao ili niwasimulie mambo ya duniani.

  Niliwaambia kama nikipata muda ningefanya hivyo, walifurahi sana ndipo walituaga wakateremka chini, haukupita muda mrefu majini wengi walipanda juu kunisalimia.

  Majini hao ambao walikuwa wakarimu sana, walimweleza Maimuna kabla sijarudi duniani ahakikishe ananipeleka nyumbani kwao ndipo jini huyo aliwafahamisha kama angepata muda angenipeleka.

  Kufuatia kitendo hicho nilielewa wale majini waliokuwa wa kwanza kuniona, walienda kuwafahamisha wenzao juu ya kuwepo kwangu pale hotelini ndiyo maana walikuja kunisalimia.

  Baada ya kuongea na majini hao, waliteremka chini na kutuacha na mpenzi wangu Maimuna na ilipofika saa nne usiku walikuja kuniaga na kumsisitiza Maimuna nisirudi duniani bila ya kwenda kuwatembelea kwao kisha wakaondoka.

  Kwakuwa nasi tulikuwa tumechoka, tuliingia chumbani kwetu, tukaoga kisha tulijilaza kitandani na kuanza kupeana mahaba mazito, siku hiyo nilimpeleka puta Maimuna mpaka akawa hoi.

  Kulipokucha alinifahamisha kwamba saa tatu asubuhi tungeenda nyumbani kwa wazazi wake kwa ajili ya kufanya maandalizi ya ndoa yetu, alinifahamisha kuwa wazazi wake walikuwa wakielewa nilifika ujijini siku kadhaa zilizopita hivyo walikuwa na hamu ya kuniona.

  Baada ya kuoga yule babu alifika akiwa na chai ya maziwa, mayai na mkate mmoja, baada ya kutuandalia alitukaribisha kisha aliondoka. Tulipomaliza kunywa chai Jini huyo alimpigia simu yule dereva Teksi aliyetupeleka pale hotelini siku ya kwanza.

  Alipofika tuliteremka chini ambapo Maimuna alimlipa yule babu pesa za siku zote tulizokaa pale hotelini ikiwa ni pamoja na chakula tukamuaga na kupanda kwenye gari na kuondoka.

  Tukiwa njiani nilistaajabu kuona uzuri wa mji huo na majini ambao walikuwa katika pilikapilika mbalimbali kama wafanyavyo binadamu duniani, kwani baadhi yao walikuwa wakiuza maduka, kuendesha magari na kusukuma mikokoteni.

  Wengine walikuwa wakisafisha jijini, kwenda mashuleni na maofisini, kwa ujumla huko ujijini kulikuwa na pilikapilika kama ilivyo hapa duniani. Tuliendelea na safari hadi tulipofika kwenye jumba moja kubwa la kifahari ambapo Maimuna alimuomba dereva asimame.

  Alipoegesha gari, tuliteremka ambapo alimuomba yule dereva atusubiri kwani tulikuwa tunakwenda kumsalimia mama yake mkubwa aitwaye Zahra.

  Tulipofika getini, Maimuna alibonyeza kitufe cha kengele ambapo haukupita muda mrefu alitokea kijana mmoja, alipomuona Maimuna alimkumbatia kwa furaha na kuhoji alikuwa wapi kwa muda mrefu.

  Jini huyo alimwambia alikuwa duniani kunifuata mimi, kijana huyo huku akitabasamu alinisalimu na kunikaribisha kwao. Baada ya salamu alitukaribisha ndani. Tukiwa katika sebule ya nyumba hiyo nilistaajabu kuona vitu vya dhahabu vilivyokuwepo.

  Mara baada ya kuketi, Maimuna alimuuliza yule kijana ambaye alinifahamisha kuwa ni mdogo wake mama yake alikuwa wapi, yule Jini alimjibu kwamba alikuwa anajisikia vibaya hivyo alilala chumbani kwake.

  Baada ya kupewa taarifa hiyo, Maimuna aliniomba msamaha kwa kuniacha peke yangu akainuka na kwenda chumbani kwa mama yake mkubwa. Nikiwa nimebaki na yule kijana sebuleni nilimuona akiniangalia na kutabasamu.

  Kufuatia kitendo hicho nilielewa alikuwa amefurahi kuniona kama ambavyo Majini wengine walivyofurahi, baada ya dakika chache Maimuna na mama yake mkubwa walikuja sebuleni ambapo yule mama alinisalimu na kunikaribisha kwao.

  Baada ya salamu, Maimuna alinitambulisha kwa mama yake kwamba mimi ni yule mchumba wake wa duniani ambaye alikuwa akimueleza habari zangu na kwamba nilifika ujijini kwa ajili ya kufunga ndoa.
   
 11. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Nilimshukuru kwa ukarimu wake ndipo aliniuliza nilipenda kunywa kinywaji gani, kabla sijajibu, Maimuna alimwambia aniletee juisi ya zabibu.

  Baada ya kumweleza hivyo, alimtuma yule kijana wake akaandae kinywaji hicho ambapo haukupita muda mrefu alikuja na jagi la dhahabu lililojaa juisi ya zabibu na kuliweka juu ya meza nzuri ya kioo iliyokuwa mbele ya masofa tuliyokalia.

  Kijana huyo alikwenda kwenye kabati kubwa la dhahabu ambapo alichukua grasi mbili na kurejea nazo mezani, wakati akimimina juisi kwenye grasi hizo walifika mabinti wawili wa kihindi.

  Wasichana hao walipomuona Maimuna, walimkimbilia, wakamkumbatia na kubusiana naye na kumwambia;
  "Za siku dada Mai?" ambapo mpenzi wangu huyo aliwajibu zilikuwa nzuri na baada ya salamu aliwatambulisha kwangu kwamba ni mchumba wake kutoka duniani aliyewaeleza habari zangu.

  Mabinti hao ambao walikuwa warembo, walikuja nilipokaa wakapiga magoti na kunisalimu kwa heshima. Baada ya salamu walinikaribisha kwao na kusema nijisikie kama nilikuwa nyumbani kwetu duniani.

  Baada ya mabinti hao kuketi kwenye sofa lililokuwa mbele yetu, Maimuna alinifahamisha kwamba wale wasichana walikuwa ni wadogo zake ambapo alinieleza mkubwa kidogo aliitwa Nasra na mdogo aliitwa Zamda.

  Walipotambulishwa yule mkubwa alimuuliza Maimuna; "Dada huyu ndiye Nassor uliyetumpa habari zake?" Maimuna aliwaambia ndiyo ndipo binti huyo alitabasamu na kuniambia walifurahi kuniona laivu kwani nilipokwenda mara ya kwanza hawakubahatika kuniona.

  Tulipomaliza kunywa juisi, tulimshukuru yule mama ndipo Maimuna alimuomba msamaha na kumuomba aturuhusu tuondoke kwani dereva teksi alikuwa akitusubiri nje kwa muda mrefu.

  Yule mama alitusii tusubiri chakula lakini Maimuna alimwambia mara tutapofika nyumbani kwa wazazi wake tungerudi kumtembelea ambapo yule mama alisema kutokana na pilika za maandalizi ya harusi yetu ingekuwa vigumu kurudi kwake.

  Baadaye yule mama alituruhusu tuondoke, tukiwa nje wale mabinti walimweleza mama yao kwamba wataongozana nasi kwenda kwa akina Maimuna kwani bado walikuwa na shauku na dada yao pia walipenda kuongea na mimi.

  Yule mama aliwaruhusu ndipo tuliingia kwenye gari na kuanza safari ya kuelekea nyumbani kwa mpenzi wangu Maimuna, tukiwa safarini nilishangaa kuona majengo, bahari na majini ambao walikuwa katika pilika kama ilivyo duniani.

  Tuliendelea na safari hadi tulipofika kwenye mzunguko wa barabara (Round about) ndipo gari letu lilisimamishwa na mzee mmoja aliyevalia kanzu ndefu na mkononi alikuwa ameshika tochi iliyokuwa ikitoa mwanga mkali sana.

  Nikiwa najiuliza sababu za mtu huyo kutusimamisha, yule dereva alilamika kuwa; "Huyu jamaa njaa kali kweli, yaani huwezi kupita hapa bila kumuachia hela!".

  Baada ya kusema hivyo aliteremka na kumfuata mzee huyo ambaye alikuwa amesimama mita chache kutoka eneo lilipokuwa gari tulilopanda ambapo waliongea kisha walikuja tulipokuwa.

  Yule mzee ambaye macho yake yalikuwa yakichezacheza kama wenzake, aliponiona alishangaa na kumuuliza yule dereva nilikuwa mgeni wa nani na tulikuwa tukielekea wapi?
  Dereva teksi alimfahamisha kwamba nilikuwa mchumba wa Maimuna, kufuatia kuelezwa hivyo aliuliza; "Maimuna binti Sharif?" Akamjibu ndiyo ndipo yule mzee alisema alipata taarifa ya harusi yetu.

  Baada ya kuongea nasi alituruhusu tuondoke, tukiwa tunaendelea na safari yule dereva alisema yule mzee aliona aibu kumtoa ‘chochote' baada ya kuniona mimi ambaye nilikuwa mgeni.

  Nilipomuuliza alikuwa nani, alisema alikuwa askari wa usalama barabarani aliyekuwa akikamata magari yenye makosa mbalimbali.

  Aliponieleza hivyo nilishangaa sana kwani mambo mengi yaliyofanyika ujijini hayakutofautiana na duniani isipokuwa askari wa huko huvaa makanzu.
   
 12. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #12
  Oct 11, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Tuliendelea na safari ndipo dereva aliacha barabara kubwa na kukata kulia ambapo kulikuwa na barabara ya kawaida ambayo ilipambwa na miti pamoja na maua yaliyotoa harufu nzuri.

  Maimuna aliyekuwa ameketi kiti cha nyuma akiongea na wadogo zake, alinigonga begani na kunifahamisha kuwa eneo tulilokuwepo ni mji wa baba yake na kwamba tulikaribia kufika kwao.

  Aliponieleza hivyo, niliongeza umakini wa kuangalia eneo hilo ambapo kila nilichokiona kilinivutia. Hatukuchukuwa muda mrefu niliona jumba kubwa la kifahari likiwa mbele yetu.

  Dereva alinyoosha moja kwa moja na kwenda kuegesha gari kwenye geti la nyumba hiyo, jambo la kushangaza nyumba hiyo ilikuwa kimya.

  Kufuatia hali hiyo nilifikiri hapakuwa na mtu yeyote, tukiwa nje ya lango kuu, Maimuna aliteremka na kwenda kubonyeza kitufe cha kengele ambapo hazikupita dakika tatu mlango ulifunguliwa na kijana mmoja wa kihindi.

  Alipomuona Maimuna alimlaki kwa furaha na kubusiana naye, kijana huyo ambaye alikuwa mrefu sana alimuuliza Maimuna mimi nilikuwa wapi?
  Maimuna alimweleza nilikuwa kwenye gari ndipo yule kijana alitimua mbio na kuja kunichungulia, aliponiona alifungua mlango akanisalimu na kuniambia; "Shemeji karibu sana kwetu!" Moja kwa moja nilielewa alikuwa anajua juu ya ujio wangu.

  Nilimshukuru kwa kunikaribisha ndipo aliwasalimia Zamda na Nasra kisha aliuliza kama kulikuwa na mizigo ambapo walimjibu kulikuwa na mfuko mmoja tu.

  Kijana huyo ambaye niligundua alikuwa ni kaka yake Maimuna, alichukuwa mfuko huo na kumuuliza yule dereva alitaka shilingi ngapi.

  Yule dereva alimjibu kwa lugha ambayo sikuifahamu ndipo alimfuata Maimuna na kumweleza ambapo jini huyo alitoa makaratasi Fulani ambayo nahisi yanatumiwa kama pesa na majini akampatia.

  Baada ya dereva kulipwa pesa alitaka kuondoka lakini Maimuna alimuomba amsubiri ambapo alimweleza siku ya harusi yetu alimhitaji kwa ajili ya kuwabeba wageni na shughuli zingine ambazo zingejiri pale nyumbani.
  Yule dereva alisema siku hiyo itakapofika ampigie simu, baada ya dereva kuondoka kaka yake Maimuna akiwa amefurahi sana alituongoza kuingia ndani.

  Tulipoingia ndani, nilistaajabu kuona vitu vilivyotengenezwa kwa dhahabu vikiwa vimetapakaa katika jumba hilo.
  Jambo lingine lililonishangaza ni kutomuona mtu wala kusikia sauti za watu, tulipita kwenye korido na kutokea kwenye sebule kubwa sana iliyosheheni vitu vya dhahabu.

  Kaka yake Maimuna akiwa mwenye furaha, aliendelea kunikaribisha na kunieleza nijisikie kama nilikuwa nyumbani kwetu. Mara baada ya kupita katika sebule hiyo nilisikia harufu ya udi na marashi mazuri.

  Ukiacha harufu hiyo nilisikia sauti za watu waliokuwa wakiongea, kijana huyo alituongoza na kwenda kufungua mlango mwingine mkubwa ambapo nilistaajabu kuwaona watu wengi wa lika mbalimbali wakiwa wameketi kwenye zulia zuri la manyoya.

  Walipotuona, wote waliinuka na kuanza kushangilia. Wanaume walikuja kunilaki kama mfalme ambapo nilisabahiana nao kisha walifuatia wanawake na watoto.

  Baada ya kunisalimu, walisalimiana na Maimuna ambaye walimpongeza kunifikisha kwao wakamalizia kwa Nasra na Zamda.

  Baada ya salamu walinikaribisha niketi katika zulia la peke yangu ambalo lilikuwa na upana wa mita mbili kila upande, nikiwa hapo alisimama bwana mmoja ambaye alikuwa amevaa kanzu nyeupe, kibaghalashia pamoja na koti jeusi.

  Jini huyo ambaye alikuwa na ndevu ndefu alisema; "Mabibi na mabwana na wanetu, yule pale ndiye mgeni wetu Nassor ambaye tulikuwa tunamsubiri kwa shauku kubwa!"
  Alipotoa kauli hiyo, wote walishangilia na baadhi ya vijana walipiga mbinja na mmoja wao kusema; "Hongera dada Maimuna kutuletea shemeji kutoka duniani!"
  Kufuatia kauli hiyo, jini mmoja wa kike aliangua kicheko na kusema; Halo...halo! leo mbona mambo! Ndipo yule jini aliyenitambulisha aliwaomba watulie kwani kuliwa na jambo muhimu alitaka kuongea.

  Ni jambo gani ambalo jini huyo alitaka kuongea? Kijana Nassor alifunga ndoa na Maimuna?
   
 13. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #13
  Oct 11, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Baada ya wote kutulia, yule jini aliwafahamisha kwamba maadam nilikuwa nimefika ujinini muda wowote ningefungishwa ndoa na Maimuna.

  Alipotoa kauli hiyo majini wenzake walishangilia na kupiga vigelegele, Maimuna naye alifurahi sana siku hiyo.
  Baada ya utambulisho, majini hao walianza kuondoka mmoja baada ya mwingine mpaka nikabaki na ndugu wa karibu wa Maimuna.

  Yule kaka wa Maimuna alinitambulisha kwa ndugu zake wengine, baba, babu, wajomba na mama yake Maimuna ambaye alikuwa amejifunika sura kama ninja.

  Mama na baba wa jini huyo walinikaribisha na kuniambia nijisikie nipo nyumbani na kuongeza kama nilihitaji kitu chochote nisisite kuwaeleza.

  Baada ya maongezi yaliyodumu kwa muda mfupi, baba yake Maimuna alimwambia kijana wake anipeleke katika chumba kilichoandaliwa kwa ajili yangu kisha wakatawanyika.

  Yule kijana aliniongoza tukapanda juu ya ghorofa la sebule tuliyokuwemo na kuingia katika chumba kimoja kizuri sana.
  Tukiwa katika chumba hicho, niliweza kuiona vizuri ile sebule na kila mtu aliyeingia sebuleni hapo.

  Baada ya kuongea na yule shemeji yangu, alinieleza kuwa sitatoka katika chumba hicho mpaka nitakapofunga ndoa na Maimuna na kwamba majini wote waliotaka kuniona wangepandisha kunisalimu.

  Nilipomuuliza sababu za kuniweka pale, jini huyo aliniambia kile chumba kilikuwa maalum kwa ajili ya kuishi na dada yake Maimuna.

  Aliongeza kuwa kutokana na heshima niliyokuwa nayo, sikutakiwa kutoka pale chumbani mpaka nitakapofunga ndoa na Maimuna ndipo nitaruhusiwa kwenda kuwasalimia ndugu wengine na kutembezwa sehemu mbalimbali.

  Baada ya jini huyo kuondoka, aliingia Maimuna na wasichana wawili ambao alikuwa amefanana nao sana mikononi wakiwa wamebeba chakula na vinywaji.

  Wale wasichana walipoweka chakula juu ya zulia, walinisalimu kwa kupiga magoti kama wafanyavyo baadhi ya wanawake wa makabila yaliyopo hapa duniani na kunisalimu kwa heshima.

  Baada ya kuandaa chakula, wale wasichana ambao Maimuna alinifahamisha kwamba walikuwa wadogo zake waliondoka.
  Tukiwa peke yetu, jini huyo alifungua mlango wa chumba kimoja kilichokuwa upande wetu wa kulia akaniomba nimfuate.

  Katika chumba hicho kulikuwa na kitanda cha futi sita kwa sita, kabati kubwa la nguo, jokofu, seti ya muziki na video pamoja na vitu vingine vingi.

  Pembeni ya chumba hicho kulikuwa na bafu pamoja na choo, Maimuna alinifahamisha kwamba kile chumba ndicho wazazi wake walituandalia tuishi baada ya kufunga ndoa.

  Nikiwa natafakari juu ya mambo niliyoona ujinini ambayo hayatofautiani na ya hapa duniani, Maimuna aliniomba twende tukaoge kisha tule na kujipumzisha.

  Kwa kuwa nilihisi joto, nilitaka kuvua shati ndipo jini huyo alinizuia na kuniambia kazi hiyo ataifanya yeye ambapo alinisogelea akaanza kufungua vifungo vya shati langu na kunichojoa suruali na kumalizia nguo za ndani.

  Baada ya kumaliza kufanya hivyo naye aliniomba nimvue baibui alilovaa, nilipokuwa nikimvua vazi hilo, jini huyo alikuwa akichezea kifua changu.

  Kitendo hicho kilinipagawisha ndipo nilimvua nguo zote tukabaki kama tulivyokuja duniani, kwa kuwa mzuka ulikuwa umenipanda, niliendelea kumfanyia ‘fujo' jini huyo na kumfanya anitumbulie macho yake mazuri.

  Baada ya kuona ameiva kama embe dodo kutoka Bagamoyo, nilianza kumshambulia mpaka nilipokata kiu yake.
  Kufuatia makasheshe niliyompa, jini huyo alinishukuru ndipo tulikwenda kuoga kisha alifungua kabati akatoa msuli wa rangi ya ugoro pamoja na fulana nyeupe akaniambia nivae.

  Yeye alijifunga khanga kiunoni iliyoandikwa maneno yasemayo; ‘Wewe ni chaguo langu', jambo hilo lilinishangaza sana ndipo nilimuuliza aliitoa wapi khanga hiyo akaniambia aliletewa zawadi na rafiki yake aliyeolewa duniani.

  Nini kilifuata na kijana Nassor alifunga ndoa na jini Maimuna?
   
 14. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #14
  Oct 11, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Ingawa niliwahi kusikia habari zinazohusu binadam kuoa majini, nilimuuliza kama jambo hilo liliwezekana ndipo Maimuna alitabasamu na kuniambia kwamba lilikuwa la kawaida ndiyo maana hata yeye alitarajia kufunga ndoa na mimi.

  Jini huyo aliongeza kuwa hata mdogo wake mmoja ambaye ni mtoto wa mama yake mdogo, ameolewa na binadamu na kwamba alikuwa akiishi Zanzibar na mumewe.

  Nilipomuuliza kama alikuwa na watoto, Maimuna alinifahamisha kuwa tangu alipoolewa hajajaliwa kupata mtoto.
  Baada maongezi hayo tulitoka ukumbini ambapo haukupita muda mrefu ndugu zake waliokuwa wakiishi mbali walifika kunisalimia.

  Siku hiyo nilitambulishwa kwa wajomba zake, kaka zake, mama zake wadogo, baba zake wadogo na wakubwa na marafiki pamoja na jamaa zao ambao walinikaribisha kwao.

  Baada ya utambulisho, majini hao waliondoka ndipo Maimuna alinieleza anakwenda kuonana na baba yake kujua alifikia wapi kuhusu muda wa kufunga ndoa.

  Jini huyo aliporejea alinifahamisha kuwa maandalizi ya ndoa yetu yalikamilika na kwamba siku iliyofuata baada ya swala ya Ijumaa ndipo tungefunga ndoa.

  Aliongeza kuwa muda wowote wangeanza kuwasili wageni na ndugu zake kwa ajili ya harusi, kama alivyonifahamisha saa moja baadaye wageni walianza kuwasili.

  Kilichonishangaza, walipowasili walikuja kunisabahi na kunikaribisha. Baada ya salamu wanaume waliketi pale ukumbini na wanawake walikwenda kukaa kwenye ukumbi mwingine.

  Ilipofika usiku nilisikia majini wakishangilia huku wakimsifia Maimuna kufanikiwa kunipata, nilipoomuuliza jini huyo kwanini wenzake walifurahi aliniambia ilikuwa ni fahari sana kwa jini kuoa au kuolewa na binadamu.

  Kulipokucha kaka yake Maimuna aliniletea kanzu nyeupe, kilemba na kuniambia vazi hilo lilikuwa maalum kwa ajili ya kuvaa wakati nikifungishwa ndoa na dada yake.

  Baada ya kunywa chai, nilisikia kijana mmoja akitangaza kwa kutumia kipaza sauti akisema; "Mabibi na mabwana, leo baada ya swala ya Ijumaa kwa mzee Sharif kutakuwa na ndoa kati ya binti yake Maimuna na kijana Nassor kutoka duniani ambaye mlifahamishwa juu ya ujio wake hivyo msikose kuhudhuria".

  Kufuatia matangazo hayo, nilimuuliza Maimuna ningefunga vipi ndoa pasipo kuwepo wazazi au ndugu zangu ambapo alinifahamisha waliandaliwa wazee wawili ambao wangechukuwa nafasi ya wazazi au ndugu zangu.

  Kadiri muda ulivyokuwa ukienda ndivyo majini walikuwa wakifika kwa wingi na kusababisha nyumba ya mzee Sharif kuwa na umati mkubwa wa watu.

  Nyumbani hapo palikuwa na vyuo karibu vitano ambavyo vilikuwa vikipiga taswida na palitawaliwa na shamrashamra, walikuwepo watu wengi waume kwa wanawake.
   
 15. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #15
  Oct 11, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Ilipofika saa sita na nusu mchana, majini hao walielekea msikitini kuswali na baada ya kumaliza walirejea nyumbani kwa mzee Sharif ndipo mmoja wao alitangaza kwamba wageni wote walitakiwa kwenda kwenye uwanja mkubwa ulioandaliwa kwa ajili ya kufungishwa ndoa yetu.

  Wakati jini huyo akitangaza, tayari mimi na mpambe wangu ambaye alikuwa jini tulikuwa tumevaa mavazi ya harusi. Wakati huo Maimuna alikuwa amekwenda kupambwa na dada zake.

  Muda wa kufungishwa ndoa ulipowadia, mimi na mpambe wangu tuliteremka chini ambapo tulianza kushangiliwa na kuelekea eneo ambalo ndoa ingefungwa.

  Tulipofika uwanjani hapo nilistaajabu kuona umati wa majini ambapo wanaume walivaa makanzu na akina mama walivaa mabaibui japo wapo ambao walikuwa wamevaa mavazi ya kawaida na kujitanda mitandio.

  Mzee mmoja alipotuona, alituongoza kwenda kuketi kwenye zulia ambapo haukupita muda mrefu tulisikia vigelegele vikipigwa vikisindikizwa na matarumbeta.

  Akina mama na majini waliokuwa wakipuliza matarumbeta walikuwa wakiimba wimbo wa Maimuna anameremeta ndipo nilimuona mpenzi wangu huyo akiwa ameongozana na mpambe wake huku dada na wadogo zake waliokuwa na furaha wakiwa nyuma yao.

  Majini hao waliokuwa wamependeza waliongozwa na akina mama waliokuwa wakiwaambia pamoja na wapiga matarumbeta waliovaa makanzu meupe na kwenda kukaa upande wetu wa kushoto.

  Dakika chache baadaye alifika mzee Sharif baba yake Maimuna na masheikh wawili ambao waliketi kwenye zulia, wakiwa wameketi mmoja wa masheikh alimtuma mdogo wake Maimuna aende akalete chetezo pamoja na ubani.

  Kijana huyo alipoleta, baba yake Maimuna aliwatangazia watu kwamba wakati wa kufungishwa ndoa na Maimuna uliwadia na kuwaomba waliokuwa wamekaa mbali kujongea kushuhudia tukio hilo muhimu kwa binti yao.

  Baada ya maandalizi kukamilika, nikiwa na mpambe wangu tulikwenda kukaa walipokuwa wamekaa masheikh na mzee Sharif ndipo sheikh mmoja aliniuliza kama nilikuwa tayari kumuoa Maimuna binti Sharif.

  Ingawa hakuwepo ndugu yangu hata mmoja nilikubali kumuoa ndipo walikwenda kumuuliza Maimuna kama alikuwa tayari kuolewa na mimi ambapo alisema ndiyo.

  Baada ya majibu hayo tulifungishwa ndoa kisha tulikwenda kwenye ukumbi ambapo sherehe kubwa ambayo nashindwa namna ya kuilezea ilifanyika, siku hiyo majini walikula kunywa na kucheza kadiri walivyoweza.

  Baada ya shamrashamra kwisha mimi na Maimuna tuliingia kwenye benzi ambayo baba yake alituandalia tukaenda kula fungate katika hoteli moja ambayo ilikuwa katikati ya jiji lao.

  Tulikaa hotelini hapo kwa muda wa siku tatu ambapo tulitembelewa na ndugu, jamaa na marafiki zao ambao walitupongeza kwa kufunga ndoa.

  Baada ya siku za fungate kwisha tulirudi nyumbani kwa mzee Sharif, kwa kuwa tulipata mialiko mingi, muda wa siku mbili tuliutumia kuwatembelea ndugu na jamaa za Maimuna.

  Siku moja kabla ya kurudi duniani, mzee Sharif aliniita katika sebule yake na kunieleza kwamba alifurahi sana mimi kumuoa binti yake lakini itakuwa vigumu kuishi naye duniani.

  Aliongeza kuwa, akiwa kama mke wangu halali atakuwa akija kunitembelea usiku na kurudi alfajiri na wakati mwingine atakuwa akija mchana lakini sio kuishi moja kwa moja duniani.

  Mkwe wangu huyo alinieleza wakati nikiishi na Maimuna atakuwa akifuatilia tabia yangu na kama sitabadilika na kumtesa binti yake, angeniwezesha kimaisha.

  Aidha, mzee huyo alinieleza kuwa hatofurahia kitendo cha kumtesa Maimuna na kama ningethubutu kufanya hivyo angeniadhibu.

  Mzee Sharif aliongeza kuwa anaelewa binadamu walikuwa wakorofi sana ndiyo maana alitoa tahadhari hiyo mapema, alinieleza kama nitachoka kuishi na bintiye ni heri nimpe talaka kuliko kumnyanyasa.

  Baada ya kunieleza hivyo, mzee Sharif aliniambia alikuwa akinipenda sana na kwamba atanilinda dhidi ya watu wabaya ili niweze kuishi na mke wangu Maimuna kwa furaha na amani.

  Alipomaliza kunieleza hivyo alinishika mkono na kunieleza kama nilikuwa na jambo lolote nililotaka kumweleza nifanye hivyo.

  Ingawa nilitamani sana kuhoji sababu ya mke wangu kuishi mbali na mimi, nilihofu kumuuliza na kuishia kumwambia sikuwa na cha kuongea naye.

  Kabla sijaondoka sebuleni kwake, jini huyo alimwita Maimuna ambaye alifika na kuketi chini. Mzee Sharif alimpongeza kwa kufanikiwa kunitafuta na hatimaye kufunga naye ndoa. Alimsifia bintiye na kumweleza kitendo hicho kilileta sifa kubwa katika ukoo wa Sharif kwani ni majini wachache walioweza kuoa ama kuolewa na binadamu.

  Mzee Sharif aliahidi kumpatia zawadi nzuri sana Maimuna ambayo alisema itatusaidia katika maisha yetu, baada ya kumsifia alimweleza amenionya nisimnyanyase hivyo naye aniheshimu kama mumewe.

  Nini kilifuata baada ya Maimuna na Nassor kufunga ndoa? Usikose kufuatilia wiki ijayo. akayeiona ‘Sticker' iliyoandikwa ‘Umepata zawadi ya simu' ambayo itabandikwa kwenye moja ya magazeti yetu.
   
 16. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #16
  Oct 11, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Baada ya Maimuna kuelezwa hivyo, aliahidi kutonidharau na kwamba atanipenda sana lakini alisema kama ningemkera naye angeniadhibu.

  Maimuna aliongeza kuwa hakuna kitu kitakachomkera katika ndoa yetu kama kumsaliti na kujihusisha na wanawake wengine, alisema kuwa adhabu yake sitaisahau katika maisha yangu.

  Kwa kuwa sikuwa na mpango huo nilimuhakikishia kwamba sitamsaliti na kumuomba nilichotaka aniwezeshe kimaisha ili niishi bila matatizo.

  Jini huyo aliniambia suala hilo kwake lilikuwa dogo sana na kwamba hakuna siku nitakayolala bila kula wala kukosa pesa za kununulia nguo lakini kuhusu utajiri alisema utatokana na kufanya kazi kwa juhudi na si kwa njia ya kupata pesa kupitia njia haramu.

  Aliongeza kuwa kwa majini wengine suala hilo liliwezekana lakini kwa ukoo wao wa Sharif ambao ulishika dini, ilikuwa ni makosa kwenda kumchukulia pesa benki au katika maduka ya watu kama ilivyo kwa majini wengine.

  Siku hiyo tuliongea mambo mengi na majini hao ndipo tulimuaga baba na kwenda katika chumba chetu, tulipoingia tu Maimuna alinivua nguo na kuanza kunifanyia fujo zake na kilichofuatia hapo ni ‘bakora' kwa kwenda mbele.

  Kwa kuwa nilikuwa na nguvu sana, siku hiyo nilimpeleka puta jini huyo mpaka akawa hoi na baada ya kumalizika ‘kibarua' hicho Maimuna alinishukuru, akanibusu na kusema alifurahi kuolewa na mtu niliyejua kumpa raha!
  Nilipomuuliza mpenzi wake wa zamani ambaye alikuwa jini hakumpa raha, alinieleza hakunifikia hata chembe na kuniambia nilijua kumburudisha.

  Kulipokucha mama mkwe wangu ambaye tulionana naye kwa nadra sana alituandalia chai na mapochopocho kibao, baada ya kunywa naye alisema alitaka kuongea nami kabla sijarudi duniani.

  Tukiwa tumekaa, mama, Maimuna na mzee Sharif mama mkwe alinipongeza kwa kufunga ndoa na binti yake na kuongeza kuwa nilitakiwa kuzingatia yote niliyoelezwa na mumewe pamoja na mke wangu Maimuna.

  Aliongeza kuwa majini ni viumbe wenye upendo sana na pia wana hasira hasa wanapokosewa na kwamba adhabu zao ni kali sana.

  Mama huyo alinitahadharisha niishi vizuri na mwanaye na kunieleza kama itatokea hali ya kutoelewana katika ndoa yetu niende nikamfahamishe.

  Kama alivyonieleza mumewe, alisema kwamba licha ya Maimuna kuwa mke wangu halali hatokuwa akiishi duniani moja kwa moja bali atakuwa akija usiku na kurejea ujinini.

  Baada ya kuongea na mama huyo, tuliondoka tukiwa na majini hao na kwenda nyumbani kwa baba yake mkubwa Maimuna aitwaye Mohamed.

  Tulipofika huko tulikuta mzee huyo na ndugu zake wengine watuandalia sherehe ya kupongezwa ambapo tulikula kunywa, kabla hatujaondoka mzee Mohamed na wadogo zake walinieleza mambo kama niliyoelezwa na mama mkwe na mzee Sharif.

  Kubwa zaidi walinitahadharisha kutokunywa pombe,kuvuta bangi na kufanya mambo machafu ambayo majini hawayapendi.

  Walinieleza kuwa walikuwa wanaelewa maisha ya ndoa yana matatizo yake, lakini walinitaka tukikorofishana na binti yao niende nikawafahamishe kuliko kumpiga au kumnyanyasa.

  Bila kuelewa kama Maimuna angenisumbua hapo baadaye, niliwaambia nisingemnyanyasa na kwamba ningetekeleza kila walichoniambia.

  Baada ya maongezi walitupatia zawadi mbalimbali na kututakia maisha mema katika ndoa yetu kisha tulipanda kwenye Hiace ya mzee Sharif tukarudi nyumbani kwake kujiandaa na safari ya kurudi duniani.

  Tukiwa tumekaa chumbani kwetu na mke wangu Maimuna, alinifahamisha kuwa katika safari yetu ya kurudi duniani mimi nitatangulia na kwamba yeye angefika siku iliyofuata usiku.

  Alinieleza kuwa hatopenda kuwafahamisha ndugu zangu mambo ya kwao na kwamba ndoa yetu ilikuwa siri yangu na majini na aliongeza kuwa nikiulizwa nilikuwa wapi niwafahamishe nilienda kijiji cha Kapalamsenga kilichopo Kigoma vijijini kuwasalimia ndugu zangu.

  Nilimwambia sitatoa siri hiyo kwa mtu yeyote japo nilijua mama alikuwa akielewa kila kitu kuhusu safari yangu ya kwenda ujinini.

  Nilipomuuliza kuhusu zawadi tulizopewa zingefikaje duniani, Maimuna alicheka na kuniambia kwamba zitabaki kwao.
  Ingawa nilipenda sana kuondoka na zawadi hizo baada ya kunieleza kuniambia zitabaki kwao, sikutaka kuhoji sana kwa kuhofia kumkera kisha kupewa adhabu kali ambazo sikutaka kuzipata.

  Kama ilivyokuwa kawaida ya Maimuna kupenda kufanya mapenzi, kabla sijaondoka alinihitaji faragha na baada ya mtanange huo tulikwenda kuoga kisha alifungua kabati akatoa kanzu mpya na kibaghalashia na kuniambia nivae.

  Nilimshukuru kwa mavazi hayo ambapo alinisifia kwa kupendeza, nikiwa nimejilaza kitandani ghafla nilipitiwa na usingizi na nilipozinduka nilijikuta nikiwa stesheni ya treni Tabora katikati ya abiria waliokuwa wamelala wakisubiri treni kutoka Kigoma.

  Kwa kuwa bado ilikuwa usiku, nilisubiri kupambazuke na kulipokucha nikiwa nimevaa kanzu yangu na kibalaghashia nilishika njia kurudi nyumbani.

  Nilipofika nyumbani nilimkuta mama akiwa amelala ambapo nilibisha hodi, aliposikia sauti yangu alifungua mlango na kunilaki kwa furaha.
   
 17. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #17
  Oct 13, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,240
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Duuuuh pole sana!!
   
 18. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #18
  Oct 13, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,240
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mambo ya utajiri wa fasta fasta huo,...
   
 19. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #19
  Oct 13, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  hivi wenzangu mnasomaga hizi tungo mie naona uvivu sana jama ingawa natamani nizisome
  FL
   
 20. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #20
  Mar 1, 2014
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,240
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  jaribu mdogo mdogo utazoea tu!!
   
Loading...