Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

MKASA WA PILI - Sehemu ya 23


Inaendelea.............


Asubuhi nilipanda zangu gari kurejea Mwanza na wembe ulikuwa ni ule ule wa kusafiri bure kama kawaida!

Niliingia Mwanza mida ya saa 2 usiku na kwakuwa nilikuwa nimechoka niliingia geto kupumzika mpaka Asubuhi ambapo niliamka na kuelekea kule kiaruani kama kawaida!

Ile shule haikuwa ya serikali bali ilikuwa ya private na kwakuwa mimi nililipwa kutokana na vipindi ninavyohudhuria hivyo haikuwa taabu sana na haikunizuia mimi kuendelea kufanya mambo yangu mengine!
Baada ya siku kama mbili nilielekea Nyumbani Nyegezi kumsalimia Bi mkubwa!,Sasa wakati naondoka hapo kwa Bi mkubwa nilikutana na demu mmoja hivi aliwahi kusoma shule moja inaitwa St mary's na alikuwa ni mzuri sana!.

Yule binti wakati yeye ndo anamaliza shule pale St Mary's mi tayari nilikuwa zangu nimemaliza shule na nilikuwa tayari nishaanza kufundisha tuition,Nilikuwa nikimfukizia sana wakati huo bila mafanikio na kwa jinsi alivyokuwa mzuri alikuwa ana maringo sana!
Kwanza nilipomuona sikuamini kwasababu alikuwa kajazia balaa na ndo alizidi kuongezeka uzuri!
Nyumbani kwao hakukuwa mbali sana na hapo nyumbani kwetu na kwao walikuwa na uwezo sana!

Basi nilimwita akasimama "Mambo Yusta"
"Poa,za siku"?,aliniuliza
Tuliendelea kupiga stori na kwakuwa nilikuwa nina mpenda sana sikuchoka kumtazama!
Nilimuuliza yuko wapi sasa hivi maana nilikuwa nina muda mrefu sijamuona,
Aliniambia alikuwa akisoma IFM jijini Dar es salaam mwaka wa pili!
Aliniambia alikuwa na haraka hivyo tungeongea siku nyingine!,Nilimuomb namba yake ya simu akaniambia kwamba yeye hana simu!,Nilimuuliza "Hiyo uliyoshika mkononi niya nani?",Aliniambia "Hii si yangu,ingekuwa yangu ningekupa namba"
Nikamwambia basi sawa tutaonana!

Aliondoka zake na mimi nikaendelea na safari,Lakini nilikuwa nikijisemea haiwezekani mtoto mzuri kama huyu akose simu na yuko mwaka wa pili!
Zamani wakati anasoma St mary's kulikuwa na stori kwamba kuna jamaa alikuwa akitembea naye ni mtoto wa kigogo mmoja hapo Mwanza ila mimi sikuwahi kulithibitisha hilo!
Kiukweli nilijisemea "Huyu mtoto lazima nayeye nimkomoe maana anajifanya yuko matawi ya juu,lazima anitambue mimi ni nani"!

Ndugu zangu labda tu niseme ya kwamba iwapo kutakuwa na muhusika yeyote ambaye alihusika kwenye harakati zangu hizo za maisha ya dhambi niliyoyaishi zamani na akafanikiwa kusoma huu uzi,tafadhali sana naomba anisamehe maana bado nilikuwa kwenye giza la Ibilisi na sikuwa na akili nilizo nazo leo,Tafadhali sana naomba mnisamehe sana,nipo tayari kubeba adhabu yeyote maana tayari nshampokea Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yangu hivyo sitaona shaka yoyote kufa nikiwa ndani ya Yesu!,Nisameheni sana ndugu zangu wa Mwanza niliowakwaza na wa maeneo mbalimbali ya nchi yetu hii ya Tanzania.

Basi niliporudi geto nilikuwa namuwaza Mtoto mzuri Yusta pamoja na Zainati na hawa wote niliapa ya kwamba Nitalala nao kitanda kimoja na niwapige bakora za kim-kakati mpaka wanyooke!
Nilitaka kuitest ile dawa niliyopewa na Mzee Nchibaronda siku chache zilizopita na tageti yangu ilikuwa kwa hao warembo wawili!

Kiukweli ndugu zangu japo nilitembea na wanawake wachache lakini walikuwa na viwango vya kimataifa,kama ni bidhaa basi hao wanawake ningediliki kusema walikuwa wamethibitishwa na shirika la viwango la kimataifa,yaani ISO

Baada ya ile wiki moja kuisha nilimpigia yule mama niliyempa kazi ya ku-decorate ile nyumba yangu na aliniambia nyumba iko tayari ila kuna vitu vidogo vidogo walikuwa wanamalizia!
Basi nilimwambia mimi nahamia hivyo hivyo kwa maana nishachoka kukaa geto maana si pa hadhi yangu tena!,Kiukweli enzi hizo na wakati huo nilikuwa nimenawili sana na kila nguo nilizokuwa navaa zilikuwa zinanikaa kwenye mwili kama nilikuwa nimeshoneshewa mimi!
Nilienda kuikagua ile nyumba na kiukweli mpaka niliogopa maana niliona serikali ingenishitaki kwa kuwa nyumba nzuri kama ile wakati kipato changu ni kidogo!
Nilikuwa nimefanya namna ambayo yoyote ambaye angeleta fyokofyoko basi alikuwa anaenda na maji!
Kwa wakati huo pia niliplan kufanya biashara ya ujenzi,yaani nilitaka niwe na kampuni ya ujenzi wa nyumba halafu zikiisha napangisha!

Biashara ambayo niliifanya lakini baada ya sekeseke moja hivi la kutisha kila kitu kilianza kupukutika taratibu!
Vile vitu nilivyokuwa nikikaa navyo geto kuna jamaa yangu yule aliyekuwa akifanya kazi kiwandani nilimwachia vyote,mle ndani mimi nilitoa kile kibuyu na yale mabegi dogo na kubwa yaliyokuwa yakizihifadhi pesa zangu!

Nilihamia kwenye nyumba yangu rasmi na kuna chumba nilikitenga rasmi na kilikuwa safi kupita maelezo!

Sasa ndipo kazi ikaanza rasmi


Itaendelea....................




..........................................................



Kutokana na kuwa watu wengi wananifuata pm wakitaka nikatishe stori ili wanunue waiandikie kitabu then wao wauze na wengine wameenda mbali zaidi kunitukana kuwa unatumiaje muda mwingi hivyo kuandaa stori isiyo na malipo na Kuna baadhi ya watu wametoa na offer ya kiasi Cha pesa wanachotaka kunipatia ili niwauzie kisa chote

Lakini baada ya Jana kuwadokeza nikaona Kuna watu wengi wanauhitaji na hiki kisa na walitaka kukisikia mpaka mwisho na ukizingatia kisa chenyewe ndo kwanza tunaelekea kwenye pointi maana saivi tupo mwaka wa 2013 ambapo mambo yote hayo yanatokea lakini kisa kitaendelea Hadi mwaka wa 2017 na hapa katikati Kuna Mambo mengi Sana ya ajabu na ya kutisha niliyoyafanya na kuyapitia hivyo Kuna mtu mmoja kanishauri pia kuwa badala ya kumuuzia kisa mtu mmoja ni Bora nikaanzisha group la WhatsApp au telegram ambapo mtu atachangia shilingi kuanzia buku (1000 ) na atapata nafasi ya kusoma kisa chote mpaka mwisho hivyo hapa naweka link ya telegram na kila ambaye anahitaji kujua kisa hiki atatakiwa kupakua application ya telegram play store na kujisajiri Kama anavofanya WhatsApp na Kisha kubonyeza link hii hapa chini na tayari ataona stori ishawekwa kutoka mwanzo mpaka hapa tulipoishia na ukihitaji mwendelezo utatakiwa kulipia shilingi 1000 au zaidi kadri utakavyobarikiwa na utaungwa group la V.I.P ambako kisa kitaendelea Hadi mwisho ahsanten Sana kwa wote mlionifuata pm na baada ya kufikiria mawazo yenu nimeona Hili litakuwa Bora kwa kila mtu anayehitaji kujifunza na Kama Kuna mtu nitakuwa nimemkwaza Basi atanisamehe maana ni Bora haya maamuzi kuliko kumuuzia mtu mmoja na ambapo hatujui atatoa lini hicho kitabu


Niungeni mkono ndugu zangu ili nami nipate tu hata hela ya maji maana nilipo achana rasmi na hizi habari za Ibilisi mambo yamekuwa ya kuunga unga,Kisa hiki ndo kwanza kinaelekea sasa rasmi kwenye vioja maana baada ya mimi kuamia kwenye nyumba yangu ndo kazi ikaanza rasmi!

Pia kuna watu wametumia hela ya vocha,niwaombe wani-pm ili niwaunge kwenye grupu la Telegram maana kisa kizima nitakisumulia huko,Niliuona mkono wa Bwana mwaka 2018 lakini kabla ya hapo nitasimulia kila kitu na kilichofanya mpaka mimi kuachana na mali za Ibilisi
Kumbe ndio iliishia hivi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom