Mikakati yafanyika kujitosheleza kwa reli

elivina shambuni

JF-Expert Member
May 31, 2018
461
295
1576317575149.png


MABORESHO ya miradi ya reli ukiwamo wa Uboreshaji wa Reli ya Kati (TIRP) ya Dar es Salaam-Isaka wa kilometa 970 ni mikakati ya kufi kia malengo ya nchi kujitosheleza kwa miundombinu ya reli. Hivi sasa nchi ina miundombinu ya reli ya urefu wa kilometa 4,700 na ili kujitosheleza zinahitajika kilometa 20,000 hivyo mahitaji ni kilometa 15,300 za miundombinu ya reli.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa alisema hayo juzi jijini Dar es Salaam, alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya shirika hilo ya miaka minne chini ya uongozi wa Rais John Magufuli.

Kadogosa akijibu maswali ya waandishi, likiwamo lililouliza kuhusu urefu wa kilometa za reli uliopo nchini na nini kinafanyika kufikia lengo alisema nchi ipo katika kipindi cha maboresho na ujenzi mkubwa wa miundombinu ya reli itakayoleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi miaka michache ijayo. Alisema hivi sasa maboresho hayo yanaifanya nchi iwe na kilometa 4,700 za reli lakini ili kujitosheleza kwa njia hiyo ya treni, nchi inapaswa kuwa na kilometa 20,000 hivyo bado kilometa 15,300 kufikia lengo hilo.

Akielezea maboresho ya mradi wa TIRP, Kadogosa alisema ni moja ya mradi unaolenga kuongeza miundombinu ya reli ya uhakika nchini na unafanywa na mkandarasi wa China (CCECC) kwa Dola za Marekani milioni 300 (TSh bilioni 69). “Lengo la mradi wa uboreshaji wa reli ya kati- TIRP ni kuongeza ubora na uimara wa njia ya reli ya kati kutoka Dar es Salaam hadi Isaka ili iweze kubeba mizigo kutoka chini ya tani 13.5 za uzito wa eskeli hadi tani 18.5 na kutoka kasi ya kilometa 35 kwa saa hadi kilometa 70 ili kuongeza ufanisi na uhakika wa huduma,” alisema Kadogosa.
 
Mkuu rekebisha hapo kwenye us$ 300m kwenda Tsh 69bn, ila yote kwa yote ni jambo jema.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom