Mikakati ya Tanesco kuhusu mgao wa umeme

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
262996_190930867634680_186255581435542_490006_3264749_n.jpg
 
mipango daima huwa mizuri (sio Tanesco tu) lakini hawa jamaa tatizo lao lipo kwenye "practice what you preach". Hapo unakuta allocation ya fedha ulaji ni kama 70% ya gharama za miradi na itakayoenda field in 30%, zitabakia kuwa mipango ndoto tu
 

hizo nguvu za maji ndo zinaleta shida bado naona ziko kwenye mipango ya muda mrefu! kweli sikio la kufa halisikii dawa. halafu huo muda mrefu unaaisha lini? tangu enzi za mwinyi kuna miradi ipo kwenye miradi ya muda wa kati!!
 
Sick and tired of being sick and tired of these mikakati hewa ya kwenye karatasi
 
MWANZONI MWA 2012......... Hapo mmenigusa inamaana mwaka huu swala la umeme tusahau kabisa! biashara yangu ya Juice kwisha kabisa.....
 
Kwakuwa umeme wa nguvu za maji umegonga mwamba,
Na kwakuwa umeme wa nguvu za upepo tumeushindwa,
Na kwa kuwa umeme wa nguvu za nyuklia hatuuwezi,
Na kwakuwa umeme wa nguvu za jua tunauogopa,
Je,Bunge hili tukufu halioni wakati umefika tujaribu umeme wa Nguvu za GIZA?
 
Kwakuwa umeme wa nguvu za maji umegonga mwamba,
Na kwakuwa umeme wa nguvu za upepo tumeushindwa,
Na kwa kuwa umeme wa nguvu za nyuklia hatuuwezi,
Na kwakuwa umeme wa nguvu za jua tunauogopa,
Je,Bunge hili tukufu halioni wakati umefika tujaribu umeme wa Nguvu za GIZA?
hli ni swali au ni msisitizo? huoni kuwa tupo gizani tayari?
 
Hiyo mipango ya mda mfupi ni mpaka mwaka gani??usikute ndo mpaka mda wa uchaguzi tena!!
 
Kwakuwa umeme wa nguvu za maji umegonga mwamba,Na kwakuwa umeme wa nguvu za upepo tumeushindwa,Na kwa kuwa umeme wa nguvu za nyuklia hatuuwezi,Na kwakuwa umeme wa nguvu za jua tunauogopa,Je,Bunge hili tukufu halioni wakati umefika tujaribu umeme wa Nguvu za GIZA?
Imepita hoja haijapita??b'' magamba''Hoja imepita mueshimiwa?
 
Ama kweli naona kijani na Njano imetuilia... Tatizo jamani sio Tanesco, hii ni mpiango ya serikali kuwekeza ktk vyanzo hivyo. Tanesco wanachofanya ni kuelezea tu mipango ya muda mrefu ya serikali ambayo mkuu wa kaya anasema yeye sio Mungu wa kuleta mvua lakini wakati huo huo nguvu kubwa ameiweka ktk matumizi ya nguvu za maji (Hydropower plant).. Kwa mahesabu ya haraka haraka naona:-
1. Nguvu za maji - Mw 3900 - Miradi 7.
2. Makaa ya mawe - Mw 1200 - miradi 3.
3. Gesi - Mw 1000 - Miradi 3 pamoja ya 3 ya dharura.
4. Geothemal - Mw 650 -Mradi 1.
5. Upepo - Mw 50 - mradi 1.

Sasa ikiwa leo mvua zenyewe ndio kisingizio cha ukosekanaji umeme!.. Kwa nini tunatumia nguvu kubwa kujenga Dams ambazo zitaathiri kilimo na tunakaribisha UKAME kama wa Ethiopia wakati gesi yetu, makaa ya mawe, Upepo na geothemal havikupewa kipaumbele zaidi ktk mipango ya muda kati na mrefu?

Inasikitisha zaidi kujua kwamba Nyakato Mwanza inapewa Mw 60 tu za gesi kwa sababu bomba la gesi ni mradi wa viongozi wetu..Kwa nini serikali isiweke mtambo mkubwa zaidi na Nyakato ikaweza ku supply mikoa yote ya kaslkazini badala ya mikoa hiyo kuendelea kutumia generata za mafuta mazito?.
 
Back
Top Bottom