Mikakati ya kuwabambika kashfa viongozi wa CHADEMA yaandaliwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mikakati ya kuwabambika kashfa viongozi wa CHADEMA yaandaliwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mtundu, Oct 17, 2011.

 1. m

  mtundu Member

  #1
  Oct 17, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NGUVU ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), imezidi kukinyima usingizi Chama cha Mapinduzi (CCM), na sasa inadaiwa kuwa mikakati imenza kusukwa ili kuwabambika kashfa baadhi ya viongozi wakuu wa CHADEMA kwa lengo la kuwadhoofisha wao binafsi na chama kwa ujumla.

  Habari za ndani zinasema kwamba baadhi ya viongozi wa CCM walikutana na kufanya kikao na wahariri kadhaa wa vyombo vya habari vinavyoegemea upande wake pamoja na maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa, ili kuweka mikakati ya kuhakikisha wanakidhoofisha CHADEMA kabla ya mwaka 2013.


  Kwa mujibu wa chanzo kimoja cha kuaminika, kikao hicho kizito kilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni katika hoteli moja maarufu , ambapo mikakati iliwekwa ya kuwabambika kesi na kashfa baadhi ya vigogo wa juu wa CHADEMA wakiwemo na wabunge.

  Miongoni mwa majina ya walengwa ni Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe, ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki na pia Mnadhimu wa Kambi hiyo na Godbless Lema, mbunge wa Arusha Mjini.

  CHANZO CHA HABARI: << KIPO HAPA>>

  WAZO LANGU

  CHADEMA NI CHAMA CHA WASOMI.TUNAWAOMBA MSICHOKE KUUSIMAMIA UKWELI KWA MANUFAA YA TAIFA LETU.

   
 2. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Crackpot!!
   
 3. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Kwa nini DR SLAA na Jakaya sio targets, Nadhani hawa ndio Hatari kwa CHAMA hiki.
   
 4. l

  luckman JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Ukosefu wa uadilifu na uzalendo, ubinafsi vimetafuna nchi yetu kwa kiasi kikubwa!usalama wanafanya nini???mambo yote haya wako wapi, na mishahara yao inalipwa na nani>????ni sisi kweli au wanalipwa na wawekezaji????
   
 5. matungusha

  matungusha JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  A drawn man can catch a straw!!!! hawawezi kushindana na nguvu ya umma kamwe!!!!!
   
 6. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  tuko wengi mnooooo sijui watawza kutumaliza wote?
   
 7. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #7
  Oct 17, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Mods iunganisheni hii thd na ile ya awali msiwachoshe wadau kuchangia huku na kule: ccm haiwezi kunyanyuka tena hata kwakutumia miujiza.
   
 8. ismathew

  ismathew JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2011
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 254
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uwoga unawasumbua kwa makosa yao, kwani ni viongozi gani wa Ccm na Serikali yake wasiyekuwa na hatia. Wote wapo katika
  mstari mmoja kujibu mashtaka kuanzia mwaka 2015. Wasijisumbue na hizo Bla Bla Bla !!!
   
 9. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #9
  Oct 17, 2011
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Kadri wanavyozidi kuwachafua viongozi wa CHADEMA ndivyo wanavyozidi kuwapandisha chati. Kweli, mfa maji heshi kutapatapa. CCM wamechanganyikiwa. Badala ya kuziba nyufa zilizopo kwenye jumba lao, wao wamekazania kwenda kuibomoa nyumba ya jirani. Nyumba imara, unavyojaribu kuibomoa ndivyo inavyozidi kuimarika, inajijenga yenyewe. Kwani watazamaji, mimi na wewe, hatuujui ukweli? Wanadhani sisi ni mambumbumbu? Yuko wapi yule aliyedai kuporwa mke na Dk. Slaa? Wakaenda kwenye magazeti lukuki, wakawahonga waandishi na wahariri, kuandika story isiyo na kichwa wala mkia! Yameishiwa wapi? Wao walidhani wanamchafua Dk. Slaa! Kumbe walikuwa wanamfanyia kampeni?

  Endeleeni kuwafanyia viongozi wa CHADEMA kampeni. Hayo matusi kwa CHADEMA ni sifa, maana kwa mtu anayeishiwa hoja huanza kutukana. Hii ni dhahiri kwamba, kwasa, CCM inajiandaa kuitwa Chama Kikuu cha Upinzani, ifikapo 2015!

  Kalaghabahoooooo!
   
Loading...