SoC01 Mikakati ya kupambana na wimbi la ukosefu wa ajira kwa vijana

Stories of Change - 2021 Competition

Kilenzi Jr

Member
Jul 29, 2021
13
245
  • Kuna kila sababu ya kupitiwa upya kwa mfumo wa elimu unaowandaa wahitimu kuingia kazini ili kuepuka makosa yanayojitokeza wakati wa maombi ya kazi na kuwaandaa kisaikolojia kujiajiri wenyewe.
  • Pia ushindani wa soko ajira inaweza kuwa sababu kwa baadhi yao kutumia vyeti vya kughushi kupata mpenyo wa ajira.
  • Vijana wajiajiri ili kuepuka usumbufu unaotokea wakati wa kufuatilia ajira za Serikali. Wachambuzi wa masuala ya ajira nchini kuna kila sababu ya kupitiwa upya kwa mfumo wa elimu unaowandaa wahitimu kuingia kazini ili kuepuka makosa yanayojitokeza wakati wa maombi ya kazi na kuwaandaa kisaikolojia kujiajiri wenyewe hali hii ni matokeo ya mfumo dhaifu wa elimu kuanzia ngazi ya chini na vijana kushindwa kujiongeza katika kuboresha maarifa na ujuzi unaotakiwa katika soko la ajira.

Sishangazwi na idadi kubwa ya waombaji kukosa ajira serikalini na sekta binafsi kwa sababu ushindani umeongezeka na nafasi za kazi ni chache kukidhi mahitaji yote ya waombaji.

Sambamba na hilo ni kuwepo kwa mianya katika mifumo inayosimamia uhakiki wa vyeti na uelewa mdogo wa wahitimu kuhusu vigezo na sifa za kuomba kazi katika taasisi mbalimbali.

“Watu wengi wana uchu wa kuingia kazini kwa namna moja ama nyingine hawajaweza kutimiza zile requirement (mahitaji) zote,”
Ata hivyo, vijana wanatakiwa kuangalia fursa nyingine za kujiajiri na kuwa huru kufanya shughuli za ujasirimali ambazo zitawasaidia kuinuana kuliko kusubiri ajira za serikalini ambazo hazitoshelezi mahitaji yao ikizingatiwa kuwa idadi ya wahitimu wa vyuo vikuu inaongezeka kila mwaka.

Hivyo basi kuna haja ya kupitia upya mitaala ya elimu tangu ngazi ya shule za msingi ili iendane na mabadiliko yanayotokea katika soko la ajira ambalo linahitaji vijana wenye ujuzi na maarifa ya kutosha kutimiza majukumu wanayokabidhiwa katika jamii.
Wahitimu nao wanapaswa kubadilika kimtazamo na kuacha kusubiri ajira za Serikali badala yake wageukie shughuli zinazoweza kuwahakikishia upatikanaji wa kipato.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom