Mikakati ya kudhibiti COVID-19 inatofautiana; WHO yatoa mwongozo wa kufuata

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,188
4,100
Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO, kesho litachapisha mwongozo wenye taarifa zaid za kuwezesha nchi kuchukua hatua za kupunguza kuenea kwa ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19 sambamba na kuwa msingi wa kuamua iwapo kurejesha shughuli za kiuchumi na kijamii au la.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus amesema hayo leo akizungumza na waandishi wa habari kwa njia ya video kutoka Geneva, Uswisi.

Dkt. Tedros amesema hatua hiyo inazingatia ukweli kwamba mataifa mbalimbali katika kukabiliana na COVID-19, yamechukua hatua nyingine zinazohatarisha haki za binadamu, na nyingine hata kusababisha watu kushindwa kujipatia kipato.“Unaishi vipi kwenye marufuku ya kutoka nje ilhali unategemea kibarua ili uweze kupata chakula? Ripoti mpya kutoka maeneo mbalimbali dunia zinaelezea jinsi gani watu wako hatarini kusalia bila chakula,” amesema Dkt. Tedros.

Amesema, shule nazo zimefungwa ambapo watoto bilioni 1.4 hawako shuleni hali ambayo amesema imesitisha mafunzo yao, huku ikifungua milango ya ukatili na unyanyasaji dhidi ya watoto huku wengine wakikosa mlo ambao walizoea kupata shuleni.

Dkt.Tedros amesema kwamba suala la kuzuia watu kuchangamana ni moja tu ya mikakati lakini kila serikali inapaswa kutathmini mazingira yake, huku ikilinda raia wake hususan wale walioko hatarini zaidi.

Ni kwa mantiki hiyo amesema mkakati huo mpya unaweka kwa muhtasari kile ambacho wamejifunza na kubainisha hatua za kuchukua ambapo kuna vipengele sita ambavyo nchi zinapaswa kuzingatia pindi zinapotaka kuondoa vikwazo au marufuku zilizowekwa katika kudhibiti COVID-19.

Vipengele 6 pendekezwa
Mosi ni kuhakikisha kuwa maambukizi yanadhibitiwa, pili, mfumo ya afya iliyopo ina uwezo wa kutambua, kuchunguza, kutenga na kutibu kila mgonjwa na mwambata wake na tatu, Hatari za mlipuko zinapunguzwa hasa kwenye maeneo ya hospitali, vituo vya afya na makazi ya kuuguza.

Kipengele cha nne, mikakati ya kinga iwepo maeneo ya makazini, shuleni na kwingineko ambako ni lazima watu waende na tano, kuwepo na hatua za kudhibiti maambukizi yanayoletwa na hatimaye sita, jamii zielimishwe vya kutosha na ziwezeshwe kuendana na mazingira mapya yaliyojitokeza.

WHO imesisitiza kuwa kila nchi inapaswa kutekeleza mikakati ya kina ya kupunguza maambukizi na kuokoa maisha, kwa lengo la kuwa na kiwango cha chini cha maambukizi na hatimaye kutokomeza kabisa maambukizi.

Hata hivyo Dkt. Tedros amekumbusha kuwa ni lazima kuwepo na mizani katika kutibu COVID-19 na magonjwa mengine wakati huu ambapo mifumo ya afya imezidiwa sambamba na kushamiri kwa athari za kiuchumi na kijamii.

Dkt. Tedros ametumia hotuba yake ya leo pia kushuruku Uingereza kwa mchango wake wa zaidi ya dola milioni 218 katika harakati za kimataifa za kutokomeza COVID-19.
 
Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus amesema hatua hiyo inazingatia ukweli kwamba mataifa mbalimbali katika kukabiliana na COVID-19, yamechukua hatua nyingine zinazohatarisha haki za binadamu, na nyingine hata kusababisha watu kushindwa kujipatia kipato.“Unaishi vipi kwenye marufuku ya kutoka nje ilhali unategemea kibarua ili uweze kupata chakula? Ripoti mpya kutoka maeneo mbalimbali dunia zinaelezea jinsi gani watu wako hatarini kusalia bila chakula,” amesema Dkt. Tedros.
Hii ni habari njema ya uthibitisho kuwa Magufuli ni shujaa.
P
 
Safi sana, well spoken Dr Tedrios.

Ni muhimu kuzingatia local context ktk vita hii ya Corona, mataifa yanayoendelea hayawezi kushinda hii vita kwa ku copy and paste kila mbinu Inayotumiwa na mataifa yaliyoendelea.

Kuna baadhi ya majirani zetu waliokurupuka kuweka lockdowns na curfews sasa wanaanza kuumbuka, wananchi wao juu ya ugonjwa pia wanaumia kwa njaa na kuamua kukimbilia huku kwetu na kuhatarisha maisha ya wananchi wa mikoa ya mipakani haswa Kilimanjaro na Arusha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyendo, Maeneo ya mashule ndio sehemu ambazo ugonjwa unaweza enea kwa kasii sanaa.. kwasababu wanafnz wanashare vitu vingii sanaa wakiwa darasani kwaiyo kufunga shule na kufanya self isolation ni jambo jema coz uhai nibora kuliko elimu
Huna lolote mkuu kwenye ushauri.

Naona unaanza kumkosoa Hadi mkuu wa WHO
 
Hivi shule zitafunguliwa kweli juma tatu?

Sent using Jamii Forums mobile app

Tusubiri.

Inasemekana serikali itatoa tamko jingine kesho tarehe 15/4/2020 la aidha iendelee kwa muda fulani ama zifunguliwe na masomo yaendelee baada ya kufanya Covid-19 situation assessment kabla ya kufikia conclusion....

Pia, za chini ya carpet ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa kuna possibility mikoa iliyoathirika i.e DSM, Arusha, Mwanza na Kilimanjaro ikaendelea na partial lockdown na sehemu zingine shughuli za kijamii kama masomo, magulio, michezo, harusi, makongamano nk zikaruhusiwa kuendelea...

SWALI NI;
Is it possible kipande kimoja cha nchi ndani ya nchi moja shughuli za kijamii ikiwemo masomo (shule kufunguliwa) zikaruhusiwa kuendelea huku sehemu zingine under partial lockdown?

Mbinu gani zitatumika mfano kuzuia muingiliano na movement za watu wa eneo lililoathiriwa wasiwe na contact na wale ambao hawajaathirika?

Mfano, wanafunzi na wanavyuo na waishio mikoa itakayokuwa under quarantine wasomao shule za bweni kuondoka na kwenda kwenye mikoa iliyo Salama?

In short, this is very challenging situation in making any decisions. But, all in all maisha ya watu ni ya thamani zaidi kuliko muda utakaopotea bila masomo kuendelea...

So long as tuko hai, we can compensate muda huo in future because maisha ya watu na watoto wetu hayana mbadala....!!
 
Kwa kuwa maambukizi mapya bado yanaongezeka kila wiki, ni heri Waziri mkuu asiruhusu shule kufunguliwa. Walau atuongezee wiki mbili za kufuatilia matibabu ya wagonjwa 49 waliopo sasa hadi May ndio watoto waweze kurudi shule.
 
Back
Top Bottom