Mikakati ya kijeshi ya Iran ni mipango isiyobadilika sambamba na kuangamizwa kwa dola laanifu la Israel

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
5,213
2,000
Kuinuliwa uwezo wa ulinzi wa Iran, stratijia isiyoweza kubadilika
Feb 05, 2019 03:42 UTC
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haiogopi dola lolote katika kuinua na kuimarisha kiwango cha uwezo wake wa kujihami.
Brigedia Jenerali Amir Hatami, Waziri wa Ulinzi wa Iran akizungumza katika moja ya hafla za kuadhimisha mwaka wa 40 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu alisisitiza kuhusu nukta hii na kuongeza kuwa: " Vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni nembo ya umoja, mshikamano na usimamizi wa kijihadi na leo vikosi hivi vimeweza kufikia kilele cha mafanikio katika sekta mbali mbali za kisayansi, kiteknolojia na kivita katika mazingira magumu yaliyolazimishwa na adui."
Brigedia Jenerali Hatami ameendelea kusema kuwa: "Hivi sasa Wizara ya Ulinzi ya Iran ina uwezo mkubwa wa kisayansi na kiteknolojia na imeazimia kuvipa vikosi vya ulinzi teknolojia ya kisasa kabisa ya kijeshi."
Kumiliki uwezo wa kijeshi na uwezo wa kumzuia adui si tu kuwa ni misingi isiyokiuka sheria yoyote ya kimataifa, bali ni kwa mujibu wa msingi wa kujihami na ni haki ya kisheria ya nchi zote.
Uwezo wa kijeshi unaojumuisha nguvu za makombora ya Iran ni sehemu ya uwezo halali wa kijeshi unaodhamini usalama wa taifa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na msingi wake mkuu ni kuwa na uwezo wa kumzuia adui kuanzisha mashambulio. Waziri wa Ulinzi wa Iran ametoa hotuba yake katika fremu hiyo hiyo.
Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika hotuba aliyowahi kutoa alikosoa hatua ya Ulaya kujiunga na Marekani katika kuishinikiza Iran kuhusu mpango wake wa makombora na kusema: " Nchi za Ulaya zinapaswa kujizuia kufuata msimamo wa Marekani katika masuala kama vile uwezo wa kujihami wa Iran na uwepo wa Iran katika eneo; hii ni kwa sababu sisi katu hatukubali kuwa Ulaya iko pamoja na utumiaji mabavu wa Marekani."
Mpango wa Iran wa makombora ya kujihami katu hauwezi kutenganishwa na haki ya kisheria ya Iran ya kujihami na ni kwa msingi huu ndio Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikautaja mpango huo kuwa mstari wake mwekundi.
Brigedia Jenerali Hussein Salami Kaimu Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, IRGC, amefafanua zaidi kuhusu nukta hii kwa kusema, kama nchi za Ulaya au mtu mwingine yeyote atajaribu kuendesha njama za kujaribu kuipokonya Jamhuri ya Kiislamu silaha zake muhimu, jambo hilo litaifanya Iran ifikirie kufanya mabadiliko muhimu sana kiistratijia. Aidha amesema uwezo wa makombora ya Iran ni kwa ajili ya usalama wa eneo na amezinasihi nchi za Magharibi zisitafakari kuhusu kuitaka Iran iachane na mpango wake wa makombora ya kujihami.
Haki ya dhati ya kila nchi huru ni kumiliki silaha zinazokubalika kwa ajili ya kujilinda na kukidhi mahitajio yake ya usalama. Kwa mujibu wa haki hii ya dhati, Iran imetegemea wataalamu wa ndani ya nchi na sasa imeweza kupata uwezo mkubwa wa kujihami kwa mujibu wa sheria na itazidi kuimarisha uwezo huo kwa mujibu wa mahitaji yake.
Ahmad Dastmalchian, balozi wa zamani wa Iran nchini Jordan ambaye pia ni mtaalamu wa masuala ya kimataifa anasema: "Uwezo wa kujihami wa kila nchi ni suala la ndani linalohusiana na usalama wa taifa na hivyo hakuna nchi yoyote nyingine yenye haki ya kuingilia masuala ya uwezo wa kujihami wa nchi nyingine na suala la makombora ya kujihami ya Iran linaweza kutazamwa pia katika fremu hiyo.
Kama ambavyo Waziri wa Ulinzi wa Iran alivyoashiria: "Vita vya Iraq dhidi ya Iran vilitufunza kuwa hatuwezi kumtegemea yoyote bali tunapaswa kujitegemea wenyewe kikamilifu."
Brigedia Jenerali Amir Hatami, pia aliwahi kusisitiza huko nyuma kuwa: "Stratijia ya adui ni kudhoofisha uwezo wa kitaifa na uwezo wa kujihami Iran lakini Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katu haitamruhusu yeyote yule atoe pigo kwa nguvu zake za kujihami."
Udharura wa kujihami na usalama unalazimu nchi kuwa tayari kukabiliana na vitisho na kwa msingi huo, kuimarisha uwezo wa kujihami na kumzuia adui ni stratijia isiyoweza kupingika wala kubadilishwa na ni kipaummbele cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
 
chikanu chikali

JF-Expert Member
Aug 29, 2017
1,043

Naona mashetani yamekurudia tena
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom