Mikakati inayokusudiwa kutumiwa kuiangamiza CHADEMA miaka mitano ijayo

Membensamba

Senior Member
Nov 4, 2010
157
10
Chadema kimetokea kuwa chama kikuu cha upinzani Tz. bara, na chachu yake imeamsha upinzani nchini. Hata vyama vingine vya upinzani vimefaidika na chachu hii. Hii sio habari nzuri kwa CCM.

Historia inaonesha kuwa CCM wamekuwa daima wakifanya juhudi za kuminya upinzani kwa nguvu zote kila inapoonekana unaibuka. Miaka mitano ijayo CHADEMA ijue itakabiliana na kila namna ya upinzani toka CCM wenye lengo la kukidhoofisha ili 2015 kisiwe tayari kwa ushindi.

Miongoni mwa mbinu hatari ambazo CCM imekuwa ikizitumia ni pamoja na: Kupandikiza watu wa usalama wa taifa ndani ya upinzani kwa lengo la kuvuruga chama husika ili kionekane kina migogoro machoni pa umma. Hivyo ndiyo NCCR MAGEUZI kilivyoporomoka. Mapandikizi haya kwa hatua ya awali huonekana kuwa msaada mkubwa wa chama, hata kuaminiwa na kupewa nafasi za uongozi chamani, lakini baadaye huanza kuzua migogoro na viongozi wakuu wa vyama hasa yule anayetarajiwa kugombea chaguzi za mbele, ili achafuke machoni mwa umma. Katika hili CHADEMA muwe macho sana, kwani hata sasa mapandikizi yamekwisha wekwa ndani yenu, mfano mzuri ni MARANDO. Msisahau kuwa huyu jamaa ni usalama wa taifa, na ndye alIyehusika na mgogoro mkubwa wa NCCR-MAGEUZI akiwa pamoja na LAMWAI, na MBATIA.

Mbinu nyingine ni kuzinyima ushirikiano wa kifedha halmashauri za upinzani, na majimbo ili yaonekane kuwa hayakufanya vyema, yashindwe chaguzi zijazo. Jipangeni vyema ku-counter hili nalo. Lingine ni kuwagawa wanachadema kwa kuchochea tofauti ndogo ndogo za viongozi na kuzikuz katika vyombo vya habari. Tafadhalini, shikamaneni, mambo kama yale yaliyotokea kati ya Kabwe, na chama yasitokee tena. Shikamaneni, malizeni mambo humo humo chamani. Wabunge, na viongozi mnatazamwa na kusikilizwa sana na umma, JIHADHARINI NA CCM HII.
 
Hiyo inawezekana lakini kwa chadema mtandao wao nimkubwa ukihusika au kuhusishwa nkkitu chochote basi ujue chadema watakuengua ila kwa angalizo lako nadhani watakuwa wameelewa na zaidi watakuwa wanalitambua hilo.
 
Membensamba umetoka angalizo zuri sana!! natamani viongozi na wanachama wote wa chadema walisome na kulielewa!!! tafadhali tuzingatie ushauri huu
 
NCCR Mageuzi haikuwa Chama cha siasa, ulikuwa mkusanyiko wa wanasiasa na ndiyo maana yalitokea yaliyowakuta

Ya NCCR hayawezi kutokea Chadema, kwani chadema. Chadema imeshikama na nadhani hata Zito Kabwe atakuwa anakubaliana na hili maana akileta za kulete yatamkuta ya Aman Kabouruo, David Kafulila na Shaibu Akwiombe
 
Membensamba,
Asante kwa angalizo lako. Kama alivyosema memba mmoja hapa chadema iko imara. Kwa taarifa yako mkakati huo ulikwisha anza siku nyingi baada ya Sisi m kugundua nguvu kubwa waliyonayo Chadema kwa nguvu waliyonayo haikuanza leo. Hili linajulikana lakini Chadema ina uongozi makini na wenye hekima. Ni wepesi kubaini kila mkakati hata kabla haujatenda kazi. Kitengo chao cha ulinzi na usalama ni makini na kina watu ambao ni well trained kwa hayo. Hivyo basi mikakati inayopangwa haitafanikiwa.

Kuhusu mipango ya maendeleo, chadema itahakikisha nguvu ya umma inafanya kazi katika kujiletea maendeleo. Kuna ushahidi kwamba majimbo na halmashauri ambazo ziko chini ya sisi m zimekuwa katika hali mbaya kuliko za vyama pinzani. Serikali ya sisi m ikija na mkakati wa kutojali majimbo yaliyo chini ya upinzani itaangushwa na wananchi wa eneo husika maana hata kura za urais walizopata huenda wasizipate tena. Lakini pia serikali inaweza kuangushwa na wananchi kwa ushirikiano wao.
 
Chadema kimetokea kuwa chama kikuu cha upinzani Tz. bara, na chachu yake imeamsha upinzani nchini. Hata vyama vingine vya upinzani vimefaidika na chachu hii. Hii sio habari nzuri kwa CCM.

Historia inaonesha kuwa CCM wamekuwa daima wakifanya juhudi za kuminya upinzani kwa nguvu zote kila inapoonekana unaibuka. Miaka mitano ijayo CHADEMA ijue itakabiliana na kila namna ya upinzani toka CCM wenye lengo la kukidhoofisha ili 2015 kisiwe tayari kwa ushindi.

Miongoni mwa mbinu hatari ambazo CCM imekuwa ikizitumia ni pamoja na: Kupandikiza watu wa usalama wa taifa ndani ya upinzani kwa lengo la kuvuruga chama husika ili kionekane kina migogoro machoni pa umma. Hivyo ndiyo NCCR MAGEUZI kilivyoporomoka. Mapandikizi haya kwa hatua ya awali huonekana kuwa msaada mkubwa wa chama, hata kuaminiwa na kupewa nafasi za uongozi chamani, lakini baadaye huanza kuzua migogoro na viongozi wakuu wa vyama hasa yule anayetarajiwa kugombea chaguzi za mbele, ili achafuke machoni mwa umma. Katika hili CHADEMA muwe macho sana, kwani hata sasa mapandikizi yamekwisha wekwa ndani yenu, mfano mzuri ni MARANDO. Msisahau kuwa huyu jamaa ni usalama wa taifa, na ndye alIyehusika na mgogoro mkubwa wa NCCR-MAGEUZI akiwa pamoja na LAMWAI, na MBATIA.

Mbinu nyingine ni kuzinyima ushirikiano wa kifedha halmashauri za upinzani, na majimbo ili yaonekane kuwa hayakufanya vyema, yashindwe chaguzi zijazo. Jipangeni vyema ku-counter hili nalo. Lingine ni kuwagawa wanachadema kwa kuchochea tofauti ndogo ndogo za viongozi na kuzikuz katika vyombo vya habari. Tafadhalini, shikamaneni, mambo kama yale yaliyotokea kati ya Kabwe, na chama yasitokee tena. Shikamaneni, malizeni mambo humo humo chamani. Wabunge, na viongozi mnatazamwa na kusikilizwa sana na umma, JIHADHARINI NA CCM HII.

Ni kweli kabisa.
 
Hiyo inawezekana lakini kwa chadema mtandao wao nimkubwa ukihusika au kuhusishwa nkkitu chochote basi ujue chadema watakuengua ila kwa angalizo lako nadhani watakuwa wameelewa na zaidi watakuwa wanalitambua hilo.

Suala hili si la kusema Chadema imejipanga au ina nguvu, ni suala nyeti, takatifu na zito linalopaswa kufanyiwa kazi muda tu baada ya wanamageuzi kupumzika kwa tafakari ya uchaguzi huu kabla ya kuanza kujipanga kwa yajayo.

Pia angalieni sana vyombo vya habari, vinapangwa kwa uchafuzi zaidi. Kama inawezekana moja ya mikakati Chadema au wanamageuzi kwa upana wao wawe na chombo chao si kwa ajili ya propaganda, bali kuwa kitovu cha fikra sahihi na kueleza ukweli wa mambo
 
Nakubaliana nawe lakini kwamba Marando ni pandikizi lina utata. C kwamba kila mwanausalama wa taifa anafurahia kuangamiza nchi yake kwa maslahi ya viongozi wachache. Waliotoa siri za wizi wa kura unaopangwa na JK na swahiba zake ni usalama wa taifa.
NCCR ilianguka sababu aidha kwa udikteta wa Mrema au Mrema mwenyewe kuwa Kibaraka. Unaweza kuona baada ya Mgogoro huo Marando hajang'ang'ania madaraka kama Lipumba, Mrema na Cheyo ila akajitoa kwenye siasa ya vyama na kuendelea na shughuli zake.
Marando alituhumiwa sana na wanamageuzi alipowazidi kete na kuchukua ubunge wa Afrika mashariki alipowatumia wana CCM kumchagua bungeni huku wenzake wakishindwa kugundua huo ujanja mdogo wa kushinda. Kumbuka Marando ni mzuri sana kujieleza na kutoa hata hotuba yenye msisimko mkubwa hivo alivosimama kujieleza alitumia hicho kipaji chake na kutombagua mbunge yeyote awe wa CCM au upinzani. Matokeo yake karibia wote walimpa kura CCM na wapinzani huku washindani wake wakigawana kura chache zilizobaki za wabunge wa upinzani.
Hajawahi kwa namna yoyote kusimama kwa upande wa watawala kama vibaraka wengine kama Mrema, mbatia na Kaburu wanavofanya bali amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali na kutetea mageuzi.
CHADEMA naamini tunamwitaji marando sana ila ni vizuri kumfundisha kuwa na lugha nzuri na ya ustaarabu kama Dr Slaa.

Angalizo lako ni muhimu. Cha muhimu ni kuanza kukijenga chama na kufungua matawi. Tujiunge wotw kuchangia chadema kifedha, kutoa habari muhimu kama tuko karibu na viongozi wanaotukandamiza au kueneza ujumbe wa mageuzi kwa kila mtanzania.
 
Nimeamua kuitumikia chadema kwa kufungua matawi na kuhakikisha yanastawi hapa nilipo. Si unajua hata huku ulaya tunaruhusiwa kufungua matawi ya vyama vyenu waafrika? Matunda tutaanza kuyaona 2014 mtu asinikatishe tamaa. Na hili nitalifanya kwa nguvu zangu zote na mali zangu zote. Mungu nisaidie.
 
Daah! ninanamba ya rafiki yake na Mbowe nimemwambia awasiliane na Mbowe ili apate meseji hii.
Wazo zuri, Gudi saana,
 
Chadema kimetokea kuwa chama kikuu cha upinzani Tz. bara, na chachu yake imeamsha upinzani nchini. Hata vyama vingine vya upinzani vimefaidika na chachu hii. Hii sio habari nzuri kwa CCM.

Historia inaonesha kuwa CCM wamekuwa daima wakifanya juhudi za kuminya upinzani kwa nguvu zote kila inapoonekana unaibuka. Miaka mitano ijayo CHADEMA ijue itakabiliana na kila namna ya upinzani toka CCM wenye lengo la kukidhoofisha ili 2015 kisiwe tayari kwa ushindi.

Miongoni mwa mbinu hatari ambazo CCM imekuwa ikizitumia ni pamoja na: Kupandikiza watu wa usalama wa taifa ndani ya upinzani kwa lengo la kuvuruga chama husika ili kionekane kina migogoro machoni pa umma. Hivyo ndiyo NCCR MAGEUZI kilivyoporomoka. Mapandikizi haya kwa hatua ya awali huonekana kuwa msaada mkubwa wa chama, hata kuaminiwa na kupewa nafasi za uongozi chamani, lakini baadaye huanza kuzua migogoro na viongozi wakuu wa vyama hasa yule anayetarajiwa kugombea chaguzi za mbele, ili achafuke machoni mwa umma. Katika hili CHADEMA muwe macho sana, kwani hata sasa mapandikizi yamekwisha wekwa ndani yenu, mfano mzuri ni MARANDO. Msisahau kuwa huyu jamaa ni usalama wa taifa, na ndye alIyehusika na mgogoro mkubwa wa NCCR-MAGEUZI akiwa pamoja na LAMWAI, na MBATIA.

Mbinu nyingine ni kuzinyima ushirikiano wa kifedha halmashauri za upinzani, na majimbo ili yaonekane kuwa hayakufanya vyema, yashindwe chaguzi zijazo. Jipangeni vyema ku-counter hili nalo. Lingine ni kuwagawa wanachadema kwa kuchochea tofauti ndogo ndogo za viongozi na kuzikuz katika vyombo vya habari. Tafadhalini, shikamaneni, mambo kama yale yaliyotokea kati ya Kabwe, na chama yasitokee tena. Shikamaneni, malizeni mambo humo humo chamani. Wabunge, na viongozi mnatazamwa na kusikilizwa sana na umma, JIHADHARINI NA CCM HII.
Mfano mwingine ni watu kama nyie kujifanya mnaishari Chadema, kwa hiyo Chadema ijihadhari sana.
 
CHADEMA should not underestimate this advice. Kweli CCm wamekuwa wakijitahidi saaana kuingiza mamluki. Vile vile kuna wanachama waliojiunga wakati wa kampeni lengo lilikua ni kupata info za ndani ya CHADEMA nao waangaliwe kwa umakini wa hali ya juu kabla ya
ya kuwapatia majukumu makubwa yanayoweza kukiangusha chama pale yanapotoshwa kwa makusudi ili kuleta mfarakano kwenye chama.
 
Nimeamua kuitumikia chadema kwa kufungua matawi na kuhakikisha yanastawi hapa nilipo. Si unajua hata huku ulaya tunaruhusiwa kufungua matawi ya vyama vyenu waafrika? Matunda tutaanza kuyaona 2014 mtu asinikatishe tamaa. Na hili nitalifanya kwa nguvu zangu zote na mali zangu zote. Mungu nisaidie.

asante sana mkuu. Vita baridi inaendelea kuikomboa TZ
 
Na ndo lengo la CCM namba moja kuhakikisha CHADEMA does not prosper towards 2015
 
Kura yangu nilimpa Dr Slaa baada ya kugundua kuwa mitandao ya simu hasa vodacom walikuwa wanatuibia watu wa kawaida kwa ajili ya kampeini zao. Mimi ni mwana ccm kabisa. Tatizo linalonikabili sasa ni dhamiri yangu hasa baada ya kuona yaliyofanywa na chama changu dhidi ya ukweli na haki. Ninapenda sana haki na kuitetea popote sasa najiuliza nimeze pini nirudi katika chama changu yataisha au nikate moja kwa moja kadi ya upinzani. je niweke mawazo yangu wazi au niendelee kimya kimya. Kuna wengi kama mimi. Siku za nyuma tuliamini kila tuliloambiwa kuhusu vyama vya upinzani hasa vurugu, uroho wa madaraka n.k Zamu hii nimeng'amua wazi nani mwenye shida hii KUMBE NI CHAMA CHANGU. Sijui kama wananchi wengine wakiligundua hili wataendelea kukubali propoganda za siku za nyuma kuhusu vyama vya upinzani!!!! MMMhhh UKWELI NI KUWA UPINZANI SASA UNAANZA KUWA MTIHANI MGUMU KWA CCM MAANA WANANCHI WA LEO SIO WA JANA.
 
Chadema ni chama kilikosa mvuto wa kitaifa na kitakufa karibuni kama kuna chama mbadala basi ningesema cuf alau kina mtazamo wa kitaifa

chama cha cuf kina wabunge sehemu zote kuu za jamhuri ya muunganlo:

Kina wabunge toka pemba

kina wabunge toka unguja ( pemba na unguja inaunda jamhuri ya watu wa zanzibar)

kina wabunge tanzania bara (ambayo inaunda jamhuri ya tanganyika)

chadema kimejionyesha kua ni chama hatari na ndio maaana wazanzibari kwanza hawakikubali

ni chama ambacho kimejikita katika ubaguzi na kubaguana na kueka udini kwa sana

ni chama hatari kwa taifa na wananchi weshaliona na watazidi kuliona

nnaona mwisho wa chadema uko karibu sana
 
naona mwisho wa chadema uko karibu sana
Pointless,! eti zanzibar hawakubali Chadema, kwa mtazamo kama wako , wazanzibar ndio wadini basi kwa sababu wao wanataka CUF ambayo walianzisha wao tuu (CUF inawafaa wazanzibar). Kama unataka tawala Tanzania kula laki nne za Zanzibar hazina maana yeyote, ndio maana hazikumsaidia hata Lipumba kupata japo 10%. Kula za Zanzibar ni kama za Wilaya 3 za Mbeya.
 
Back
Top Bottom