Mikakati inayokusudiwa kutumiwa kuiangamiza CHADEMA miaka mitano ijayo

Hakuma lolote... Chadema imeweza na kitaweza, Hata kabwe anaweza hamia NCCR kama alivyoweza kuwasimika washikaji wake huko ... Chadema ni mtandao wa mageuzi Tanzania, Viongozi wasaliti na wanafiki watajiengua wenyewe...
 
Chadema ni chama kilikosa mvuto wa kitaifa na kitakufa karibuni kama kuna chama mbadala basi ningesema cuf alau kina mtazamo wa kitaifa

chama cha cuf kina wabunge sehemu zote kuu za jamhuri ya muunganlo:

Kina wabunge toka pemba

kina wabunge toka unguja ( pemba na unguja inaunda jamhuri ya watu wa zanzibar)

kina wabunge tanzania bara (ambayo inaunda jamhuri ya tanganyika)

chadema kimejionyesha kua ni chama hatari na ndio maaana wazanzibari kwanza hawakikubali

ni chama ambacho kimejikita katika ubaguzi na kubaguana na kueka udini kwa sana

ni chama hatari kwa taifa na wananchi weshaliona na watazidi kuliona

nnaona mwisho wa chadema uko karibu sana

Chadema ni chama hatari sana kwa ccm na si kwa taifa kwa kuwa kinawapa ukweli wananchi jambo ambalo ccm hawawezi hata kidogo. Kwa upande wa zanzibar, tatizo na waznz wenyewe, wamejaa udini na ndo maana wamejaa umaskini, na wataendelea kuwa hivyo. Chadema kilitumia busara sana kumuunga mkono Seif kama mgombea uraisi znz, lakini hakuna hata mwana-cuf aliyesimama kupongeza hilo. Ukiunga mkono cuf na ccm, ujue umeunga mkono umaskini.
 
CHADEMA should not underestimate this advice. Kweli CCm wamekuwa wakijitahidi saaana kuingiza mamluki. Vile vile kuna wanachama waliojiunga wakati wa kampeni lengo lilikua ni kupata info za ndani ya CHADEMA nao waangaliwe kwa umakini wa hali ya juu kabla ya
ya kuwapatia majukumu makubwa yanayoweza kukiangusha chama pale yanapotoshwa kwa makusudi ili kuleta mfarakano kwenye chama.
I think Chadema is beyond that. CCM imeshachelewa, moto umeshawashwa, kuuzima inahitaji nguvu kubwa kuliko kuzima moto wa California. Chadema ina wazee wenye busara, na hawa ndio wanaoifanya Chadema ishinde majaribu ya CCM. Kumbukeni msuguano wa Zito na Mbowe kwenye nafasi ya uenyekiti, Zito alitumika, lakini sense zikamrudia baada ya wazee wa Chadema kutumia busara kumtuliza.

Kuhusu kuzinyima Halmashauri fedha, hilo haliwezekani, kwa taarifa yako Halmashauri zenye wapinzani zimefanya vizuri zaidi kuliko zile ambazo hazina kwa sababu wapinzani wamekuwa kama check and balance.

Nadhani kitu muhimu kwa Chadema sasa ni kuunda organizesheni ya propaganda, ikiwezekana wawe na kituo cha TV yao, ambayo itakuwa inaiponda CCM na serekali ya JK kwa kila inachokifanya. Hiyo strategy imefanikiwa kummaliza nguvu Obama kule US, Republican wanaitumia Fox News kummaliza Obama na Democrat. Chadema wafungue TV station asp, iwe na kazi moja tu muhimu, kuipiga madongo CCM na Serekali ya JK kwa kila kitu inachokifanya, kwa mfano JK akienda nje ya nchi, waponde safari hizo kwa kuanisha gharama za safari na nini manafuaa kama yatakuwepo, akiteau mtu, wapige critic kucheck facts za huyo mteule na kuuponda uteuzi wake, yaani wamnyime raha JK na serekali yake. .
 
watajiua wenyewe, acha kuwafanya chadema ni vitoto vidogo, waswahili bwana!!
 
1. CHADEMA KIMESHINDWA UCHAGUZI, KIKUBALI.

2. CHADEMA INABIDI KIJISAFISHE NA KITAKATE, kwani kutumia barua ya kuchakachua ili kutoa TUHUMA NZITO ni kudhihirisha umakini mchache; haiwezekani kutumia Barua ya kuchakachua na kuiwasilisha NEC au popote pale kama ushahidi. Chadema itakufa natural death if corrective measures hazitochukuliwa na Chama hicho; ikiwemo:-

(a) Kutambua matokeo ya Uchaguzi na kumtambua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni kinyume na utawala wa sheria kwa mtu, kikundi au taasisi kutotambua uongozi wa mamlaka nchini.

(b) kukubali kushindwa ili kuheshimu demokrasia.

(c) Kuomba radhi Watanzania kwa kosa la kuwadanganya kwa kutumia barua iliyochakachuliwa.

(d) Kuwaambia wafuasi wake kuwa fujo na vurugu sio vitissho vitakavyowafanya watanzania waogope kupiga kura kufanya uchaguzi wanaoutaka.
 
(e) Kuingia kwenye uchaguzi wakijua NEC ni ya CCM! hivyo walilijua kabla!!!! (kalagabhao)
 
Chadema ni chama kilikosa mvuto wa kitaifa na kitakufa karibuni kama kuna chama mbadala basi ningesema cuf alau kina mtazamo wa kitaifa

chama cha cuf kina wabunge sehemu zote kuu za jamhuri ya muunganlo:

Kina wabunge toka pemba

kina wabunge toka unguja ( pemba na unguja inaunda jamhuri ya watu wa zanzibar)

kina wabunge tanzania bara (ambayo inaunda jamhuri ya tanganyika)

chadema kimejionyesha kua ni chama hatari na ndio maaana wazanzibari kwanza hawakikubali

ni chama ambacho kimejikita katika ubaguzi na kubaguana na kueka udini kwa sana

ni chama hatari kwa taifa na wananchi weshaliona na watazidi kuliona

nnaona mwisho wa chadema uko karibu sana

Keep on dreaming and you might not wake up.
 
Miaka hii mitano itakuwa na hujuma nyingi sana na hapa inawapasa vijana kama Zitto et al ndani ya CHADEMA waachane na utoto vinginevyo yatawakuta kama ya NCCR Mageuzi baada ya 1995
 
Mambo mengine mtu unatakiwa ufikiri kabla ya kuandika,ungekuwa si mbaguzi wala usingeleta ya unguja na pemba,wala zanzibar na bara,wala uislam na ukristo.swala chama fulani kiko wapi zaidi inategemea uanzishwaji wake,sehemu ambapo kimepata wafuasi wengi n.k.Lakini mwisho wa siku wanachama wake ni watanzania na ni chama cha watanzania.Kama kila mtu ana haki ya kujiunga na kushiriki katika shughuli za chama,na hakuna sera za kibaguzi katika kujiunga na kuhudumia jamii iweje mkiite cha kibaguzi.Nyie watu mnaoongelea ubaguzi na kutugawanya sijui mna mpango gani hata ccm imetumia sana aina hiyo ya maneno kukipaka matope kitu ambacho hakipo.Watanzania tuwe wamoja kuwapiga vita wanaotugawa na hawa ni maadui wetu wakubwa.
 
huu ni usahauri murua kabisa,mwenye masikio asikie,na mwenye macho basi ajionee mwenyewe:doh:
 
Back
Top Bottom