Membensamba
Senior Member
- Nov 4, 2010
- 157
- 10
Chadema kimetokea kuwa chama kikuu cha upinzani Tz. bara, na chachu yake imeamsha upinzani nchini. Hata vyama vingine vya upinzani vimefaidika na chachu hii. Hii sio habari nzuri kwa CCM.
Historia inaonesha kuwa CCM wamekuwa daima wakifanya juhudi za kuminya upinzani kwa nguvu zote kila inapoonekana unaibuka. Miaka mitano ijayo CHADEMA ijue itakabiliana na kila namna ya upinzani toka CCM wenye lengo la kukidhoofisha ili 2015 kisiwe tayari kwa ushindi.
Miongoni mwa mbinu hatari ambazo CCM imekuwa ikizitumia ni pamoja na: Kupandikiza watu wa usalama wa taifa ndani ya upinzani kwa lengo la kuvuruga chama husika ili kionekane kina migogoro machoni pa umma. Hivyo ndiyo NCCR MAGEUZI kilivyoporomoka. Mapandikizi haya kwa hatua ya awali huonekana kuwa msaada mkubwa wa chama, hata kuaminiwa na kupewa nafasi za uongozi chamani, lakini baadaye huanza kuzua migogoro na viongozi wakuu wa vyama hasa yule anayetarajiwa kugombea chaguzi za mbele, ili achafuke machoni mwa umma. Katika hili CHADEMA muwe macho sana, kwani hata sasa mapandikizi yamekwisha wekwa ndani yenu, mfano mzuri ni MARANDO. Msisahau kuwa huyu jamaa ni usalama wa taifa, na ndye alIyehusika na mgogoro mkubwa wa NCCR-MAGEUZI akiwa pamoja na LAMWAI, na MBATIA.
Mbinu nyingine ni kuzinyima ushirikiano wa kifedha halmashauri za upinzani, na majimbo ili yaonekane kuwa hayakufanya vyema, yashindwe chaguzi zijazo. Jipangeni vyema ku-counter hili nalo. Lingine ni kuwagawa wanachadema kwa kuchochea tofauti ndogo ndogo za viongozi na kuzikuz katika vyombo vya habari. Tafadhalini, shikamaneni, mambo kama yale yaliyotokea kati ya Kabwe, na chama yasitokee tena. Shikamaneni, malizeni mambo humo humo chamani. Wabunge, na viongozi mnatazamwa na kusikilizwa sana na umma, JIHADHARINI NA CCM HII.