Mikakati 10 ya Mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali inanvyogusa makundi mbalimbali ya jamii Nchini

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
295
679
Bajeti iliyowasilishwa ni TZS Trilioni 41.48 ikiwa ni ongezeko la 9.2% ukilinganisha na mwaka jana. Sehemu kubwa ya bajeti hii inategemea fedha za ndani (kwa zaidi ya 67%, hili ni jambo la kihistoria na la kipekee).

Baada ya uwasilishwaji wa Bajeti ya mwaka 2022/23, wananchi wengi wameonyesha kufurahishwa na mipango ya serikali inayolenga kuboresha maisha ya mtu mmoja mmoja na ustawi wa Taifa kwa ujumla, baadhi ya maeneo ni misamaha ya kodi kama vile;

1. Kupunguza tozo katika miamala ya simu katika kutuma na kupokea fedha kwa zaidi ya 40%. (Tozo ya juu kabisa itapungua kutoka 7000 hadi 4000).

2. Kupunguza kodi(With holding tax) katika Tasnia ya Filamu kutoka 15% hadi 10%.

3. Kuondoa kodi (Zero rating) kwa bidhaa za mafuta ya kula (edible oils)

4. Kuondoa kodi (Zero rating) kwa mbolea inayozalishwa hapa nchini na vifaa mbalimbali vinavyotumika katika kupima udongo, net zinazotumika katika kilimo cha maua na mbogamboga pia vifaa vingine vinavyotumika katika horticulture.

5. Kuondolewa kwa kodi katika malighafi zinazotumika kutengeneza mitungi ya gas hapa nchini.

6. Kuondolewa kwa kodi zinazohusisha vifaa/mahitaji muhimu ya viwanda vya usindikaji wa nyama, maziwa na samaki.

7. Kuhakiki madai ya ritani za VAT kidijitali. Hii itawezesha sekta binafsi kupewa stahiki za madai yao kwa wakati.

8. Kutambuliwa rasmi kwa njia mbadala za kifedha. Hii itaongeza ujumuishi katika huduma za kifedha kwa wananchi.

9. Asilimia 5 ya mapato ya Halmashauri kutumika kuboresha miundombinu ya wajasiriamali.

10. Kuondolewa kwa kodi katika mahitaji ya wakulima kama vile mbegu.

Hii ni baadhi ya misamaha na punguzo zilizowekwa katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kustawisha maisha ya wananchi, kuchochea shughuli za uzalishaji mali na kukuza uchumi wa Taifa letu. Hongera Rais Samia kwa uongozi thabiti.
 
Back
Top Bottom