Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,658
- 20,889
Nilikuws nasoma stori moja kuhusu Shanghai, Shanghai ni moja ya miji yenye watu wenye elimu ya kieango cha juu sana. Watoto wa shule za msingi walivyopimwa uwezo wa hesabu na sayansi walikuww ni moja ya wanafunzi bora duniani.
Watu kotoka miji ya ndani ya China walikuwa wwnatamani watoto wao wakasome Shanghai. Ilifika kipindi mamlaka za mji zikaweka sheria za watu wasio wa Shanghai kutosoma hapo maana shule zilikuwa zinazidiwa.
Kwa Dar ni tofauti sana, kihistoria watu walikuwa wanatoka Dar na kwenda kusoma mikoani. Dar ina shule shule chache sana. Fikiria Dar yenye wakazi zaidi ya 6m ina shule za sekondari zenye class size ya 40+ kama 240. Kilimanjaro yenye watu 2m na kidogo ina Shule kama hizo 275!. Ili Dar walau iwe na standard za kilimanjaro ilitakiwa kuwa na kama shule 800 hivi.
Kihistoria Dar huwa haifanyi vizuri kwenye matokeo ya shule za msingi, wala sekondari. Ukiachana na elimu ya chuo kikuu, huwezi kumsikia mtu wa mkoani eti anaenda Dar kufuata elimu bora. Kwanini huu mji upo tofauti na miji mingine mikubwa duniani? Wafanye nini ili walau wafikie Standard za Kilimanjaro?.