Mijadala ya Mawazo na Michanganuo mbalimbali ya Biashara na Uchumi kwa Ujumla

Wadau naomba ushauri kwa mtaji wa laki mbili naweza Fanya kitu gani ili niweze kukidhi mahitaji mbalimbali katika maisha, eneo nililopo ni Mara-Tarime.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nunua birika tano zile za kuuzia kahawa,tafuta vijana watano wakabizi hizo birika wauze kahawa maeneo ya mikusanyiko ya watu,baada ya hapo anza kuhesabu faida.
 
naombeni idea ya biashara ambayo ninaweza nikaanza na mtaji ambao mtu wa hali ya kawaida anaweza akaaford


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nimeahidiwa mkopo wa 2m kwa riba ya 5% ambao nitatakiwa kuulipa kwa miezi 6. Kabla sijaenda kuuchukua nimeona ni vema nikaja humu kuomba ushauri kwa great thinkers mnisaidie ushauri kutokana na uzoefu wenu ni biashara gani nikifanya nitakidhi terms za mkopo? Ninamtanguliza shukrani zangu za dhati..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeahidiwa mkopo wa 2m kwa riba ya 5% ambao nitatakiwa kuulipa kwa miezi 6. Kabla sijaenda kuuchukua nimeona ni vema nikaja humu kuomba ushauri kwa great thinkers mnisaidie ushauri kutokana na uzoefu wenu ni biashara gani nikifanya nitakidhi terms za mkopo? Ninamtanguliza shukrani zangu za dhati..

Sent using Jamii Forums mobile app
Mm nazani ungesema upo maeneo gani ili uweze kushaurika kulingana na aina ya biashara utakayoshauriwa na wanajamvi hapa wkt wa uchangiaji mada kulingana na mazingira uliopo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fanya ufugaji wa kuku wa kisasa ila tafuta elimu yake maana ukikosea kidogo itakulamba pesa yote
 
Samaki wa kukaanga wanalipa sana mkuu, hasa huku Mtoni, Mtongani.
 
Inategemea upo maeneo gani. Mjini au Kijijini? Kuna fursa gani? Kama ni Mjini anza Biashara ya mtumba (maana mtumba utavaliwa sana kwa hali hii ya Uchumi).
 
Habari zenu Wandugu! Nimekuja hapa kuomba ushauri wa Biashara ya Kufanya kwa Mtaji wa mil 1 ambayo itazalisha Zaidi pamoja na Changamoto zake. Asanteh.

Sent using Jamii Forums mobile app
Fungua account ya kutrade FOREX kwa blocker Templer, weka huo mtaji then nitumie accounts detail nimanage accnt... Profit tunashare 50/50 weekly


Kwa huo mtaji profit ni Tsh300000 kila wiki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom