Mijadala ya Bajeti Bungeni iko Live, Kumekucha kimya kimya?

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,227
35,151
Mabibi na mabwana ITV wanaonekana live bungeni na mijadala ya bajeti inaendelea. Mambo sasa mwendo mdundo!

Kulikoni?

Itakuwa yale mambo yetu ya bunge live yamerejeshwa kimya kimya au ni kwa bajeti hii ya Mwigulu peke yake?

Je, au ndiyo rasmi kuwa yale ya watu kufanya kazi badala ya kuangalia mambo ya bunge sasa ndiyo basi?

Au je, pengine mabadiliko haya ni kwa sababu waliokuwa wanatuchelewesha kimaendeleo hawapo tena bungeni?

Au labda ni katika yale ya moto moto yajayo ya awamu ya sita ya mama Samia Suluhu rais wetu wa JMT kazi inapoendelea?

Si kuwa ilikuwa vyema ikajulikana kama huu ndiyo ulio msimamo mpya na kwa uwazi?

Ninawasilisha.
 
Nimejaribu kuangalia, nimeshindwa! Kiukweli Bunge la sasa halina kabisa mvuto.

Mbunge mmoja anataka kodi ya jengo kuhusianishwa na matumizi ya umeme kwa units.

Maajabu mengine ya Mussa. Nyumba ikiwa na leakage kwenye umeme kama failure ana ufahamu wowote na mambo hayo?
 
njaa mbaya sana mnalalamika nini sasa kwani hata mlipokuwepo bungeni mlifanya nini zaidi yakuwa mnajitahidi kupinga kila kitu sasa ndiyo wanaume wapo kazini sasa kuipangia nchi mambo mema
 
Kwa hiyo sasa watu wanafanya kazi saa ngapi?
 
Mabibi na mabwana ITV wanaonekana live bungeni na mijadala ya bajeti inaendelea. Mambo sasa mwendo mdundo!

Kulikoni?

Itakuwa yale mambo yetu ya bunge live yamerejeshwa kimya kimya au ni kwa bajeti hii ya Mwigulu peke yake?

Je, au ndiyo rasmi kuwa yale ya watu kufanya kazi badala ya kuangalia mambo ya bunge sasa ndiyo basi?

Au je, pengine mabadiliko haya ni kwa sababu waliokuwa wanatuchelewesha kimaendeleo hawapo tena bungeni?

Au labda ni katika yale ya moto moto yajayo ya awamu ya sita ya mama Samia Suluhu rais wetu wa JMT kazi inapoendelea?

Si kuwa ilikuwa vyema ikajulikana kama huu ndiyo ulio msimamo mpya na kwa uwazi?

Ninawasilisha.
Vipi yule Mbunge wa Uwele aliyekuwa Waziri nyakati hizo alipinga bunge live mpaka mishipa inamsimama na mate kumtoka kama cobra naye amekubali kuonekana runingani?
 
Nadhani hii U turn ni katika kumalizana na yenye ukakasi tokea kwake wakulungwa.
 
Ni muhimu wananchi nao wakafuatilia mijadala live...

Acha mama aendelee ku strike points. Maana approval rates zake zinaendelea kupaa siku hadi siku.

Atakapofika kwa akina Mdude nani ataikumbuka tena awamu ile nje ya ile misukule yenyewe kweri kweri?
 
Kama wameamua kuwa live iwe kwa mujibu wa sheria, isiwe kwa matakwa ya watu wachache... maana huko mbele tukifanikiwa kumpata shujaa mwingine ataliondoa tu na kutuchanganya.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom