Miili ya watu saba waliokufa mto Ruvu

Swelana

JF-Expert Member
Sep 24, 2016
412
1,000
Wananchi tunahitaji kujua suala la miili ya watu saba waliokotwa mto ruvu.
Mh mwigulu nchemba alinukuliwa na vyombo vya habari kwamba miili hiyo ni ya wahamiaje bado tunataka kujua yeye alijuaje kwamba ni wahamiaji?
Hata kama ni wa wahamiaji ilikuaje wafungwe kwenye viroba na mawe na kisha kutumbukizwa mtoni?
Suala la mmiliki wa mtandao wa jamii forum limetufanya kusahau kuhoji suala hili kitu ambacho sio sahihi.
Ikumbukwe mpaka sasa haijafahamika wapi alipo Ben sanane labda akiwa hai au amekufa sasa ni lazima tujue kama labda na yeye ni miungoni mwa hao miili saba ya mto ruvu kama mhamiaji haramu au la.
Watanzania tujipambanue sasa,kuna watu wanatumia matukio kusahaulisha matukio mengine.
Waziri mkuu ktk sikuu ya maulid alisema kwamba serikali ichunguze kuhusu hiyo miili saba,je uchunguzi umefikia wapi?na je uchunguzi huo unafanywa na tume huru?
Kumewahi kuuwa watu kwenye mkutano wa chadema arusha baada ya kurushwa bomu na watu ambao mpaka sasa hawajulikani sasa ninaliona na hili likipotea hivi hivi.
Wanaouawa au kupotea ktk mazingira ya kutatanisha ni ndugu zetu,unaweza chukulia kawaida ila siku likifika ktk familia yenu ndio utajua uchungu,tupaze sauti kupinga wenzetu kutishiwa amani na kuuawa kwa tofauti za kivyama,hii nchi ni yetu sote na kila mtu ataiacha.
Tunamhitaji Beni sanane akiwa hai na tutaendelea kupaza sauti zetu.

[HASHTAG]#Maxaachiwehuru[/HASHTAG]
[HASHTAG]#HakikwaGodblesslema[/HASHTAG]
[HASHTAG]#TunamtakaBensananeakiwahai[/HASHTAG].

Swelana.
 

Werrason

JF-Expert Member
Nov 5, 2014
12,335
2,000
Hii ishu ya Max kweli imekuja kusahaulisha hao Maiti, Kwanini wasingeonyeshwa na je wamezikwa wapi?

Wasijeenda ihamisha!!!

Ikumbukwe damu yao haitawaacha Salama


[HASHTAG]#BringBackBenAlive[/HASHTAG]
 

Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
21,676
2,000
sure mkuu tunataka mrejesho ktk hili na serikali itwambie ukweli sio kusema kwamba wahamiaji haramu.. na pia watwambie bensa8 yupo wapi?
[HASHTAG]#BringBackBenAlive[/HASHTAG]
 

Maga

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
329
225
Kuna wakati huwa nawaza kwanini huwa tunapenda kutoa majibu mepesi kwa maswali magumu? Je ni kwamba hatuna muda wa kufanya utafiti kidogo au huwa hatutaki kusumbua akili zetu
 

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,047
2,000
Tena kwa kauli nyepesi sana.. "Wale ni wahamiaji haramu..!", Kwani ni mbuzi wale?

Halafu mnataka mpewe urasi wa Nchi..!!
 

Mdudu halisi

JF-Expert Member
May 7, 2014
2,730
2,000
Hivi kwanini huyu malaika wetu asishitakiwe kule the Hague, kwa maana dollar yake imekithiri kwa vitendo vya uhalifu dhidi ya binadamu.
 

dyngrey

New Member
Dec 17, 2016
2
20
Kwanza wanaleta utata....kwann hawakuichunguza miili yote kabla ya kufukiwa na sio hata kuzikwa...wanatuonyesha nn?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom