Miili ya watu 9 waliokufa maji wakivuka Mto Ruvuma bado haijapatikana


Pistol

Pistol

Senior Member
Joined
Oct 13, 2015
Messages
184
Likes
66
Points
45
Pistol

Pistol

Senior Member
Joined Oct 13, 2015
184 66 45
Miili ya watu tisa waliokufa maji wakivuka Mto Ruvuma kutoka Mkenda Wilayani Songea kwenda Mitomoni Wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma wakitokea Mkenda kwenye mnada bado haijapatikana.

Wananchi wanaoshiriki zoezi la kutafuta watu waliokufa maji wanasema wanakwazwa na vifaa vya uokaji ambapo wametega nyavu mita kadhaa kutoka waliko zama watu hao tisa ili wakwame baada ya kukokotwa na maji.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Hassan Bendeyeko amepongeza jitihada za wananchi kufanikisha kuokoa watu 36 na kwamba uzoefu unaonyesha watu wanaokufa maji miili yao huanza kuonekana baada ya siku tatu.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dokta Binilith Mahenge ameelekeza kuwa jitihada za kutafuta miili ya watu waliozama Mto Ruvuma ziendelee na kwamba jitihada zinafanyika ili kupatikana vifaa vya kusaidia kutafuta miili hiyo.


Chanzo: ITV
 

Forum statistics

Threads 1,235,884
Members 474,808
Posts 29,239,483