Miili ya wanajeshi 14 wa Tanzania imewasili muda huu katika uwanja wa ndege wa Jeshi la wananchi JWTZ.
=>Miili imewasili kupitia ndege ya UN
=>Wanajeshi wamejitanda uwanjani tayari kupokea miili
=>Wapo maafisa waandimizi wa wizara ya ulinzi akiwemo waziri wa ulinzi Husein Mwinyi
=>Miili inaanza kutolewa kwenye ndege
=>Miili hii inaenda kufanyiwa uchunguzi(postmotum) na kuhifadhiwa katika hospitali ya jeshi Lugalo.
Waziri wa Ulinzi Mh Hussein Mwinyi;
=>Tumepokea kwa masikitiko makubwa vifo vya wanajeshi wetu 14 na leo tupo hapa kuwapokea na tutawaaga rasmi siku ya alhamis katika viwanja vya ulinzi.
=>Hili ni tuki ambalo ni la kushtukiza ni ambush. Tumesikitika kwa tukio hili
=>Jeshi letu lipo imara na linafanya kazi kwa weledi mkubwa. Umoja wa mataifa nao wamesikitika na kuhuzunisha. Matukio kama haya huwa yanatokea ni mategemeo yetu kwamba kila juhudi zitachukuliwa ili yasitokee tena.
=>Tunawapa pole ndugu wote waliopoteza ndugu na msiba huu sio wao peke yao bali wetu sote.
Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo;
=>Matukio haya ni sehemu ya mapambano
=>Wale 44 hali zao zinaendelea vizuri; Kuna wengine wako Goma, wengine hali zao siyo nzuri sana wamepelekwa Kinshasa na wengine wamepelekwa Uganda kwa ujumla wanaendelea vizuri.
Kuhusu wale wanajeshi wawili waliokuwa wamepotea mmoja ameshapatikana na mwingine bado anatafutwa.