Miili ya wanajeshi 14 waliouawa DRC yawasili katika uwanja wa ndege wa jeshi, kuagwa Lugalo Alhamis Desemba 14

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,692
2,000
WhatsApp Image 2017-12-11 at 17.43.31.jpeg

Miili ya wanajeshi 14 wa Tanzania imewasili muda huu katika uwanja wa ndege wa Jeshi la wananchi JWTZ.

=>Miili imewasili kupitia ndege ya UN

=>Wanajeshi wamejitanda uwanjani tayari kupokea miili

=>Wapo maafisa waandimizi wa wizara ya ulinzi akiwemo waziri wa ulinzi Husein Mwinyi

=>Miili inaanza kutolewa kwenye ndege

=>Miili hii inaenda kufanyiwa uchunguzi(postmotum) na kuhifadhiwa katika hospitali ya jeshi Lugalo.

Waziri wa Ulinzi Mh Hussein Mwinyi;

=>Tumepokea kwa masikitiko makubwa vifo vya wanajeshi wetu 14 na leo tupo hapa kuwapokea na tutawaaga rasmi siku ya alhamis katika viwanja vya ulinzi.

=>Hili ni tuki ambalo ni la kushtukiza ni ambush. Tumesikitika kwa tukio hili

=>Jeshi letu lipo imara na linafanya kazi kwa weledi mkubwa. Umoja wa mataifa nao wamesikitika na kuhuzunisha. Matukio kama haya huwa yanatokea ni mategemeo yetu kwamba kila juhudi zitachukuliwa ili yasitokee tena.

=>Tunawapa pole ndugu wote waliopoteza ndugu na msiba huu sio wao peke yao bali wetu sote.

Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo;

=>Matukio haya ni sehemu ya mapambano

=>Wale 44 hali zao zinaendelea vizuri; Kuna wengine wako Goma, wengine hali zao siyo nzuri sana wamepelekwa Kinshasa na wengine wamepelekwa Uganda kwa ujumla wanaendelea vizuri.

Kuhusu wale wanajeshi wawili waliokuwa wamepotea mmoja ameshapatikana na mwingine bado anatafutwa.
 

ngudengude

JF-Expert Member
Jul 2, 2015
1,178
1,500
Wanajesh 14 ni wengi sana ..tunaambiwa 44 wanejeruhiwa vibaya...sasa walikuwa wamelala ama vip
itakuwa wali relax na kuweka ulinzi mdogo wa kujihami. Pia inawezekana waasi walisha wa study kwa kina, idadi yao wapo wangapi? wana siraha gani za kujilinda na taadhari yao ipoje? kwa hiyo wakawavamia kwa wingi na silaha nzitonzito walizoshindwa kumudu. UN inatakiwa ilinde askari wetu au la tuwarudishe nyumbani. Maana japo ni wa tz lakini kule wapo chini ya maagizo ya UN, kwaiyo UN iengeze ulinzi na intelijensia ya eneo la kuweka kambi kabla na baada ya kuwaweka askari wetu hapo.
 

mjingamimi

JF-Expert Member
Aug 3, 2015
25,837
2,000
itakuwa wali relax na kuweka ulinzi mdogo wa kujihami. Pia inawezekana waasi walisha wa study kwa kina, idadi yao wapo wangapi? wana siraha gani za kujilinda na taadhari yao ipoje? kwa hiyo wakawavamia kwa wingi na silaha nzitonzito walizoshindwa kumudu. UN inatakiwa ilinde askari wetu au la tuwarudishe nyumbani. Maana japo ni wa tz lakini kule wapo chini ya maagizo ya UN, kwaiyo UN iengeze ulinzi na intelijensia ya eneo la kuweka kambi kabla na baada ya kuwaweka askari wetu hapo.
Mwanajeshi alindwe?
 

Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
10,910
2,000
Ndio tujifunze......tuko vitani na wapinzani wetu vitani ni majirani zetu ambao eti ghafla ni marafiki wa kutusaidia mawazo kuendesha nchi na usalama! Kweli??? Urafiki wa mashaka.......na PK
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom