Elections 2010 Mihuri na form za matokeo zakamatwa Anatoglo!

Kagalala

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
2,403
1,132
Jamani mnasikia habari za mama (AFISA MTENDAJI KATA YA TABATA) alivyokamatwa na karatasi (form za kujaza matokeo). Hii habari hiko live ITV hebu mwenye data arushe zaidi. Mama yuko Polisi na Mpendazoe huko polisi kufatilia
 
Hii habari inarusha vilevile na bongoradio ambao wameunganisha na ITV
 
Collection of such evidences is of great importance ili kuwaadabisha hawa CCM mahakamani
 
Nimetembelea Kimanga. Mida hii wamekata umeme na watu wameanza kushangiria. Hapa nilipo Bar iko karibu na kituo cha ccm lkn hakuna bashasha. Tafadhari anayeangalia luninga anijuze nn kinaendelea
 
Inatisha kama hali ni hiyo, maana nilisikia Mahanga kakamatwa na mabox ya kura!!! Kabla ya hii haijatulia imekuja hii ya fomu za matokeo ambazo hizo ni muhimu balaa!!!! Aiseee hali ni ngumu nchi hii kama ndiyo hivyo!!!!!
 
huo ni mchezo wao katika chaguzi zote ..tangu 2005 ..mwaka huu tu wadau wamewadhibiti kiasi ! ingawa still wameiba katika majimbo mengi
 
WANA JF NINAOMBA KUTUMIA MSEMO WA Rev. Chris Mtikila, unaosema " saa ya ukombozi ni sasa"
 
Nimetembelea Kimanga. Mida hii wamekata umeme na watu wameanza kushangiria. Hapa nilipo Bar iko karibu na kituo cha ccm lkn hakuna bashasha. Tafadhari anayeangalia luninga anijuze nn kinaendelea

Omutwale jeshi la ubungo mmelihamishia huko segerea au?
 
Na kuna kijana pale alikutwa na mhuriwa Nec na makasha matatu ya wino. Wanasema alipelekwa polisi kwa mahojiano then polisi wakachukua hiyo mihuri halafu wakamuachia.
 
Jamani mnasikia habari za mama (AFISA MTENDAJI KATA YA TABATA) alivyokamatwa na karatasi (form za kujaza matokeo). Hii habari hiko live ITV hebu mwenye data arushe zaidi. Mama yuko Polisi na Mpendazoe huko polisi kufatilia

Nilipotune ITV habari hiyo ilikuwa inamalizikia hata hivyo huyo mtangazaji akaeleza habari nyingine kuwa mnamo jioni kuna kijana alifika eneo hilo akiwa anauza mihogo mibichi na akataka kuingia huko ndani, lakini vijana wengi waliokuwepo hapo wakamzuia na kuamua kumkagua. Walipomkagua waliikuta mihogo lakini pia alikuwa na mhuri wa tume ya taifa ya uchaguzi. na alipohojiwa alieleza kuwa aliiokota hiyo mihuri na akaambiwa na ktendaji wa kata moja huko ubungo aipeleke huko. Polisi walichukua mihuri hiyo lakini wamemwachia kijana huyo

Kweli matokeo yanaibwa sana
 
kuna mwingine kamatwa na mihuri ameweka kwenye mihogo kakamatwa na watu polisi wamemuachia.mpaka kieleweke.
 
Jamani mnasikia habari za mama (AFISA MTENDAJI KATA YA TABATA) alivyokamatwa na karatasi (form za kujaza matokeo). Hii habari hiko live ITV hebu mwenye data arushe zaidi. Mama yuko Polisi na Mpendazoe huko polisi kufatilia

Je huyo mama alikamatwa na hizo karatasi wapi na alieleza zilikuwa ni za nini?
 
Huyu mama anaitwa mama Tairo afisa mtendaji kata ya Tabata , alitoka kituo cha kuhesabia kura za Segerea, Arnatoglo hall, mama huyo alijidai anaenda nje kununua msosi, na aloprudi watu walimwomba wamsachi ana nini watu baada ya kumsachi wakakuta anamakarasi ya majumuisho wa matokeo ambayo yalikuwa hayajapigwa muhuri wa tume, wananchi wenyehasira kali wakataka kumpa kichapo, bahati nzuri polis walikuwa karibu wakamchua yeye pamoja na hayo makaratasi wakaendae central police, Mpendazoe nae akaingia kwenye mchuma na wadau wachache na wenyewe wakaelekea central Police.

Vile vile kuna bwana mdogo muuza mihogo amekamatwa na mihuri na wino vyote mali ya Tume ya Uchaguzi, lakini baada ya mahojiano kidogo na polis katika kituo cha central walimwachia na bila aibu wala nini alirudi tena arnatoglo kucheck mambo yanaendaje.

Bado niponipo
 
Na kijana aliyekatwa na muhuri hapo Anatoglo na eti polisi wamemnganya huo muhuri na kumwachia. Habari ni kwamba huo muhuri atapewa kijana mwingine au polisi wenyewe waupele. This is bad, it makes me sick. Mtu anakamatwa na nyara za serikali na kuachiwa, Hii nchi sasa ni balaa
 
Ukiyashangaa ya form utayachoka ya NEC na CCM kukubaliana Rais yupi apate ngapi na sehemu gani 75:18:7 JK:Slaa:Lip.

Kwa hiyo hayo madogo!
 
Na kijana aliyekatwa na muhuri hapo Anatoglo na eti polisi wamemnganya huo muhuri na kumwachia. Habari ni kwamba huo muhuri atapewa kijana mwingine au polisi wenyewe waupele. This is bad, it makes me sick. Mtu anakamatwa na nyara za serikali na kuachiwa, Hii nchi sasa ni balaa

Wenyewe wanaita umafia
 
Jamani mnasikia habari za mama (AFISA MTENDAJI KATA YA TABATA) alivyokamatwa na karatasi (form za kujaza matokeo). Hii habari hiko live ITV hebu mwenye data arushe zaidi. Mama yuko Polisi na Mpendazoe huko polisi kufatilia

Habari nyingine pia kupitia STAR TV, mtangazaji ameripoti kuwa msimamizi katika wilaya ya ilala ameondoka kwenda kule makao makuu ta tume kwa majadiliano zaidi, lakini hajaeleza wanaenda kujadiliana nini hasa
 
Back
Top Bottom