Tanzania: Mihimili mitatu ya Dola na mwingiliano unaokanganya

!
!
Matusi Au Kejeli Hazitusaidii Sana Mkuu. Nchi Inaweza Kwenda Bila Bunge Wala Mawaziri. Bunge Au Baraza La Mawaziri Linapovunjwa Selikali Huendelea Na Shughuli Zake Kama Kawaida, Huku Ikiandaa Na Kutkeleza Utaratibu Wa Kupata Bunge Lingine.
Ni pale tu tunaposubiri uchaguzi ufanyike na si vinginevyo. Wewe hoja yako ilikuwa siyo hiyo unayoleta sasa. Ulidai serikali ni muhilili uliokamilifu, hautegemei mingine jambo ambalo siyo kweli. Sijakutukana!
 
Ni pale tu tunaposubiri uchaguzi ufanyike na si vinginevyo. Wewe hoja yako ilikuwa siyo hiyo unayoleta sasa. Ulidai serikali ni muhilili uliokamilifu, hautegemei mingine jambo ambalo siyo kweli. Sijakutukana!

!
!
Vyovyote Vile Lakini Imejidhihirisha Kuwa Inaweza Kufanya Kazi Yenyewe. Vipi Bunge Hata Kwa Masaa Mawili Tu Linaweza Kufanya Kazi Lenyewe Bila Uwepo Wa Selikali? Wabunge Vikao Vyao Posho Wanalipwa Na Selikali, Au Bunge Lina Vyanzo Vya Mapato?
 
46a bunge lina mamlaka ya kumwondoa rais madarakani.(3) viongozi watakao husika na masharti ya ibara hi ni(a)rais wa jmt (b( vice presdent(c)rais wa znz(d) waziri mkuu wa jamhuri ya tanz
 
Kwa katiba hii iliyopo sasa, separation of power ni dhana tu ambayo kiuhalisia haitekelezeki. Kuna muingiliano mkubwa sana wa madaraka, huu muhimili unaodaiwa umejichimbia chini zaidi ya mingine kuingilia mingine. Wawakilishi wetu(wabunge) wanateuliwa na raisi kuwa mawaziri. Jaji mkuu, mwanasheria wa serikali na majaji wanateuliwa na rais na kuapishwa na rais.
Ile rasimu ya katiba ya Warioba ilikuwa inajibu huu utata wa separation of power, lakini kwa katiba hii tuliyonayo rais akiamua kuwa dikteta anaweza tu na hakuna wa kumzuia.
 
Bunge linaweza kumtoa Rais madarakani kwa kumpigia kura ya kutokuwa na imani nae.
Kiongozi, kabla bunge halijapiga kura ya kutokuwa na imani na MKUU, mkuu anapewa official notice ya jambo hilo prior. Yaani, umepanga kumuacha mkeo, kabla ya kumuacha ni lazima umpe taarifa kuwa NAKUSUDIA KUKUACHA rasmi wiki ijayo, kaa ukijua hilo. Yeye anaweza amua kukuacha wewe kabla ya tarehe uliyopanga au akakuacha utende ulilodhamiria pengine atapata HURUMA ya umma.
 
Nimeshuhudia Rais wa JMT akimteua na kumuapisha Jaji mkuu na pia nimeshuhudia Jaji mkuu akimuapisha Rais wa JMT baada ya kuwa amechaguliwa kihalali na wananchi.
Hapa naiona ile dhana ya mihimili iliyo sawa, sijajua kwa uhakika Spika akisha kuchaguliwa kihalali na wabunge huapishwa na nani?

Msaada tutani tafadhali
Ushindi wa Simba hauna vyama!
 
Salaam.

Wakuu, ukisoma maswala ya Babeli kwenye Biblia Mwanzo 11:1-9, unaambiwa kwamba, "Kwanza, watu wote duniani walikuwa na lugha moja na walitumia maneno yaleyale" .

Ukisoma 7 unaambiwa.. "Haya, na tushuke chini na kuivuruga lugha yao ili wasielewane wao kwa wao.” Mwisho wa kunukuu. Nchi yetu sasa hivi tunashuhudia kila Mwenye Cheo anaongea lugha yake.

Ni wakati wa kuombea taifa ili watendaji na wale wenye Mamlaka watende haki katika kutimiza Majukumu yao.

Katika kuleta usawa, tusiangalie huyu ni Sukuma gang mwenzangu, au huyu ni wa kaskazini tumsingizie kuua Viongozi wa Serikali , au Huyu anatokea Nungwi sisi tunatokea Nangurukuru hivyo hatuhusu, au huyu anatupigia kelele tukiwa tunakula Keki ya taifa tumpe kesi ya Ugaidi ili tufaidi nchi kwa raha.

Ni jukumu la kila Mtu kwa nafasi yake kuhakikisha anatenda haki kwa wote. Vyama vya Siasa vipo kuleta Demokrasia sio chuki na Uhasama..

Wafu ambao hawajaacha maandishi, kuwalinda na kuwatetea na kukumbukwa ni ngumu sana. Hata Nyerere anaishi kwa Vitabu vyake.

Nani asimame Nchi ipone?

#Katibampya.
Screenshot_20210818-044543.png
 
CDF Mabeyo alivyozima mahafadhina wa ccm walivyotaka kumpora mama uongozi
Vivyo hivyo awabane Katiba inayo ondoa kukamatana kama kuku wenye kideri
Mabeyo Mungu alimuandaa ni Mcha Mungu tenda

JWTZ jinyimeni posho simamieni hili acheni kwenda Msumbiji nnchi inazidi kudidimia malumbano tu mama ameshindwa kuisimamia Jini ccm linatoka kwenye chupa linaanza kuwatafuna wenyewe wakimaliza tozo watatunyonya damu
 
Is the presidency of 6th regime captured by a wrong state establishment?
“Deep State” kwa tafsiri isiyo rasmi ni “Waundaji na Waendeleza Taifa”. Tanzania neno “System” (Mfumo) huwa linatumiwa sana kumaanisha deep state lakini kiuhalisia deep state sio system. System ni mojawapo ya zao dogo tu la deep state na inaweza kusambaratishwa wakati wowote.

Deep State ni kundi lisilo rasmi la kiintelijensia ambalo hujumuisha makundi mbalimbali. Hujumuisha baadhi ya watu waliopo katika utumishi na wastaafu na hata marehemu (maandishi yao) katika intelijensia ya jeshi, usalama wa taifa na hawa huja pamoja si kwa kuambiwa au kuelekezwa bali kwa yale ambayo wao wanayaamini kimapokeo kuwa ni misingi ya uhai wa taifa. Watu hawa huamua nani awe mgombea Urais kwa mfano, nani awe Makamu wake, nani awe Waziri Mkuu, nani awe tajiri mkubwa (kwa nchi nyingi za Afrika kwa mfano matajiri wengi wamefanikiwa kwa kupitia kazi za miradi ya umma) kadhalika. Maamuzi haya hayafanywi usiku mmoja, wakati mwingine huchukua miaka wakitumia njia zote zinazowezekana kuhakikisha nani anafikia nafasi ya juu kabisa ya uongozi wa nchi au sehemu fulani nyeti na nani hafiki.

Wakiamua wewe hutakaa uwe Rais wa nchi kwa mfano, huwezi kuwa. Huwa hawana upendeleo, wana roho ngumu, maamuzi magumu, hakuna anayemzidi mwingine kwa uzito na umuhimu wa maoni na hutazama mustakabali wa nchi kwa miaka mingi mbele, tofauti na wanasiasa ambao wao hutaka tu kushinda chaguzi. Ifahamike kuwa inawezekana hata Rais aliye madarakani asifahamu kwa hakika watu hao wote kwa ujumla wao. Hii hutokea hasa katika nchi zinazofanya chaguzi kila baada ya miaka michache. Waasisi wengi wa mataifa huwa ni sehemu ya deep state mfano Mwalimu Nyerere ambaye maandiko yake ndicho chanzo cha Waziri Kiongozi wa zamani wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad kufungwa gerezani na hadi leo kuendelea kuota ndoto za kuwa Rais wa Zanzibar ambazo huenda anakwenda nazo kaburini. Deep state huwa ni kama jini, wakati mwingine unaweza kusema halipo ni maneno tu.

Deep state huweza kutikisa nchi kwa kuuhujumu uongozi ulio madarakani kama ikidhihirika walikosea katika kumpitisha kiongozi husika au wakipoteza nguzo inayowalinda ambayo ni uhai wa taifa. Nchini Tanzania kundi la “deep state” halizidi watu 50 katika wakati wowote.
 
Kwahali nayoiona kwasasa, nchi haina chamaa inachofanya au kutekeleza zaidi ya kuhakikisha iankusanya kodi ili watumishi wapate mishahara yao kila mwezi na kugharamia shughuli za kilasiku za serikali. Miradi ya maendelo tuwasubiri Mabeberu watusaidie.
 
Sasa mnamlaumu nani kwani mwendazake kama asingekimbiza wawekezaji hali ingekuwa hivi leo? Msimlaumu rais wa sasa kwa hili! Rais wa sasa alaumiwe kwa kufuata nyayo za mwenzake kuiua democracy Tanzania!!
Kwa hilo la uchumi namtetea!!
 
Kutokana na bandiko lako na kazi ya hao uliosema "Deep state" wenye uwezo wa kuamua mambo mazito wao ndiyo wenye uwezo wa kuliponya taifa kwa maamuzi yao juu ya hali zinazoendelea ila kama wanabarikiwa na jinsi hali zilivyo basi wananchi hawana budi kuiponya nchi yao.
 
Salaam.

Wakuu, ukisoma maswala ya Babeli kwenye Biblia Mwanzo 11:1-9, unaambiwa kwamba, "Kwanza, watu wote duniani walikuwa na lugha moja na walitumia maneno yaleyale" .

Ukisoma 7 unaambiwa.. "Haya, na tushuke chini na kuivuruga lugha yao ili wasielewane wao kwa wao.” Mwisho wa kunukuu. Nchi yetu sasa hivi tunashuhudia kila Mwenye Cheo anaongea lugha yake.

Ni wakati wa kuombea taifa ili watendaji na wale wenye Mamlaka watende haki katika kutimiza Majukumu yao.

Katika kuleta usawa, tusiangalie huyu ni Sukuma gang mwenzangu, au huyu ni wa kaskazini tumsingizie kuua Viongozi wa Serikali , au Huyu anatokea Nungwi sisi tunatokea Nangurukuru hivyo hatuhusu, au huyu anatupigia kelele tukiwa tunakula Keki ya taifa tumpe kesi ya Ugaidi ili tufaidi nchi kwa raha.

Ni jukumu la kila Mtu kwa nafasi yake kuhakikisha anatenda haki kwa wote. Vyama vya Siasa vipo kuleta Demokrasia sio chuki na Uhasama..

Wafu ambao hawajaacha maandishi, kuwalinda na kuwatetea na kukumbukwa ni ngumu sana. Hata Nyerere anaishi kwa Vitabu vyake.

Nani asimame Nchi ipone?

#Katibampya.
View attachment 1896416
I foresee from a shorter a distance an impeachment motion in the national assembly. Big changes are on the way, they be willing to find out hiding grounds for the atrocities they commited but it will be too late.......................Jiandaye kisaikolojia.

Uhuhitaji kugombana na adui yako ndiyo ujidanganya unajenga uchumi wako!!🤣🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom