Tanzania: Mihimili mitatu ya Dola na mwingiliano unaokanganya

Sukari Yenu

JF-Expert Member
Dec 8, 2014
1,698
1,253
Nawaza jambo hapa, kuwa kuna mihimili 3 ya Dola.

1. Bunge ambalo kiongozi mkuu ni speaker wa Bunge

2. Serikali ambayo kiongozi mkuu ni Rais na

3. Mahakama ambayo kiongozi mkuu ni Jaji Mkuu, na kuna dhana kwamba mihimili hii haingiliani.

Swali: Kwanini kwenye Bunge na Mahakama kuna picha ya Rais ambaye ni kiongozi wa Serikali? Kwanini pasiwe na picha za viongozi wote 3 wa dola au kila sehemu kuwa na picha ya kiongozi wake Mkuu?

Wajuzi mtuambie.
 
Hiyo huwa ni lugha ya kuwatawala watu. Ukweli ni kuwa serikali ni kubwa na inayaingilia hiyo mihimili mingine, na ndiyo maana hiyo mihimili mwingine iko chini ya wizara zinazoongozwa na serikali kuu.
 
Siasa tu, serikali ndo kila kitu hasa kwetu hapa maana hata Jaji Mkuu anateuliwa na Rais
 
Mihimili ya dola iko mitatu kwa maana ya mamlaka.

Rais ni sehemu ya Bunge, kwa maana Bunge limegawanyika katika sehemu mbili:
1. Raisi
2. Bunge
Serikali hupeleka MSWAADA bungeni, unajadiliwa, unapitishwa, kisha kupelekwa kwa raisi kusainiwa ili uwe sheria. Raisi akigoma basi....

Raisi ana uwezo wa kuvunja Bunge. Bunge kiutendaji, hawana uwezo wa kumtoa Raisi madarakani.

Mahakama, kwa nadharia, ni mhimili. Kiutendaji, iko kwenye wizara ya katiba na sheria, hivyo unaweza kuona, chain of command kutoka Ofisi kuu inavyoathiri moja kwa moja utendaji wa huu mhimili mwingine.

Mkuu wa nchi ndio mkuu wa mihimili yote ya Dola.
 
Raisi ni mkuu wa Nchi. Na alama ya nchi. Hivyo kutumika kwa picha yake ni sahihi!

Kumbuka Raisi ni:
- Mkuu wa Nchi. (head of state)
- Amiri jeshi mkuu.
- Mkuu wa executive arm of the state.

Kasome const. law
 
Raisi ni mkuu wa Nchi. Na alama ya nchi. Hivyo kutumika kwa picha yake ni sahihi!

Kumbuka Raisi ni:
- Mkuu wa Nchi. (head of state)
- Amiri jeshi mkuu.
- Mkuu wa executive arm of the state.

Kasome const. law
Asante sana kaka. Lakini hatuwezi sote kuwa wanasheria. Constitutional Law mi yanini bwana.....by the way sidhani ntakuwa mwanasiasa.

Hizi mimi zinanitosha:

Law of Contract Act
Law of Torts
Law of Agency
Labor and Relations Act
Banking and Financial Institutions Act
 
N
Nawaza jambo hapa, kuwa kuna miimili 3 ya dola. 1. Bunge ambaye kiongozi mkuu ni speaker wa Bunge, 2. Selikari ambaye kiongozi mkuu ni Raisi na 3. Mahakama ambaye kiongozi mkuu ni Jaji mkuu, na kuna dhana kwamba mihimili hii haingiliani.

Swali ni kwamba kwann kwenye Bunge na Mahakama kuna picha ya Raisi ambaye ni kiongozi wa serikali? Kwann pasiwe na picha za viongozi wote 3 wa dola au kila sehemu kuwa na picha ya kiongozi wake Mkuu

Wajuzi mtuambie.
Ni kweli kuna mihimili mitatu ya dola,yaani serikali,bunge na mahakama na kila mhimili una kiongozi wake mkuu,lakini katika utendaji kazi zinategemeana,kazi ya Bunge ni kujadili na kutunga sheria pamoja na kushauri na kuisimamia serikali katika kutekeleza sera za taifa,mahakama ni mtafasiri wa sheria na msimamizi mkuu wa sheria za nchi,serikali ndiye msimamizi mkuu na muidhinishaji wa sheria zilizotungwa na bunge ndiye anayetoa pesa kwa ajili ya ufanisi wa mihimili mingine,ndiye msimamizi mkuu wa shughuli za mihimili mingine,hivyo kiongozi wa mhimili wa serikali ni mkuu kuliko wale wa mihimili mingine maana anawakilisha alama za taifa
 
Imefika wakati Wanasheria muache kudanganya watu kwamba eti TZ Mihimili yote inategemeana na hakuna ulio na nguvu klk mwingine kama ni hivyo iweje Raisi wa JMTZ awe na uwezo wa kumtoa mtu Jela? Au iweje aweze kulivunja Bunge muda wowote amuapo na yeye kubakia kuwa Raisi wa nchi?

Hakuna kitu kama hicho, Raisi wa Tanzania Kikatiba yuko JUU ya Mihimili yote na vile vile JUU ya Sheria za JMTZ, acheni kudanganya watu na ndo maana tls na chadema hawampendi Raisi wetu lkn wako powerless, zaidi ya kukimbilia kwa Muzungu hakuna kingine mnaweza fanya ndani ya JMTZ, ...
Mbona wewe ni mpuuzi sana ? Hivi mtu kama wewe umewezaje kutumumia smart phone? Kumbafu kabisa.
 
!
!
Ni Kweli Kabisa. Selikali Iko Juu Ya Mihimili Mingine Yote. Selikali Inaweza Kuwepo Bila Uwepo Wa Bunge Au Mahakama. Lakini Bunge Au Mahakama Haviwezi Kuwepo Bila Selikali.
Mfano Selikali Ikiamua Kukuacha Isikukamate Au Isikupeleke Jela Baada Ya Mahakama Kukutia Hatiani What Can Mahakama Do? Au Bunge Likitoa Mapendekezo Selikali Ikayapiga Chini What Can Bunge Do?
 
!
!
Ni Kweli Kabisa. Selikali Iko Juu Ya Mihimili Mingine Yote. Selikali Inaweza Kuwepo Bila Uwepo Wa Bunge Au Mahakama. Lakini Bunge Au Mahakama Haviwezi Kuwepo Bila Selikali.
Mfano Selikali Ikiamua Kukuacha Isikukamate Au Isikupeleke Jela Baada Ya Mahakama Kukutia Hatiani What Can Mahakama Do? Au Bunge Likitoa Mapendekezo Selikali Ikayapiga Chini What Can Bunge Do?
Kumbe kuna semi- illiterate humu! Basi!
 
Mtoa mada yupo sahihi. Rais ni mkuu wa nchi (head of state) na kiongozi wa mhimili was serikali (head of government). Kama mkuu wa nchi yeye ni msimamizi wa mihimili mingine.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom