Steve Dii
JF-Expert Member
- Jun 25, 2007
- 6,402
- 1,262
Ndugu wasomaji,
Naomba mawaidha yenu katika maswala yafuatayo bila kujali kama yamekukuta, yamekuhusisha au laa:
Naomba kuzingatia moja wakati unatafakari jinsi ya kutoa maoni yako; nalo ni kwamba, maswali haya yanahusu 'aftermath' ya tukio, kile unachohisi ulihusika nacho kina kuletea kero gani moyoni mwako kama lipo. Unajua pale unapotenda kitu ukitegemea kuwa umefanya la maana, lakini baadae unaanza kuwa na majuto, basi ni katika hiyo hali ya 'ki professional' au mazingira yanayopelekea hilo tukio na aftemath yake. Cha nyongeza ni kuwa jamii haijengwi kwa majuto, lakini majuto tunaishi nayo, basi na hapa ni namna tu ya kuyajadili.
Ahsanteni.
SteveD.

- --Kama wewe ni Mwanausalama, unajisikiaje pale ulipo amua kumpiga mtu risasi na kufa ukiwa vitani au ukiwa katika doria?
- --Kama wewe ni Raia, unajisikiaje pale ulipo amua kumuua mtu ukijihami baada ya kuvamiwa nyumbani kwako au katika ugomvi?
- --Kama wewe ni Daktari, unajisikiaje pale ulipo amua kukatisha matibabu ya mgonjwa mahututi ili bora afe?
- --Je, unajisikiaje pale ulipo ua mtu bila kukusudia - mfano katika ajali?
- --Kama wewe ni Mwenye mamraka kisheria, unajisikiaje pale ulipotoa hukumu ya kifo?