Migomo ya Madaktari zao la udhaifu wa Watanzania walio wengi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Migomo ya Madaktari zao la udhaifu wa Watanzania walio wengi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Joblube, Jul 3, 2012.

 1. J

  Joblube JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2012
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wana JF mgomo wa Madaktari unaorindima na matokea ya udhaifu wa Watanzania walio wengi. Hii ni kutokana na sababu zifutatazo: Serikali ilioyopo kwa sasa ni dhaifu mno, baadhi ya watendaji wake wengi ni dhaifu mno kwa kuwa wanatokana na viongozi dhaifu mno wanaotumia akili dhaifu mno kwa hoja dhaifu zisizo na mashiko. Nahili kama Watanzania wala tusikwepe viongozi hawa dhaifu inaimanisha kuwa Watanzania waliowengi ni dhaifu mno kwa kuwa kundi kubwa limewachagu hawa dhaifu.

  Sasa ndugu zangu kwa kuwa sasa wengi wa Watanzania wameshagundua na kutambua udhaifu wetu, tufike mahali tuseme tumeingia choo kisicho, tukubali yaishe mpaka ifike 2015. Nasema hivyo kwa sababu malumbano yale ya bungeni ya jana ni dhahiri kuwa wenzetu hawa waliopewa dhamana hawaelewi na wala hawataelewa matatizo tuliyonayo. Fikiria kiongozi nyumbani kwako kuna matatizo wewe unasafiri kwenda kwenye sherehe badala ya kutuma mwakilishi ili hata kuwatia moyo Watanzania japo kuwa kiuhalisia hauko nao jifanye tu kuwa uko nao, lakini katika msiba wa Kanumba mstari wa mbele,ni sawa na wewe uko nyumbani kwako umealikwa kwenye sherehe kwa bahati mbaya ukaamka asubuhi katoto kako kamepigwa na maleria na joto limepanda, wewe badala ya kukasponji ili kushusha joto ili uweze kupata namna ya kumpeleka hospital wewe unaamua kwenda kwenye sherehe kwanza, akili ya kawaida tu utaonekena hauko sawa.

  Ndugu zangu hawa si kosa lao au kuwa wanaroho mbaya kiasi hicho ila wamefikia mwisho wa uwezo wao wa kuona na kupambanua mambo sana sana huko mbeleni watasema mnawaonea wivu au kuingiza udini kwa kuwa hata madhara ya udini kutokana na udhaifu wao hawajui (elastic limit: liwalo na liwe)
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  udhaifu wa JK ndo chanzo cha mgomo ....na watagoma mpka wapishi wake ikulu mwache alete mzaha tu
   
 3. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Yale yale Mh. WASHA WASHA na dawa ya kitu kinacho washa ni kukunwa tu !
   
Loading...