Migomo ya haki isiyokwisha somo lisilokuwa na faida kwa serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Migomo ya haki isiyokwisha somo lisilokuwa na faida kwa serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by avint, Jan 30, 2012.

 1. a

  avint Member

  #1
  Jan 30, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Migomo ya haki isiyokwisha somo lisilokuwa na faida kwa serikaliHabari waungwana wenzangu mnaoipenda nchi yenu iliyo na utajiri wa madini,mito, maziwa,bahari, misitu, pamoja na milima,bunga za wanyama na sehemu nyingi zenye utajili usio kipimo ila kwa bahati mbaya sisi ndio maskini wa kutupwa ambao tunaishi chini ya dora moja kama wanavyotufariji wakati kiukweli tunaishi chini ya robo dora, natumaini wote ni wazima najua nchi mnaipenda tatizo ni hawa wanaowaongoza hawana mapenzi ya kweli kwetu sisi wananchi na nchi yetu Leo nazungumzia migomo mbalimbali inayoendelea katika nchi yetu hasa hii migomo mikubwa ambayo inaathili wananchi maskini wa Tanzania ni kweli tatizo la migomo halijaanza leo wala jana limekuwepo siku nyingi katika Tanzania ila kwa kadili linavyoendelee ndivyo linavjokuwa tatizo sugu huku serikali yetu inashindwa kujifunza kitu katika hili la kuongezekaa kwa migomo mbalimbali katika sekta za serikali. Binafsi huwa napenda kuchunguza kitu ili kujua chanzo cha tatizo Fulani kabla ya kufikia tamati katika kuchunguza hii migomo ya wafanyakazi nataka niangalie chanzo cha hii migomo ya wafanyakazi nchini mwetu je sababu ni nini hasa?Sababu kubwa na ndiyo ambayo naiona hapa ni serikali kutowajali wafanyakazi wake hasa katika sekta za kijamii kama walimu na madaktari ambao ndio hasa walengwa ambao wanaathilika sana kwa kuwa wanafanya kazi katika mazingira magumu,ninapozungumzia kuwa serikali haiwajali wafanyakazi wake hapa namaanisha mishahara yao ni midogo kulinganisha na kazi kubwa wanazofanya,hawapati posho zao katika wakati muafaka, hawana makazi/nyumba bora za kuishi, malimbikizo ya madeni yote haya yanawafanya wafikili kuwa serikali haiwajali na kwao njia pekee ya kutafuta haki zao ni kugoma kwa hali hii ninavyoiona sasa imefikia hatua kuwa ili upate haki yako inakulazimu ugome. Nafahamu shida anayoipata mwananchi maskini kama mimi panapotokea mgomo kama huu wa madaktari pamoja na athari zake kwa taifa changa kama letu ila sasa hakuna njia ya mkato zaidi ya serikali kutatua matatizo na madai yote ya madaktari.kwa bahati mbaya serikali yetu haijui kujifunza bali inajua kutoa amri! Serikali nchinii Tanzania imewafanya walimu kama watoto siku zote mtoto ukiona anakusumbua kwa kulialia mpe ahadi ya pipi atanyamaza akiendelee mwambie kesho utamununulia juice atatulia ila ukiona hataki kunyamaza shika fimbo harafu mtishie kumchapa hapo lazima anyamaze kwa sababu anajua machungu ya fimbo sasa hivi ndivyo serikali inavyowafanyia walimu ikiona wanadai haki zao inawapa ahadi hewa zisizo na faida yoyote wakiendelea kudai inawatisha kuwafukuza kazi na kwa kuwa wao ni wanyonge wasio na mtetezi kesho yake wanaingia kufundisha. Poleni walimu! Ila amkeni.Prime minister soma alama za nyakati, wakati tulionao si wakati wa kutoleana vitisho kama anavyofanya huyu kaka mkubwa katika kutimiza majukumu yake,namkumbusha kuwa sasa ivi hatuko katika siasa za ujamaa na kujitegemea kipindi ambapo kiongozi wa serikali anaogopwa kupita kiasi tamko lolote baya linafatwa bila kupingwa wala kuhojiwa na yeyote ili mradi tu limetoka kwa kiongozi ,zama hizo zilishapita kitambo sasa ivi watu wanahoji,wanapima mawazo yako na ikionekana hayako sahihi wanayapinga kwa hoja wala sio kwa amri kama viongozi wetu mnavyofanya.
   
Loading...