Migomo na Ubabe wa Serikali, nini hatma ya Maisha ya Watanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Migomo na Ubabe wa Serikali, nini hatma ya Maisha ya Watanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by HorsePower, Mar 9, 2012.

 1. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Kwa muda mrefu sana tumekuwa tukishuhudia serikali yetu ikishindwa kuwasaidia wananchi wake na mara kwa mara ikijikuta inatumia nguvu nyingi sana kuwalinda na kuwatetea viongozi wasio na sifa za uongozi na pia hata wale walioingiza serikali kwenye hasara ya mabilioni ya shilingi ya wavujajasho wake.

  Tumeshuhudia haya kwa namna ambavyo walioingiza Tanzania kwenye mikataba feki ya Richmond jinsi ambavyo wamelindwa, na wale wa Kigoda, Deep Green, mikataba ya Radar na benki kuu na mambo mengine mengi yanayoitesa mioyo ya watanzania wengi.

  Kwa sasa madaktari wameingia kwenye mgomo kudai kuondolewa kwa viongozi wawili wa ngazi za juu wa wizara husika ya afya. Serikali inajaribu kutumia nguvu kuwalazimisha madaktari kurudi kazini kwa kutumia vyombo vyake kama mahakama badala ya kusolve tatizo dogo tu la kuwaondoa viongozi wanaolalamikiwa kushindwa kutekeleza majukumu yake. Ni nani hasa serikali inapaswa kumsikiliza au kumtetea, ni mwananchi aliyeiweka serikali madarakani au kiongozi?

  Nimekuwa najiuliza maswali mengi kuhusu serikali, hivi wananchi tumeiweka serikali madaraka kwa maslahi ya nani hasa? Ni sisi wananchi au kuwalinda wale walioingia madarakani kwa njia za rushwa na kushindwa kutekeleza au kutuwakilisha wananchi ipasavyo? Hivi tutavumilia hali hii mpaka lini? Ni nini sasa hatma ya maisha yetu watanzania?
   
 2. Jamani mbona si poa

  Jamani mbona si poa Member

  #2
  Mar 9, 2012
  Joined: Mar 6, 2012
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tupo kikaoni tunajadili yoteee pamoja na la madaktari ndugu mwananchi.
   
 3. MTENGETI

  MTENGETI JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,330
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  hivi si nasikiaga jk alikuwa luteni jeneral wa geshi?
   
 4. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,872
  Likes Received: 6,222
  Trophy Points: 280
  nasubiri kuona outcome....haswa baada ya amri ya mahakama..... ila mwisho wa siku walalahoi ndo tutaumia...wao na familia zao watatibiwa india...
   
 5. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Sina hakika na hilo, mwanajeshi anatakiwa kuchukua maamuzi magumu.
   
Loading...