Migomo katika Vyuo Vikuu na serikali ya awamu ya Nne

Bwana Masanja na wengine wenye mawazo kama haya wasalaam;

Naongea kwa uchungu na masikitiko makubwa kama mwalimu wa hawa wanafunzi waliofukuzwa well rank yangu ni junior, not senior nadhani mnanielewa.

Kuna siku nilipata kigugumizi pale ambapo mwananfunzi wa kike alinijia na kunieleza kuwa bodi ya mikopo imempa 60% wazazi wake hawana uwezo kwa hiyo hataweza kuhudhuria kipindi anataka aende kwa ndugu zake na jamaa akatafute chochote kile, alikuja kunieleza prior to kipindi, kwani they know sitaki mwanafunzi akose kipindi changu. Wakati ananieleza, msichana mdogo sana akiwa amejifunga ushungi anatokea Tabora, she real changed my mood of teaching.

Nimemaliza mlimani, wakati huo mkopo ulikuwa asilimia 100% I real feel proud kwani sasa serikali inakata deni lao, hili linanipa raha na kuona kuwa kama inafanyika hivi kwa watu wote basi there is no need ya kuwagawa watu kuwa hawa ni wa matajiri na hawa ni wa maskini!

We are all Tanzanian, nchi za kibepari kama USA na Canada japo wana uwezo lakini wanatoa mkopo asilimia 100. Kumbuka hela hii ina riba,unauwa unaua ndege wawili kwa jiwe moja, you ra building country at the same time mnatengeneza profit. Hebu fikiria wamegraduate wanafunzi 2000 kwa mwaka hawa wanafunzi wakianza kulipa deni let say kila mwezi sh.10000 Bodi ya mikopo ina hakika kukusanya sh.milioni 20 kila mwezi, kwa mwaka.....

Hii tabia ya kuitetea serikali inatupa wasiwasi sana, maana hata huko hospitali hali ni mbaya, tumebaki kung'ang'ania serikali ina mambo mengi! wapi ambako serikali haina mambo mengi, angalia Botswana,Nigeria they have lots of educated people ngalia walivyotuacha.Tusiwaze wala kutamani kuwa na taifa la watu mbumbumbu.

Wanafunzi wanaokuja UDSM wanatoka kila pembe ya TZ, fikiria wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa kike, hawana nauli wanarudi nyumbani! hivi tunajua wanaenda wapi?? wanafanya nini?

Wanafunzi wametoa hoja nzito hakuna aliyeiona wana statistics kuwa walipoanza haya mambo ya asilimi asilimia wengi wamefeli miaka hii kulinganisha na miaka iliyopita(kumbuka yule msichana wa tabora kakosa kipindi kwenda kuomba hela), they have to find money, some of them is just money dont mind how I will get it! Kama kuna mtu haamini aende maeneo ya Jolly Cluba na kwingineko we have university and colleges student that are selling themselves!

Kuna wanachanganyikiwa na wale wanaofanya matanuzi ,well hao ni wachache kulinganisha na idadi ya wanafunzi wengi ambao ni maskini.

Simu za mikononi za miaka ya tisini zina tofautiana sana na za miaka ya sasa, magari ya manual taratibu yanapotea yanakuja automatic, window 97 imekuwa upgraded to 2007, Nyerere na Mwinyi waliofunga chuo na wakawafukuza wanafunzi miaka yao tunaendelea kushuhudia same style inatumika!!still hamna solution yeyote ya maana mpaka leo hii isipokuwa ni kutumia teknik ile ile ya zamani ''kufukuza'' wanafunzi watarudi na mwakani watagoma tena!

Kuna kiongozi wa wizara alihaidi kuja kuongea na wanafunzi mchana, wanafunzi walimsubiri Nkrumah mpaka saa 12 jioni!

Ukiona maprofesa hawana utatuzi mwingine isipokuwa kufukuza ujue bado tuko gizani, na giza hilo litaondoka kwa watu wengi kusomeshwa! na kusomeshwa ndio huku wanafunzi wanalilia! ''VC =JK''!!!!

Ni kilio cha kila mtanzania anayetaka maisha ya vizazi vijavyo yawe mazuri.Obama amemaliza juzi juzi tu kulipa deni lake la Havard.

Bodi inaweza kukusanya mikopo inaweza ikawabana watu ndani na nje ya nchi, ni kuwa na system, inawezekana wala mtu asifikirie kuwa inashindikana.

Kuna watu watauliza mimi nafanya nini sana, mimi ni mmoja wao lakini niko upande wa wanafunzi, sauti yangu kubwa lakini haisikiki, maana ya wanafunzi zaidi ya 5000 waliosimamia ukweli wanashindwa kusilizwa je mimi? Acha nisemee JF angalau maandiko yangu na nafsi yangu ishuhudie milele.

That was right move, they dont have support, they need every Tanzanian to be behind them, wanahitaji support yako wewe!!

Mungu Ibariki Tanzania

waberoya

I am sorry kama nitakuwa nime mkwaza mtu, nchi yenyewe katibu wa Chama tawala katibu wa chama mwenye kutengeneza sera au anaye takiwa kusaidiana na wenzake shule ni ya kijeshi, sasa hapo mnategemea mtu kuwa na muono wa mbali.
Pili naungana mkono na wewe kuhusu huko kuchangia 60% ni kugumu kwa watu wengi kwani mishahara yao haiwafikishi hata mwisho wa mwezi, sasa ukiongezea na hili inakuwa taabu.
Wenzetu kenya kuna wakati walikuwa wakifanya harambe ili mtoto wa kijijini kwao aende shule wakijua kwamba baadae atawafaa, lakini tanzania hatuna mwamuko wa namna hiyo, labda watu wamikoa michache ambao wanajua umuhimu wa elimu na wenzao waliotangulia, basi huchangiwa changiwa na ndugu na jamaa mpaka mtu ana maliza Chuo etc.
Tatu wakulima wakitaka kuuzamahindi yao iwe zambia au kenya ili kupata bei ya soko wanakatazwa, anaambiwa hauze humu humu, lakini ikija kuchangia elimu au afya anaambia nguvu ya soko au gharama halisi.
Sasa uyaona hii sera inashindwa kabla hata haajianza.
Kwa hiyo ili tufanikiwe kwa hili Chama na Serekali, iwe na watu wenye kuweza kuwa na mawazo haya ya kimaendeleo ukizungumzia nguvu ya soko etc iwe kila mahali, na ili upate faida lazima u-invest.
 
Ndio nilisoma vyuo vya Tanzania. Na pesa nilizopewa mwanzo wa semeter nilinunua Samsonite, Friji n.k Na mwisho wa semester nilikuwa broke.
Hii inthibitisha kuna matatizo ktk elimu Tanzania hasa hapo iliposomea ww maana umetanguliza kununua miundo mbinu kabla ya shule kuisha hilo pia ni tatizo !!!
 
Kwa wenye uelewa, hivi hiyo mikopo kweli inalipwa au? Na kama jibu ni ndio, wanatumia utaratibu gani maana kuna wanaomaliza hapo chuo hawana kazi/kipato na anuani zao hazijulikani.Nchi ilivyo hakuna jinsi ya kuwafuatilia.Sasa inakuwaje kwa mfano kama watapewa wote mkopo 100% halafu wasirejeshe. Mzungumzaji hapo juu analingalisha na mikopo ya vyuo Marekani ambapo huku kuna mifumo inayoeleweka na mtu hawezi kukwepa kulipa labda ahame!
 
Bwana Masanja na wengine wenye mawazo kama haya wasalaam;

Naongea kwa uchungu na masikitiko makubwa kama mwalimu wa hawa wanafunzi waliofukuzwa well rank yangu ni junior, not senior nadhani mnanielewa.

Kuna siku nilipata kigugumizi pale ambapo mwananfunzi wa kike alinijia na kunieleza kuwa bodi ya mikopo imempa 60% wazazi wake hawana uwezo kwa hiyo hataweza kuhudhuria kipindi anataka aende kwa ndugu zake na jamaa akatafute chochote kile, alikuja kunieleza prior to kipindi, kwani they know sitaki mwanafunzi akose kipindi changu. Wakati ananieleza, msichana mdogo sana akiwa amejifunga ushungi anatokea Tabora, she real changed my mood of teaching.

Nimemaliza mlimani, wakati huo mkopo ulikuwa asilimia 100% I real feel proud kwani sasa serikali inakata deni lao, hili linanipa raha na kuona kuwa kama inafanyika hivi kwa watu wote basi there is no need ya kuwagawa watu kuwa hawa ni wa matajiri na hawa ni wa maskini!

We are all Tanzanian, nchi za kibepari kama USA na Canada japo wana uwezo lakini wanatoa mkopo asilimia 100. Kumbuka hela hii ina riba,unauwa unaua ndege wawili kwa jiwe moja, you ra building country at the same time mnatengeneza profit. Hebu fikiria wamegraduate wanafunzi 2000 kwa mwaka hawa wanafunzi wakianza kulipa deni let say kila mwezi sh.10000 Bodi ya mikopo ina hakika kukusanya sh.milioni 20 kila mwezi, kwa mwaka.....

Hii tabia ya kuitetea serikali inatupa wasiwasi sana, maana hata huko hospitali hali ni mbaya, tumebaki kung'ang'ania serikali ina mambo mengi! wapi ambako serikali haina mambo mengi, angalia Botswana,Nigeria they have lots of educated people ngalia walivyotuacha.Tusiwaze wala kutamani kuwa na taifa la watu mbumbumbu.

Wanafunzi wanaokuja UDSM wanatoka kila pembe ya TZ, fikiria wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa kike, hawana nauli wanarudi nyumbani! hivi tunajua wanaenda wapi?? wanafanya nini?

Wanafunzi wametoa hoja nzito hakuna aliyeiona wana statistics kuwa walipoanza haya mambo ya asilimi asilimia wengi wamefeli miaka hii kulinganisha na miaka iliyopita(kumbuka yule msichana wa tabora kakosa kipindi kwenda kuomba hela), they have to find money, some of them is just money dont mind how I will get it! Kama kuna mtu haamini aende maeneo ya Jolly Cluba na kwingineko we have university and colleges student that are selling themselves!

Kuna wanachanganyikiwa na wale wanaofanya matanuzi ,well hao ni wachache kulinganisha na idadi ya wanafunzi wengi ambao ni maskini.

Simu za mikononi za miaka ya tisini zina tofautiana sana na za miaka ya sasa, magari ya manual taratibu yanapotea yanakuja automatic, window 97 imekuwa upgraded to 2007, Nyerere na Mwinyi waliofunga chuo na wakawafukuza wanafunzi miaka yao tunaendelea kushuhudia same style inatumika!!still hamna solution yeyote ya maana mpaka leo hii isipokuwa ni kutumia teknik ile ile ya zamani ''kufukuza'' wanafunzi watarudi na mwakani watagoma tena!

Kuna kiongozi wa wizara alihaidi kuja kuongea na wanafunzi mchana, wanafunzi walimsubiri Nkrumah mpaka saa 12 jioni!

Ukiona maprofesa hawana utatuzi mwingine isipokuwa kufukuza ujue bado tuko gizani, na giza hilo litaondoka kwa watu wengi kusomeshwa! na kusomeshwa ndio huku wanafunzi wanalilia! ''VC =JK''!!!!

Ni kilio cha kila mtanzania anayetaka maisha ya vizazi vijavyo yawe mazuri.Obama amemaliza juzi juzi tu kulipa deni lake la Havard.

Bodi inaweza kukusanya mikopo inaweza ikawabana watu ndani na nje ya nchi, ni kuwa na system, inawezekana wala mtu asifikirie kuwa inashindikana.

Kuna watu watauliza mimi nafanya nini sana, mimi ni mmoja wao lakini niko upande wa wanafunzi, sauti yangu kubwa lakini haisikiki, maana ya wanafunzi zaidi ya 5000 waliosimamia ukweli wanashindwa kusilizwa je mimi? Acha nisemee JF angalau maandiko yangu na nafsi yangu ishuhudie milele.

That was right move, they dont have support, they need every Tanzanian to be behind them, wanahitaji support yako wewe!!

Mungu Ibariki Tanzania

waberoya

Mkuu, heshima mbele,

Mimi nakupata kabisa. Hakuna anayeitetea serikali. LAKINI naomba nikukumbushe (hata mimi nilisoma wakati bado tunapewa 100% ya mkopo, kwa hiyo sasa hivi nalipa deni). Bandiko langu limelenga kufikisha ujumbe kwamba...ni kweli Jamhuri yetu imeshindwa kutatua hili tatizo kwa miaka mingi. Lakini vile vile na sisi hebu tujiulize tumeanza kutumia migomo lini ku-achieve tunachokitaka? Ni siku nyingi sana. Na matokeo tumeyaona kwamba migomo haisaidii, sana sana wanafunzi wanafukuzwa..wanarudishwa kwa masharti bila hata kutatuliwa yale ya mwanzo!. Kifupi serikali na wanafunzi wote ni losers katika hili la mgomo. Kama serikali haijifunzi katika hili so is wasomi wetu.

Mimi maoni yangu, ni kwamba hawa wanafunzi wabadilishe strategies za kudai haki zao. By the way Waberoya: WE ARE DEALING WITH UNIVERSITY STUDENTS. Kifupi hii ndiyo cream ya taifa! Sasa mkuu wewe unataka tuwahurumie kama wanafunzi wa certificate pale Butimba au Bunda? Hawa ndo inabidi wawe majemedari wetu. Sasa kama mwanafunzi wa Chuo Kikuu hawezi kutumia njia mbadala ya mgomo kudai haki yake kama intellectual..mwananchi wa kijijini..unategemea afanye nini?

Hapana, much as I understand and feel their plight as students, lakini lazima nao wajue kwamba migomo tangu tuanze kuitumia vyuo vikuu haijawahi kutusaidia! sana sana inapostpone matatizo.

Kwa mfano: Hawa wanafunzi ingebidi wajiorganize kama wanafunzi wa sekta ya elimu ya juu Tanzania nzima waichambue ile sera waone mapungufu yake, waende kuongea na serikali wakiwa na (the datazz) kuhusu kipi wanakipinga. Infact wangetuletea hata humu JF vipengele wanavyoona vinawakandamiza tukavichambua! Hii ingewasadia kupata support ya umma (atleast hata humu JF). Mpaka leo wanafunzi wa vyuo vikuu wameshindwa kusolve matatizo yao kwa kutumia vyombo kama mahakama. (yes you might say its a far fetched idea!). Lakini mpaka leo Tanzania unafuu wa kikatiba tulio nao..ulitetewa na mtuu mmoja in the name of Mtikila (usijali matatizo yake mengine). Usishangae kuna baadhi ya waliogoma.......Hawajui wanagomea nini haswa..sana sana watakwambia ni 40% ya mkopo. Kuna wengine hawajawahi hata kuiona hiyo sera! University students need to sit down and do their homework!

Hata wengine humu JF tunailaumu hiyo serikali ya kifisadi ya JK, lakini ukweli inawezekana hatujawahi hata kuiona hiyo sera ya mikopo na kuisoma vizuri!

Yes, serikali yetu ni ya kifisadi, yes hawawajali wanafunzi na proletariats wengine..., yes watoto wa wakulima wanaumia and on and on..but at the end of the day...mgomo ndo utampa nafuu mtoto wa mkulima? What we need ni hawa jamaa wakae chini wahangaishe ubongo. Enzi za rev square zimeshapitwa na wakati! By the way na serikali hata kama ni mafisadi inaongozwa na watu..ukiwatight kwenye kona...wanaelewa..!

I say it again; swala la mikopo linahitaji mjadala wa umakini sana kati ya wanafunzi/wawakilishi wao na serikali. Na they should know..wameshikilia makali wakati serikali imeshikiria mpini! Hapa JF..we can blame the government in all possible terms..but at the end of the day...Lazima tujue kwamba mGomo hautawasaidia hawa wanafunzi.... Nadhani wengi mnakumbuka enzi za marehemu mzee Abdallah Ngororo....

Mkopo hauwezi kuwa haki (ukiachilia mbali public sentiments za wengi wetu humu..kwamba serikali ina wajibu wa kukupa mkopo..). Yaani kweli na akili yako ya chuo kikuu..can you convincingly argue that serikali (ya Tanzania) ina WAJIBU wa kukupa Mkopo? Really? You better go back to your constitutional and human rights law class! Ndo maana nasema wanafunzi wawe smart waache longo longo za kukimbia bara barani..we did..it never helped us! Neither will it help them this time around. Na aneyekwenda hospitali..serikali ina wajibu wa kumpa dawa..kama akiambiwa alipe atagoma?

Tuache utani wakuu..wengi humu mnakaa majuu..you sshould know better than we do hapa bongo!

Wakuu nchi yetu ina matizo ya kiutawala...ila kuweza kupata tunachokihitaji..inatakiwa tuwe werevu zaidi yao!

Masanja,
 
Utamaduni wa kulalamika na kujitia unyonge unaendelea kutulostisha wabongo mpaka lini? Mbona wengine maisha yetu ni ya kuunga unga na poa tu na degree tunazo hii dhana ya kutilisha huruma ni mpya na sijui inatoka wapi. Mnatumia muda mwingi kuandaa pointi za kulalamika na kuonewa huruma kuliko kutafuta majibu makini kwa matatizo yenu.

Quote! Dr. Ngoi (UDSM Statistics) "Even God is not fair, i am disabled your abled" sasa mnataka fair ipi. katika dunia hii you cannot get what you deserve, what you can get is what you can negotiate.

Wanafunzi na viongozi wao wajifunze kunegotiate. Nyerere alichukua nchi kwa kunegotiate hii shortcut yakutaka kuonewa huruma sijiu inatoka wapi.
 
Kwa wenye uelewa, hivi hiyo mikopo kweli inalipwa au? Na kama jibu ni ndio, wanatumia utaratibu gani maana kuna wanaomaliza hapo chuo hawana kazi/kipato na anuani zao hazijulikani.Nchi ilivyo hakuna jinsi ya kuwafuatilia.Sasa inakuwaje kwa mfano kama watapewa wote mkopo 100% halafu wasirejeshe. Mzungumzaji hapo juu analingalisha na mikopo ya vyuo Marekani ambapo huku kuna mifumo inayoeleweka na mtu hawezi kukwepa kulipa labda ahame!

Hapa ndipo lilipo tatizo kubwa maana nadhani aliyeandika proposal hii ya cost sharing hakufiri kua atawapata wapi wadeni wake walipe mikopo yao.
Tanzania hatuna permanent adress nyumba za kupanga kiholela vijiji hakuna hata mitaa utapata wapi wadeni kama hata uhakika wa kuwapatia ajira baada ya shule hakuna????
Ni wachache tu ambao wapo ktk sekta za serikali na wizara huko ndio ambao wanakatwa na loan board madeni yao. ila walio na ajira ktk sekta binafsi bado ufuatiliaji ni mgumu kwa vile hata waajiri binafsi wamepewa tahadhari kuripoti watu wote amabao wamewaajiri na wana stahili kukatwa mikopo waliosomea lakini hamna matunda.
Wasio na ajira ndo kabisa utawapata wapi? waliotoka nje ya nchi ndo ndoto kabisaa,
na ndio maana ni moja wapo ya sababu bodi inashindwa kujiendesha kwa kutoa mikopo 100%
 
DUCE nacho kimefungwa leo. Kutoka Morogoro SUA nako, kampasi ya Mazimbu, wameanza mgomo leo
 
...mwisho wa yote anaumia mwanafunzi...serikali wala vyuo havina mwili, haviumiii...

serikali ni ya wananchi (inatakiwa kuwa ya wananchi) na hao wanafunzi ni wananchi pia. Kama wao wanaumia, basi wananchi wanaumia na mwisho wa yote serikali itaumia (kama kweli serikali iko kwa niaba na manufaa ya wananchi wake). Ni rahisi sana kunyanyasa wananchi kama inavyofanyika hapa dhidi ya wanafunzi, lakini ikumbukwe kuwa, hawa wanafunzi ni sehemu ya nchi yetu na yanayowapata kama ni mabaya basi madhara yake yataifikia jamii yote ya watanzania mwisho wa siku.
 
Mkuu, heshima mbele,

Mimi nakupata kabisa. Hakuna anayeitetea serikali. LAKINI naomba nikukumbushe (hata mimi nilisoma wakati bado tunapewa 100% ya mkopo, kwa hiyo sasa hivi nalipa deni). Bandiko langu limelenga kufikisha ujumbe kwamba...ni kweli Jamhuri yetu imeshindwa kutatua hili tatizo kwa miaka mingi. Lakini vile vile na sisi hebu tujiulize tumeanza kutumia migomo lini ku-achieve tunachokitaka? Ni siku nyingi sana. Na matokeo tumeyaona kwamba migomo haisaidii, sana sana wanafunzi wanafukuzwa..wanarudishwa kwa masharti bila hata kutatuliwa yale ya mwanzo!. Kifupi serikali na wanafunzi wote ni losers katika hili la mgomo. Kama serikali haijifunzi katika hili so is wasomi wetu.

Mimi maoni yangu, ni kwamba hawa wanafunzi wabadilishe strategies za kudai haki zao. By the way Waberoya: WE ARE DEALING WITH UNIVERSITY STUDENTS. Kifupi hii ndiyo cream ya taifa! Sasa mkuu wewe unataka tuwahurumie kama wanafunzi wa certificate pale Butimba au Bunda? Hawa ndo inabidi wawe majemedari wetu. Sasa kama mwanafunzi wa Chuo Kikuu hawezi kutumia njia mbadala ya mgomo kudai haki yake kama intellectual..mwananchi wa kijijini..unategemea afanye nini?

Hapana, much as I understand and feel their plight as students, lakini lazima nao wajue kwamba migomo tangu tuanze kuitumia vyuo vikuu haijawahi kutusaidia! sana sana inapostpone matatizo.

Kwa mfano: Hawa wanafunzi ingebidi wajiorganize kama wanafunzi wa sekta ya elimu ya juu Tanzania nzima waichambue ile sera waone mapungufu yake, waende kuongea na serikali wakiwa na (the datazz) kuhusu kipi wanakipinga. Infact wangetuletea hata humu JF vipengele wanavyoona vinawakandamiza tukavichambua! Hii ingewasadia kupata support ya umma (atleast hata humu JF). Mpaka leo wanafunzi wa vyuo vikuu wameshindwa kusolve matatizo yao kwa kutumia vyombo kama mahakama. (yes you might say its a far fetched idea!). Lakini mpaka leo Tanzania unafuu wa kikatiba tulio nao..ulitetewa na mtuu mmoja in the name of Mtikila (usijali matatizo yake mengine). Usishangae kuna baadhi ya waliogoma.......Hawajui wanagomea nini haswa..sana sana watakwambia ni 40% ya mkopo. Kuna wengine hawajawahi hata kuiona hiyo sera! University students need to sit down and do their homework!

Hata wengine humu JF tunailaumu hiyo serikali ya kifisadi ya JK, lakini ukweli inawezekana hatujawahi hata kuiona hiyo sera ya mikopo na kuisoma vizuri!

Yes, serikali yetu ni ya kifisadi, yes hawawajali wanafunzi na proletariats wengine..., yes watoto wa wakulima wanaumia and on and on..but at the end of the day...mgomo ndo utampa nafuu mtoto wa mkulima? What we need ni hawa jamaa wakae chini wahangaishe ubongo. Enzi za rev square zimeshapitwa na wakati! By the way na serikali hata kama ni mafisadi inaongozwa na watu..ukiwatight kwenye kona...wanaelewa..!

I say it again; swala la mikopo linahitaji mjadala wa umakini sana kati ya wanafunzi/wawakilishi wao na serikali. Na they should know..wameshikilia makali wakati serikali imeshikiria mpini! Hapa JF..we can blame the government in all possible terms..but at the end of the day...Lazima tujue kwamba mGomo hautawasaidia hawa wanafunzi.... Nadhani wengi mnakumbuka enzi za marehemu mzee Abdallah Ngororo....

Mkopo hauwezi kuwa haki (ukiachilia mbali public sentiments za wengi wetu humu..kwamba serikali ina wajibu wa kukupa mkopo..). Yaani kweli na akili yako ya chuo kikuu..can you convincingly argue that serikali (ya Tanzania) ina WAJIBU wa kukupa Mkopo? Really? You better go back to your constitutional and human rights law class! Ndo maana nasema wanafunzi wawe smart waache longo longo za kukimbia bara barani..we did..it never helped us! Neither will it help them this time around. Na aneyekwenda hospitali..serikali ina wajibu wa kumpa dawa..kama akiambiwa alipe atagoma?

Tuache utani wakuu..wengi humu mnakaa majuu..you sshould know better than we do hapa bongo!

Wakuu nchi yetu ina matizo ya kiutawala...ila kuweza kupata tunachokihitaji..inatakiwa tuwe werevu zaidi yao!

Masanja,
Bw Masanja, lakini hata kama constitution haikupi nafasi hiyo mojaa kwaa mojaa ya kupata mkopo, lakini ni wajibu wa serekali kuweka mazingira hayo ya kukuwezesha kupata mkopo, na sio tu wa chuo kikuu nk, bali hata wakujenge nyumba, kununua jokofu, gari etc etc.
Sasa hili la chuo ni changamoto mojawapo, serekali ikilirekebisha hili , basi yatafuata mengine, iwe kwa serekali kuelewa wajibu wake au kwa kusukumwa. na kwa kuwa wewe ni msomi kama ulivyo jieleza huko mwanzo i.e ume-graduate hapo mlimani, basi ni wazi unafahamu mfumo wa uchumi unavyo kwenda, kwamba kitu kimoja ndio kinafungua mlango kwa maendeleo mengine. eg elimu, ndio itatuletea wakulima, madaktari, wanasiasa, walimu, wachumi nk, ndio watawekeza kwenye vitu vingine, ndio wanasababisha wakufunzi kupata ajira, nyumba kupangishwa, dala dala kufanya kazi, mabenki nk
nafikiri kwa maelezo hayo mafupi umenielewa au umeelewa.
Sasa tukirudi kwa serekali yetu kama kweli inataka maendeleo au kutufikisha kwenye hayo maendeleo basi ni wazi wanatakiwa wawekeze saaana tu kwenye elimu na vitu vinavyo endana na elimu.
 
Mhh, ndugu yangu wewe unataka kumtangaza mwenzako hapa kwenye jamvi?[/QUOTE]

Hehehe simaanishi hivyo kaka.....

Internal news nilizozipata ni kuwa kulikuwa na kikao kati ya walimu na uongozi wa chuo ambapo walimu wote wamegoma kuendelea kufundisha wale wanafunzi waliobakishwa wakiwemo foreigners, walimu wamesema kamwe hawataingia darasani kufundisha foregners pekeee kama vp ni bora wafukuzwe wanafunzi wote au wanafunzi warejeshwe as soon as possible na inasemekana kuwa ndani ya wiki tatu wanafunzi wote watarejeshwa ingawa kutakuwa na masharti magumu zaidi.............. WABEROYA UPOOO TUPE MORE INFO HAPA
 
Kwa wenye uelewa, hivi hiyo mikopo kweli inalipwa au? Na kama jibu ni ndio, wanatumia utaratibu gani maana kuna wanaomaliza hapo chuo hawana kazi/kipato na anuani zao hazijulikani.Nchi ilivyo hakuna jinsi ya kuwafuatilia.Sasa inakuwaje kwa mfano kama watapewa wote mkopo 100% halafu wasirejeshe. Mzungumzaji hapo juu analingalisha na mikopo ya vyuo Marekani ambapo huku kuna mifumo inayoeleweka na mtu hawezi kukwepa kulipa labda ahame!

Ufanisi kwenye ukusanyaji wa mikopo kwa nchi kama yetu ni kitu kinachowezekana. Wachache watafanikiwa kukwepa kwa muda na wengine watafariki; hata hivyo hiyo haiwezi hata kidogo kupelekea kusitisha utoaji wa mikopo.

Kwa muda sasa, ukusanyaji wa madeni ya mikopo umelegalega, na moja ya sababu (kwa maoni yangu) ni kwamba mikopo imekuwa ikitolewa kama takrima kuwanufaisha wanasiasa, hasa katika miaka ya karibuni. Utaona pia, fikra za kwamba huu ni msaada na si mkopo.

Kwanini 100% na sio 90%? Dhana ya uchangiaji wa pande zote mbili ni muhimu sana. Huko vijijini siku hizi miradi bora inayosimamiwa vyema na wadau ni ile iliyoibuliwa na kuchangiwa kwa asilimia fulani ya fedha za wananchi. Hii pia imeanza kuondoa dhana ya utegemezi wa fedha za wafadhili. Inajenga fikra kwamba si lazima kungoja fungu toka serikalini.

Pamoja na kwamba serikali haishindwi kutoa 100%, italeta shida mkopo ukiwa ni wa zaidi ya 80% - maana hata pale ubora wa elimu utapodorora, huyu mwanafunzi hatojali. Ni mara ngapi hawa wanafunzi wa elimu ya juu wameonesha kutoridhishwa na kiwango cha elimu nchini kwa kusimama kidedea katika msimamo thabiti?

Huko mamtoni wanakotoa mikopo kwa ajili ya elimu, wanafunzi wa huko hawasomi kwa bidii kama ilivyo hapa nyumbani. Na pia, serikali zao zinakumbana na matatizo kwenye utoaji huu wa mikopo, ikiwemo wanafunzi kuzembea masomo hata kuchelewa kumaliza degree katika muda uliopangwa, na hivyo kuhitaji fedha zaidi.

.
 
Chuo Kikuu kingine chafungwa
Joyce Macha
Daily News; Thursday,November 13, 2008 @19:01

Siku moja baada ya uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani kuwasimamisha masomo wanafunzi wa Shahada ya Kwanza, uongozi huo umechukua hatua nyingine ya kuwasimamisha masomo wanafunzi wote wa Chuo Kikuu cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) kwa muda usiojulikana.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya wanafunzi hao kukaidi agizo la Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe la kuwataka warejee madarasani juzi ifikapo saa moja asubuhi. Hata hivyo, wanafunzi hao waliendelea na mgomo huo, huku wakifanya vurugu kwa kuzuia magari na kukata miti kwa lengo la kutaka kuwachapa wenzao wanaodai wamewasaliti.

"Kufuatia hali hii, ililazimu uongozi wa chuo hiki kuchukua hatua za kuwasimamisha kwa lengo la kurejesha amani chuoni na kuepuka uharibifu wa mali za chuo," alisema mmoja wa wahadhiri chuoni hapo alhamisi ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa kuwa yeye si msemaji. Wanafunzi hao wapatao 3,884 waliamriwa kuondoka katika maeneo yote yanayomilikiwa na chuo hicho ifikapo saa 7:00 mchana.

Polisi walitumika kuhakikisha wanafunzi hao wanaondoka maeneo hayo bila kufanya uharibifu wowote. Uamuzi huo umechukuliwa baada ya wanafunzi hao kukiuka sheria za chuo hicho kwa kutoingia darasani kwa siku mbili mfululizo pamoja na kufanya vurugu, kwa madai ya kupinga sera ya uchangiaji na kutaka serikali iwapatie mikopo kwa asilimia 100.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi ya DUCE, Profesa Rwekaza Mukandala, alisema amri hiyo haiwahusu wanafunzi wa mwaka wa tatu. "Wanafunzi hawa walikuwa wakiendelea na masomo kama kawaida, lakini kutokana na vurugu za wenzao iliwalazimu kutoka madarasani," alisema Profesa Mukandala.

Profesa Mukandala alisema siku ya kuwarudisha chuoni haijafahamika mpaka hapo vikao vya chuo vitakapokaa na kujadili ndipo watatoa tamko rasmi. "Kwa sasa ni vigumu kusema ni lini watarejea chuoni au ni masharti gani tutawapa watakaporudi, suala hilo ni mpaka vikao vya chuo vikae, ndipo tutasema lini warejee na masharti gani tutawapa," alisema.

Naye Rais wa Serikali ya Wanafunzi (DUCE), Ambege Uswege alisisitiza kuwa kufunga chuo sio kutatua tatizo na kwamba wakifungua madai yao yakiwa hayajatekelezwa, wataendelea kushinikiza. "Hata kwa upande mwingine nimefurahi kwa chuo kufungwa maana hali ilishabadilika hapa chuoni, kama tungeendelea kuwepo nadhani damu zingemwagika, wewe si uliona zile fimbo zilizokatwa pale unadhani ingekuwaje hapa, afadhali tu," alisema.

"Vurugu hizi zilianza tangu jana, lakini leo kuanzia saa 12 asubuhi zilizidi sana hasa kutokana na kundi la watu lililoongezeka kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, sehemu ya Mlimani," alisema Uswege. Kuhusiana na suala la masharti, Uswege alisema kwa sasa hana jibu la nini watafanya ila watajua cha kufanya pindi watakapoyapokea masharti hayo.

Katika kuhakikisha hakuna vitendo vyovyote vya uvunjaji wa sheria na kuhakikisha wanafunzi wote wanasambaratika ifikapo saa saba, magari matano ya askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), yalikuwapo katika maeneo hayo. Magari hayo ni pamoja na Toyota Land Rover Defender ambazo zilikuwa tatu, gari moja la maji ya kuwasha na karandinga moja.

Hadi gazeti hili linaondoka katika eneo la chuo, asilimia kubwa ya wanafunzi wanaokaa katika hosteli za chuoni hapo na maeneo ya chuo walikuwa wameanza kuondoka. Wakati hayo yanaendelea, wanafunzi wawili wa chuo hicho waliwekwa katika karandika la FFU kwa madai ya kufanya vurugu chuoni hapo.

Wanafunzi hao walioonekana kuchaniwa nguo walitambuliwa kwa majina ya Luvanda Hofuman wa mwaka wa tatu na Thomas Isaya. Juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Emmanuel Kandihabi ziligonga mwamba baada ya simu yake kuwa imezimwa kwa muda mrefu. Mgomo wa DUCE ulianza jana asubuhi na kudumu kwa siku mbili, wakiishinikiza serikali iwapatie mkopo kwa asilimia 100 pamoja na kubadili sera ya uchangiaji.
 
Pesa zipo ila ufisadi ndo umechukua kasi sana kiasi kwamba mabilioni yanaliwa na wachache. Wapeni 100% vijana wasome. Mbona nyie mlisoma bure kwa kodi za babu na bibi zao? Tatizo ni ubinafsi wa Viongozi wa CCM. Na nyie wanafunzi ni wakati muafaka kujiandikisha kwa wingi ili 2010 msaimie kuling'oa hili jinamizi CCM linaloimaliza nchi yetu. Nothing is impossible to the willing souls. Amerika wamekubali changes itakuwa Tanzania? Time has arrived wake up all Students of Tanzania to liberate our Country. Big up to all Udsm Students.
 
Wana JF hebu turushieni nyuzi kidogo nasikia kuna mgomo mzito hapo TZ wa vyuo Vikuu.
 
Back
Top Bottom