Migomo katika Vyuo Vikuu na serikali ya awamu ya Nne

...kwamba kuna nguvu kubwa ya chama kimoja cha siasa ndio natamani kujua hapo!ufafanuzi tafadhali kwa mwenye taarifa

Kuna nguvu ya CCM nyuma maana wanaona siku zao zina hesabiwa so wameamua kufunga na kujaribu ku divide and rule .
 
Nani anawapenda wanafunzi hawa? Nani anawajali? Nani anawathamini na kuwaona kama watu muhimu katika soko la ajira kwa siku chache zijazo? Kwa kuwakana wakati huu, viongozi wetu wanasahau walikotoka au ni kweli wamekosa nyenzo za kuwasaidia vijana? Hapana shaka vijana wanahitaji mchungaji.

wachungaji tuwe mimi na wewe, nasi tugome kufanya kazi kuishinikiza serikali isikilize kilio cha vijana wetu.
 
did you pay back?? ama ndio ulikimbilia nchi za nje? ndio wenzako wanakosa hata ya kulipia pango?

Ina maana nimesababisha credit crunch na serikali inashindwa kutoa loans kwa wanafunzi kwa sababu yangu?
 
ha ha haha...

kumbe hukujua uko porisi? wanafunzi wako kwenye hali ngumu sasa hivi. Discipline ya kipolisi inabidi kutumika hapa. Au wewe unasemaje?

Model ya kutoa elimu ya juu ibadilike hili wanafunzi wengi waande shule na vilevile gharama za kuwasomesha zisiwe mzigo kwa sisi walipa kodi
icon10.gif
.

Ni kweli kila nchi au jamii inahitaji wasomi. Lakini haitakuwa na maana kwa wasomi kutumia pesa nyingi mashuleni na wanapomaliza pesa au investments zitakazotumika kuwapa wao ajira na kutumia elimu yao.
 
Model ya kutoa elimu ya juu ibadilike hili wanafunzi wengi waande shule na vilevile gharama za kuwasomesha zisiwe mzigo kwa sisi walipa kodi
icon10.gif
.

Ni kweli kila nchi au jamii inahitaji wasomi. Lakini haitakuwa na maana kwa wasomi kutumia pesa nyingi mashuleni na wanapomaliza pesa au investments zitakazotumika kuwapa wao ajira na kutumia elimu yao.

Una mapendekezo ya moja ya model ambazo ungependa kuona zinatumika?

Nchi nyingi zilizoendelea ziliwekezwa zaidi kwenye elimu (iwe kupitia vyuo vya kiraia au vya kijeshi) zaidi ya kwingine kule.

Au wewe unaonaje?
 
Waswahili walinena kutueleza kwamba “kawaida nikama sheria” yaani kwa kawaida mwanadamu akikizoea sana kitu hufikia hatua akafikiria kwamba ni sheria. Wakati mwingine kuna mambo ambayo tunayafanya na tukimuona mtu hayafanyi tunamshangaa.

Kama ulivyo msemo huo kwa muda mrefu sasa kumekua na Shahada ya muda mrefu kwenye vyuo vyetu vikuu hapa nchini, shahada ambayo sio rasmi na wala sio sheria, lakini imekuwepo na inaendelea kuwepo kwa vile wahusika wameshindwa kusoma alama za nyakati.

Hata mimi sikuwahi kuifanyia shahada hiyo tafakuri jadidi lakini Makala ya Dk. Shoo kwenye gazeti la Rai tarahe 17 Mei mwaka huu ilinifungua macho na kunifanya niifikirie shahada hii kwa kina.

Shahada hii sio nyingine bali ni ile ya mgomo ambayo msomi wa nchi hii ambaye hakuwahi kugoma akiwa chuo kikuu anaonekana kama mtu wa ajabu, ni mtu wa ajabu kwa sababu kama ilivyo kwamba “kawaida nikama sheria” na ndivyo ilivyo kwenye vyuo vyetu..

Dk. Shoo aliitaja kama shahada ambayo mkufunzi wake hafahamiki na pengine hata muanzilishi pia huenda hafahamiki na hata faida yake au kazi anayotarajiwa kuipata mwanafunzi baada ya kuhitimu pia haifahamiki.

Lakini pamoja na makala ile ya Dk. Shoo, kilichonisukuma zaidi mimi kuandika makala hii ni mgomo wa wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wa tarehe 4 Juni.

Mgomo huo ulikua unakusudia kuushinikiza uongozi wa chuo hicho uwarudishe chuoni wenziwao wanne waliofukuzwa kutokana na mgomo wa awali wa kushinikiza bodi ya mikopo iongeze fedha za mafunzo kwa vitendo na ada ambayo inatolewa kwa asilimia 40 tu.

Wanafunzi wa IFM wanaushangaa uongozi wa chuo kuwasimamisha viongozi wao akiwemo Rais kwa madai eti aliongoza mgomo. Wao wanasema kwamba kimsingi Rais hakuhusika na maandalizi ya moja kwa moja ya mgomo. Wala hakushinikiza wanafunzi wagome.

Pia wanasema kwamba ni uvivu wa kufikiria wa viongozi wa chuo hicho na kuto kuona mbali pia kushindwa kusoma alama za nyakati ambako kumewapelekea kutoa maamuzi kama hayo.

Kimsingi wanasema kwamba kwa Professa aliyekwenda shule, mtanzania na mwenye uzoefu wa kufanya kazi ya kufundisha au kusimamia uendeshaji wa chuo kikuu chochote nchini, lazima awe na uwezo wa kutambua kwamba sio kweli kwamba migomo inayotokea vyuo vikuu inachochewa na viongozi wa wanafunzi.

“kwa mfano tukiangalia kama pale UDSM wanafunzi waligoma, sio kwa sababu Rais aliwashinikiza, ila ni kwa sababu tangu mwanzo wakati Rais anaomba kura aliambiwa kabisa kwamba suala la kugoma ili kudai haki za wanafunzi lazima liwe kwenye ajenda zake, na ndio maana alipopata nafasi hiyo wanafunzi wakamkumbushia ahadi ile na alikua hana budi afanye hivyo” haya yalikua ni maneno ya mwanafunzi mmoja wa mwaka wa tatu IFM.

“migomo mingine wala Rais hakuhusika. Kwa mfano mgomo wa wanafunzi wa mwaka wa kwanza haukumhusisha Rais moja kwa moja, lakini lawama zote anatupiwa Rais na sisi wengine tunaonekana kama tumeburuzwa” aliongeza mwanafunzi mwingine aliyejitambulisha kwa jina moja la Ali.

Lakini kimsingi elimu ya juu kama inavyoitwa ni ya watu wa juu, yaani watu wenye akili ya kutambua kipi kibaya na kipi kizuri, wazee wenye mvi na wajukuu kwa kifupi watu wazima.

Hii ndio maana baadhi ya wadau wanashindwa kuelewa kwamba ni kwa misingi ipi inayowapelekea wakuu wa vyuo kama wale wa IFM kufikiria kwamba kuna watu wanne tu waliowashinikiza wenzao kugoma? Na je hao walioshinikizwa hawana akili? Au nani miongoni mwa wanafunzi aliwahi kusema mimi sikugoma kwa hiyari yangu?

Hata kama kuna aliyegoma kwa shinikizo, pia lazima aulizwe aeleze kwa nini alikubali kushurutiswa na mtu ambaye hana mamlaka kwenye taasisi na wala hawezi hata kumfukuza chuo au kumchukulia hatua za kisheria? Huyu anaye goma kwa kushurutishwa ndiye anayepaswa kufukuzwa mwanzo. Nasema hivi kwa sababu huyu hajui anachotaka na mtu wa namna hiyo hata kwenye ujenzi wa taifa hatufai kwa sababu atakua mtu wa kuyumbishwa.

Lakini hebu tujiulize kumfukuza mtu chuo kuna faida gani? Nani anaweza kusimama mbele ya umma akasema kwamba ukimfukuza mwanafunzi mmoja wa kitanzania chuo kuna faida? Nchi ambayo msomi mmoja anategemewa na maelifu ya watu. Tunategemea nini tunpowafukuza wanafunzi?

Uongozi wa IMF uliwafukuza wanafunzi wanne ambao walisemekana kua ni wachochezi wa migomo. Lakini baada ya wao kua wamekushafukuzwa kukatokea mgomo mwingine wakuwataka wenzao warudishwe chuo.

Sasa kama wao ndio chanzo, wakati hawapo nani tena alikua chanzo? Je vyanzo vipya navyo vitafukuzwa chuo? Na mwisho wa mchezo huu mbaya ni nini ambacho watanzania, waliofukuzwa na familia zao zitafaidika nacho?

Nchi masikini kama Tanzania, nchi ambayo karibia asilimia tisini na tisa ya wananchi wake hawawezi kumudu gharama za kuwasomesha watoto wao elimu ya juu, tunawafukuza wanafunzi ambao kimsingi wanasomeshwa kwa mkopo. Mkopo ambao wanatakiwa waulipe na kibaya zaidi ni kwamba wakifukuzwa wanatakiwa walipe maramoja kwa mujibu wa kanuni za bodi ya mikopo.

Sasa naanza kupata picha juu ya ni nani waanzilishi wa shahada hii ambayo kimsingi viongozi wake na wasimamizi wake na waanzilishi wake ni viongozi wa vyuo husika na wizara husika kwa kushindwa kutekeleza madai ya wanafunzi na pia kushindwa kusuluhisha matatizo yanapotokea kwa njia ya busara na amani.

Kwa sababu kama yalivyo madai ya wanafunzi viongozi wa vyuo vikuu ambao ni maprofesa walitakiwa kua na uwezo wa kufikiria na kuona mbali zaidi kuliko mtu mwingine yeyote, sasa kwa nini wanajitia upofu? Hili ni suala ambalo kila anayeitakia mema nchi hii anapaswa alifikirie.

Kimsingi kumfukuza mtu chuo tukilinganisha na adhabu za kimahakama ni kama kumfunga mtu maisha. Nasema hivi kwa sababu mtu ambaye anasoma kwa mkopo anapofukuzwa chuo wala hatakua na jeuri ya kusema kwamba atakwenda kusoma sehemu nyingine kwa vile uwezo huo hana.

Nchi inayodai kufuata misingi ya kidemokrasia kama Tanzania lazima ijizatiti kuvumilia maudhi, maudhi ya wananchi wanaodai haki zao za msingi kwa mujibu wa demokrasia ambayo imewapa uhuru wa kujieleza, kupata habari na uhuru wa kusikilizwa. Kwa sababu tangu hapo serikali hii ni ya watu kwa ajili ya watu kama ilivyo maana ya demokrasia.

Sasa kwanini tunawafunga watu midomo? Tunawafunza wataalamu ambao watakua waoga, waoga wa kudai haki zao za msingi? Tunataka wakienda kazini wakipewa kazi bila vifaa wasihoji? Kwa vile tumewajaza ujinga wa kuto kuhoji, na pindi wanapo hoji tunawafukuza chuoni.

Ipo haja ya kubadilika na kufanya mambo kisomi zaidi la sivyo kutakua hakuna maana ya mtu kuitwa Profesa kama atakua hawezi kufanya uchambuzi wa mambo. Akajua faida na hasara na akazipima halafu ndio akatoa hukumu ambayo haitalenga kumkomoa mwanafunzi.

Ukweli ni kwamba suala la kumfukuza mtu chuo linawaogofya wale wanaobaki, pia huenda likasaidia kupunguza vurugu na migomo. Lakini bado suala liko palepale kwamba faida ni ndogo kuliko hasara.

“kama kweli viongozi wa vyuo vyetu wana nia ya kutusaidia, kwanini wasiwasimamishe wanafunzi kwa muda? Kwanini wanawafukuza kabisa?” hili lilikua swali la mdau mmoja ambaye ni mwanafunzi.

Baadhi ya wanafunzi wanadai kwamba kuna watu amboa wanachuki binafsi na wanafunzi na huwa wanasubiria kukiwa na kosa lolote wawafukuze vyuoni kuwakomoa.

“mara kwa mara vyuo vimekua vikiripotiwa vibaya kwenye magazeti na wakati mwingine miongoni mwa Maprofesa huwa wanaandikwa vibaya pia. Sasa hutoke Profesa akawashuku watu baadhi labda kwa umaarufu wao na baada ya hapo huwasubiria wafanye kosa ili awakomeshe” alinena Bw. Juma ambaye ni mdau wa elimu ya juu.

Migomo Vyuo Vikuu Ni Lazima? by saiboko on Blogster
 
ANAYESEMA kwamba haiwezekani wanafunzi kupewa mkopo asilimia 100 kawauliza Barricks, DeBeers, Anglo-American na wenye migodi wengine. Mimi nadhani huo mrabaha au mrahaba ukiongezwa hadi asilimia 10 tu basi shida zote za wanafunzi zitakwisha.

Pili taasisi inayotoa mikopo ifutwe. Mikopo itolewe na TIGGO kupitia kwenye simu zao za mkononi kwa fedha za matumizi na zile za kulipa Chuo zipewe Benki yangu nitakayoianzisha kwa mtaji wa fedha toka BOT kama haki yangu baada ya wenzangu wa EPa kunitosa mapema mwaka juzi!

Halafu tuache hii tabia ya kuona kwamba matatizo yako upande wa WANAFUNZI DAIMA DAWAMU?


Mnataka kunamambia Wakuu wa vyuo hawachemshi tena kwa saaana! Mnataka kunambia idara ya fedha na administrators wengine hawana vijambo na vijambazi vyao?


Tuwe watu wa haki. Na hivi huko kwa kina OBama mbona sijasikia migomo ya wanafunzi. Siri ya mafanikio yao nini. Balozi wa Marekani wape vijana tripu wakajifunze kwanini Marekani wanafunzi hawagomi labda iwe bahati mbaya mmoja wao avute bangi au unga kisha apige wenzie na walimu risasi tu....


Kwa Marekani wanafunzi wanapewa 100% Education Loan. Ndo maana hakuna migomo. Obama Mwenyewe kamaliza juzi juzi kulipa deni lake la shule.
 
Una mapendekezo ya moja ya model ambazo ungependa kuona zinatumika?

Nchi nyingi zilizoendelea ziliwekezwa zaidi kwenye elimu (iwe kupitia vyuo vya kiraia au vya kijeshi) zaidi ya kwingine kule.

Au wewe unaonaje?

Nchi zilizoendelea zilipiga hatua wakati technologia ya mawasiliano bado haijaendelea.

Model yangu ni radical ya matumizi ya mawasiliano. Pesa wanazopewa wanafunzi zinatosha
kuwanunulia TV, satellite receiver, cellular phone, solar panel n.k

Wanafunzi wabaki kwa wazazi wao na wapate shule kwa njia ya TVs.
 
Kwa Marekani wanafunzi wanapewa 100% Education Loan. Ndo maana hakuna migomo. Obama Mwenyewe kamaliza juzi juzi kulipa deni lake la shule.

Na mwanafunzi aliyemaliza shule Marekani alisipolipa deni lake anaripotiwa kwa vyombo husika. Na riba hipo kwenye mikopo.
 
Ndugu Wana JF,

Kumekuwa na matukio mbalimbali ambayo JamiiForum kama jamii, ilisimama na kutoa msimamo. Mfano mmoja ni ule wa lobbyists wa makampuni ya madini kutaka kurubuni serikali yetu na wabunge . JF stood up firm and was counted ! Matokeo yake sote tunayafahamu. Napendekeza kwamba kwa mara nyingine, Jamii Forum itoe mapendekezo ya nini kifanyike kwa ajili ya suluhisho la kudumu.


Wengi wetu tutakuwa kwa namna moja au nyingine tumepitia kwenye vyuo vyetu vya Tanzania, kwa hiyo migomo si kitu kigeni kwetu na tuna experience ya kutosha.

Ni hivi:

1. Sisi kama jamii ya Jamii Forum, tuje na mikakati/ufumbuzi wa nini kifanyike kuondoa matatizo ya mikopo na uchangiaji wa elimu.
2. Tusiwe wabinafsi wa kutoa maelekezo kwa wadogo/ndugu zetu walioko mashuleni/vyuoni. Kwa sababu, naamini, wengi wetu tumepitia katika njia hii wanayopitia, lakini pia tuna uzoefu na upeo wa kuona zaidi kwenye masuala ya uendeshaji wa uchumi (binafsi, kifamilia, na nchi kwa ujumla). Pale penye kosa, tuliseme kosa, na pale panapohitaji hongera vivyo hivyo. Tusibaki kulalama kwamba wanafunzi wamekosa au Serikali haiwajali/haiku makini, tupendekeze suluhisho.
3. Baadhi yetu, kama sio wengi wetu, tunajua kheri ya mikopo ilivyotusaidia katika maisha yetu. Tujiulize, je, ikiwa isingekuwa mikopo, tungekuwa wapi? Lakini pia, ni nchi ngapi ambazo serikali hazitoi kabisa mikopo kwa wanafunzi?

4. Nchi kama Marekani na Uingereza wanatoa mikopo kwa wanafunzi wao, lakini ni makundi yapi yanayonufaika na mikopo hiyo ?? Je, vigezo vipi vinatumika ? Nchi kama Sweden,Norway,Denmark na Finland, vyuo vikuu ni bure kwa wananchi wao, wanawezaje ?


Mapendekezo binafsi:

1.Itungwe sheria (mara moja) ya watu wote waliopitia vyuo vikuu vya Tanzania kuanza kurudisha mikopo waliochukua toka miaka ya tisini (1992) na kuendelea. Kwa watu wengi (walioko makazini), mikopo hii wana uwezo wa kuirudisha, tatizo hakuna utaratibu thabiti wa kurudisha mikopo hii ili iwe fursa kwa wengine kuitumia. Sheria hii inaweza kuwa na makali kama ile ya mafao ya NSSF ambapo kila mwajiri anatakiwa kisheria kuwasilisha makato ya mafao kwa NSSF/PPF kila mwezi. Pia katika sheria hii, waajiri wote lazima wapewe clearance certificate ya mkopo kwa wafanyakazi wao ambao wamesomea Tanzania. Hii itasaidia ku-track wahitimu wote ambao watakuwa hawajarudisha mikopo yao.

2. Bodi ya Mikopo ifutwe. Iundwe taasisi nyingine itakayokuwa na nguvu kisheria kutoa mikopo na kuifuatilia.Taasisi itakayojiendesha yenyewe na ambayo haitakuwa na mashinikizo yoyote ya kisiasa. Taasisi hii iwe na nguvu kama taasisi nyingine za serikali kama TRA, PCCB, EWURA na kadhalika.

3. Serikali iache matumizi yasiyo ya lazima. Kwa mfano, mwaka huu tu, serikali imeingiza mashangingi (Land Cruisers 2008 Model) nyingi tu. Ikiwa gari moja ni zaidi ya milioni 100, magari 20 tu ni bilioni 2. Je bilioni 2 zingesomesha wanafunzi wangapi ?


I stand to be counted !
 
hivi ile hela ya rada ingewekezwa si ingekuwa kama revolving fund kwa ajili ya hawa wanafunzi? ukiongezea na hela aliyeto fadhili moja wa UVCCM kwa ajili ya uchaguzi? mimi nafikiri huo umoja wa vijana waamue ku-divert hiyo fund vijana wenzao wa chuo watafurahia saana. then kila mjumbe wa mkutano huo wa vijana ajigaramie ikiwa ni contribution ya UVCCM kwa vijana wenzao
 
I really feel these students. Maisha ya mlimani ni magumu, bila bumu hali ni ngumu.

Lakini napenda kuangalia upande wa pili wa shilling. Leo hii 80% ya watanzania wanaishi vijijini wakitegemea jembe la mkono. zaidi ya raia million kumi na tano wako kwenye UMASIKINI WAKUTUPWA. Walio na nafuu wengi wao wanabangaiza mno. Kwa hiyo swala kwamba watoto wengi wanaosoma mlimani ni watoto wa wakulima ni kweli lakini hilo inabidi tufike point tulitafutie muafaka. Nchi yetu ina matatizo mengi mno. Wewe atleast unalalamika lakini kuna millions ambao hata hiyo chuo kikuu ni ndoto ya mchana. wanataka tuu wapate ugali wa mchana. Kuna akina mama wanakufa kwa sababu hawana aspirini, kuna sehemu umeme ni anasa, maji ya bomba ni ndoto..and on and on...Sasa jamani haya ni matatizo ambayo yanaiangalia hiyo hiyo bajeti na kodi zetu.....Think about it..matatizo ni mengi mno....Ingawa watu ni mafisadi wanaiba..lakini hatuwezi kuendelea kutumia kigezo cha umasikini forever...

Tanzania haiwezi KUWAKOPESHA wanafunzi WOTE wa elimu ya juu. Huo uwezo hata kama upo....itatuchukua miaka mingi kuwa na vigezo halali vya kujua nani anastahili...especially kipindi hiki ambacho kila mtu ni fisadi anadanganya... Mimi naamini ile ya kukopesha (60% not sure) was the best way kuwasaidia watoto wa wakulima.... Wazee elimu ya siku hizi ni aghali mno......

Swala kwamba tuna raslimali ambazo zinaweza kuwakopesha wanafunzi kama zingetumika vyema..ni kweli I agree..lakini wote tunajua kabisa..nchi haiendeshwi hivyo...Hata mimi ningesema..yale mabillion ya EPA yangerudishwa..hali za watanzania zingekuwa bora zaidi..lakini we all know what is happening.

Ushauri wangu kwa wanafunzi wa mlimani na kwingineko..inabidi wajue kwamba maisha na zama zimebadilika. huwezi kuishi kwa zile slogans zetu eti..mbona "serikali zamani ilikuwa ikiwasomesha watu wake bure". Hizo slogans hazisaidii tena. Lazima wanafunzi wakae chini waangalie hiyo 40% inapatikana vipi. Mgomo siyo suluhisho....Serikali haina wajibu wa kukusomesha! na wala haina wajibu wa kuwapa mikopo! ni swala la sera tuu.

Kifupi wanafunzi wa elimu ya juu...inabidi waanze kusolve matatizo yao kiutu uzima..sana sana leo wamegoma...watoto wa wenye uwezo..wataenda zao nje..mtoto wa mkulima utarudi Kigoma (kama bado una nauli)..after two moths utaambiwa uandike barua uitume kwa registered mail ya kuomba kurudishwa chuo na masharti yale yale au zaidi! upo hapo?

hivi kweli na hizi shule za Yebo yebo za Lowassa...in ten years kutakuwa na thousands wanaingia chuo kikuu..do you expect serikali iwakopeshe wote? you are kidding! Tujiulize tunaoandika hapa kwenye forum..ni wangapi tumeshalipa mikopo yetu kuwasaidia wenzetu wa nyuma?

Hili swala ni gumu halihitaji mgomo wala papara...

Bwana Masanja na wengine wenye mawazo kama haya wasalaam;

Naongea kwa uchungu na masikitiko makubwa kama mwalimu wa hawa wanafunzi waliofukuzwa well rank yangu ni junior, not senior nadhani mnanielewa.

Kuna siku nilipata kigugumizi pale ambapo mwananfunzi wa kike alinijia na kunieleza kuwa bodi ya mikopo imempa 60% wazazi wake hawana uwezo kwa hiyo hataweza kuhudhuria kipindi anataka aende kwa ndugu zake na jamaa akatafute chochote kile, alikuja kunieleza prior to kipindi, kwani they know sitaki mwanafunzi akose kipindi changu. Wakati ananieleza, msichana mdogo sana akiwa amejifunga ushungi anatokea Tabora, she real changed my mood of teaching.

Nimemaliza mlimani, wakati huo mkopo ulikuwa asilimia 100% I real feel proud kwani sasa serikali inakata deni lao, hili linanipa raha na kuona kuwa kama inafanyika hivi kwa watu wote basi there is no need ya kuwagawa watu kuwa hawa ni wa matajiri na hawa ni wa maskini!

We are all Tanzanian, nchi za kibepari kama USA na Canada japo wana uwezo lakini wanatoa mkopo asilimia 100. Kumbuka hela hii ina riba,unauwa unaua ndege wawili kwa jiwe moja, you ra building country at the same time mnatengeneza profit. Hebu fikiria wamegraduate wanafunzi 2000 kwa mwaka hawa wanafunzi wakianza kulipa deni let say kila mwezi sh.10000 Bodi ya mikopo ina hakika kukusanya sh.milioni 20 kila mwezi, kwa mwaka.....

Hii tabia ya kuitetea serikali inatupa wasiwasi sana, maana hata huko hospitali hali ni mbaya, tumebaki kung'ang'ania serikali ina mambo mengi! wapi ambako serikali haina mambo mengi, angalia Botswana,Nigeria they have lots of educated people ngalia walivyotuacha.Tusiwaze wala kutamani kuwa na taifa la watu mbumbumbu.

Wanafunzi wanaokuja UDSM wanatoka kila pembe ya TZ, fikiria wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa kike, hawana nauli wanarudi nyumbani! hivi tunajua wanaenda wapi?? wanafanya nini?

Wanafunzi wametoa hoja nzito hakuna aliyeiona wana statistics kuwa walipoanza haya mambo ya asilimi asilimia wengi wamefeli miaka hii kulinganisha na miaka iliyopita(kumbuka yule msichana wa tabora kakosa kipindi kwenda kuomba hela), they have to find money, some of them is just money dont mind how I will get it! Kama kuna mtu haamini aende maeneo ya Jolly Cluba na kwingineko we have university and colleges student that are selling themselves!

Kuna wanachanganyikiwa na wale wanaofanya matanuzi ,well hao ni wachache kulinganisha na idadi ya wanafunzi wengi ambao ni maskini.

Simu za mikononi za miaka ya tisini zina tofautiana sana na za miaka ya sasa, magari ya manual taratibu yanapotea yanakuja automatic, window 97 imekuwa upgraded to 2007, Nyerere na Mwinyi waliofunga chuo na wakawafukuza wanafunzi miaka yao tunaendelea kushuhudia same style inatumika!!still hamna solution yeyote ya maana mpaka leo hii isipokuwa ni kutumia teknik ile ile ya zamani ''kufukuza'' wanafunzi watarudi na mwakani watagoma tena!

Kuna kiongozi wa wizara alihaidi kuja kuongea na wanafunzi mchana, wanafunzi walimsubiri Nkrumah mpaka saa 12 jioni!

Ukiona maprofesa hawana utatuzi mwingine isipokuwa kufukuza ujue bado tuko gizani, na giza hilo litaondoka kwa watu wengi kusomeshwa! na kusomeshwa ndio huku wanafunzi wanalilia! ''VC =JK''!!!!

Ni kilio cha kila mtanzania anayetaka maisha ya vizazi vijavyo yawe mazuri.Obama amemaliza juzi juzi tu kulipa deni lake la Havard.

Bodi inaweza kukusanya mikopo inaweza ikawabana watu ndani na nje ya nchi, ni kuwa na system, inawezekana wala mtu asifikirie kuwa inashindikana.

Kuna watu watauliza mimi nafanya nini sana, mimi ni mmoja wao lakini niko upande wa wanafunzi, sauti yangu kubwa lakini haisikiki, maana ya wanafunzi zaidi ya 5000 waliosimamia ukweli wanashindwa kusilizwa je mimi? Acha nisemee JF angalau maandiko yangu na nafsi yangu ishuhudie milele.

That was right move, they dont have support, they need every Tanzanian to be behind them, wanahitaji support yako wewe!!

Mungu Ibariki Tanzania


waberoya
 
Naungana na wana JF kuchangia katika hili suala la wanachuo, kwakweli kama maamuzi haya yangechukuliwa na serikali hata kwa mafisadi basi leo hii mafisadi wote wangekuwa wameishafilisiwa lakini hatua kali huchukuliwa kwa wale wanyonge wanaodai haki zao tu, kusoma ni haki ya msingi na pia serikali kuhakikisha raia wake wanapata elimu bora na sio ora elimu ni hali ya msingi.

Ningependa kulizungumza hili kwa kuangalia hali halisi, kama tunavyofahamu kwa sasa serikali inawakata wahitimu wa chuo wote wa kuanzia miaka ya 90's kama sikosei, na hii unakatwa bila hata kutakiwa kukubali kama kweli pesa ulizokopeshwa zinafika kiasi ambacho utakatwa au la! wakati huohuo wahitimu wa miaka ya kabla ya 90's wengi wao ni hawa mafisadi wetu hawpo katika makato hayo je ni vigezo gani vilitumika kutowajumuisha hao katika makato? na je pesa zinazokatwa zinasadia vipi kuongeza idadi ya asilimia ya mikopo ya wanafunzi wa elimu hii ya juu, kama mwanzo wanafunzi walikuwa wakipata 100% na hapakuwa na wanaolipa je sasa makato yamechachamaa sidhani kama pana sector iliyosahaulika kukatwa wafanyakazi wake inakuwaje serikali ishindwe kuwapa hiyo asilimia 100, potelea mbali ongezeko la wanafunzi kwani hili linaenda sambamba na ongezeko la raia wote na makusanyo ya kodi kwa mtazamo wangu,

kwa kusema hayo nadhani wanachuo wanastahili wapatiwe 100% ili waweze kuzingatia masomo yao ukizingatia elimu hii ni full time hupati muda hata wa kufanya kazi na ahata ukijibana bado kazi huwezi kupata, hakuna part times au night jobs huku kwetu kama nchi za wenzenu je unataraji hawa wanafunzi watapata wapi hizo 40%, na kama niwazazi jamani ebu tujiweke sisi ambao tulibahatika kusoma kwa 100% kwenye nafasi hii, je tungekuwa wapi? ni wangapi wangeweza hasa ukizingatia ugumu wa maisha na hii hali ya wananchi kutegemea kilimo kisichokuwa hata na pembejeo! JAMANI TUSIWE NI WENYE KUJISAHAU POLICY MAKERS; UDSM ADMIN (VC; DVC'S) mnatakiwa mtoe tamko lililowazi kuzingatia hali ahalisi kwani huenda serikali ikaelewa kama mtazungumza hili kwa mtizamo wenu, na sio kuwakandamiza wanafunzi ambao ndio haswa wanawaweka hapo mlipo, kubwa tusihamaki tu na kuona unwezekana kwa kuwa haswa nyie sasa mpo pazuri mnapata mishahara na sitting allowance mnapokaa kujadili kuwafungia chuo wanachuo, bila kujadili na kungalia je ni hali au madhila ganii waliyonayo hawa wanachuo, kumbukeni mlipotoka maghembe, uongozi wa chuo, mheshimiwa raisi na system yote je mngeweza kulipa hizo 40% enzi zenu???? INAUMA sana kuona rasilimali za nchi zinafaidiwa na wachache wenye madaraka na wasiwasi wangu mkubwa hao wenye pesa ndio wenye hizo 100% na walalahoi ndio hao wenye 60%, 40%. TANZANIA NI YA WATANZANIA WOTE
 
In Tz, money is not a problem, the main issue is goodwill and selfishness! Very few people(particularly leaders) are selfless. Let me give few examples to prove my case!

Firstly I am a cvil servant (middle cadre, not a senior officer ) but my situation might show just a tip of an iceberg

1. Though there is cost sharing in health, my medical care (including my family) is paid by my employer. Thus, I am not sure if I am in the cost sharing scheme (in health care) like my relatives back home in rural arears.
2. My car is fueled on my employer's bill. If not, I am being paid transport allowance each month
3. In case I attend any meeting (during working hours), I get a sitting allowance ranging from 40,000/- to 100,000/- (irrespective of length of the meeting, even a 2 hr meeting). At times my sitting allowances are 4 times higher than my monthly salary of about $1000 per month!
4. My rent is paid by my employer
5. In case I travel out of, my employer pays me a per diem of over 60,000/-

I can go on and on, but just note that this is for a junior/middle cadre officer. For senior officers, you just have to double the amounts I quoted above. Above all, they have other benefits (eg full time vehicles such as VX) and provisions for personal staff such as drivers, housekeepers etc.

I have never seen such as system in any of the developed countries I visited (I stand to be corrected). For that matter, I will be the last person to be made to believe that our Gvt cannot provide high quality social services including medical care and education. The major problem is that majority of the beneficiaries of the current system (Ministers, Professors.. etc) have already forgotten where they came from and are on the fore front to harrass sons and daughters of poor peasants!
 
LOL siku hizi ndo imeshakuwa utaratibu wetu...fikiria mambo ya TRL utapata jibu ni kwa nini mgomo unaweza kutatua hali kama hii

nakumbuka enzi nasoma chuo kikuu, mambo yalikuwa hayaeleweki hadi mgomo..cha ajabu mkishagoma mnatatuliwa shida zenu ambazo zilionekana hazitatuliki wakati wa mazungumzo!


Mkuu Kz, wakati unasoma au???
Hehehehe mwaka wa tatu FASS. socialogy............... we bado mwanafunzi bwana
 
Back
Top Bottom