Migogoro ya wafugaji na wakulima yamshinda mwingulu nchemba mapigano yaendelea

Dec 25, 2016
63
83
Mkoani Morogoro mkulima amechomwa mkuki mdomoni na kutokezea shingoni hivyo ni mwendelezo wa matukio haya mwigulu uko wapi ?
707621b48218dd8dcd7c0d8f527c111b.jpg
58a3a2d2b80cf7a02e32c653d08c971a.jpg
f25e3052c9020f6e5619c98e8f21ef4f.jpg
 
Haya ni mambo yanayotakiwa yashughulikiwe na waziri anayehusika na Kilimo na Ufugaji.Kama ni kushindwa kazi huyu ndio anatakiwa awajibike.
Waziri wa Mambo ya ndani anaingia hapo baada ya kuona mapigano yameanza au yanaelekea kuanza.
 
Hoja yako ipi unajua majukumu ya Waziri wa mambo ya ndani ? Au unajibu kimapenzi ?
 
Ukiangalia kirahisirahisi unaweza kufikia hitimisho kuwa waziri wa Mambo ya Ndani anahusika na kila tatizo nchini.
Kazi kubwa ya waziri wa mambo ya ndani ni kulinda usalama wa Raia na Mali zao.
Migogoro inatakiwa isuluhishwe na wizara husika kabla haijaleta madhara sio wizara ya mambo ya ndani.
 
Nimekuuliza unajua maana ya usalama wa RAIA na Mali zao ???
 
Migogoro ilishaleta madhara mda mrefu sana,uko morogoro kunatakiwa kuanzishwe kanda maalum ya ile ya Rorya mkoani Mara. Mapigano ya yanatokea kila mara.
 
Najua.
Na mimi nakuuliza.
1.Unajua Jukumu la kwanza la Usalama wa Raia na Mali zao lipo kwa nani?
2.Unajua viashiria vya uvunjifu wa Usalama?
3.Unajua majukumu ya Waziri anayehusika na Mifugo na Kilimo?
 
Waziri anayehusika na mifugo plus kilimo ndoo anahusika na usalama unajua maana ya criminal investigation ??? Lengo la askari wetu ni kuzuia tukio lisitokee au kusubiri litokee ndoo wazuie ???
 
Migogoro ilishaleta madhara mda mrefu sana,uko morogoro kunatakiwa kuanzishwe kanda maalum ya ile ya Rorya mkoani Mara. Mapigano ya yanatokea kila mara.

Tatizo la Wafugaji na Wakulima wa Morogoro ni tofauti sana na lile la Tarime/Rorya.Tarime/Rorya ilikuwa ni mapigano ya koo ambayo chanzo chake ni kuibiana Mifugo.Hapo Jeshi la Polisi lilihitajika kuongeza nguvu.
Tatizo la Morogoro ni Sehemu ya kulishia Mifugo.Wakulima wanadai wafugaji wanalisha mifugo kwenye Mashamba yao wakati wafugaji wanadai hayo ni maeneo ya Malisho.
Hapa hapahitaji Jeshi la Polisi bali mgawanyo sahihi wa maeneo yenye utata ambao utafanywa na wizara husika.
 
Waziri anayehusika na mifugo plus kilimo ndoo anahusika na usalama unajua maana ya criminal investigation ??? Lengo la askari wetu ni kuzuia tukio lisitokee au kusubiri litokee ndoo wazuie ???

Wewe unaongelea matokeo badala ya chanzo.
Ukitaka kudhibiti tatizo anza na chanzo.Wanaotakiwa wadhibiti chanzo ni wizara husika sio Polisi.
 
Kwa hiyo kwa kauli yako unahalalisha mapigano yaendelee ? Kama wizara ya mambo ya ndani haihusiki kwanini Polisi wanakwenda ?
 
Sijakataa Polisi kwenda,ninachokataa ni Waziri wa Mambo ya ndani kulaumiwa.
Polisi wanaingia kila sehemu.Ukikataa kulipa Kodi watakuja,ukibaka watakuja,Ukikata Misitu hovyo watakuja,Ukitiririsha Maji machafu mtaani watakuja,nk.
Hii haina maana walaumiwe usipolipa Kodi,Ukibaka,Ukikata Misitu Ovyo au Ukitiririsha maji machafu mtaani.
 
Kwanini intelijensia za polisi zisitumike kuzuia hii migogoro kama zinavyozuia mikutano ya kisiasa
 
Jaman, tumeshasema sana kuhusu suala la migogoro nchini. Inavyoonekana ni kama Awamu hii nayo imeshindwa kutatua tatizo hili. Ikiwa wamachinga wanaondolewa mtaani Rais anajitokeza kwenye TV kutangaza uamuzi wa serikali iweje anashindwa kujitokeza na kutolea maamuzi sala hili? au ndo tuamini wakubwa kweli ndo wanaomiliki mifugo na labda yao imo? Hii inasikitisha. hatuwezi kuwa na uongozi halafu umekaa kimya kuhusu suala hili nenda rudi. kama wameshindwa uongozi wawape wengine wenye uwezo wa kutatua shida hii. Tumesema wafugaji wana kiburi na mifugo yao itaifishwe ikiingia mashambani mwa watu. jamani iliyobaki ni kuandamana, nchi nzima tutoke mtaani kupaza sauti zetu. Bila kujali itikadi, wajitokeze watu kuongoza kilio hiki. Hatuwezi tena kuvumilia. Tunakimbilia kununua ndege na kutangaza kila kukicha wakati watu wanamatatizo kama haya hayashughulikiwa manake nini. Historia itawahukumu......ndo maana watu wanatfika mahala wanaita majina ya ajabu (uchwara, mtakatifu) kwa sababu ya vitu kama hivi. yunahitaji serikali inayofanya kazi sio one man show
 
Back
Top Bottom