SoC01 Migogoro ya Wafugaji na Wakulima, kweli ni Donda ndugu lisilopona mbele ya Serikali na wasomi?

Stories of Change - 2021 Competition

ROJA MIRO

Member
Jul 19, 2021
52
56
Athari za Migogoro ya Wafugaji na Wakulima.
Migogro hii imekuwa ikisababisha upotevu wa rasilimali kwa raia, jamii na serikali kwa ujumla, uharibifu wa mali, uhai wa raia na mifugo kwa ujumla.

Kwa miaka mingi katika nchi yetu tumekuwa tukiishi na jamii za kifugaji (pastoralists) kama wamasai na wasukuma. Wafugaji hawa wamekuwa wakitumia ufugaji wa asili nakuchangia katika ukuaji wa soko la nyama hapa nchini pamoja na kuchangia pato la taifa.

NB:- Kwa maana hiyo ni kwamba wafugaji na wakulima wote ni muhimu hivyo lazima tufikirie namna njema ya kutatua migogoro hii bila kuathiri upande wowote kwani wote ni watanzania.

Kipi huchangia migogoro hii.

-Kilimo cha kuhama hama,
tumekuwa tukishuhudia wakulima wengi wakilima bila kutumia teknolojia ya kuhifadhi ubora wa udongo. Wamekuwa wakihama kufatana na ardhi inavyopoteza ubora wa uzalishaji,hivyo watumiaji wengine wa ardhi kuharibu mapalio ya mifugo, hizi ni njia za mifugo zinazowafanya wafugaji kupitishia na mifugo kutoka eneo moja hadi lingine.

-Serikali kutokutenga maeneo ya machunga kisheria, katika mipango bora ya ardhi, serikali inatakiwa kutenga maeneo ya malisho na kuyatambua kisheria ili kuzuia uvamizi unaofanywa na watumiaji wengine wa ardhi na atakaekiuka sheria zichukuliwe kwa uthabiti na isiwe siasa.

-Ukosefu wa elimu kwa wafugaji, elimu ya utunzaji na usimamizi wa machunga ni muhimu kwa wafugaji ili waweze kuhudumia maeneo yao ya machunga.Kinachotokea kwa sasa ni wafugaji kufuga kwa mazoea.

-Utamaduni wa makabila ya kifugaji kuona fahari kuwa na ng’ombe wengi.Kwa jamii za wafugaji hususani wamasai wao kuwa na ng’ombe wengi ni fahari sana kwao ni utamaduni wa zamani sana hivyo wanakuwa na ng’ombe wengi kiasi ambacho hufikia hatua kushindwa kuzuia mifugo na kuingia kwenye mashamba ya watu na kupelekea migogoro.

Suluhu.
-Kwanza jamii ya wafugaji wabadili mtazamo kwamba ni fahari kuwa na mifugo mingi.
Hii inahitaji elimu ya kutosha kwa wafugaji kuwafanya wafuge kisasa wazalishe maziwa mengi kwa kutumia mifugo michache wani watakuwa na uwezo wa kuwashibisha kwa uchache wao.

-Utengwaji wa maeneo ya Kulima na Kufuga yawe kiuhalisia.Pamoja na kwamba vijiji vinatenga maeneo hayo ila bado hakuna uhalisia wa ufuatiliaji moja kwa moja,kwa sababu pamoja na kuengwa kwa maeneo hayo ila usimamizi unaonekana bado muingiliano wa wafugaji na wakulima bado upo palepale.

-Hati za umiliki ardhi, inaelezwa kuna uandikishaji duni wa umiliki wa ardhi ambao kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na shirika uwazi la kimataifa yaani Transparency International 2014 Global Corruption mchakato wa upimaji nchini Tanzania umegubikwa na rushwa.

Hivi ndio ninavyoangalia suala hili kupitia Sanaa ya ushairi.

1
.Nawaza natafakari,bado sijapata jibu,
Ni chumvi ama sukari,hebu nipeni jawabu,
Kufuga ni uhodari,nacho kilimo ni tabu,
Wakulima wafugaji,hivi wanagombenii?

2.
Weza sikia habari,mazao wameharibu,
Wa mfugaji hodari,ng’ombe wa Juma Rajabu,
Na mkulima Shomari,akapandwa na ghadhabu,
Wakulima wafugaji,hivi wanagombeani?

3.
Sasa bila tahadhari,shambulizi kalijibu,
Ng’ombe wa Sefu Omari,kaenda kuwasulubu,
Kawaaachoma misumari,eti amwaadhibu.
Wakulima wafugaji,hivia wanagombeani?

4.
Maziwa mbona mazuri,hadi sumu yaharibu,
Au yaweke sukari,unywe kwa ustaarabu,
Cha mana kutafakari,hili tatizo kutibu,
Wakulima wafugaji,hivi wanagombeani?

5.
Wali mtamu hatari,nausifu kwa sababu,
Upate kwa kachumbari,samaki wa tui bubu,
Ufgaji ni ambary,na kilimo ni dhahabu,
Wakulima wafugaji hivi wamagombeani?

6.
Kula ugali fahari,na nyama iwe karibu,
Tena iwe ya kidari,tamu utastajabu,
Kilimo ndefu safari na kufuga ni sulubu,
Wakulima wafugaji hivi wanagombeni?

7.
Kilimo uwe ngangari,sio bahati nasibu,
Mvua kama tayari,havikui taratibu,
Ukiivuna shayiri,njaa haitokusibu,
Wakulima wafugaji,hivi wangombeani?

8.
Na mbuzi wakinawiri,utakijaza kibubu,
Leo ninawapa siri,niloirithi kwa babu,
Kaeni na mfikiri,makosa yenu kutubu,
Wakulima wafugaji,hivi mnagombeani?
 
Mfano TANAPA wanaweza kuzuia ng'ombe kuingia mbugani tunafikiri inashindikana kuzuia mifugo kuingia kwenye mashamba ya watu? Pliz nipigie kura yako na share mawazo kwa huu mjadala
 
Back
Top Bottom