Migogoro ya muungano ni sawa na ndoa, hii kauli inamaanisha mkubwa ndoa yake imemshinda?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Tutafakari,

Mkubwa siku ya muungano alisena matatizo ya muungano ni kama ndoa hili swala linaleta maswali mengi.

Hivi mkubwa mara kadhaa akisikika akitaka kuoa mara watu wa pwani mara watu wa kusini toka akiwa waziri wa ujenzi.

Na majuzi tena akasema siri ya kuishi maisha marefu ni kuoa wake wengi ushauri kaupata kwa Mzee Mwinyi.

Kwenye mazishi ya kada wa chama akadai wanajuana kwani anawajua zaidi ya wake 5. ( wanajuana means wako wote)

Juzi kasema kero za muungano ni sawa na ndoa hii inatoa picha gani?

Najua upendo huanzia nyumbani hasa kwenye familia yako na watu hupenda kuangalia tokea nyumbani ili upewe uongozi hata kazini, kiongozi wakitarajia una nguvu ya kustahimili.

Hizi kauli za mkubwa zinamaanisha nini?
 
Mkuu nadhani unaham ya kumfuata Ben Saanane, hayo mambo yaache kama yalivyo bado tunakuhitaji humu jamvini, zama za kikwete zilishapita, huyu tulie nae hana uvumilivu kabisaaa shauri yako usije sema sikukuonya.
 
Ilishamshinda, ukiona mtu mara kwa mara anaongea kitu kile kile, ujue yameshamkuta, nakumbuka kule bandarini (PTA) aliwaambia ndoa zinavunjika sembuse mkataba wa kazi!! Kwahiyo huyu mtu ni mhanga wa ndoa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom