Migogoro ya kisiasa Mbeya Chanzo Utendaji Mbovu wa Viongozi wa serikali! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Migogoro ya kisiasa Mbeya Chanzo Utendaji Mbovu wa Viongozi wa serikali!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwamakula, Nov 28, 2011.

 1. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #1
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  [h=3]SERIKALI MBARALI YAMTEGA KANDORO NA USALAMA WA TAIFA [/h]
  [​IMG]
  MKUU WA MKOA WA MBEYA ABBAS KANDORO

  OFISI ya Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya imempa kazi nzito ya kutatua migogoro Mkuu wa mkoa Abbas Kandoro na idara ya usalama wa Taifa ikihofia kusutwa na wananchi wakiwemo wananchi wa kijiji cha Isunura, imebainika.


  Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa ofisi hiyo imekuwa ikipelekewa malalamiko na wananchi juu ya utendaji mbovu wa viongozi wake lakini haitaki kuchukua hatua zozote mpaka imefikia hatua wananchi kuanza kujichukulia hatua mikononi kudhibiti viongozi wabadhilifu wa mali za umma.

  Wakizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki, wananchi wa kijiji cha Isunura chini ya baraza la wazee wa kijiji hicho walisema kuwa kwa sasa kijiji chao hakina uongozi wa Serikali ya Kijiji jambo ambalo limesababishwa na ofisi hiyo ya Mkurugenzi wa wilaya ya Mbarali.

  Mwenyekiti wa baraza hilo Chifu Victory Mpalile alisema kuwa, kijiji hicho kimekuwa kikiyumbishwa mara kadhaa na ofisi ya Mkurugenzi hali ambayo imekuwa ikizorotesha maendeleo ambapo mpaka sasa zaidi ya miezi kumi hakuna shughuli zozote zinazoendelea kutokana na Serikali kutoweza kutoa maamuzi yaliyo wazi ya kijiji hicho kuwa katika kata ipi kati ya kata ya Igava na Mawindi.

  ‘’Wialaya hii rushwa imezidi na wananchi wanapodai haki tunaonekana ni wakorofi kwasababu hatukubaliani na mambo yao ya kutuburuza na kutokana na hilo mpaka sasa hatuna uongozi wa Serikali ya kijiji kwasababu hawa waliokuwepo wamevuliwa uongozi kutokana na vitendo vyao vya rushwa’’ alisema Chifu Mpalile.

  Alisema Novemba 20, mwaka huu, wananchi wa kijiji hicho baada ya kuiandikia ofisi ya Mkurugenzi barua na mihutasari tangu mwanzoni mwa mwaka huu juu ya malalamiko ya kutokuwa na imani na Ofisa mtendaji na Mwenyekiti wa Kijiji hicho Silivyo Mbishila na kupuuzwa waliamua kuchukua funguo za ofisi na mihuri ya Kijiji hicho chini ya uangalizi wa Jeshi la Polisi.

  ‘’Tulipochukua mihuri hiyo tukawaambia Polisi waliokuwa wamekuja kuwa tunawahitaji Mkuu wa wilaya au Mkurugenzi lakini mpaka sasa wameshindwa kuja kutokana na kutambua makosa yao ya kuwalinda watendaji hawa mafisadi’’ alisema Mpalile.

  Sanjari na hayo alimuomba Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro na idara ya usalama wa Taifa kufika kijijini hapo na kuwasikiliza kilio chao ili pia waunde serikali ya muda kwa ajili ya huduma za kijamii za Kijiji hicho.

  Kwa upande wake Katibu wa baraza hilo la wazee Vitus Mbishila alisema kuwa kilichowapelekea wananchi hao kuchukua mihuri kwa maandamano kutoka kwa ofisa mtendaji na Mwenyekiti wake ni kutokana na kuwepo mazingira ya kuuza ardhi yao zaidi ya kilomita 3.
  ‘’Unajua tuliamua kuchukua mihuri hiyo kwasababu viongozi hawa walitaka kuuza ardhi kwa wafugaji wa Kijiji cha Ikanutwa Novemba 21, mwaka huu hivyo tungechelewa tungeuzwa lakini viongozi wilayani hawalioni hili’’ alisema Mbishila.

  Mwenyekiti wa wafugaji wa Kijiji hicho Nicorous Kikwembe alisema kuwa kabla ya suala hilo, baadhi ya wafugaji walikamatwa katika kijiji hicho na kupelekwa mahakamani lakini kutokana na Mwenyekiti huyo kutokuwa mwaminifu alienda kuwa shahidi wa wafugaji hao hatimaye wafugaji wakashinda kesi.

  Kwa upande wao Josephine Mdimilage ambaye ni Mwenyekiti wa kitongoji cha Luvalanda, Bibi kizee Ashura Nguluva (90) walisema kuwa eneo hilo lililotaka kuuzwa na viongozi hao lina hati miliki ya mawe na hata wilaya pia wanalijua hilo.

  Aidha mbali na hilo waliiomba Serikali kufanya hima kutatua matatizo baina ya hicho na Serikali ya wilaya hiyo kwasababu kutokana na Serikali kukisusa kijiji hicho imefikia wanawake wajawazito kukosa hata huduma za kliniki katika zahanati iliyopo Kijijini hapo ambapo hulazimika kutembea zaidi ya kilomita Nane mpaka eneo la Rujewa.


  Juhudi za kumpata Mkurugenzi mtendaji wa wilaya hiyo George Kagomba ziligonga mwamba baada ya kufika ofisini kwake na kuelezwa na katibu muhtasi wake kuwa alikuwa nje ya ofisi.


   
 2. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #2
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  [h=3]MKURUGENZI NA MEYA JIJI LA MBEYA KUCHUKULIWA HATUA KISA, KUWA VINARA WA VURUGU ZA MWANJELWA NA KUMSINGIZIA KANDORO [/h]
  [​IMG]
  MKUU WA MKOA WA MBEYA ABBAS KANDORO

  * N i kutokana na kupimana nguvu za maamuzi

  Na, Gordon Kalulunga, Mbeya

  MAASKOFU,Wachungaji na wanataaluma mkoani Mbeya wametoa tamko la kumtaka Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, kuwachukulia hatua za kinidhamu Meya wa Jiji la Mbeya, Athanas Kapunga na Mkurugenzi wa Jiji hilo Juma Idd kutokana na kuwa chanzo cha vurugu zilizotokea jijini hapa hivi karibuni


  Tamko hilo limetolewa leo katika Kongamano la kujenga mkakati wa maendeleo ya Mkoa wa Mbeya ambalo liilifanyika katika ukumbi wa Kanisa la Winners lililopo jijini hapa kutoka makanisa yote yaliyopo mkoani Mbeya ambalo Mkuu wa Mkoa alikuwa mgeni rasmi.

  Mchungaji William Mwamalange, ambaye pia ni Mkurugenizi wa taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya kuhifadhi Mazingira mkoani Mbeya (MRECA) alisema maaskofu na wachungaji wanasikitishwa na vurugu zilizotokea eneo la Mwanjelwa Jijini Mbeya na kwamba hata Meya na Mkurugenzi wa Jiji wachukuliwe hatua za kinidhami kutokana na kuwa chanzo cha vurugu hizo.

  Alisema ''Vurugu zilizotokea haikuwa ni siasa bali ni maamuzi mabaya yaliyofanywa na viongozi waAndamizi wa Jiji la Mbeya katika kushughulikia tatizo la wamachinga wanaouza bidhaa zao eneo la Mwanjelwa''

  "Tukiwa na uongozi wa uongo jiji halitasonga mbele kimaendeleo, vurugu zilizotokea kimsingi pale siyo siasa bali ni maamuzi mabaya ya baadhi ya watu, "alisema Mwamalange huku akishangiliwa na mamia ya viongozi wa dini walioshiriki kongamano hilo.

  Alisema maaskofu na wachungaji wanasikitishwa na kitendo cha baadhi ya watu kumsingizia Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Kandoro kwamba yeye alikuwa ndiye chanzo cha vurugu hizo wakati siku ya tukio alikuwa katika ziara wilayani Mbozi kukagua miradi ya maendeleo.

  Mchungaji Mwamalange alisema kimsingi viongozi wa Jiji la Mbeya hasa Meya na Mkurugenzi hawawezi wakakwepa katika suala la vurugu za Mwanjelwa kwasababu walikiwa na nafasi ya kuzungumza na wamachinga kwa utaratibu ambao usingezua vurugu.

  Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro alisema anashangaa na baadhi ya watu wanaomsingizia kwamba alishiriki kuchochea vurugu za wamachinga wakati siku vurugu zinatokea alikuwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani Mbozi na kwamba Serikali inawatambua wamachinga kama sehemu ya jamii na haiko tayari kukaa nao mbali na katika soko linalojengwa Mwamnjelwa watapata nafasi.

  Kandoro alisema tangu ateuliwa hajawahi kumwagiza mtu au kiongozi yeyote wa Jiji la Mbeya achukue hatua yeyote dhidi ya wamachinga na kusababisha kutokea vurugu.
  "Sijawahi kumwagiza mtu achukue hatua yeyote iliyosababisha vurugu na kimsingi sina sababu maana kwanza ilikuwa ni mapema mno kuchukua maamuzi hayo maana sisi wageni unapofika katika mkoa unahitaji kwanza kusoma mkoa na siyo ghafla unaanza kuchukua hatua,"alisema Kandoro

  Kandoro alisema hata hivyo Halmashauri ya Jiji la Mbeya ipo katika mpango wa kuweka utaratibu mzuri wa kuwafanya wamachinga kufanya biashara zao.

  Aliongeza kuwa kinachotakiwa ni kuwajengea mazingira wamachinga kufanya biashara zao na pia kufufua viwanda vilivyosimama uzalishaji ili waweze kupata ajira katika viwanda hivyo.

  Tamko hilo limekuja wiki moja tu tangu Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya kilipotoa tamko la kuchukua maamuzi magumu ya kuwachukulia hatua kali za kinidhamu viongozi wandamizi na watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya walioshindwa kutimiza wajibu wao na kupelekea kutokea kwa vurugu zilizozua mapambana kati ya wamachinga na polisi jijini hapa.

  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Nawab Mullah alitoa tamho hilo tamko hilo kwa kusema kuwa CCM haiwezi kuacha viongozi wachache ndani ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya wawe chanzo cha vurugu hizo na kusababisha kuvunjia kwa amani kwa maslahi yao binafsi na kupelekea wananchi kuilaumu serikali ya CCM.


  "Kutokana na vurugu za Mwanjelwa CCM baada ya kutafakari kwa kina suala hili na kufanya utafiti wake wa jinsi vurugu zilivyokea na wananchi wa ndani na nje ya mkoa wanavyolizungumzia kimeazimia kuchukua hatu kali kwa viongozi na watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya walioshinda kutimiza wajibu wao,"alisema Mullah katika tamko hilo.

  Mullah alisema CCM ni chama makini ambacho kinawajali na kuwapenda wananchi wake kwa hiyo italazimika kuchukua maamuzi hayo magumu kwa kuhakikisha wale wote wanaoharibu sifa ya Jiji la Mbeya wanaondolewa ili kurejesha imani ya wananchi kwa jiji na serikali ya CCM.


  Alisema wananchi lazima watambue kuwa vurugu ni kama mvua zinanyesha na kuleta mafuriko ambayo huleta madhara makubwa kwa kusomba kila kitu ambapo nchi kadhaa za Afrika zikiwemo Libya,Misri na Somalia zimeingia katika machafuko ya vita ambayo chanzo chake ni baadhi ya vyama vya siasa kutaka madaraka kwa nguvu kwa kuwashinikiza wananchi kufanya maandamano na vurugu.


  Mullah alisema kwa kuwa CCM na serikali yake vipo makini kitaendelea kudumisha amani ya nchi hasa kwa kutambua kuwa hakuna nchi dunia iliyofanikiwa kujenga amani kwa kuvurugu hivyo wanaokuwa chanzo cha kutaka kuvunjika kwa amani watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

  Vurugu hizo za wamachinga waliokuwa wakipinga kuhamishwa maneeo yao ya kufanyiwa biashara zilianza tangu Novemba 11 mwaka huu na kudumu kwa takribani siku tatu zilisababisha kifo cha mtu mmoja, watu 17 kujeruhiwa kati yao watano kwa kupigwa risasi za moto ambapo polisi walifanikiwa kuwatia mbaroni watu zaidi ya 300 wanaosadikika kushiriki katika vurugu hizo.


  Hata hivyo wamachinga hao walisitisha mapambano hayo ambayo pia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) lililazimika kuingilia kati baada ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi kuwasili mjini hapa akitokea mkoani Dodoma ambako alikuwa akihudhuria vikao vya bunge na kuwaomba kusitisha vurugu ambapo walimsikiliza na kuacha kuendelea na vurugu.
   
 3. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #3
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145

  [TABLE]
  [TR]
  [TD="class: reactions-label-cell, width: 1%"]
  [/TD]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  [​IMG]
  WACHANGIAJI
  WACHANGIAJI wengine katika Kongamano hilo wamekazia sana masuala ya utalii, miundombinu, maisha ya wananchi, kodi kwa wafanyabiashara na kilimo kwa ujumla wake, na maendeleo ya kiroho kwa mkoa wa Mbeya.

  BIASHARA,KILIMO NA MINDOMBINU
  Katika suala kodi kwa wafanyabiashara, wamesema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekuwa ikifanya makadirio ya juu kwa mfanyabiashara hali ambayo imewafanya wengi wao kuukimbia mkoa wa Mbeya licha ya tunu kubwa iliyopo.

  Suala la Kilimo limeonekana kutotiliwa mkazo licha ya mkoa wa Mbeya kuwa miongoni unaochangia chakula katika nchi ya Tanzania kwamba mikoa mingine imekuwa ikipewa upendeleo wa kupewa hata matrekta kwa wakulima lakini mkoa umekuwa ukisahaulika sana na kuhoji dhana ya kilimo kwanza ipo wapi sasa.

  Suala la miundombinu katika mkoa wa Mbeya inashangaza kuona serikali inajivunia kuwa na barabara moja wakati barabara za mji zikiwa chakavu kabisa, vilevile hata uwanja wa ndege wa Songwe usingetiliwa mkazo na Waziri Mkuu Pinda usingeweza kujengwa kwani nyuma yake kulikuwa na njama za kuupeleka mkoani Arusha.

  RUSHWA KATIKA JESHI LA POLISI
  Polisi haikusahaulika kuongelewa katika Kongamano hilo kwani maendeleo yamekuwa yakinyonywa na watendaji wake na kwamba madereva wa mabasi wa abiria kuwa na kiasi kisichopungua Tshs 19,000/= kwa ajili ya kuwapa Trafiki ili waweze kuruhusiwa katika vizuizi.

  Wakaongeza kwa sababu ni kwamba hata Polisi nao wanaishi kwenye mazingira magumu hali inayosababisha na kuendeleza rushwa kwenye magari.

  WASOMI WATUPIWA ZIGO LA LAWAMA
  Wasomi pia wametupiwa sana shutuma za mkoa wa Mbeya kuwa chini kimaendeleo na kwamba wao ni kizuizi, kwani wameshindwa kushawishi viongozi wa kitaifa kuukumbuka mkoa huu.

  Katika hili kina Profesa Mwakyusa, Profesa Mwandosya, Dk. Mwakyembe walitupiwa zigo hilo kutokana na ushawishi wao katika taifa hili kwa kutousemea mkoa wa Mbeya katika ngazi ya waliyofikia.

  MAASKOFU WA MAKANISA NAO KIKAANGONI
  Maaskofu wakuu wa makanisa ya Kikristo mkoa wa Mbeya wametupiwa mzigo kwani wao ni viongozi wa juu sana na hata Mamlaka kubwa zimekuwa zikiwaheshimu lakini wameshindwa kuusemea mkoa wa Mbeya katika ngazi ya mkoa na kwamba Mungu atawauliza kwa nafasi zao.

  SUALA LA WATOTO WA MITAANI
  Mchangiaji mwingine kutoka Kanisa la Baptist Mchungaji Mwakang'ata amekazia zaidi kuhusu watoto wa mitaani kuwa ni wengi mno na kwamba miaka ya mbele itakuwa vigumu kuwashughulikia na hali itakuwa mbaya sana, kwa kanisa na serikali.
   
 4. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #4
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
  DK. JOEL LAWI KITENGO CHA ULTRA SOUND HOSPITALI YA RUFAA YA MBEYA AKICHANGIA MADA[​IMG]
   
 5. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #5
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  MCHUNGAJI WA KANISA LA MORAVIAN TANZANIA JIMBO LA KUSINI CHRISTOPHER MWENGA AMBAYE NI MKURUGENZI WA MIRADI YA KANISA HILO AKICHANGIA MADA
  [​IMG]
  MCHUNGAJI EZEKIA JAMES MWAMPEMBE WA KANISA LA PENTEKOSTE
  [​IMG]
  MCHUNGAJI FRANCIS THOMAS WA KANISA LA EAG(T) MBALIZI, MBEYA
  [​IMG]
  MCHUNGAJI ISSA MWASINYAGA WA KANISA LA BAPTIST JIJINI MBEYA
  [​IMG]
  MCHUNGAJI MWAKAMELA WA KANISA LA T.A.G SAE JIJINI MBEYA
  [​IMG]
   
 6. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #6
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145


  [​IMG]
  MCHUNGAJI OSCAR JOHN ONGERE WA KANISA LA CALVARY ASSEMBLIES OF GOD.
  [​IMG]
  MCHUNGAJI ROSE NICOLAUS NTAMBI WA KANISA LA KLPT
  [​IMG]
  MJASIRIAMALI AMBAKISYE MWAKIFYOGO
  [​IMG]
  [​IMG]
   
Loading...