Migogoro ya ardhi ni vita inayoinyemelea mikoa ya kusini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Migogoro ya ardhi ni vita inayoinyemelea mikoa ya kusini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ileje, May 22, 2012.

 1. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Kifo cha mkulima pale Ikwiriri kilichosababishwa na mfugaji ni dalili tosha kuwa sasa vita ya ardhi imeanza rasmi kuinyemelea mikoa ya kusini!

  Itakumbukwa kuwa wafugaji wengi walihamishwa kutoka Ihefu na kupelekwa mikoa ya Lindi na Pwani. Zoezi hili lilifanyika bila kuweka miundombinu muhimu kwa ajili ya mifugo kama majosho, maeneo ya malisho, maji kwa ajili ya mifugo na matumizi ya nyumbani, maeneo ya makazi ya wakulima na wafugaji nk.

  Changamoto kubwa ni uhaba wa maji hasa wakati wa kiangazi ambapo madimbwi yote ya maji na mito mingi ambayo hutumika kunyweshea mifugo hukauka na hivyo wafugaji kulazimika kupeleka mifugo yao katika makorongo ya mito sehemu ambazo pia wakulima ambao ni wakazi asili wa huko wamekuwa wakitumia kupata maji kwa matumizi yao ya nyumbani. Hali hii imekuwa ikisababishwa ugomvi ukubwa baina ya jamii hizi mbili za wafugaji wenye asili ya wasukuma na wenyeji.

  Hivyo wakati umefika kwa viongozi wa kisiasa, wizara zinazohusika na maswala ya jamii, halmashauri za wilaya wakakaa pamoja na wananchi kutafuta ufumbuzi wa changamoto hii vinginevyo tutegemee vifo vingi zaidi vya wananchi na mifugo yao, uharibifu wa mali na mazingira.

  WAKATI NI HUU HAKUNA MUDA WA KUPOTEZA!
   
 2. O

  OMEGA JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 671
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  You are right ,hata Katavi Jana wameuawa watu watatu ugomvi wa ardhi na hospitali kuna majeruhi 25 or more wa mishale,nadhani hakuna waandishi huko ndio sababu hakuna matangazo,lakini ni serious zaidi ya Ikwiriri.FFU wamemwagwa toka Sumbawanga kutuliza.
   
 3. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  tena rufiji ikae chonjo sana maana wana eneo kubwa sana ambalo liko wazi na lenye rutuba ila linahitaji uwekezaji wa hali ya juu. Na hapa tutashuhudia uporaji wa hali ya juu wa ardhi toka kwa wawekezaji wa nje
   
 4. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Nakumbuka kulikuwa na azimio la Mtowisa miaka ya 1990 ambalo kwa kiasi kikubwa lilikuwa linatatua migogoro baina ya wafugaji wa kisukuma na wenyeji kwa kufanya mikutano ya mara kwa mara. Aidha nakumbuka ujumbe kutoka mkoa wa Morogoro ukiongozwa na mkuu wa mkoa wa enzi hizo uliwahi kufanya ziara mkoani Rukwa ili kujifunza namna ya kutatua migogoro ya aina hii. Ni vizuri azimio lile likapitiwa upya ili lliendelee kutumika katika kusuluhisha migogoro ya aina hii.
   
 5. J

  JokaKuu Platinum Member

  #5
  May 22, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,769
  Likes Received: 4,982
  Trophy Points: 280
  ..migogoro yote hii bado kuna wa-Tz wanataka tukaribishe jumuiya nzima ya Afrika Mashariki kumiliki ardhi Tanzania.
   
Loading...