Migogoro ya ardhi:Kati ya mikaba na sheria ya ardhi,kipi hutumika kuamua migogoro/mashauri yanayohusu ardhi katika vyombo vya kutoa haki?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,982
144,308
Hivi katika utatuzi wa migogoro ya ardhi au mashauri ya ardhi katika vyombo vya kutoa haki(mabaraza ya ardhi na mahakama) kipi hutumika katika kufanya maamuzi?

Kwa maneno mengine,inapotokea mikabata ya watu kuuziana ardhi au watu kuweka ardhi rehani ili kupata mkopo,n.k na baadae ukaibuka mgogogoro,vyombo vya kutoa haki vitatumia mkataba baina ya pande mbili katika kutoa hukumu au vitatumia sheria ya ardhi?

Au kwa lugha nyingine,ikitokea mkataba baina ya pande zinazolalamikiana unakinzana na sheria ya ardhi,kipi kita-prevail kati ya mkataba husika na sheria ya ardhi?

Au mikataba yoyote inayohusu ardhi inapaswa kuongozwa na sheria ya ardhi?

Wanasheria na wadau wengine tusaidiane.
 
Kikawaida sheria ya umilikishaji wa ardhi kwa maana nzima ya upimaji na mchakato wa utoaji hati,huhusisha hatua kadhaa ambazo nyingi kati ya hizo serikali ya mtaa/kijiji huhusika kwa nafasi kubwa.
Zoezi la utambuzi wa umiliki/historia ya umiliki wa ardhi linaratibiwa na serikali ya mtaa/kijiji husika,ambapo hata mikataba ya mauziano hufanyika hapo.
Hati ya umiliki huweza kufutwa/kubatilishwa ikiwa hatua muhimu katika upatikanaji wake hazikufuatwa,mmiliki wa ardhi ni lazima atambuliwe na baraza la ardhi la kata,pamoja na majirani anaopakana nao.
Hivyo unaweza kuwa na hati miliki ya ardhi lakini bado usiwe salama.
Mfano;mzee Rungu ana ardhi kijiji cha kidomole bagamoyo,historia ya umiliki wake inatambulika serikali ya kijiji,na majirani anaopakana nao.eneo hilo hilo anajitokeza mtu anaetwa Juma akadai ni lake na katika namna isiyoelezeka akamuuzia Raphael sehemu hiyo ya ardhi,Raphael naye akatumia njia zake akapata hati miliki ya eneo,bado Raphael umiliki wake upo shakani ukitokea mgogoro WA ardhi,ijapokuwa ana hati miliki!
 
Back
Top Bottom