fikirikwanza
JF-Expert Member
- Jan 25, 2012
- 7,452
- 3,065
Nimekuwa nikiandika sana kuhusu ardhi, viwanja vya makazi vipatikane kwa bei nafuu sana ili kila mtanzania apate haki yake ya kuzaliwa, ya kumliki japo kiwanja kimoja cha kujenga makazi yake na familia yake, mara kadhaa waziri wa Ardhi Tibaijuka amebeza michango yetu kuhusu kuhakikisha viwanja vinapatikana kwa kila mtz mwenye nia hiyo.
waziri amediliki kusema hatujui wizara inavyoendeshwa na tusitegemee yeye kufanya mambo kwa mtindo wake mwenyewe, waziri anataka kutushawishi tuamini kuwa hana mchango ktk kuboresha shughuli za wizara ikiwa ni pamoja na kuleta sera bora ya ardhi ambayo itasaidia kupata makazi bora.
Ardhi kuwa ya shida, hasa ardhi ya makazi unasababisha migogoro ambayo mara kadhaa imetoa uhai wa waTZ, leo wakati naandika watu wawili Mwanza wamekufa kwa hii hii migogoro ya ardhi. Tibaijuka pamoja na kutetea kukosekana kwa sera ya ardhi (business as usual pale wizarani), kutetea bei kuwa kubwa kwa kila kiwanja eti Halmashauri zinakopa benki, Je kodi zetu zinaenda wapi??? Wakope benki kulipa mishahara, kupima viwanja watumie kodi zetu au kipaumbele ni mishahara yao??? Hata kama hawatufanyii kazi yoyote walipa kodi??, lakni pia ameshindwa kuzuia kabisa viwanja kupimwa vidogo mno kukidhi haja ya makazi bora utasiki 15x20, 20x20, 25x30. Tibaijuka mbona wewe uko kwenye kiwanja kikubwa mno??? Au ni raia daraja la kwanza na wengine ni la tatu????
Anasema teknolojia inayotumika kupima ndo inasababisha ardhi iwe bei mbaya, je teknolojia hiyo inatusaidia nini kama mwisho wa siku hatuna uwezo wa kununua hivyo viwanja baada ya kupimwa???? Kweli nchi maskini hata na maprofesa wake ni maskini wa taaluma. Kwani mbona makudu yanapima viwanja huko vijijini, pia mbona vijijini kiwanja ni 70 kwa 70mita??? Mbona bei kijijini ni nzuri kwa kila kiwanja??
Kushindwa kuja na sera ya ardhi mjini na vijijni ambako hali sio mbaya sana, ni kusubiri watu wafe kila siku harafu rambirambi ziwe nyingi, bwana ametoa bwana ametwaa za uongo, ni wizara imetwaa, na kwasasa watu wanaokufa kwa migogoro ya ardhi ni Tibaijuka ametwaa. Unakuwaje waziri usikua na mchango kwenye wizara??? Mimi suala la kupatikana sera ya ardhi na viwanja kwa bei nzuri kama laki 2 au 5 kwa vikubwa ndo shughuli za wizara mengine ni kutuibia tu waTZ.
Wewe ni prof, kama teknolojia ni aghali, tumia njia mbadala wa kupima viwanja, tunufaike na shule yako, vinginevyo ni penye hamna. Ni majanga tu, faida ya kuwa na wizara inageuka hasara.
Tuletee sera ya ardhi haraka, itoe mwanya kwa
1. kila mtanzania kupata kiwanja kama anataka
2. Kiwanja cha kawaida kiwe 40x30 yaani nusu eka, Kikubwa 70x70m yaani eka kwa wanaotaka kuweka na swimming pools
3. Viwanja sio biashara, kama umepewa na hujengi anapewa mtu mwingine na unarejeshewa fedha yako. Hii itafanya watu wasijilimbikizie ardhi leo kwa malengo ya kuuza kesho kwa bei mkasi
4. Udalali wa viwanja, na ulanguzi uwe ni kosa kisheria na ni uhujumu maendeleo
5. Upimaji wa viwanja hata kwa makudu, japo GPS sio bei ghali kama bei ya square mita moja dar TZS 8,000, Kibaha nako nasikia tangazo TZS 5,500 kwa sq meter. Hii ni aibu WaTZ wote ni wezi tu, mfanyakazi gani atanunua kwa hela ya mishahara ambapo kodi nayo ni 30%%%%
Ukiona huwezi, Uwaziri ni Mzigo unaomba kuacha, waje wanaoweza kuthubutu na kuleta mabadiliko kwa manufaa ya waTz. Sio dhambi kusema kweli Mhe, Rais siwezi, naomba nifanye kazi nyingine kijijini kwangu.
Nawasilisha