Migogoro ya ardhi inaua,mh. Tibaijuka sera ya ardhi wapi?

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,448
2,000
Nimekuwa nikiandika sana kuhusu ardhi, viwanja vya makazi vipatikane kwa bei nafuu sana ili kila mtanzania apate haki yake ya kuzaliwa, ya kumliki japo kiwanja kimoja cha kujenga makazi yake na familia yake, mara kadhaa waziri wa Ardhi Tibaijuka amebeza michango yetu kuhusu kuhakikisha viwanja vinapatikana kwa kila mtz mwenye nia hiyo.

waziri amediliki kusema hatujui wizara inavyoendeshwa na tusitegemee yeye kufanya mambo kwa mtindo wake mwenyewe, waziri anataka kutushawishi tuamini kuwa hana mchango ktk kuboresha shughuli za wizara ikiwa ni pamoja na kuleta sera bora ya ardhi ambayo itasaidia kupata makazi bora.

Ardhi kuwa ya shida, hasa ardhi ya makazi unasababisha migogoro ambayo mara kadhaa imetoa uhai wa waTZ, leo wakati naandika watu wawili Mwanza wamekufa kwa hii hii migogoro ya ardhi. Tibaijuka pamoja na kutetea kukosekana kwa sera ya ardhi (business as usual pale wizarani), kutetea bei kuwa kubwa kwa kila kiwanja eti Halmashauri zinakopa benki, Je kodi zetu zinaenda wapi??? Wakope benki kulipa mishahara, kupima viwanja watumie kodi zetu au kipaumbele ni mishahara yao??? Hata kama hawatufanyii kazi yoyote walipa kodi??, lakni pia ameshindwa kuzuia kabisa viwanja kupimwa vidogo mno kukidhi haja ya makazi bora utasiki 15x20, 20x20, 25x30. Tibaijuka mbona wewe uko kwenye kiwanja kikubwa mno??? Au ni raia daraja la kwanza na wengine ni la tatu????

Anasema teknolojia inayotumika kupima ndo inasababisha ardhi iwe bei mbaya, je teknolojia hiyo inatusaidia nini kama mwisho wa siku hatuna uwezo wa kununua hivyo viwanja baada ya kupimwa???? Kweli nchi maskini hata na maprofesa wake ni maskini wa taaluma. Kwani mbona makudu yanapima viwanja huko vijijini, pia mbona vijijini kiwanja ni 70 kwa 70mita??? Mbona bei kijijini ni nzuri kwa kila kiwanja??

Kushindwa kuja na sera ya ardhi mjini na vijijni ambako hali sio mbaya sana, ni kusubiri watu wafe kila siku harafu rambirambi ziwe nyingi, bwana ametoa bwana ametwaa za uongo, ni wizara imetwaa, na kwasasa watu wanaokufa kwa migogoro ya ardhi ni Tibaijuka ametwaa. Unakuwaje waziri usikua na mchango kwenye wizara??? Mimi suala la kupatikana sera ya ardhi na viwanja kwa bei nzuri kama laki 2 au 5 kwa vikubwa ndo shughuli za wizara mengine ni kutuibia tu waTZ.

Wewe ni prof, kama teknolojia ni aghali, tumia njia mbadala wa kupima viwanja, tunufaike na shule yako, vinginevyo ni penye hamna. Ni majanga tu, faida ya kuwa na wizara inageuka hasara.

Tuletee sera ya ardhi haraka, itoe mwanya kwa
1. kila mtanzania kupata kiwanja kama anataka
2. Kiwanja cha kawaida kiwe 40x30 yaani nusu eka, Kikubwa 70x70m yaani eka kwa wanaotaka kuweka na swimming pools
3. Viwanja sio biashara, kama umepewa na hujengi anapewa mtu mwingine na unarejeshewa fedha yako. Hii itafanya watu wasijilimbikizie ardhi leo kwa malengo ya kuuza kesho kwa bei mkasi
4. Udalali wa viwanja, na ulanguzi uwe ni kosa kisheria na ni uhujumu maendeleo
5. Upimaji wa viwanja hata kwa makudu, japo GPS sio bei ghali kama bei ya square mita moja dar TZS 8,000, Kibaha nako nasikia tangazo TZS 5,500 kwa sq meter. Hii ni aibu WaTZ wote ni wezi tu, mfanyakazi gani atanunua kwa hela ya mishahara ambapo kodi nayo ni 30%%%%

Ukiona huwezi, Uwaziri ni Mzigo unaomba kuacha, waje wanaoweza kuthubutu na kuleta mabadiliko kwa manufaa ya waTz. Sio dhambi kusema kweli Mhe, Rais siwezi, naomba nifanye kazi nyingine kijijini kwangu.

Nawasilisha
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
79,151
2,000
wanawake wakiwezeshwa wanaweza , UN siyo Tanzania bhana , nchi hii hata waziri anapokea bahasha .
 

Thesi

JF-Expert Member
Aug 8, 2010
1,000
1,195
Mkuu umeandika mada ambayo ina mantiki sana. Migogoro ya ardhi imezidi. Lazima tufike sehemu tuchukue hatua kabla haijatokea madhara makubwa.
Mimi nashangaa nchi ya Mwalimu Nyerere iliyotaka haki sawa kwa wote siku hizi imekuwa haki sawa kwa wenye pesa tu.
Inakuwaje serikali inafanya biashara kwenye ardhi? Kama ni hivyo serikali ijiondoe kweye ardhi tujue moja na hiyo ardhi iwanufaishe raia maskini badala ya kuuzwana serikali kwa faida zao.
 

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Aug 9, 2007
18,439
2,000
Ukiona huwezi, Uwaziri ni Mzigo unaomba kuacha, waje wanaoweza kuthubutu na kuleta mabadiliko kwa manufaa ya waTz. Sio dhambi kusema kweli Mhe, Rais siwezi, naomba nifanye kazi nyingine kijijini kwangu.

Nawasilisha

Huyu MAMA si yupo humu?
CC: Tibaijuka
 
Last edited by a moderator:

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,448
2,000
hoja ya ardhi naomba tuisemee mpaka kieleweke, maana kama watu hawapati ardhi/viwanja, makazi bora ni kwa nani???
 

Bulesi

JF-Expert Member
May 14, 2008
8,691
2,000
Tibaijuka ana nadharia nyingi lakini prictice zero!!! Mimi nina issue nae na kodi za viwanja ambazo wamezipandisha bila kuwatayalisha wananchi. Kodi haina maana kwa serikali kama wale walengwa hawatamudu kuilipa ile kodi, hivyo serikali itakosa mapato, ni vyema kodi ya ardhi ikakadiliwa kwa kiwango ambacho wananchi based on their real income wanaweza kulipia viwanja. Hali ya kodi ya viwanja ilivyo hivi sasa baada ya review ya Tibaijuka is not people friendly!!!
 

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,448
2,000
Tibaijuka ana nadharia nyingi lakini prictice zero!!! Mimi nina issue nae na kodi za viwanja ambazo wamezipandisha bila kuwatayalisha wananchi. Kodi haina maana kwa serikali kama wale walengwa hawatamudu kuilipa ile kodi, hivyo serikali itakosa mapato, ni vyema kodi ya ardhi ikakadiliwa kwa kiwango ambacho wananchi based on their real income wanaweza kulipia viwanja. Hali ya kodi ya viwanja ilivyo hivi sasa baada ya review ya Tibaijuka is not people friendly!!!

Sio tu hayupo people friendly, hana uwezo wa kuendesha wizara yoyote, kwani gigiri alifanya nini cha maana???
 

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,597
2,000
Happy New Year, 2014 Fikirikwanza,

Nakupongeza kwa post yenye maana kwa maisha ya Watanzania. Naomba Mods waweke post hii Sticky.

Maana suala la makazi ni la kila mtanzania, sio la itikadi za vyama, Kila mtanzania suala la ardhi lina mgusa, kama sio wewe ndugu yako linamgusa.

Kwanza Biashara ya kuuziana ardhi ni Holela sana, Hakuna mamlaka kama TCRA, SSRA, EWURA, Nk ili kudhibiti. Kodi za Nymba zinatozwa Holela Holela tu....

Viwanja Vinauzwa ovyo ovyo tu

Hakuna mipango miji hata kwa majiji kama Dar, Arusha, Mwanza, Mbeya, na mikoa kama Manyara. It is shame kwa Geneva Africa /Arusha kuachwa ijengwe ovyo ovyo. Waziri na Naibu wake watoe mwongozo kwa Manispaa, huo ndo uongozi...

---Kila siku damu za watanzania zinamwagika, migogoro ya ardhi, Tuanza na Mabina wa CCM, Wakulima na wafugaji Moro, Kiteto, na Manyara inakuja, nimesoma katika gazeti la Raia mWema leo..

- Napendekezo ardhi yote Tanzania ipimwe, maeneo yenye kufaa kwa kilimo na maeneo ya mifugo yatengwe. maeneo yatengwe ili mifugo ikae kwenye malisho kama Ranch. Wafugaji wamilikishwe ardhi na walipe kodi kwa kila hecta, ni ubunifu nawapa. Ile hoja Binafsi ya Mh. Mdee imeishia wapi?

Pia Ardhi ya Kilimo, wananchi wapewe, walime na walipe kodi, serikali itapata pesa.


- I wonder hawa Mawaziri wapo Ofisini tu, Hawajajiuzulu???!!!!
 

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,448
2,000
Halima J Mdee vipi umeishiwa pumzi kuhusu sera ya ardhi?? maana wewe ndo waziri kivuli, tunalalamikia makazi bora, upatikanaji wa viwanja na kodi kubwa za nyumba kwa serikali, Je dada yetu, mbunge wetu, pumzi imekuishia???
 

lyinga

JF-Expert Member
Nov 18, 2013
2,498
0
Halima J Mdee vipi umeishiwa pumzi kuhusu sera ya ardhi?? maana wewe ndo waziri kivuli, tunalalamikia makazi bora, upatikanaji wa viwanja na kodi kubwa za nyumba kwa serikali, Je dada yetu, mbunge wetu, pumzi imekuishia???

Halima mdee anajitahidi sana nampa big up huyu mama anna zile spidi zake alizoanza nazo sasa hivi hamna kitu anapiga mak time tu siku ziishe arudi bk kulima ndizi.
 

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,448
2,000
Sera ya ardhi ili kuwapa haki watz kwamiliki ardhi kwa kuchangia kulingana na uwezo wa mishahara ya serikali ni lazima ili mtz asije kuwa mkimbizi nchini kwake, kiwanja 40x40 TZS 200,000 hivi, 70x70 TZS 500,000/- as maximum.
 

nyumba kubwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
10,313
2,000
NK nimejikuta nasoma land policy na land laws kama nimekuwa lawyer; kwa hiyo naomba niwaambie wadau wenzangu tatizo siyo sera ni utekelezaji...policy tuliyonayo ambayo ilikuja baada ya tume ya Shivji iko very protective kwa walala hoi...suala ni hakuna utekelezaji...

Kuna mapungufu ndiyo lakini pungufu kubwa ni kwenye utekelezaji...mfano ardhi ni mali ya umma; hivyo basi hizi lawama za commodification and marketization zinatoka wapi kama si utendaji duni?

Nilikutana na jamaa mmoja ni bosi mkubwa tu wa wizara nikawa nataka anipe data fulani; tena ni lawyer nikashangaa analeta bla bla nyingi...nikagundua hata yeye hajuhi sheria ya ardhi ikabidi ni google nilichokuwa nakitafuta nikakipata kwenye Village Land Regulation of 2001...kama wasomi wote wa hiyo wizara ni sampuli hii basi tusishangae wadau...

Najua hiyo new Act (land Act 1999 and Village land Act 1999) imeandaliwa na consultant wa UK inawezekana watumishi wa Wizara hawajaisoma yote maana ni like 300 pages; kwa mvivu hawezi jua kilichomo...
 

Sinywalulenga Muvina

Senior Member
Jun 14, 2013
124
225
Naunga mkono kwa mtoa hoja. Hoja hii ni ya msingi sana sana kwa watanzania ambao wanakosa ardhi hata ya kujenga kibanda chumba kimoja kutokana na bei kubwa ya viwanja.
Na mara nyingi hoja nyingi zenye mantiki kubwa kama hii huishia kusomwa na kuachwa tu.
Je, hakuna uwezekano wa kuanzisha/kufanya movement kushinikiza hili suala la ardhi kwa watunga sera, bungeni, wizarani na hata kwa mkuu wa nchi???
 

nyumba kubwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
10,313
2,000
Kabla ya kushinikiza land reform inatakiwa ujue kuna upungufu gani kwenye existing land policy au Act...

Tafuteni hizo sheria na sera mzisome...ziko online...

Hata tufanye reforms kila mwaka haitasaidia kama hatujuhi tatizo ni nini (law au agency)


Naunga mkono kwa mtoa hoja. Hoja hii ni ya msingi sana sana kwa watanzania ambao wanakosa ardhi hata ya kujenga kibanda chumba kimoja kutokana na bei kubwa ya viwanja.
Na mara nyingi hoja nyingi zenye mantiki kubwa kama hii huishia kusomwa na kuachwa tu.
Je, hakuna uwezekano wa kuanzisha/kufanya movement kushinikiza hili suala la ardhi kwa watunga sera, bungeni, wizarani na hata kwa mkuu wa nchi???
 

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,448
2,000
maisha bila kumliki ardhi ni sawa na kuwa mtumwa, je Tibaijuka ametusaidiaje waTz kumiliki ardhi kihalali na kwa gharama ambazo tunazimudu???
 

baharia Ar

JF-Expert Member
Dec 1, 2013
839
250
kama kuna mtu ana namba za tibaijuka plz anipe ninashida nae sana jaman,nimezunguka sana sijazipata humu naamin sikos plz plz plz
 

nyumba kubwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
10,313
2,000
Nenda kwenye blog ya Bunge nasikia wanaweka namba (sina hakika ila tokana na mjadala wa Kapuya inaonyesha hizi namba zinapatikana)

kama kuna mtu ana namba za tibaijuka plz anipe ninashida nae sana jaman,nimezunguka sana sijazipata humu naamin sikos plz plz plz
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom