Migogoro ya ardhi ilitulia sana awamu ya tano na nimpongeze Lukuvi, awamu hii ya kina Ridhiwani mbona kasi ya migongano inazidi?

omtiti

JF-Expert Member
Jun 19, 2019
1,022
1,590
Ukweli lazima usemwe awamu ya tano ilijitahidi sana kushughulikia migogoro ya ardhi kwa kiwango kikubwa sana na pongezi zimuendee hayati Magufuli pamoja na wasaidizi wake hasa waziri Lukuvi na timu yake yote ya wizara ya ardhi.

Mipango yao ilikuwa mizuri na yenye ufanisi hasa walipobuni ule mkakati mahususi wa kushirikisha wizara zote kwenye utatuzi wa migogoro ya ardhi nchini, walikwenda kwa pamoja na kumaliza kero mbalimbali.

Sasa tukija kwa hili la Ngorongoro na Loliondo inashindikana vipi?

Serikali iache ubabaishaji, tunayo wizara ya ardhi,maliasili utalii, sheria, na hata mambo ya ndani wajitokeze watupe tafsiri ya kinachoendelea katika eneo la Ngorongoro na Loliondo, vinginevyo ni hujuma inafanyika dhidi ya wananchi wa maeneo hayo kwa maslahi ya wachache
 
Back
Top Bottom