Migogoro kwenye vyama vya siasa chanzo ni wapambe wenye njaa kwenye vyama hivyo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Migogoro kwenye vyama vya siasa chanzo ni wapambe wenye njaa kwenye vyama hivyo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DT125, Dec 18, 2011.

 1. D

  DT125 JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2011
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 203
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Bila kubadilisha utaratibu wa kuendesha vyama vya siasa migogoro haitaisha. Haiwezekani tukawa na wanasiasa wanaoshinda maofisini kwa kujitolea huku wanafamilia na wategemezi mwisho wa mwezi unapita bila bila. Ukitembelea ofisi nyingi za vyama utawakuta watu wa namna hii. Kwa vyama vya siasa hasa vya upinzani vyenye ruzuku ambayo haitoshi kuwalipa mishahara kuanzia ngazi ya mkoa, wilaya na kata wangetafuta namna ya kuendesha ofisi zao huku wakiwa na muda wa kujishughulisha na shughuli za kiuchumi. Kwa mfano ili mtu apewe vyeo hivi ambavyo vinaendesha kwa kujitolea basi lazima ajulikane anapataje riziki yake ya kila siku, kuwachukua watu wa kijiweni wanaoishi kwa kupiga mizinga wenye nazo hawawezi kuvisaidia vyama hivi zaidi ya kufanya kazi za upambe kwa kuwachonganisha viongozi wao wa ngazi za juu ili wanufaike. Hata CCM Kuna watu utawakuta kazi yao ni kutembea na viongozi wa kitaifa, mikoa, wilaya na wabunge kila siku huku wakiwa hawana kazi nyingine ya kiuchumi. Wapambe wa namna hii ni kuwachonganisha viongozi wao. Ushauri wangu kwa vile vyama visivyo na ruzuku ya kutosha ofisi za wilaya na mikoa waweke mhudumu mmoja tu wa kuwahudumia wanachama kama kukatia watu kadi na kupokea barua. Viongozi wao wawe na muda na siku maalumu za kuwepo ofisini.
   
 2. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Kweli kabisa , Lakini pia vyama karibu vyote vya hapa Tz vinaungana kuilinda CCM na kuboma CDM
   
Loading...