Migogoro katika familia yachangia ongezeko la watoto mitaani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Migogoro katika familia yachangia ongezeko la watoto mitaani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Feb 17, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD]
  [​IMG]
  TANZANIA imeadhimisha miaka 50 ya uhuru, huku ikiwa na changamoto kubwa ya ongezeko la watoto wa mitaani na wale wanaoishi katika mazingira magumu.

  Ongezeko hilo la watoto wanaoishi katika mazingira magumu wakiwamo wale wa mitaani inatokana na kukithiri kwa migogoro katika familia pamoja na njaa.

  Tumeona mara nyingi wazazi wengi wanapokuwa na migogoro katika familia, wanashindwa kutunza familia zao kikamilifu, ikiwamo kushindwa kuwapa malezi bora watoto wao.

  Takwimu kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto(UNICEF) zinasema kuwa, idadi ya watoto wanaoishi mitaani na wale wanaoishi katika mazingira magumu inakadiriwa kufikia 120 milioni duniani.

  Taarifa inasema, asilimia nne ya watoto hao wa mitaani hufanyiwa ukatili baada ya kuvunjika kwa ndoa.
  Miongoni mwa watoto hao, 30 milioni wako katika bara la Afrika ambapo Tanzania ni moja kati ya nchi hizo yenye changamoto kubwa ya ongezeko la watoto wa mitaani kila kukicha.

  Watoto milioni 50 kati ya hao ni yatima kwa sababu mbalimbali likiwamo gonjwa la Ukimwi.
  Ripoti hiyo inaeleza kuwa eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara limeripotiwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya watoto wanaofanyishwa kazi ngumu na hatari katika bara la Afrika.

  Takwimu hizo zinaeleza kuwa zaidi ya theluthi moja ya watoto hao wana umri ulio kati ya miaka 5 hadi 14 na wanafanyishwa kazi ngumu.
  Kulingana na UNICEF, katika bara hilo la Afrika, maelfu ya watoto wanateswa, kutumiwa vibaya pamoja na kufanyiwa ukatili.

  Ripoti inasema ni wakati sasa kwa jamii kujikita katika kuimarisha misingi ya familia bora na malezi, kwani hatua hiyo itasaidia kupunguza watoto wa mitaani.
  Mbali na takwimu hizo, Utafiti uliofanywa hapa nchini Agosti, mwaka 2009 na shirika lisilo la kiserikali la Uingereza “Consortium for Street Children,” umebaini kuwapo idadi kubwa ya watoto wa mitaani.
  Utafiti huo uliofanyika katika miji mikuu saba hapa nchini umebaini sababu mbalimbali zinazochangia kuwapo kwa idadi hiyo, huku njaa na ukatili wa majumbani vikiongoza.

  Miji hiyo ni Dar es Salaam, Morogoro, Iringa, Mbeya, Dodoma, Singida na Kilimanjaro ambako utafiti ulibaini ongezeko kubwa la idadi ya watoto wanaoishi mitaani huku jiji la Dar es Salaam likiongoza kwa kuwa na watoto wengi wanaoishi mitaani.

  Mbali na takwimu hizo, imebainika kuwa asilimia 50 ya watoto wanaoishi mitaani pamoja na wale wanaoishi katika mazingira magumu inatokana na ukatili unaofanywa majumbani dhidi ya watoto hao.
  Kadhalika asilimia 35 ya watoto hao wanaoishi mitaani inatokana na watoto hao kuzikimbia familia zao kutokana na njaa pamoja na umasikini uliokithiri.

  Kwa mujibu wa ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, idadi ya watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani duniani kwa sasa inakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 100.

  Licha ya kuwapo sheria zinazowalinda watoto juu ya ukatili lakini inaonekana kuwa sheria hizo bado hazijapewa kipaumbele kama sheria nyingine.

  Katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika ya mwaka jana, ambayo hufanyika Juni 16 ya kila mwaka, Mkurugenzi wa Idara ya maendeleo ya watoto nchini, Tukae Njiku, alisema serikali inapaswa kuangalia upya tatizo la ongezeko la watoto wanaoishi mitaani kutokana na hali halisi na ukubwa wa tatizo hilo hapa nchini.

  Njiku anasema hivi sasa wizara imeandaa mpango mkakati wa kutokomeza tatizo la watoto wanaoishi mitaani na kuimarisha ushirikiano kati yake na halmashauri za wilaya na manispaa, miji pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali katika kukabiliana na tatizo hilo.

  Anasema wizara imeamua kubadilishana uzoefu wa jitihada zilizopo kutoka kwa wadau ili kuelewa majukumu na wajibu wa kila mmoja katika kudhibiti tatizo hilo.

  Kadhalika wizara hiyo imeweka mikakati kwa halmashauri na jamii ili kupambana na changamoto za kuondoa kero ya ongezeko la watoto wanaoishi mitaani hususan katika miji mikuu.

  Sanjari na wizara hiyo kuonyesha njia ya kupunguza idadi ya watoto wanaoishi mitaani lakini bado ina changamoto kubwa ya kuhakikisha kuwa inapunguza idadi hiyo kama sio kuondoa kabisa watoto hao wa mitaani na wale wanaoishi katika mazingira magumu.

  Anasema wizara tayari ipo katika mchakato wa kuandaa kanuni za maadili ya sheria ya mtoto ya mwaka 2009 ambayo inalenga kumlinda mtoto dhidi ya ukatili na kumpatia fursa ya kumwendeleza.

  Njiku anasema kabla ya kutungwa kwa sheria ya mtoto ya mwaka 2009, masuala ya mtoto nchini yalikuwa yameainishwa katika sheria ya malezi sura ya 278,sheria ya kuasili mtoto sura ya 335,sheria ya udhibiti wa nyumba za watoto sura ya 61 pamoja na sheria ya watoto na vijana sura ya 13.

  Anasema mbali na kutungwa kwa sheria hiyo, bado inaonekana kuwa sheria nyingi zinasababisha ugumu katika uelimishaji na utekelezaji wa masharti, hali ambayo inalazimisha kuwa na idadi kubwa ya watoto wa mitaani hapa nchini.

  Hata hivyo inaonekana kuwa pamoja na sheria hiyo kupitishwa lakini utekelezaji wake ni mdogo ikilinganishwa na jinsi matukio yaliyopo.

  Anasema wazazi na walezi wana wajibu wa kuhakikisha kwamba wale wote watakaobainika kufanya vitendo vya ukatili kwa watoto watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria hiyo.

  “Ifike wakati kwa wadau na jamii kwa ujumla kushirikiana na serikali kuhamasisha watoto hao juu ya kujenga ufahamu na kusimamia sheria na haki za watoto ili kupunguza kasi ya kuwapo kwa watoto wa mitaani,” anasema Njiku.

  Aidha Njiku anasema, wazazi hawana budi kurudi katika misingi ya maadili ili waweze kuwajibika kuwatunza watoto.
  Vilevile anasema serikali na jamii kwa ujumla vina wajibu wa kuongeza juhudi katika kulinda maslahi ya watoto[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  chanzo. Migogoro katika familia yachangia ongezeko la watoto mitaani
   
Loading...