Migodi Mikubwa na Viwanda vya Bia Tanzania Kufungwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Migodi Mikubwa na Viwanda vya Bia Tanzania Kufungwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by spencer, Jul 6, 2012.

 1. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #1
  Jul 6, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,556
  Likes Received: 945
  Trophy Points: 280
  GreatThinkers,
  Kwa mujibu wa duru za uhakika, wataalamu wengi wazalendo wameendelea kuacha kazi migodini hii inatokana na sera chafu za Unyang'anyi za serikali ya CCM kuwa hakuna kuchukua NSSF hadi ufike miaka ya kustaafu. Sheria iko mbioni kuanza kufanya kazi mwaka huu.
  Taarifa nilizozipata mpaka sasa ni kama ifuatavyo.
  NorthMara-43 Geita-86 Buzwagi-33. TBL Mwanza 4, SBL Mwanza-6 hii record ni kuanzia Jumatatu wiki hii.
  Kwa nini wanaresign?
  • Hawataki kunyanyasika kama wastaafu wa Afrika Mashariki wanavyohangaishwa
  • Inawezekana pesa zao zikaibiwa na waezi wao wakakimbia nchi na kuwa raia wa nchi zingine kama ilivyotokea kwa baadhi ya wezi waliozushiwa kufa wakati wanakula bata Boston
  • Ni afadhari wale jasho lao, kwani wakichua hela zao na kujenga nyumba wakapangisha wataishi hata bila mafao toka NSSF
  • Inflation ya kutisha
  • Hakuna dalili za watu kuogopa au kuacha kuiba mali ya umma
  • nk
   
 2. Mshuza2

  Mshuza2 JF-Expert Member

  #2
  Jul 6, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 3,427
  Likes Received: 1,011
  Trophy Points: 280
  'Duru za uhakika'...kama ndivyo basi kazi ipo,jamaa wanabuni mbinu mpya kila siku kutudhulumu!
   
 3. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #3
  Jul 6, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,830
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  ccm km kiwavi fedhuli
   
 4. mgodi

  mgodi JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,039
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Hiyo sheria yao wakiipitisha watatumaliza wengi
   
 5. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #5
  Jul 6, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,889
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Mkuu kama hiyo sheria inaandaliwa ni wazi kwamba ikipelekwa kwenye bunge la magamba itapita tu kwa "asimilia 200". Wabunge wa magamba hawako pale kuwawakilisha wananchi bali kulinda chama chao legelege na serikali yake dhaifu.
   
 6. Nyasirori

  Nyasirori Senior Member

  #6
  Jul 6, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 166
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Sijawahi kushabikia chama chochote cha siasa, lakini kwa kwa sheria hata mimi nimehisi kuanza kuichukia CCM.
   
 7. w

  wikolo JF-Expert Member

  #7
  Jul 6, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 801
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Serikali huwa zinakuwepo kwa lengo la kulinda masilahi ya watu waliozichagua lakini hii ya kwetu iko tofauti kabisa kwani inalinda masilahi yake kwanza! Mfanyakazi huyu ndo mtu anayelipa kodi kubwa kabisa kutoka kwenye kipato chake cha kila mwezi kwa ajili ya mapato ya serikali na kiasi kinachobaki kwa ajili ya kuweka akiba ya baadaye ni kama hakipo kabisa. Ni wachache sana wanaoacha au kuachishwa kazi Tanzania hii ambao huwa tayari wamekwisha jenga japo nyumba na hii ni kutokana na hali halisi ya vipato vya wafanyakazi wa nchi hii (kwenye kundi hili nimewatoa wale wanaofanya ufisadi). Ukweli ni kwamba mtu anaacha kazi akiwa hana akiba yoyote ya kumsaidia na kwa maana hiyo akiba pekee ambayo anaitegemea ni NSSF/PPF na mifuko mingineyo.

  Hivi leo hii kwa mfano nina miaka 40 halafu unaniambia nisichukue pesa hiyo ya akiba hadi nitakapofikisha miaka 55, familia itakula na kulala wapi kwa miaka hiyo 15 wakati nasubiri kufikisha miaka 55? Karo ya shule kwa ajili ya watoto itatoka wapi? Kikubwa zaidi ni kuwa uhai unatoka kwa muumba, kama nakufa sijafikisha umri huo, familia itapata shida kwa kiasi kikubwa na pengine hawataweza hata kuzipata hizo fedha kutokana na dhuluma za ndugu na jamaa. Ninachokiona hapa ni uandaaji wa kundi lingine la wazee ambao watakuja kuhangaishwa kama jinsi tunavyowaona wale wa afrika mashariki sasa!

  Ni bora nikaacha kazi sasa hivi kuliko kusubiri kuja kulala kwenye lami na kumwagiwa maji ya kuwasha hapo mwaka 2025 wakati nikiwa nadai pesa zangu!
   
 8. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #8
  Jul 6, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,952
  Likes Received: 262
  Trophy Points: 180
  Karibu kwenye kundi la watu enye akili mfano wa wapenda CDM. Binafsi ndo nasikia leo, na kama ni kweli basi serikali ina dhamira ya kutaka kuwauwa watu wake. Sipati picha yaani kama leo nimeachishwa kazi na mwajiri wangu, then ili niweze kupata haki yangu basi kama nina miaka 40, itabidi nisubiri miaka 20 mbele ndo nije kupata hiyo haki yangu, looooooooh jamani CCM mbona wanatumia masaburi kiasi hiki ktk kufikiri, kuamua na kutenda!.

  Ukion hivi ujue tayari NSSF inaelekea kufilisika maana kutumia hela za wafanyakazi kujengea vitega uchumi ambavy vina-break even after half a century unategemea nini hapo? Waangalie namna nyingine ya kuzirundika hizo hela sio kwa kutumia njia hii. Yaani hii serikali inataka kuleta mtindo wa kijinga kama wanaotumia kwa watumishi wao kwa mashirika kama ya LAPF, PPF na PSPF, waachane na huo ujinga kabisa.

  Kama ni maandalizi ya mahali pa kupata hela kwa ajili ya kampeni zao za 2015, kwa kweli waangalie source nyingine sio hii NSSF ambayo kimsingi ndiyo yenye kipato kikubwa na ambayo waliitumia sana kukopa hela kwa ajili ya kumuweka Mkapa madarakani. jamani serikali inatosha kwa mliyoyafanya kwa EPA, huku kwa sisi wanyonge tuachineni wenyewe, chonde chonde Mgimwa na wenzako mlioko hazina, NSSF ingawa ndio kimbilio lenu la kukopa, haitakuwa na maana kukopa kwenu NSSF basi shurti muwaletee mateso watumishi wa sekta binafsi, chonde chonde!

  Mmesha fanya maovu mengi na ni kama nchi imebaki mifupa tupu, basi ondokeni salama mtuachie mifupa hii ili tuangalie utaratibu wa kujazia nyama upya, maana nyie mmeshindwa kutuondoa toka hapa tulipo, mweeeeeee! Kwanini watanzania walihadaiwa wakamchagua RAIS mwenye mikosi kiasi hiki?
   
 9. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #9
  Jul 6, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,952
  Likes Received: 262
  Trophy Points: 180
  Jinsi serikali inavyocheza na hela za mfuko huu, ni wazi unakaribia 'kukauka' hivyo huu ni mkakati wa kujaribu kuulinda ili walau bumu hili lisjie likailipukia serikali mikononi kabla ya 2015
   
 10. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #10
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,556
  Likes Received: 945
  Trophy Points: 280
  hali ni mbaya sana Bulyanhulu.
  karibia wamegoma.
  wakati wowote HR kuwafukuzwa
   
 11. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #11
  Aug 3, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,877
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  Ooooh My Gosh! Bora MIGODI YA MADINI tu ndiyo ifungwe kwasababu yenyewe haichangii kitu kwenye pato la TAIFA. Ipo kwaajili ya kuwanufaisha wazungu na mafisadi wachache wa Kitanzania. Lakini siyo viwanda vya bia kama TBL ambaye ndiye MLIPAJI NAMBA MOJA wa kodi Tanzania.

  Mark my words Kama viwanda vya bia vikifungwa SERIKALI ita collapse within a couple of months. Na ka-Banana republic (Read Malawi) katachukuwa ziwa Nyasa lote because tutakuwa hatuweza kupigana tena VITA!

  Mungu wangu hebu wape SENSE hawa "WATAWALA" wafutulie mbali hii sheria ya SSRA.
   
 12. Pelekaroho

  Pelekaroho JF-Expert Member

  #12
  Aug 3, 2012
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,490
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Hiyo mkuu ishapitishwa na baba mwanaasha ashairuhusu kuanza kutumika kwa hiyo tayali ipo kazini.
   
 13. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #13
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,723
  Likes Received: 979
  Trophy Points: 280
  hatuitaki hii sheria! Kwisha!!
   
 14. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #14
  Aug 3, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,489
  Likes Received: 429
  Trophy Points: 180
  Hamuitaki sheria ambayo isha pitishwa april! Wabunge wa upinzani waliipinga ila walizidiwa na sauti za ndioooo!
   
 15. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #15
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,275
  Likes Received: 353
  Trophy Points: 180
  Slaa aliwai sema hii nchi haita tawalika sijui ndo imeanza kutotawalika
   
 16. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #16
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 5,918
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mkuu unadhani hata hiyo vita na Malawi ingeanza leo jeshi letu lina uwezo wa kupigana? Kuanzia logistics hadi personnel kila kitu fake.
   
 17. Makala Jr

  Makala Jr JF-Expert Member

  #17
  Aug 3, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 3,398
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Ndiyo maana siku hizi hata ile hamasa ya kuimba wimbo wa taifa imepungua...watu wanapotezewa uzalendo wao na serikali ya chama cha zamani
   
 18. Lawrence Luanda

  Lawrence Luanda JF-Expert Member

  #18
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 707
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sheria ilishapita tangu April na Raisi keshai sign.............tunachosubiri ni kama kutakuwa na marekebisha bungeni
   
 19. M

  Mwanaharakatihuru JF-Expert Member

  #19
  Aug 3, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 480
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Bunge walifanya makusudi ili wapate allowance
   
 20. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #20
  Aug 3, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,133
  Likes Received: 1,515
  Trophy Points: 280
  Eeeh. Hii kali. Kama kweli wanaacha kazi watakuwa wamesaidia kuwa na nafasi kwa ajiri ya ajira mpya.

  Hivi mtu unafanya kazi ili upate pension ya ujanani???
   
Loading...