Sophist
Platinum Member
- Mar 26, 2009
- 4,484
- 3,400
Ndugu yangu inaelekea Siasa zinakupeleka mahali pabaya. Kama ungekuwa umefanya utafiti usiokuwa na mawaa si ungegundua ukweli kuwa Acacia tangu wawekeze kwenye dhahabu hapa nchini hawajawahi kulipa CIT? Sasa kuna mantiki gani kuwa na ulichokiita tozo kubwa ya CIT (30%) wakati wala tozo hiyo hailipwi? Lakini iwapo ulifanya utafiti kweli si ungegundua kuwa Zambia inatoza CIT asilimia 35 kwa Shaba yake? Lakini si ungegundua kuwa GGM walianza kulipa CIT waka 2012? na Resolute Mining vilevile? Sasa hizo discouraging CIT payables yamelipa makampuni gani? Ndugu yangu unafunikwa/utafiti wako umefunikwa na mahaba ya Siasa za upande fulani.Ni nini kisicho sawa? Watanzania wanaendeshwa kwa hisia. Niliwahi kufanya utafiti wa kodi zinazotozwa kwenye migodi ya Tanzania, nikalinganisha na mataifa mengine, sisi tupo kwenye kundi linalotoza kodi kubwa, japo siyo juu kushinda mataifa yote. Tunatoza corporate tax 30%, hakuna anayetoza zaidi ya hiyo lakini wapo wanaotoza pungufu. Tunatoza mrabaha 4%, ya juu kabisa inatozwa na Zimbabwe 7% lakini wao wanatoza corporate 28%, nchi kama Canada na Australia mrabaha ni asilimia sifuri. Tunasema tunaibiwa, tunajua tunachoibiwa?
Sidhani ban ya kupeleka nje concentrate imetokana na kuibiwa. Nadhani ni kutaka kuwalazimisha Acacia kujenga mitambo ya kuchenjulia shaba ndani ya nchi kwa nia ya kuongeza ajira na wala siyo kwa nia ya kuzuia 'kuibiwa', kama wengi wanavyoropoka.