Migiro kuwa mbunge, je ni mpango wa Rais kumteua kuwa Waziri?

mkigoma

JF-Expert Member
Jul 26, 2011
1,180
309
Rais jakaya mrisho kumteua kuwa mbunge, je ni mpango wa kumuandaa kuwa waziri ili kumtengeneza 2015 kuwa Rais wa Tanganyika au makamu wa Rais wa JMT?
 
Rais jakaya mrisho kumteua kuwa mbunge, je ni mpango wa kumuandaa kuwa waziri ili kumtengeneza 2015 kuwa Rais wa Tanganyika au makamu wa Rais wa JMT?

Kumteua migiro maana yake Mulugo, Malima, Magembe na Chiza waanze kufungasha!
 
mmhh, kukubali uwaziri kwenye Serikali hii tena kwa muda huu uliobakia unaweza kuharibu CV yako!!
 
Rais jakaya mrisho kumteua kuwa mbunge, je ni mpango wa kumuandaa kuwa waziri ili kumtengeneza 2015 kuwa Rais wa Tanganyika au makamu wa Rais wa JMT?

Huyu yupo katika mchakato - anapikwa kuwa mgombea wa urais wa JMT kwa tiketi ya ccm 2015. Wale wa Lowasa walie tu.
 
Siyo kwamba anamuandaa kumrithi Prof. Mgimwa. Nasikia yuko mahututi huko Afrika ya Kusini
 
Huyu yupo katika mchakato - anapikwa kuwa mgombea wa urais wa JMT kwa tiketi ya ccm 2015. Wale wa Lowasa walie tu.

Komredi Lowassa ataiua ccm kabisa wasimpompa 2015...atasponsor upinzani na wagombea binafsi na kumeguka na kipande kikubwa cha ccm...watz hawako tayari kwa kuwekewa Rais wa kulinda usultani wa Bagamoyo
 
Lowassa hata akiwa ni kiongozi mzuri lakini tatizo hasafishiki.

Siyo kwamba anamuandaa kumrithi Prof. Mgimwa. Nasikia yuko mahututi huko Afrika ya Kusini

Umeshirikisha vema sense yako ya hisia. Hili ndo neno la mujini.
Ila usishangae ukisikia kimya kwa sababu mkuu wa kaya anafatiliaga tetesi. Akiona mmeongea sana anapotezea.
Si unajua watu wakikushtukia unatokea mlango huu unazuga unatokea mlango mwingine?
Wanaita poteza maboya kumbe wapiiiiiiiiiiii.
Jamaa wamestukia chezo unazuga zuga.
Hi hi hi hi hi hi hi.
Hata hizi ni hisia zangu tu mkuu. Nichukulie poa.
(Ila ulichonena hapo juu chote ni ukweli, wala sio hisia)
 
Watu wengi hatulitambui hili mtu anaweza kusimama upande mmoja akafanya vizuri na upande mwingine akaboronga mfano enzi za keenja kuwa mkuu wa mkoa wa dar alisimama vizuri jiji likawa safi kutokana na umahiri wake akatumia nyota ile kuombea kura kupitia ubunge jimbo la ubungo akashinda kwa kishindo waliokuwa wakazi wa jimbo hilo wanajua alivyoboronga wapo viongozi wengine wengi tu wanaofanana na hawa kwa ndg asharose kwa mimi naona nyota yake ilikuwa u.n lakini kuwa kuwa kiongozi wajuu sijaona bado
 
Back
Top Bottom