Migiro (for Presidency 2015) na Tibaijuka (Uwaziri Mkuu 2010) Wanatosha Kuitakasa CC

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
1,190
Naona kwa sasa CCM ghafla wamekuja na ghiliba mpya kwa kuegemea NGUZO mpya ya

(1) JINSIA ya kike katika siasa ya nchi yetu. Hali hii inafuatia baada ya zile ghiliba za ->

(2) UDINI na siasa za Kadhi Mkuu mara Tanzania yangu kuvikwa kanzu ya OIC, zote kushindwa kufua dafu. Nako pia ->

(3) Mbinu ya kutumia silaha ya HOFU YA KUMWAGIKA DAMU na sasa _>

(4) UCHAKACHUAJI kuchukua mimba toka kwa UFISADI wa kukwapua hadi MBEGU zinazohitajika kupanda shambani ili wananchi nasi tupate japo ka-ahueni ya maisha kidogo, zote kukubuhu.

Je, kuja kutubadilishia tu SURA na JINSIA kwenye safu ya uongozi wa Juu kwa kuwaleta Asha-Rose Migiro (Urais 2015) na Tibaijuka (Uwaziri Mkuu 2010) itageuka kuwa sabuni tosha ya kuitakasha CCM na UCHUNGU MKALI waliotuletea kimaisha hata wasomi tunaoneka wehu mbele ya waungwa Waopoaji Wazoefu kama Rostam Aziz, Lowasa, na wengineo kweli?? Hebu nipeni maoni yenu hapa.

Nahitaji KATIBA mpya sasa hivi!!!
 
Kinachoangaliwa na kukubaliwa na jamii ni uwezo wa mtu na c jinsia aliyonayo... Kama Migiro ni msafi na ana uwezo , basi hata jamii itasupport kugombea kwake, na si suala la eti kufanya hivyo ni kufumba macho ya wananchi juu ya kashfa za chama tawala. Sasa wananchi wenye uwelewa hawadanganyiki.. they know what is right and wrong.. Problem ni mfumo uliopo wa mabavu na lazima..
 
Nini tangible for Tanzania kimefanywa na hawa watu mpaka wastahili nafasi hizo?
 
Kwa lipi ndugu yangu!huyu mama ameifanyia nchi nini mpaka apewe nafasi kubwa ya juu kama hii?
 
Kama wanaweza sisi wapambane na wanaume na wawashinde! Sio kuondoa wanaume mnasimamisha wanawake watupu kwa kisingizio cha jinsia! Wanawake hawawezi mnawabeba!
 
Nafikiria kuurudisha mfumo DUME uwe mfumo rasmi kuwabana hawa!!
 
Si mama Migiro alikuwa waziri tena kwa muda mrefu tu lakini hatukumsikia makali yake kama akina Magufuli. Sasa leo akija tutegemee jipya kutoka UN au??

Hata hivyo CCM haitaki uwezo kama ingekuwa hivyo mbona Salim alikataliwa??

CCM ina wenyewe na sidhani kama Migiro yuko kwenye hilo kundi.
 
Mimi nafikiri tusiwakubali sana hawa watu wa kuandaliwa kwa ajili ya kulinda maslahi ya mafisadi, cha msingi hapa ni kuangalia ni nani anipenda Tanzania na watu wke kwa vitendo.

Kuna watu ni wasafi ila kwa kuwa wanaandaliwa na mafisadi kushika vyeo tunakuwa hatujafanya kitu, just imagine JK alivyokuja 2005, mbowe alikuwa anawaambia watu ukweli lakini hawakuamini na sasa wameamini kwa hiyo tusiwarudishe nyuma. tusonge mbele.

Peoples Power
 
iNASIKITISHA SANA TENA SANA KUONA KUWA HAWO AKINA MIGIRO HAWAPO KWA INTEREST YA KUPAMBANA NA MAFISADI BALI KUTIMIZA INTEREST ZAO YAANI NIONA TANZANIA 2020 ITAKUA IMEKONDA NA KUWA NA MAJERAHA MENGI HAPO NDIPO KILO MOJA YA NYAMA ITAUZWA TSH 15,000, MCHELE 9000TSH, UNGA KILO 1 5000 MANA HALI ITAKUA MBAYA

WANA JF KARIBU WENGI WETU NI WASOMI TUJE NA MIKAKTI MBADALA YA KUHAKIKISHA TUNEENGUA TANZANIA KWENYE MIKONO YA MAFISADI OTHERWISE ITAKUA MBAYA , HAWA JAMAA WANAONGELEA SWALA LA UJINSIA HAWALIONGELEI SWALA ZIMA LA MASLAHI YA TAIFA KUWEKA HISTORIA NI KITU KINGINE NA SWALA LA MASLAHI NI SWALA LINGINE

MZEE GOMEZI
 
Mimi naona hii tabia ya ku-speculate ya 2015 kwa sasa tuyaache, ila labda mtoa mada haja yake ni kupotosha au kuponza magumu ya maisha wanayo pata sasa hivi. kwa sababu matatizo ya watanzania ni ya sasa na wala kesho hatujui tutaingiaje. Ingekuwa nchi yetu imetulia kiuchumi au kisiasan kupanga hayo ya 2015 ni sawa, lakini leo hii hata waziri mkuu wa 2010 to 2015 hatumjui, baraza la mawaziri hatulijui, lakini tuna diriki kuanza gombania/kuzozana raisi au waziri mkuu wa 2015.
hayo ni maoni yangu.
 
Now that some names have been speculated for the 2015 general elections on ccm ticket, can't hide my feelings on the top three ladies who can be earmarked as candidates for the first ever, woman president in Tanzania. Amongst them, Dr. Migiro ranks top, followed by Speaker Anne Makinda and prof. Tibaijuka respectively. GO LADIES GO!
 
Back
Top Bottom