Zed
JF-Expert Member
- Mar 28, 2009
- 434
- 252
Tatizo la siasa zetu ni za "personality cult", tunaweka rehani future ya watu million 40 na kitu kwa mtu fulani! Yaliyotupata na serikali hii JK bado haijatufundsha! Jirani zetu Kenya, ambo matatizo yao yalikua makubwa zaidi wameanza kufunguka macho. Sasa wako kwenye mchakato ulionza na katiba mpya na unaendelea na kujenga "institutions" au taasisi ambazo zitawahakikishia utawala bora! Mfano ni process ya kumpata jaji mkuu imefanywa kwa umakini mkubwa na sasa wanendelea na taasisi nyingine! Sisi bado tunajadili watu, oh Migiro! Watanzania! Kikubwa sasa ni Katiba Mpya, amabayo Itatuhakikishia Uchaguzi huru na wa haki, Bunge Huru na lenye standard, Serikali inayoweza kuwajibishwa, Mahakama Huru... Tubdilike tupigania katiba mpya na uundwaji wa taasisi madhubuti! Obama alitupa waafrika ushauri wa maana sana. Ninamnukuu katika tafsiri: Afrika haiitaji strong men, Afrika inahitaji taasisi madhubuti! Miaka 50 ya Uhuru tusirudie makosa tujifunze kutokana na makosa!