Migiro Aapishwa Rasmi

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,442
113,452
Mhe. Dr. Asha Rose Migiro ameapishwa rasmi asubuhi hii, kuwa Mbunge wa Bunge la JMT.

Dr. Asha Rose Migiro, Akiapa Kiapo cha Ubunge wa Bunge la JMT.

Dr. Asha Rose Migiro akiingia bungeni huku akitanguliwa na wapembe wa bunge, na nyuma akisindikizwa na wapambe

Picha ni kwa hisani ya Mwanajf GRANDPUBA
Pasco

Namaanisha kwamba kuwa yule aliyekuwa naibu katibu wa UN

hilo nijambo zuri lakini bado najiuliza kwanini JK ameamua kumteua katika nafasi hiyo ya ubunge right now?
 
Mkuu kwa standard yoyote iliyokwenda shule. Kwa kigezo chochote cha busara za kisiasa, Migiro hapaswi kuwa waziri, leave alone mbunge wa kuteuliwa. Nadhani ingekuwa busara kama angesubiri kugombea jimbo mwaka kesho. Sidhani kama mbunge wa kuteuliwa anaweza kuwa PM (stand to be corrected)
 
Asha Rose Migiro ameapishwa rasmi asubuhi hii

Hongera yake kwa kuingia kwenye mjengo. Anaandaliwa for 2015 highest position. Pasco unacheza na alama za nyakati wewe!!!!!! Lowassa akipigwa chini mdada unaye, akipigwa chini machinga uko naye hahahaaaaaa
 
Last edited by a moderator:
Ahaaa sasa nimeelewa kwa nini mizengwe anaandaliwa 'No Confidence Vote' kumbe kale kamkakati kaliko mtoa machozi 6 kameisha anza rasmi ' tusubiri hili 'li-move' la kihindi litakuaje
 
Nadhani ni mkakati mzuri kwa CCM na Taifa kwa ujumla. Rais amefanya vema kwa sababu amemteua mtu mwenye sifa nzuri kitaaluma-mama msomi aliyebobea, mjuzi wa siasa za kimataifa ambazo ilikuwa ni kwa sababu ya kufaulu siasa za nyumbani. Lakini pia uwezo binafsi wa Dr Migiro, uadilifu wake na unyenyekevu unanifanya niamini tunamhitaji mama sio tu kwa bunge na chama chake ambapo ni mjumbe wa Kamati kuu lakini nashawishika kusema wa nchi ya Tanzania kwa ujumla. Ninachomshauri mama ni kujaribu kujiondoa kwenye makundi maovu ndani ya chama chake, kutetea sifa yake njema, kusimama na wananchi wanyonge na kujionyesha kama msomi. Hongera mama Migiro. Naunga mkono hoja ya JK.
 
Ahaaa sasa nimeelewa kwa nini mizengwe anaandaliwa 'No Confidence Vote' kumbe kale kamkakati kaliko mtoa machozi 6 kameisha anza rasmi ' tusubiri hili 'li-move' la kihindi litakuaje

Huyu Asha hawezi kupata uwaziri mkuu kwa ubunge wa dezo.

Waziri mkuu ni lazima awe mbunge wa kuchaguliwa na wananchi jimboni.
 
Huyu Asha hawezi kupata uwaziri mkuu kwa ubunge wa dezo.

Waziri mkuu ni lazima awe mbunge wa kuchaguliwa na wananchi jimboni.

Unahangaika na mtu mwenye uwezo mdogo wa kufikiri, yeye kila kitu ni kuchangia tu.
 
kwahiyo hiyo mukulu ameona ndiiiioooo za ccm hazitoshi, kaamua kuongezea nguvu? kwani anaenda kuleta mada mpya?
ni kumwongezea mzigo mwananchi tu!
 
tamaa mbele and two feast kuna mdau humu anafanana kitabia na mzee wa kwenye hii story, kaenda kwenye harusi ya lowasa kaona msosi unachelewa kakimbilia kwenye harusi ya migiro akikuta msosi umeisha atarudi kwa lowasa ambapo atakuta geti limefungwa hivyo kukosa vyote
 
Hongera yake kwa kuingia kwenye mjengo. Anaandaliwa for 2015 highest position. Pasco unacheza na alama za nyakati wewe!!!!!! Lowassa akipigwa chini mdada unaye, akipigwa chini machinga uko naye hahahaaaaaa

Hii nimeipenda sana!!! Kumbe nawe unafuatilia nyendo zake? ila #Pasco ni mtu safi anafaa kila idara maana hachukui bahasha kabisa!!
 
Back
Top Bottom