Mifuko yetu ya hifadhi ya jamii na athari kwa wa-tz

Jayfour_King

JF-Expert Member
Nov 15, 2009
1,135
128
Mimi ni mdau kwa maana ya kuwa mteja wa mmojawapo wa mifuko hii. Leo ningependa niongelee matatizo ambayo yanatuathiri sisi kama wanachama na jinsi ambavyo watunga sera wasivyo na habari,ukereketwa na wala taarifa sahihi kama malengo ya mifuko hii yanafikiwa.
Kilichonifanya nishawishike kuandika kuhusu suala hili ni kufuatia marekebisho yaliyofanywa na bunge mwezi April na kusababisha migomo katika baadhi ya taasisi ikiwemo migodi. Kikweli suala hili ni la kitaifa na lilipaswa kukemewa hivyo na wafanyakazi wote wa nchi hii kama walivyoonyesha wenzetu hao wa migodini.
Naamini kilichopelekea ukimya ni ule ukondoo wa kawaida wa watanzania kutokuwa na hasira stahili kwenye mambo ya msingi kama hili, ambalo linahusu mafao ambayo ndio dira ya pale utakapokuwa huna uwezo tena wa kipato.Tunakaa kimya na baadaye ndipo unakuja kutambua kwamba sheria Fulani ilikuwa mbaya wakati athari imeshachukua nafasi yake. Wakati huo utakuwa sio wa kuzungumzia marekebisho ya sheria bali utekelezaji na athari zake.
Mfano hai ambao mimi naweza kuutoa ni kwamba: Mimi kama muhusika wa hili niliajiriwa kwenye taasisi mojawapo ambazo kimfumo nililazimika kuunganishwa na mfuko uliokuwa unaitwa NPF ambao ndio sasa unaoitwa NSSF.
Baadaye Vigezo vyangu vya ajira vilibadilika na hivyo nikalazimika kuunganishwa upya na PPF haya yalifanyika na bila kuhamisha chochote ambacho nilikuwa nimechangia kwenye mfuko nilioanza nao, hivyo mafao ambayo nilichangia kwa miaka 11 nikawa nimeyaacha nyuma. Hii ilikukwa mwaka 2001 na kiwango cha michango ambayo nilikuwa nimeshachangia tayari kwenye mfuko niliotoka ilikuwa kama 2,000,000 tu hivi. Pamoja na kuhama huko mfuko bado sheria hairuhusu kuchukua pesa hizo wala kuhamisha!
Leo hii ikiwa ni miaka 11 baadaye kiwango cha pesa ki idadi kiko vilevile. Hapa utaona kwamba thamani halisi ya pesa ile imeshuka kwa zaidi ya mara mbili. Kwani wakati huo (2001) wakati naachishwa kuchangia kiwango cha $ US (Dola ya kimarekani) ilikuwa Tshs 800 ambapo sasa ni zaidi ya Tshs 1600.
Tunachoomba kiangaliwe hapa pamoja na mambo mengine kuhusu hii mifuko yetu ya pensheni ni kwamba iwepo sheria ya kuthaminisha pesa ki thamani sambamba na wakati iliyo wekwa na sio kuangalia tu idadi kama wafanyavyo sasa huu kwa kweli ni wizi, ikizingatiwa kwamba pesa zenyewe zinafanyiwa biashara na zinaleta faida.
Haifai hata kidogo risk ya kushuka thamani akaachiwa mtu ambaye hafaidiki kwa chochote na hiyo pesa kwa wakati huo. Hebu fikiria wakati wa kustaafu mtu unakuja unapewa pesa ambayo ilikuwa na idadi hiyo hiyo mika ishirini baadaye, bila kuzingatia thamani itakuwa na maana yoyote?
Hapa tunawaomba wabunge wetu marekebisho haya yatakaporudishwa bungeni hapo mwezi wa kumi, wajaribu kuwa makini katika kunusuru mustakbali wa suala hili kwani suala hili ni tete, ikizingatiwa kwamba mishahara yenyewe ni midogo kuweza kukidhi mfanyakazi kujiwekea pensheni ya kutosha. Sasa hata pale ambapo amefanikisha hicho kidogo na bado kinachakachuliwa inafaa jambo hili liangaliwe kwa umakini mkubwa sana.
 
Yote uliyosema yalisha lalamikiwa muda mrefu nyuma. Huwezi kupata haki kwenye sahani, this will never change kama mwendo ndio huu. Katiba iseme wazi kuhusus thamani ya hele inayowekwa leo, baada ya miaka 30 thamani yake itakuwaje. Judges, Presidents and other high ranking officials, pension zao zinakuwa rated according to the current pay ya presiding officer-80%
 
Ni vyema sasa pamoja na mchakato wa katiba unaoendelea lakini pia watunga sera wetu wakawa na utashi wa kisiasa na kuangalia hali halisi kuhusu maslahi ya umma na sio kujali mambo ambayo yana maslahi kwao binafsi na familia zao pekee.
 
Kwa serikali na watendeaji/watunga sera wa sasa hawawezi kuleta mageuzi. Incredible kuwa Irene Kisaka anaafiki bila kuhoji practicality na cosequencies za kuondoa fao la kujitoa katika mifuko ya hifadhi ya jamii! Hapo ndipo unaona kuwa no one is serious na hatima ya wanachama wa mifuko.
 
Well said Mkuu.
 
Back
Top Bottom